Hapana Chakaza, usisikilize propaganda za akina Kingunge ingawaje kwako ni muhimu kwa kuwa ni UKAWA! Katiba ya CCM inasema Kamati Kuu itapokea majina yasiyopungua matano kutoka Kamati ya Maadili na Usalama! Wakati nakupa hilo dokezo, ngoja nikutafutie screenshot ya Katiba ya CCM!
Kazi za kutumwa zinatufanya tusiwe na uwezo kukamilisha tunachosema! Anyway, nimeipitia tena katiba ya CCM. Kwa kifupi, kuna mkanganyo kidogo ambao bila shaka unatokana na nguvu iliyonayo Kamati ya Maadili na Usalama ambayo haijataja kazi zake kwenye katiba zaidi ya kutaja uwepo wake kwenye Ibara ya 107 (23).
Katika pekua pekua, nikakuta kumbe, according to
Mwananchi, kazi za Kamati ya Maadili na Usalama zimetajwa kwenye Kanuni za Uongozi na Maadili, toleo la 2012 kifungu cha 4(ii). Unfortunately, sijui hizi kanuni zinapatikana wapi tena nakumbuka siku za nyuma nilizitafuta sana lakini sikuzipata! Lakini Mwananchi wanaojua ni wapi wamezipata hizo kanuni wanasema:
"…wanachama wanaogombea uongozi ambao uteuzi wao hufanywa na vikao vya kitaifa, watachunguzwa kwanza uadilifu wao na chombo cha maadili cha CCM kwa ushirikiano na vyanzo vingine.
....................................
Ikiwa mwanachama hakupendekezwa kwa sababu ya kukiuka Katiba ya CCM, Kanuni za CCM na sheria ya nchi, hatakuwa na haki ya kukata rufaa kwa mtu yeyote au kikao chochote. Lakini ikiwa mwanachama atakataliwa kugombea kwa sababu ya madhambi yake katika chama, basi ni wajibu wa Kamati ya Usalama na Maadili kumjulisha makosa yaliyomnyima haki ya kugombea, naye anaweza kukata rufaa kwa mujibu wa haki zake kikatiba.
On the other hand, wakati kazi za Kamati ya Maadili hazijaoneshwa kwenye katiba zaidi ya kuwepo kwenye kanuni, moja ya kazi za Kamati Kuu kwenye hili suala zinaishia tu kusema: 109 (6)Unapofika wakati wa Uchaguzi Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itashughulikia mambo yafuatayo:-
(b)
Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu majina ya Wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo basi, kwa maoni yangu nadhani mkakati wa kumkata Lowassa ulianza mwaka 2012 lakini wafuasi wake wakachelewa kuliona! Walichelewa kuliona kwa sababu, wakati wao walikuwa na imani kwamba EL ana timu yake kwenye Kamati Kuu, katiba yao wenyewe haijasema popote kwamba itajadili majina ya wagombea WOTE bali itapendekeza majina yasiyozidi matano!
Wakati katiba haijasema popote kwamba Kamati Kuu itajadili majina yote ya wagombea, kanuni zinasema majina ya wagombea yataanza kwanza kujadiliwa na Kamati ya Maadili na Usalama na kutoka hapo; wapo ambao hawatapendekezwa na hawatakata rufaa popote lakini pia wapo ambao hawatapendekezwa na kupewa haki ya kukata rufaa!! Haki ya kukata au kutokata rufaa itategemea na "makosa" watakayokukuta nao Kamati ya Maadili!!! Sasa endapo Timu Lowassa (CCM) wangekuwa makini, since 2012 wangegundua kwamba kuna watu wameandaliwa kupelekwa Qibla na wakishapelekwa; hakuna kukata rufaa!!!