mchawi wa kusini
JF-Expert Member
- Apr 18, 2018
- 805
- 810
Habari ya siku ya leo wana JF, naamini leo ni siku ya Sabatho takatifu wenye kumuabudu Mungu waandelee na juhudu maana Mungu ni Msikivu.
Twende na mimi pamoja;
Bila shaka umesikia viongozi wengi wa Afrika wakizungumzia umoja wa Afrika. Umesikia wakisema wanataka Afrika moja iliyoungana lakini dhamira zao sio kweli, wengi ni wanafiki sana na hawapendi hicho kitu. Ni waoga na wenye tamaa lakini sio Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.
Tazama, juzi tu nchi yake ilialika nchi ya DRC kwenye maonyesho ya kibiashara nchini humo. Wananchi wa DRC waliingia nchini Rwanda kama kwao, bila pingamizi zozote, wakafanya biashara na wakarudi kwao. Huu ni mfano wa kuigwa kiukweli. Nchi hizo mbili zilipata faida kubwa.
Hiyo haitoshi, Rwanda mwaka huu 2022 imemwajiri msomi maarufu wa maswala ya kifedha, Tidjane Thiam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rwanda Finance Limited. Bw. Tidjane ni raia wa Ivory Coast na msomi aliyebobea kwenye maswala ya fedha.
Baado hiyo haikutosha, Rais Kagame sasa amemwajiri Profesa Robert Ebo Hinson kuwa Naibu
Chansela wa Chuo Mkuu cha Kigali, nchini Rwanda. Profesa Robert ni raia wa Ghana.
Huyu profesa ni msomi anayefundisha kwenye vyuo mbalimbali Afrika na nchi za Magharibi.
Rais Kagame anastahili pongezi kwa kusema na kutenda, hebu mpe neno moja Rais Kagame bila kupepesa macho na bila kuangalia madhaifu yaliyonayo.
Sent from my SM-A146P using JamiiForums mobile app