Paul Kagame umeongea ukweli hataki unafiki!

Paul Kagame umeongea ukweli hataki unafiki!

Bwn ...Chige usitete ujinga hapa...Kagame anabadilisha katiba kwa matakwa ya Wananchi wake wenyewe....Huu ni wakati wa RAIS KIKWETE kuonyesha democrasia kwa vitendo ndani ya uchaguzi huu...

Kwa matakwa ya wananchi wake eeeeee? Inaelekea hujafunguka macho wewe. Pole sana.
 
Nimependa maneno ya Paul Kagame ameongea ukweli na siyeye tu bali ni jamii yote ya kimataifa wanasubiria huu uchaguzi kwa hamu maana sisi tumekuwa wakwanza kuwanyoshea wenzetu vidole utadhani sisi ni makaika!Haya sasa mpira huko kwetu kupiga penati je tutapaisha au tutalenga goli???

Hamia Rwanda kabisa. Huyo asiyeheshimu katiba na muuaji mkuu ndiye unayemsifia?
 
Nina hakika kagame angekuwa rais wa tanzania..

Kusingekuwa na umoja unajiita UKAWA

Kusingekuwa na Jamiiforums at list msingekuwa na uhuru wa ku post upuuzi na uzushi wenu kuhusu yeye popote..

Chadema siyo kwamba hawamjui Dikteta Kagame.Wanamjua sana ila wanamshabikia kwa kuwa wanachuki na CCM na Kikwete.Hivi ungekuwa na rais kama Dikteta Kagame ungekuwa na Forum humu unaamka kila siku unamtukana na uko huru "Kule watu wanaotofautiana naye kimtazamo anawaua hata Kama wakimkimbia anawafuata huko huko anaua.Leo Rais JK anatangaza hadharani "Najua mtanitukana sana huko kwenye blog zenu lakini nimeshazoea.Ingekuwa ni Dikteta Kagame!!Thubutuu.Maslahi yenu Chadema yasizidi maslahi ya "Tanzania".Kagame afanye yake aachane kabisa na nchi yetu-Mtu mrohooo na anatamaa sana ya RASLIMALI ZA NCHI Nyingine na anavyoona anatawala ka nchi kadogo kama kaya ya MKURYA anahuzunika sana.RWANDA=MLELE District Katavi.Kagame ni mtu hatari sana hata kama akitoa ushauri mzuri
 
Ndo maana kila mara JK anasema akili za kuambiwa... kwa hiyo kwako wewe kanchi kadogo hakana maana kwako? Umbumbumbu mwingine ni shida! Ingekuwa hivyo sisi tungekuwa juu ya china, marekani, algeria nk. Shule jamani!
 
Kagame huna cha kutuambia wewe,kwanza umepindisha katiba,JK SIYO KAMA WEWE,MAANA YEYE MUDA WAKE UMEISHA NA ANAONDOKA,SASA KAGAME WEWE UMEKATAA KUWAACHIA WENGINE NA UTAGOMBEA TENA,HUNA TOFAUTI NA HYABIRAMA

Kagame si rais wako lakini mbona unachuki naye, au wewe ni mhutu.
 
Ndo maana kila mara JK anasema akili za kuambiwa... kwa hiyo kwako wewe kanchi kadogo hakana maana kwako? Umbumbumbu mwingine ni shida! Ingekuwa hivyo sisi tungekuwa juu ya china, marekani, algeria nk. Shule jamani!

Sasa wewe jiulize ni "Kwanini mataifa makubwa tena pamoja ukubwa walionao bado wanaungana kutengeneza nchi kubwa zaidi??Unafikiri Dikteta Kagame anapenda hako kanchi kadogo?Angetamani kukamilishwa kwa makubaliano ya REMERA???Kuendelea amma kutoendelea kwa nchi hakutegemei ukubwa wala udogo wa nchi.
 
Akili za ma-CCM hizi! Kwao nchi ni ukubwa! Na vi-nchi vidogo kama Norway vinavyowasaidia hao mafisadi wanaokuchagua kwenye bunge la ''vitu maalum'' basi ni mikoa!
Au kama kigezo ni udogo wa nchi basi iltakiwa tuwe juu kimaendeleo kupita china na urusi
 
Natamani kagame angekuwa rais wetu wa tz kwa kipindi cha 2005-2015!! Tusingekua hapa!!

Saa hizi ungekuwa kaburini.

Unamjuwa Kagame au unamsikia tu? Uliza kishaua wapinzani wake wangapi uelezwe.

Au hujaona wakimbizi wake waliopo Tanzania?

Ushaona mkimbizi wa Kikwete hata mmoja?
 
..........Kagame ni mnafiki na anatamaa ya madaraka kinachompa tabu ni pesa yake kupotea baada ya kumpa Lowassa kwa ajili ya kampeni anajua fika Tanzania haiwezi kuwa stable chini ya Lowassa...... unapaswa kujiuliza why Rwanda,Kenya na Uganda hawapendi Magufuli ashinde coz they know our country will be stable chini ya Magufuli kila mtu haipendi CCM but mwaka hutuna jinsi ni bora Magufuli kuliko Lowassa wabunge tutachagua wa UKAWA.

Wakuu,
Tuweke ushabiki pembeni lakini kuna issues za kufa na kupona ambazo wote tunapaswa kuzingatia.
Je, Kagame anaweza kuipenda Tanzania baada ya kuwafumua M23 huko DRC? Je anaweza kuipenda Tanzania baada ya kuwafumua wahamiaji haramu Kagera na kwingineko ? Je baadhi ya hao majirani wenye uchu wa ardhi ya Tanzania wanaweza kuipenda Tanzania au serikali ijayo kama itaendelea kugomea kuharakisha muungano wa kisiasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ? Serikali yoyote ijayo itambue kuwa maslahi ya Tanzania ni muhimu kuliko maslahi ya chama, uchu binafsi wa madaraka au hisia zetu binafsi kama wanajamvi. Kumbukeni kuwa msiba wa ng'ombe huwa furaha kwa kunguru ! Simply tuiwekeTanzania kwanza !
 
Nimependa maneno ya Paul Kagame ameongea ukweli na siyeye tu bali ni jamii yote ya kimataifa wanasubiria huu uchaguzi kwa hamu maana sisi tumekuwa wakwanza kuwanyoshea wenzetu vidole utadhani sisi ni makaika!Haya sasa mpira huko kwetu kupiga penati je tutapaisha au tutalenga goli???

Kagame na mahakama wamechemka mno swala la kubadilisha katiba ili aendelee kutawala

Katiba zote duniani zinapoandikwa huwa haziangalii mtu usoni.Huwezi andika katiba ukimlenga mtu.Katiba ukiandika unafumba macho.Unaandika raisi wa Rwanda atatawala miaka 10 kwa mfano bila kujali ni nani.Sababu katiba uandikapo huwi na jina au sura ya mtu.Unaendelea kuandika waziri mkuu atakaa miaka mingapi unaandika kwenye katiba bila kuwa na jina wala sura sasa au miaka ijayo.

Rwanda ndio nchi pekee duniani inayoandika katiba kwa kuangalia mtu usoni.Wanaandika katiba ya Kusema Kagame atawale miaka mingapi!!!!! Rwanda wanachokwenda kuandika si katiba ni takataka sababu inatizama mtu usoni kwa jina.Hata katiba za vyama tu vya kuweka na kukopa huwa havina sura au jina la mtu.

Jina la mtu kuwa chanzo cha kubadili katiba ni ujinga.Hiyo mahakama iliyoamuru katiba ibadilishwe ili Kagame aendelee kutawala.Hawajui sheria za uandishi wa katiba.Ilibidi ombi hilo walitupilie mbali hata kama wanyarwanda wote wangesema tunataka.Walichofanya ni kuweka precedence mbaya mno kuwa katiba yaweza badilishwa kwa sababu ya mtu! Ukomo wa uongozi kwenye katiba yoyote haulengi mtu kwa jina.

Majaji wa Rwanda na mahakama hawajaitendea haki fani ya sheria.Wamegeuza mahakama kuwa chombo cha kisiasa badala ya chombo cha kisheria.
 
Kwani mmeambiwa upinzani wameshinda hadi awaachie nchi?
 
Kagame huna cha kutuambia wewe,kwanza umepindisha katiba,JK SIYO KAMA WEWE,MAANA YEYE MUDA WAKE UMEISHA NA ANAONDOKA,SASA KAGAME WEWE UMEKATAA KUWAACHIA WENGINE NA UTAGOMBEA TENA,HUNA TOFAUTI NA HYABIRAMA

Hakuna point uloiongea apo..
 
Wakati yeye na timu yake wanabadilisha katiba ili aendelee msimu wa tatu, JK anaondoka baada ya misimu yake miwili kwisha kwahiyo he's no match JK!

NO JK ANAAKIKISHA CHAMA CHAKE HAKITOKI MADARAKANI, IVYO HAINA TOFAUTI KATI YA JK NA NKURUNZIZA NA NADHANI DAWA YAO NI KUWASHITAKI THE HAGUE, UNO PIA AU NADHANI au
 
Uzalendo kwanza. Kauli ya kagame imemhusu kikwete maana alimwambia kagame apatane na wapinzani wake wa kihutu, sasa anamtaka amuoneshe na yeye demokrasia kwa kufanya haki kwa wapinzani wake wa kisiasa. Sasa ninyi mnaoingiza mambo ya uchumi na bandari yanahusiana vipi na maneno ya kagame?

Mwacheni amzungumzie kikwete maana ana uhalali wa kufanya hivyo kama kikwete alivyokuwa na uhalali wa kumuambia apatane na waasi wa kihutu kwa kufanya nao mazungumzo ya amani.
 
Hivi Watanzania tumekuwaje? Huyu bwana tunajua ana inda na Tz kwasababu ya kichapo cha M23 na uwepo wake kule DRC.

Tunajua ana inda na kauli ya JK na tunajua ni dereva wa CoW kwa nia ile ile
Hana jema analoweza kuongelea kuhusu nchi yetu

Hatusimami kwa U-CCM au UKAWA , tunaangalia masilahi mapana ya taifa.

Anaposema ata 'hit hard kwa JK' haa maana kwa JK kama mtu, ana maana kwa Tz.

Jirani mwema anapaswa kukaa kimya kwa wakati huu. Ndivyo tuliyokaa kimya chaguzi za nchi jirani.

Kenya walipopata matatizo tuliweza kuwaweka pamoja kwasababu kila mmoja alikuwa na trust nasi

Leo Museveni akiibuka na lake, Uhuru na lake, Nkurunzinza na lake juu ya Tz hatuoni tatizo?

Hivi PK amesema kwa nia njema kweli! angalieni anaweza kutupa uchafu ilimradi tuvurugane arudi DRC

Mambo yetu yanatuhusu wenyewe, PK aendelee na kubadili katiba atawale kama chief, hatuhusu

Hadi hapa amefanikiwa maana hatujadili hatma yetu tunamjadili PK ! who's PK kwetu?

Huyu PK anaweza kusema tukamsikiliza kweli!

Hawa watu wanashangaza sana! Sijui ndio yale yale ya adui wa adui yako ni rafiki yako?
 
UJUMBE MUHIMU WA KAGAME KWA JAKAYA KIKWETE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU!!

"Kuhubiri kuhusu demokrasia ni jambo moja na kusimamia demokrasia ni jambo jingine!!Kama Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tunafuatilia yale yanayoendelea Tanzania wakati ikielekea katika Uchaguzi wao Mkuu; hivyo tuna hamu ya kuona rafiki yetu na Mwenyekiti wetu anayesimamia jumuiya yetu akithibitisha kwetu namna demokrasia inavyotakiwa kusimamiwa kwa vitendo nchini Tanzania ili ajitofautishe nami ama na Nkurunzinza"...Kagame, Paul....Je unakubaliana na Paul Kagame kwa niaba ya Viongozi wenzake wa Afrika Mashariki? Unadhani Jakaya Kikwete anatakiwa kuwathibitishia namna gani demokrasia inavyotakiwa kutekelezwa hapa Tanzania?..Je kunaviashiri vyovyote vya demokrasia kuvunjwa na haki kuzimwa chini ya Usimamizi wa Jakaya Kikwete?..Usiogope TIRIRIKA!!
 
Back
Top Bottom