Ugomvi na mke wangu kila nikipata pesa

Mwasapile

JF-Expert Member
Apr 20, 2020
206
441
Yaani imekuwa kila mara nikipata pesa mke wangu analeta kamzozo.. Mpaka imefika mahala nawaza au hapendi nipate pesa!

Nikipokea mshahara mara zote anasema nitoe pesa yote benki nilete mezani. Ofcourse anaweza akawa na hoja zake kuwa hata zikikaa benki huwa tunazitumia na zinaisha haibaki hata senti. Nikimwambia pesa hazitolewagi zote benki haelewi hata kidogo anakuwa mkali sana na anazira

Pia analalama sana kuwa mimi ni mbinafsi kwenye suala la pesa; kitu ambacho nikijitathimini naona kama ananionea tu, over 90% of my income inaishia kwenye matumizi ya familia, sinywi pombe wala sihongi. I am a family man with three sons

Nikimuuliza mke wangu mbona unakuwa mkali kuhusu suala la pesa anazira huku akiniambia kwa kejeli "Samahani nimekuingilia kwenye pesa zako".

Na mara nyingi sana huwa ananilalamikia kuwa nafanya maamuzi yanayohusu pesa mwenyewe kwasababu yeye hana mchango wowote wa kipesa anaounesha kwenye familia; mke wangu ni mama wa nyumbani by default analea watoto watatu.

Imefika mahala mpaka natamani tubadilishane majukumu. Nikae nyumbani yeye akatafute hizo pesa ambazo huwa natafuta ili aridhike na aone kuwa ana mchango kwenye hii familia.

NIFANYAJE WANA JF?
 
Wanawake na pesa hutuwezi....gubu bila sababu ya msingi ndiyo hutupati....kubadilika ghafla na kuanza kumchukia mume ndiyo hutukamati Kabisa.....kisirani juu ya mambo hata si ya msingi ndo usiseme.

WANAUME KUMBUKENI DHAMBI YOYOTE ULIYOWAHI MFANYIA MWANAMKE HUKO NYUMA KABLA HUJAOA MWANAMKE MWINGINE KATU HUWEZI KUWA NA NDOA YENYE AMANI.Chema hupewa chema na Kibaya hupewa kibaya🙏🏽
 
Wanawake na pesa hutuwezi....gubu bila sababu ya msingi ndiyo hutupati....kubadilika ghafla na kuanza kumchukia mume ndiyo hutukamati Kabisa.....kisirani juu ya mambo hata si ya msingi ndo usiseme.....WANAUME KUMBUKENI DHAMBI YOYOTE ULIYOWAHI MFANYIA MWANAMKE HUKO NYUMA KABLA HUJAOA MWANAMKE MWINGINE KATU HUWEZI KUWA NA NDOA YENYE AMANI.Chema hupewa chema na Kibaya hupewa kibaya🙏🏽
Chuma hunoa chuma 😁
 
Msitutishe nyie kwani hamfanyi dhambi mbona mnajipa utakatifu sana .. Chanzo cha matatizo yote dunia hii ni mwanamke tangu Bustani ya Eden

Hatupo hapa kujisifu kwa dhambi zinazofanywa..
Mwanamke wa namna hiyo sio salama kwa afya ya mwanaume na amani pia andiko lake hilo likisomwa na vijana ambao wanatamani waoe watabadili maamuzi wataishi maisha ya wasiwasi kifupi radha ya ndoa wanawake ndio mnaichachua sababu ya ULIMI
 
Wanawake na pesa hutuwezi....gubu bila sababu ya msingi ndiyo hutupati....kubadilika ghafla na kuanza kumchukia mume ndiyo hutukamati Kabisa...
Ume prove kwamba Nyie Wanawake ni Total Failure kwa wanaume na Kwenye Ndoa pia. Kila aina ya majanga na nyie kuanzia kununa kuzira,kuchukia na mengineyo ume ongea mwenyewe hapo.

Asante sana kwa kuongea ukweli.
 
Wanawake na pesa hutuwezi....gubu bila sababu ya msingi ndiyo hutupati....kubadilika ghafla na kuanza kumchukia mume ndiyo hutukamati Kabisa.....kisirani juu ya mambo hata si ya msingi ndo usiseme.....WANAUME KUMBUKENI DHAMBI YOYOTE ULIYOWAHI MFANYIA MWANAMKE HUKO NYUMA KABLA HUJAOA MWANAMKE MWINGINE KATU HUWEZI KUWA NA NDOA YENYE AMANI.Chema hupewa chema na Kibaya hupewa kibaya🙏🏽
Usitutishe😂
 
Back
Top Bottom