Orodha hii ya matokeo ya Form 4 kwa mikoa imenistua. mikoa tunayoichukulia poa inaongoza kitaifa na mingine imebaki historia haina tena uwezo

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,450
Nikiwa naperuzi mtandaoni nimeikuta hii orodha ya mikoa

SAT ni idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani



Nimeshangaa sana kuona kuna mikoa ambayo hatuizungumzii sana imefanya vizuri na kuna mikoa ambayo ilikuwa navuma hapo zamani lakini kwa sasa hali ni mbaya,

Dar es salaam shule za day zina heka heka nyingi sana, Vigodoro mitaani, vibanda vya games kila kona, studio za kurekodi mziki, kutumia muda mwingi Tiktok, kuna makundi mengi sana, n.k.

Manyara wameupiga mwingi sana, sikuwahi kuwadhania kabisa.

Mkoa wa Mara ndio mkoa pekee ambao umefanya vibaya kanda ya ziwa, hivi ni kweli kuna wasomi huko kama tunavyoaminishwa au ilikuwa ni miaka ya zamani ?

Morogoro kuna shida gani mbona matokeo ni mabovu sana
 
Kanda ya ziwa wanatisha sana
 
Dar ni halali kuwa na matokeo hayo. Nashuhudia sana wanafunzi mienendo yao.
Hatarii tupuu. Lol
Mambo ni mengi sana kwa wanafunzi wanaosoma Day Daresalaam, ndio maana wazazi wengi wanapeleka watoto shule za boarding au za day mikoani
 
Natazama baadhi ya wazazi wanashangilia watoto kufaulu kidato cha nne… najisikitikia kuona kijana kapoteza miaka minne for nothing na anaenda kupoteza miaka mingine miwili na baadae atapoteza miaka mingine mitatu ama zaidi. Wazazi tunachangia sana kupotezea pesa na muda wa vijana wetu.
Kam mzazi najikunja hadi nitoke damu Goodluck(mwanangu) aende English medium. Nimekazia lazima katika masomo yake akomalie kijeruman na kifaransa. Hata akifeli lasaba sijali.
Nilimwambia achague fani, gereji,masofa, cherehani, mziki, upishi,ushonaj n.k kachagua gereji
Kila jion akitoka shule jumatatu, jumatano na ijumaa.anaenda gerej kwa mjomba ake anapata mawili matatu. Jumamosi saa nne mpaka saa 10 anashinda gereji. Kwa sasa anaweza kazi ndogo ndogo kama kumwaga oil, kubadili tairi, kuweka maj n.k pia anaweza kuendesha. Yuko la tano mpaka akifika la saba atakuwa angalau ana ideas kuhusu ufundi wa magari.
Wakati unashangilia wakwako amefaulu sekondari mimi nasali afeli ili isiwe vita nimpeleke ufundi ki urahisi na hata akifaulu bado atakwenda njia ninayotaka… ufundi wa magari veta. Akimaliza miaka minne huko teyari ni fundi wako akimaliza miaka minne o-level atarudi kula ugali wako wa shikamoo.
Goodluck akimaliza certificate ya ufundi nitampeleka diploma. Miaka sita ya ufundi na wako atakua kamaliza kidato cha sita unashangilia anakwenda chuo. Mimi wangu hapo nitakua nashangilia ameingia kwenye mchakato wa ajira. Nimeshajivua jukumu akiwa bado na umri mdogo akiwa anaweza kuongea lugha kadhaa na akiwa ni fundi kamili. Akitaka sekondari akajisomeshe QT mwenyewe ila mimi nimeshampa elimu muhimu ya maisha.
Kuna mtu atasema mafundi wako wengi… Yes mafund ni wengi ila mafundi wazuri ni wachache. Bidhaa bora ziko chache sana sokoni.

Cha kuomba Mungu tu asiharibike na miadarati na pombe, asiwe mlevi, ama tapeli ama shoga maana dunia imearibika.

Ila wazazi tunatakiwa tuwachongee vijana njia sahihi mana wasomi wameshakuwa wengi. Hakikisha njia unayompitisha kijana ya ma form six na chuo bhasi uwe hata na connection ya ajira
 
Haupo peke yako na mimi nina hayo mawazo, niliweka nyuzi kadhaa humu ndani wazazi wasikomae na elimu tu, skills ni muhimu sana, kuna uzi niliweka wiki iliyopita daftari la hesabu za kinyozi anaingiza 30 hadi 70 daily. so ni lazima mzazi kumjenga mtoto awe na skills na zipo nyingi sana.

Lakini na huko vyuoni bado kuna vitu vingi sana ambavyo wanaweza kusomea na kujiajiri, Mfano wanasheria wapo waliofanikiwa kama kina Kibatala, Mainjinia wapo wengi sana wanapiga pesa ya kutosha kwenye mambo ya ujenzi na utengenezaji, wahasibu wapo waliosajiliwa wanaoajiriwa na makampuni kuandaa hesabu kwa mfumo wa TRA, madaktari wapo wenye zahanati zao, n.k. Elimu ni muhimu lakini hakikisha unachosomea kinaweza kukupa direction nzuri, sio kusoma sana bila direction
 
Kuna shule ya kutwa inaitwa Pugu station, Dsm ni majonzi kila mwaka. Watoto bangi na ngono kwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…