Kushambulia watu binafsi kwa mgongo wa ripoti ya CAG hakusaidii taifa

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
Ukiwa mtu wa kufuatilia Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa miaka kadhaa utagundua kuwa kumekuwa na kukosekana kwa uwajibikaji hasa kwa watumishi wengi wa umma mara kwa mara.

Imekuwa ni kama kawaida kuona CAG anatoa ripoti kunakuwa na ubadhirifu mkubwa unafanyika, japokuwa kinachoripotiwa huwa ni sehemu ya uhalisia wa kilichopo lakini hiyo ni wazi kuwa kuna mambo mengi hayapo vizuri katika suala la uwajibikaji Nchini.

Ni kawaida kuona Wanasiasa wakipiga kelele kiasi fulani kila Ripoti hiyo inapotoka pia lakini si kama ilivyo safari hii.

Binafsi natamani ifike hatua kama wenzetu katika Nchi zilizoendelea kunakuwa na uwajibikaji, yani mfumo uwafanye watu wawe wanawajibika wenyewe badala ya kuishia kupiga kelele kila jambo linapotokea kisha baada ya muda linapotezewa.

Pamoja na hayo, Mwaka huu (2023) kelele kuhusu ripoti za CAG zimekuwa nyingi kutoka kwa Wanasiasa, lakini kwa jinsi wanavyochangia unaona wanafanya hivyo ili kumkomoa mtu fulani au kikundi cha watu fulani.

Nimefuatilia hoja za Wabunge kadhaa wakiwemo Luhaga Mbina ambaye ni Mbunge wa Kisea, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na wengine wanaochangia kuhusu ripoti hiyo unaona kabisa hoja zao si kusaidia jamii au kusaidia Serikali au mamlaka mbalimbali zilizotajwa bali zinawalenga watu binafsi.

Ripoti za CAG zimetaja taasisi ngapi miaka ya nyuma na hakukuwa na hatua stahiki zinazochukuliwa?

Mijadala iliyokuwa ikifanyika Bungeni tena ikajadiliwa na Wapinzani waliokuwa na nguvu Bungeni ililenga taasisi au mifumo mibovu na sio watu binafsi.

Sipingi viongozi ambao walihusika na ubadhirifu kuwajibishwa, lakini Wabunge na wachangia hoja wengine wanatakiwa kukemea mifumo inayoruhusu kufanyika kwa ubadhirifu na kuacha kuwashambulia watu binafsi, hilo haliwezi kusaidia.

Anaposhambuliwa Waziri wa Fedha, Dr Mwigulu Nchemba au Waziri fulani au hata mawaziri waliopo madarakani sasa, hata wakibadilishwa kama mifumo ya uendeshaji ofisi zao au bila kuwadhibiti watendaji wa chini yao ambao ndio wanaohusika kwa asilimia kubwa itakuwa ni kazi bure.

Ukitaka kubaini hilo, Mpina wakati anatoa hoja zake Bungeni akiingia mtu na kumjibu kwa hoja kwa lengo la kumrekebisha kile alichokisema, unaona anashindwa kuitetea hoja yake kwa hoja, bali anakuwa mkali na kutoa maneno ya kuonesha hajafurahishwa kujibiwa kwa hoja.

Kinachofanyika siku chache hizi Bungeni ni ile “Tunaenda kuwakomoa”, watu wasioelewa vizuri wanaona Wabunge wanafanya kazi kweli waliyotumwa lakini kiuhalisia wenzao ni kama wapo kwenye “misheni” ya kuwachafua watu wachache na hilo haliwezi kusaidia kuondoa ubadhirifu kwenye ripoti zajazo za CAG.

Nimetazama mijadala inayoendelea kwa jicho la utofauti, nipo tayari kupingwa na kujibiwa kwa hoja sio matusi au kebehi.

MDAU WA SIASA
 
Esther unampambania mumeo kwa nguvu zote
 
Nimesema asubuhi na narudia tena kusema;
Mwigulu ana haki ya kuwa na Chawa aidha wa ridhaa (amateurs) au wa kulipwa (professionals).
 
Jambo la muhimu ni kuangalia hao wanaochambua ripoti ya CAG na kuwahusisha watu binafsi kwa majina yao, kuhusika na ufisadi, hoja zao ni za kweli au siyo za kweli? Hoja zao zina mantiki au hazina mantiki?

Sijaona mapungufu kwenye hoja za Mh. Mpina.

Wanaowataja watu binafsi, wapo sahihi kabisa. Maana ufisadi haufanywi na taasisi bali watu binafsi.
 
Back
Top Bottom