Pamoja na kwamba Taifa la Norway lina kiwango kikubwa cha gesi linategemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji (Hydroelectric power)

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,327
8,243
Pamoja na kwamba Taifa la Norway lina kiwango kikubwa cha gesi linategemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji (Hydroelectric power)

Kwenye suala la umeme uchaguzi wa kutumia umeme wa maji (hydroelectric power) ni bora zaidi ukilinganisha na vyanzo vingine vya umeme.

Nchi ya Norway ni moja ya nchi duniani inayotegemea pia uchumi wa gesi. Lakini pamoja na kwamba Norway wana kiwango kikubwa cha gesi lakini bado umeme wa maji umekuwa wa gharama nafuu na ndio unatumika sana kama chanzo cha umeme.

Kwa Norway umeme wa gesi huwa wanautumia kipindi cha baridi pale ambapo umeme wa maji umezidiwa.

Gesi ni nishati ambayo mara nyingi ni nzuri kwa matumizi ya kupikia. Hivyo mimi nadhani kama serikali ina nia ya kuendeleza uchumi wa gesi. Basi ijikite kuitumia hiyo gesi katika mambo mengine mfano kupikia, na kuanzisha viwanda vinavyotumia gesi asilia. Mfano viwanda vya mbolea ni viwanda ambavyo hutumia gesi asilia kuzalisha mbolea.

Pamoja na kwamba tutaitumia gesi pia kuzalishia umeme lakini tuyape maji kipaumbele cha kwanza kwasababu maji ni bure na pia ni renewable resources. Na uzuri ni kwamba geographia ya taifa letu tumejaliwa vyanzo vingi vya maji, hivyo tukizitumia akili zetu vizuri tutaweza kufanya vizuri hata dunia ikatushangaa.

mmexport1618038529876.jpg
mmexport1618038503242.jpg
mmexport1618038492504.jpg
mmexport1618038465821.jpg
mmexport1618038451210.jpg
 
Muhongo haifai kuzungumzia suala la electrical power.

Hatujasahau aliwaambia watanzania wanafaa kuwekeza kwenye juice tu na siyo gasi ili wazungu wake wapate vitalu vya gas.

Hao hao aliowagawia vitalu ndo anawapigania sasa hv wapate soko la gasi.

Watanzania siyo wapumbuvu na wajinga kiasi hicho. Mradi wa Bwawa la Nyerere uendelee na umaliziwe una tija kubwa kwa Taifa!!

Ingekuwa gasi ina manufaa tungeshaona bei za umeme zikishuka bei! Mbona hamna unafuu wowote?

Hatupendi udalali sisi!!
 
Thanks maneja kwa DATA; ukweli alioyasema profesa Muhongo hata kama yana ukweli but kwa gharama ambazo tumeisha ziingia, sioni kama ni busara kuachana na mradi ule wa Rufiji. Asante pia kwa hizi data; binafsi maprofesa wa Tanzania hua nawaamini pale wanapokua darasani kufundisha, huku field wana pwaya sana, sijui tatizo huaga ni nini? Tumeisha tumia zaidi ya Trilion kadhaa halafu eti tusitishe tu kwasababu umeme wa dunia ni wa gas? Point nyingi alizozingumza Muhongo pamoja na CAG ukweli zote Zitto Kabwe alizizungumza bungeni, kwamba utafiti wa mradi ule ulifanywa na mwalimu Nyerere miaka ya 70, kapitieni Hansard za Bunge, wabunge wa ccm walipinga, Muhongo (nadhani alikua bado waziri ) alikaa kimya, hakum support Zitto wakati ule halafu leo tumetumia pesa nyingi hivyo, "wasomi" wa bungeni wanataka tusitishe, BIG NO, twendage hivyo hivyo
 
Mtanzania gani anauwezo wa kuwekeza kwenye gesi?
Hata Mo na Bakhresa wakiungana hawawezi
 
Hivi pamoja nayote mleta Uzi ardhi yetu inamaporomoko yakutosha tupe idadi pia ,fananisha na hiyo nchi
 
Mkuu, kunawatu wanataka kutumia ushawishi wao Kwa hoja za kijinga ili kumsogeza Raisi karibu nao Kwa minajili ya kupewa uwaziri!!

Na wanataka hivyo, ili kuturudisha kwenye mgao wa umeme, wauze majenereta kariakoo,

Kuna maprof nchi hii ni kama misukule isiyo na maana, mtu na akili zako, unawaambia Watanzania wote hawana uwezo wa kuwekeza Kwenye gesi, hizi ni dharau kabisa
 
Thanks maneja kwa DATA; ukweli alioyasema profesa Muhongo hata kama yana ukweli but kwa gharama ambazo tumeisha ziingia, sioni kama ni busara kuachana na mradi ule wa Rufiji. Asante pia kwa hizi data; binafsi maprofesa wa Tanzania hua nawaamini pale wanapokua darasani kufundisha, huku field wana pwaya sana, sijui tatizo huaga ni nini? Tumeisha tumia zaidi ya Trilion kadhaa halafu eti tusitishe tu kwasababu umeme wa dunia ni wa gas? Point nyingi alizozingumza Muhongo pamoja na CAG ukweli zote Zitto Kabwe alizizungumza bungeni, kwamba utafiti wa mradi ule ulifanywa na mwalimu Nyerere miaka ya 70, kapitieni Hansard za Bunge, wabunge wa ccm walipinga, Muhongo (nadhani alikua bado waziri ) alikaa kimya, hakum support Zitto wakati ule halafu leo tumetumia pesa nyingi hivyo, "wasomi" wa bungeni wanataka tusitishe, BIG NO, twendage hivyo hivyo
Hizo data sio za zama hizi.TUSIDANGANYANE.Norway kamwe hawatumii hydroelectric power.Wana Mafuta na gesi kibao.Wanatumia Nuclear Plant unaoendeshwa na Gesi.Isitoshe ni kisiwa kidogo hata Zanzibar kubwa.Nchi zote alizozitaja huyo Profesa Bashite mpya hazitumii (H.E.P).Zote zinatumia aidha Nuclear Plants,Gesi,Diesel.Huu mradi wetu ni upotevu wa pesa.Isitoshe Dunia inakabiliwa na janga liitwalo Climate Change,ambalo Mfadhili mkubwa Marekani wamejitoa.Hii hali inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kama vile joto kali sana,Ukame,Nchi nyingi kugeuka Jangwa n.k.Profesa Original Mr Muhongo yupo sahihi kabisa.Nyie ndio wale CAG aliwataja kwenye ripoti yake.
 
Pamoja na kwamba Taifa la Norway lina kiwango kikubwa cha gesi linategemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji (Hydroelectric power)

Kwenye suala la umeme uchaguzi wa kutumia umeme wa maji (hydroelectric power) ni bora zaidi ukilinganisha na vyanzo vingine vya umeme.

Nchi ya Norway ni moja ya nchi duniani inayotegemea pia uchumi wa gesi. Lakini pamoja na kwamba Norway wana kiwango kikubwa cha gesi lakini bado umeme wa maji umekuwa wa gharama nafuu na ndio unatumika sana kama chanzo cha umeme.

Kwa Norway umeme wa gesi huwa wanautumia kipindi cha baridi pale ambapo umeme wa maji umezidiwa.

Gesi ni nishati ambayo mara nyingi ni nzuri kwa matumizi ya kupikia. Hivyo mimi nadhani kama serikali ina nia ya kuendeleza uchumi wa gesi. Basi ijikite kuitumia hiyo gesi katika mambo mengine mfano kupikia, na kuanzisha viwanda vinavyotumia gesi asilia. Mfano viwanda vya mbolea ni viwanda ambavyo hutumia gesi asilia kuzalisha mbolea.

Pamoja na kwamba tutaitumia gesi pia kuzalishia umeme lakini tuyape maji kipaumbele cha kwanza kwasababu maji ni bure na pia ni renewable resources. Na uzuri ni kwamba geographia ya taifa letu tumejaliwa vyanzo vingi vya maji, hivyo tukizitumia akili zetu vizuri tutaweza kufanya vizuri hata dunia ikatushangaa.

View attachment 1748264View attachment 1748265View attachment 1748266View attachment 1748267View attachment 1748268
Hali ya Norway ni tofauti. Nchi yao ina miamba na fjords ambayo kwa asili imekuwa ikitumika kuzalisha nishati hata kabla gesi yao ya North Sea kupatikana. Kwa sababu ya miamba, mabwawa yao hayajai matope hata siku moja, na kwa sababu ya wingi wa fjords maporomoko ya maji ni mengi na hivyo kufanya uzalishaji wa umeme kuwa wa gharama ndogo. Ingekuwa vizuri kama ungetuambia Norway imejenga miradi mingapi ya hydro power toka gesi yao ipatikane. Ninavyojua Norway wako mestari wa mbele kupinga ujenzi wa hydropower projects. Ndio maana walikataa kuufadhili huu mradi pamoja na kuwa walifadhili hatua zote za awali za utafiti. Athari ya mabwawa makubwa inajulikana dunia nzima. Ni nchi chache sana ambazo zinawekeza kwenye miradi ya aina hii.

Amandla...
 
Hydro inaonekana ina bei nafuu kwa sababu gharama za uharibifu wa mazingira haziingizwi kwenye hizo hesabu. Ni kama vile mkaa unaonekana ni nafuu kuliko gesi kwa sababu gharama za deforestation haziingizwi kwenye bei. Tungekuwa tunajumuisha na gharama ya kupanda upya miti na athari katika tabia nchi, bei ya mkaa isingeshikika.

Amandla...
 
Thanks maneja kwa DATA; ukweli alioyasema profesa Muhongo hata kama yana ukweli but kwa gharama ambazo tumeisha ziingia, sioni kama ni busara kuachana na mradi ule wa Rufiji. Asante pia kwa hizi data; binafsi maprofesa wa Tanzania hua nawaamini pale wanapokua darasani kufundisha, huku field wana pwaya sana, sijui tatizo huaga ni nini? Tumeisha tumia zaidi ya Trilion kadhaa halafu eti tusitishe tu kwasababu umeme wa dunia ni wa gas? Point nyingi alizozingumza Muhongo pamoja na CAG ukweli zote Zitto Kabwe alizizungumza bungeni, kwamba utafiti wa mradi ule ulifanywa na mwalimu Nyerere miaka ya 70, kapitieni Hansard za Bunge, wabunge wa ccm walipinga, Muhongo (nadhani alikua bado waziri ) alikaa kimya, hakum support Zitto wakati ule halafu leo tumetumia pesa nyingi hivyo, "wasomi" wa bungeni wanataka tusitishe, BIG NO, twendage hivyo hivyo

Bila kupinga maelezo yako mazuri, huo umeme wa gas ulitumia kiasi gani, mpaka ukatelekezwa na kuamua kuwekeza fedha kwenye huu wa maji?
 
Back
Top Bottom