Paul Kagame: Dikteta katili anayefugwa na Wamarekani

Mzee2000

JF-Expert Member
Aug 7, 2009
523
250
Kagame anapata sifa nyingi sana hasa kwenye vyombo vya habari vya magharibi lakini ukweli ni kwamba sababu kubwa ya kupendwa ni kwamba yeye pamoja na Museveni ndio walinzi wakuu wa western interests katika great lakes region (hasa Marekani).

Katika historia ya Afrika Mashariki na kati hakuna mtu aliyehusika kuua watu wengi zaidi either directly au indirectly kama Paul Kagame.

Report ya ICTR (International criminal tribunal for Rwanda) ilipata Ushahidi wa kutosha kumshitaki Kagame kwa Genocide kwamba yeye na majeshi yake ndio chanzo kikuu kilichosababisha mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 .

Wamarekani walikataa kufuatilia matokeo ya uchunguzi wa ICTR kwa sababu zao wenyewe. ICTR ilitoa maujumisho yafuatayo kuhusu ni nani aliyetungua ndege iliyomuua Habyarimana.

1) Frank Nziza wa RPA( RPF sasa) ndiye aliyekuwa mkuu wa timu ya RPF iliyotungua ndege. Huyu alikiri kuwa ndiye aliyefyatua mizinga iliyotungua ndege

2) Matayenga Nyakarundi (wa RPF) ndiye aliyempa Frank hayo makombora mawili yaliyosafirishwa kwenda Masaka ( Rwanda, karibu na airport) ambapo yalitumika kutungua ndege.Makombora yalifichwa kwenye shamba la Didier Mazimpaka, karibu na uwanja wa ndege.

3) Kayumba Nyamaswa( sasa yuko South Afrika) alihudhuria mikutano mitatu ndani ya RPF iliyopanga kutungua ndege. Mikutano hiyo ilikuwa ‘chaired’ na Paul Kagame.Kayumba alisha kiri kuwa RPF ilitungua hiyo ndege.

4) Serial numbers za Kombora lililotumika kutungua ndege zilikuwa traced mpaka kwenye maghala ya silaha ya jeshi la Uganda. Makombora ya namna hiyo hayajawahi kutumika katika jeshi la Burundi. Kumbuka RPF ilikuwa sehemu ya jeshi la Uganda( waasi) na walitumia silaha zilizotoka Uganda.

Kuna report ya wafaransa pamoja na nyingine ya serikari ya Spain ambazo zilitoa majumuisho hayohayo kwamba RPF ndio waliotungua ndege ya Habyarimana. Kagame aliua watu wengi sana Rwanda (maelfu kwa maelfy ya wahutu) pamoja na wacongo( kutoka ripoti za mashirika ya haki za kibinadamu) lakini kwa sababu ni mtoto mteule haguswi na mtu yoyote.

Kagame hakupenda mapatano yaliyokuwa yanazumgumzwa Arusha, ambapo walikubaliana kugawana madaraka na Habyarimana .Wakaamua kutungua ndege ili wachukue madaraka peke yao kwa kuwa jeshi lao kwa wakati huo lilikuwa na nguvu kuliko la Burundi.

Ila mwishoni, kama ilivyotokea kwa Mobutu, Wamarekani watamchoka na siku hiyo ikija, hatakuwa na pa kukimbilia, na madhambi aliyoyafanya yatalipizwa kisasi na wanyarwanda na waathirika wengine wengi wa RPF maziwa makuu.

Sent from my SM-A505FN using JamiiForums mobile app
 

Bepari2020

JF-Expert Member
Nov 7, 2020
522
1,000
Vipimo vya rais kupendwa na Marekani ni vipi? Kama ni sifa tuu kwenye vyombo vya habari labda ufafanue ni vyombo vipi maana vingi ni vya binafsi siyo vya serikali. Kama ni vyombo vya habari binafsi vinampa sifa hiyo siyo Marekani rasmi. Hivyo vyombo vya habari binafsi vina ajenda zao ambazo zinaweza kuwa tofauti na sera za Marekani. Kama vipimo ni ushirikiano baina ya nchi, hata sisi tunao ushirikiano mzuri tuu na Marekani. Haina maana Marekani inailinda serikali ya CCM kwa sababu Tanzania na Marekani wana ushirikiano.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,983
2,000
Mzungu hana rafiki wa kudumu wakishafikia malengo yao au wakimaliza walichokuwa wanakitaka basi na urafiki unafika kikomo

Vipi Mfaransa hahusiki humo maana wote hao uchumi wao unategemea na kuiba sana na ili kuiba ni lazima uchonganishe na uwe na kundi lako la Uasi

Ila yote yana mwisho na sisi ni Taifa kubwa ila tumelala kama kwa upole

Always tunasaidia tu ila wenzetu waafrika jirani wanafuata mkondo wa wazungu yaani kuongeza uchumi kwa kuuwa na kupora
 

kasigazi kalungi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
3,953
2,000
Vipimo vya rais kupendwa na Marekani ni vipi? Kama ni sifa tuu kwenye vyombo vya habari labda ufafanue ni vyombo vipi maana vingi ni vya binafsi siyo vya serikali. Kama ni vyombo vya habari binafsi vinampa sifa hiyo siyo Marekani rasmi. Hivyo vyombo vya habari binafsi vina ajenda zao ambazo zinaweza kuwa tofauti na sera za Marekani. Kama vipimo ni ushirikiano baina ya nchi, hata sisi tunao ushirikiano mzuri tuu na Marekani. Haina maana Marekani inailinda serikali ya CCM kwa sababu Tanzania na Marekani wana ushirikiano.
Wanachompendea ameshakisema kwamba Kagame na Mseveni ndo viranja wa Marekani kuhakikisha maslahi ya Marekani yanalindwa. Kama hujaelewa mpaka hapo basi unahitaji darasa
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
8,316
2,000
Ukweli hauozi. Kagame anajidai na kufanya usanii wa kutisha hata mabwana zake wa magharibi. Ila kila mwenye akili anajua ni muuaji katili. Siku ikifika kama yuko hai ataburuzwa kujibu kama atakua amekufa historia itaandikwa ukweli tofauti na uongo anayoandika yeye.
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
13,072
2,000
Sera nzuri ya kiuchumi ya Rwanda ndio imefanya nchi nyingi za magharibi zimpende PK.

Kwamba ameruhusu uchumi uwe huria kwa sheria za Rwanda na kuondoa vikwazo kadha wa kadha kwa wafanyabiashara lakini wanalipa kodi inavotakiwa.

Pili, amegeuza kilimo cha kizamani kuwa kilimo chenye kutumia ujuzi na elimu yaani knowledge based ecomony ambapo wakulima wanaboresha masoko ya bidhaa za kilimo.

Tatu, Rwanda ya PK inatumia uzuri madini ya Congo ambapo kwa kutumia madini hayohayo Rwanda imeweza kuwekeza kwenye viwanda vikubwa kama kwanda cha magari ya VW.

Ila bado Rwanda inashikilia njia kuu za uchumi kwa kuhakikisha kwamba wafanyabiashara na makampuni yote yana "connection" na chama na serikalini.

Imaaminika kuwa sehemu ya Kivu ni ya Rwanda na imejimilikisha eneo hilo na pana kambi kubwa ya jeshi.

Utegemezi wa nchi za magharibi kwa Rwanda upo katika utulivu wakati wao wakichukua maliasili kule Congo na Rwanda ikihakikisha "security stability" katika eneo lote la maziwa makuu.

Ukimuongelea M7 ndo wahitimisha kwani hawa ni ndege wawili wafananao wenye mbawa sawa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom