Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,895
SHERIA YA KUMHUDUMIA MWANAMKE IFUTWE, KWA SASA AJIRA ZINATOLEWA KWA WOTE BILA UPENDELEO.
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Sheria ya Mwanaume kumhudumia Mwanamke ifutwe. Sheria ya mke kuchukua mkopo kwa Jina la mumewe nayo ifutwe. Ni sheria zilizopitwa na wakati na zisizoendana na ulimwengu wa sasa.
Ni sheria kandamizi, zinazomkandamiza Mwanaume.
Kwa zamani zilikuwa sheria nzuri lakini sio sasa. Zilikuwa nzuri kwa sababu Wanaume walipewa fursa zaidi kuliko wanawake.
Wanaume walipewa fursa ya kumiliki Mali huku wanawake walikatazwa.
Wanaume walipewa fursa ya kusoma na kutafuta elimu huku wanawake wakiachwa nyuma.
Wanaume walipewa fursa ya kutafuta kazi na kufanya shughuli za uzalishaji huku wanawake wakibaguliwa.
Ndio maana sheria ya kumhudumia Mwanamke ilikuwa ya maana na tunaweza kuiita sheria ya haki kama Watibeli tupendavyo Haki
Lakini siku hizi Kila mtu anahaki. Haki sawa baina ya jinsia zimeboreshwa na kulinganishwa.
Ikiwa ni hivyo basi na wajibu lazima uboreshwe.
Isiwe wajibu kwa mwanaume kumhudumia Mwanamke katika ulimwengu wa haki Sawa.
Vijana, sio wajibu wako kumhudumia Mwanamke katika ulimwengu huu wa haki sawa. Ndio maana dunia ya sasa imetoa usawa wa kifursa.
Mwanamke afanye kazi na wewe ufanye kazi. Wote mlete mezani. Hiyo ni Haki.
Mwanamke akifanya kazi alafu anataka kuhudumiwa tuu yaani hela yako anaikodolea macho fukuza. Usiwe mjinga. Huo ni ubinafsi.
Mwanamke ambaye atakuambia pesa ya Mwanamke hailiwi wakati unamuita sijui mpenzi, sijui mkeo, huyo ni tapeli, nyonyaji. Huyo hakufai. Piga chini wala usisite mara mbili mbili.
Ndoa za kitapeli, mahusiano ya kibeberu na kikoloni. Unakuta mwanaume mzima kumbe ni koloni la mtu. Unanyonywa kama mwendawazimu. Alafu miaka 45 hii hapa kisukari, presha, mara Stroke unaacha mke Watu tunapiga. Shauri yako. Usijesema sijakuambia.
Alafu kwa ujinga wenu mnauliza maswali ya kijinga, ooh! Mbona wanaume wanawajibika kufa mapema kabla ya Wake zao. Hivi utaachaje kufa mapema ikiwa wewe umegeuzwa kisukule, kuzuka. Mbona kwetu Babu zetu wamepiga age ya kutosha. Tumieni akili. Jinga kabisa.
Usiendekeza ujinga. Mimi nimemaliza. Mwenye hasira za karibu aje tupigane.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam