Operation Sangara: Chadema yajipanga Upya

CCM wameamua kufunika hiyo op Sangara kwa kuwatuma Tambwe na Akwilombe. Wamefanya mkutano eneo la bus stop mjini Musoma jioni hii. Katika hali ya kushangaza, katibu wa chama hicho mkoa amesema kesho kutakuwa na msako nyumba hadi nyumba kubaini watu wa Tarime warudishwe kwao. Hiyo ni baada ya zomea zomea. Huyu bwana haamini kuwa wakazi wa Musoma wanaweza kuzomea.
 
tatizo la Tanzania ni watu wa mjini.
Vijijini tumeamka tupo gado, na m/kiti ama balozi wa kitongoji akitufisadi huwa tunamkamata na na sungusungu kumchapa viboko na tunamkataa ktk kijiji.
Ikija swala la diwani/mbunge sisi huwa tunachagua mtu anayetufaa bila kuangalia itikadi zao na ndio maana ukiangalia kwa makini wabunge kutoka vijijini huwa mara nyingi wana alternate mara cuf,mara ccm ,mara chadema,mara udp hapo huwa tunatafuta wakutufaa.

Tatizo la Tanzania ni ninyi watu wa mjini hasa ngazi ya wilaya hadi Taifa Chunguzeni jinsi mnavyochaguwa wa bunge wenu na madiwani wenu mkiona mnafanya vizuri ktk uteuzi wenu ndipo njooni mtuelimishe sisi wa vijijini

Angalieni watu wa mjini mmeshindwa kufanya lolote kwa MAFISADI wenu wa mjini eti nalo mje mtuelimishe!!!! Hivi ninyi watu wa mjini ni nani aliyewaloga?

Maana haya mafisadi yangekuwa level yetu tungeyakamata tukayachapa viboko harafu tukayaamulu yatoweke ktk vijiji vyetu mara moja ,Ninyi watu wa mjini mmeshindwa kufanya lolote.

Na kwa kiwango ambacho mlivyo ma kondoo mnataka mje mtuelimishe ili iwe je? mkituelimisha?
sisi huku vijijini hatuna Polisi polisi wako mjini kwenu,huku hatuna mahakama mahakam yako mjini ,huku hatuna magereza magereza yako mjini kwenu.Sasa mnakuja kutuelimisha ili iweje?? maana haya mafisadi mnaishi nayo huko mjini.

Na kama tatizo ni CCM basi ninyi watu wa mjini ndio mnapaswa mtuombe sisi watu wa vijijini tuje tuwaelimishe AMa kwa vile mna uwezo wa kufikia media ndio mnaamua kutufanyia UFISADI sisi watu wa vijijini??

Kama kuichagua CCM nyie wasomi na wa mjini ndio vinara kwa hilo Angalia kama kinondoni na ILALA walishawahi chagua upinzani??

Angalia morogoro mpinzania wamemchagua lini? nenda dodoma mpinzani kachaguliwa lini haya ingia mwanza niambie ninyi watu wa mjini mpinzani katokea?
Haya kule Arusha na mbeya pia Iringa jamani wapinzani mmewachagua?

Angalia vijijini Biharamulo sio mjini wala hakuna high school ,Tarime napo sio mjini japo kuna chuo cha ualimu,Bariadi napo si mjini na hakuna hata high school na kwingineko naamini ukimtuoa NDESAMBULO wengine wote wapinzani watoka vijijini.
Sasa mnataka kuja kutuelimisha kwa lipi??

sisi Watanzania wa vijijini tumesha declare TATIZO letu LIMESABABISHWA na wasomi wetu kutusaliti,Limesababishwa na watu wa mjini waliokaribu na media na huduma mhimu KUTUSALITI.
Wasomi wetu vijana wetu tumewatuma gulioni kuhemea chochote huko mjini ili watachopata huko watuletee sisi wa vijijini tusio na shule tumegeane LAKINI badala yake wametugeuka na kutuharamia ,wasomi wamekatalia mjini na huko wanatumia kalamu zao tulizowapa sisi kutumaliza harafu wakitia dhihaka eti waje watuelimishe sisi tuliona umuhimu wa elimu na kuamuwa kuwatuma huko.

Watu wa mjini MIMI nafikiri hakuna haja ya kuja kutuelimisha sisi watu wa vijijini ila mnachotakiwa kuanza nacho anzeni huko huko mjini kwenu na kwa wasomi wenu kuhubiri PATRIOTISM NA SOLIDARITY .HILO NDILO TATIZO KTK NCHI YETU na mizizi yake mibovu imeanzia mijini na kwa wasomi.


Kwanza MkamaP pole sana na kipigo cha Tarime .Maana ulitoa matamko makali sana hapa nikaogopa mno lakini ukweli umeisha jinsi wengi tulivyo tarajia kwamba Tarime si kama watu wa Wilaya ya Musoma Mjini ambao walikuwa nyumbu 36 wa Mathayo then wakapiga kura .

OP Sangara inaendelea .

Kwa mfano Musoma wananchi walisema juu ya ugumu wa maisha na kwamba Mathayo anawaumiza kwa kununua nyama yote .Sijui habari hii ina ukweli gani lakini niliifuatilia bado naifuatilia .

Chadema wame enda kila Jimbo la Uchaguzo hapa Musoma na wanaenda kila Kata na kulala huko huko .Wanaongelea matatizo ya kawaida ya wananchi ya kila siku .Kuanzia Mjumbe wa nyumba kumi na pesa za shule kuliwa na wajanja wa CCM .Ndilo wanalo fanya na naamini watafanikiwa kwa njia hii .

Chiligati na CCM sasa wamelipuka nadhani hawakujua kwamba wananchi wamechoka .
 
Lunyungu,

Hilo la nyama Matahayo kalitolea ufafanuzi jioni hii. Anasema yeye hununua ng'ombe ambao huwa wanapelekwa kuuzwa Kenya na kuwatunza kwa miezi mitatu. Baada ya hapo huwa wamenona na hivyo kuchinjwa na nyama kuuzwa DRC. Kwa maneno yake, alipanga wananchi wa Musoma waweze kupata utumbo kwa bei nafuu lakini zoezi hilo likahujumiwa na wenye mabucha.
 
Lunyungu,

Hilo la nyama Matahayo kalitolea ufafanuzi jioni hii. Anasema yeye hununua ng'ombe ambao huwa wanapelekwa kuuzwa Kenya na kuwatunza kwa miezi mitatu. Baada ya hapo huwa wamenona na hivyo kuchinjwa na nyama kuuzwa DRC. Kwa maneno yake, alipanga wananchi wa Musoma waweze kupata utumbo kwa bei nafuu lakini zoezi hilo likahujumiwa na wenye mabucha.

Ni yale yale ya Sangara wa Mwanza. Yaani nyama nono ipelekwe DRC ndugu zetu wabaki kula utumbo tu. Ndio maana wakazi wengi wa Musoma wamekondeana.
 
Watu wametoa maoni mazuri sana kuhusu hii hoja. Wapo waliosema kuwa ingependeza sana kama hii operesheni ingefanywa na Watanzania wote bila kujali itikadi au vyama vyao. Nakubaliana nao kwa kiasi kikubwa tu!

Hata hivyo, hilo ndilo limekuwa tatizo letu kama jamii ya Watz. Kuendelea kusubiri na kutothubutu kufanya kitu eti tunasubiri watu wengine waamke. Tutasubiri hadi lini?

Dhambi kubwa ya binadamu ni kutofikiri na/au kutothubutu kufanya jambo hasa pale anapoamini kwamba hilo jambo ni la muhimu sana kwa mstakabali wake, jamii na kizazi chake chote (not daring and inactivity are our grave sins).

CHADEMA washa moto tu. Waliokwishaamka watakuwepo na watakaoamka baadaye watapanda gari likiwa kwenye mwendo. Katu hatuhitaji kusubiri kitu wala mtu. Dakika inayopotezwa sasa itatugharimu miaka zaidi ya 5 kama ambavyo makosa yetu ya 1995 yalivyotugharimu kiasi kikubwa. Na sasa tumeona upenyo inabidi iwe mwendo mdundo hadi kieleweke. Hakuna kulala, mapambano yanaendelea. Ole wao wote wanaoendelea kusita sita na kukumbatia mafisadi na wasanii!
 
CCM wameamua kufunika hiyo op Sangara kwa kuwatuma Tambwe na Akwilombe. Wamefanya mkutano eneo la bus stop mjini Musoma jioni hii. Katika hali ya kushangaza, katibu wa chama hicho mkoa amesema kesho kutakuwa na msako nyumba hadi nyumba kubaini watu wa Tarime warudishwe kwao. Hiyo ni baada ya zomea zomea. Huyu bwana haamini kuwa wakazi wa Musoma wanaweza kuzomea.

wanaendelea kuvunja katiba kila kona, watazidi kuvuka kila mstari gues what wanna happen...
 
wanaendelea kuvunja katiba kila kona, watazidi kuvuka kila mstari gues what wanna happen...

Wanazidisha urefu wa kaburi lao!! Wameshajichimbia ila hawaamini kama urefu wake unatosha. Let them continue to dig dipper...!
 
CHADEMA juu kwa Warioba

[Source Tanzania Daima]


na Kulwa Karedia, Bunda

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeshusha mauaji makubwa katika Kijiji cha Ikizu alikozaliwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, baada ya kuchukua wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); kimechukuliwa kijiji kizima!
Tukio hilo lilitokea jana nyumbani kwao Jaji Warioba katika mkutano wa hadhara maarufu kama ‘Operesheni Sangara' uliohutubiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.

Zitto aliwaambia wananchi hao kuwa wametumia fursa yao ya kidemokrasia kuchagua chama wanachokipenda na ni funzo kwa CCM kutokana na kupoteza mwelekeo mzima wa kuongoza taifa.

"Tunapenda kuwakaribisha wote mliojiunga CHADEMA kwa moyo mkunjufu; tunasema karibuni… Mmetumia nafasi yenu ya kidemokrasia kujiunga na sisi. Hii inaonyesha wazi kwamba mmechoka na sera za CCM; chama kilichopoteza mwelekeo wa serikali," alisema Zitto.

Zitto aliwakabidhi kadi mpya wanachama hao na kuwataka kuwa mabalozi wa Watanzania wengine katika ukombozi wa awamu ya pili inayoendeshwa na CHADEMA.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Bunda katika uwanja wa Stendi ya Zamani, aliwataka wakazi wa mji huo kufanya mabadiliko ya dhati, ili kulikomboa taifa.

"Ndugu zangu wana Bunda, CHADEMA imeanzisha vuguvugu la ukombozi wa awamu ya pili katika taifa letu… hii yote imetokana na CCM kulipeleka bapaya taifa letu. Naamini kwamba mko tayari kutupokea katika Operesheni Sangara, ili kujenga taifa jipya," alisema Mbowe.

Alisema wananchi wa Bunda walipewa ahadi nyingi na mbunge wa jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wassira, kwamba angewapelekea maji, mbolea ya ruzuku na sasa ahadi hizo zimegeuka kuwa kitendawili.

"Huyu Wassira aliwadanganya mara nyingi kwamba atawaletea maji, mbolea ya ruzuku; lakini imegeuka kuwa ndoto kwenu, sasa umefika wakati wa kumuondoa … ili tufanye mabadiliko ya kweli ya kuwakomboa," alisema Mbowe.

Alisema pamoja na mambo mengine aliwaahidi wakulima wa zao la pamba kuwapatia dawa za kuulia wadudu, lakini ahadi hiyo nayo imeota mbawa na kuwaacha wananchi wakitaabika.

Alisema wananchi wengi wanaoishi kandokando mwa Ziwa Victoria wamebaki maskini wa kutupwa kutokana na kufungiwa kuvua samaki na kuambulia kula mabaki maarufu kama ‘mapanki'.

Baada ya mkutano huo, katika tukio la kushangaza mke na mume, Christopher Matata na Mary Charles walirudisha kadi za CCM kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mwelekeo.

Naye Katibu Mkuu wa chadema, Dk. Willboard Slaa, alisema hawatakubali kubaki kimya licha ya kupata chokochoko kutoka CCM kwamba wanaendesha siasa za kihuni.

"Napenda kuwahakikishia kwamba ile kazi tuliyoamua ya kupambana na mafisadi tutaendelea nayo mpaka siku ya mwisho… hizi kelele za CCM hazitunyimi usingizi hata siku moja," alisema Dk. Slaa.

Mikutano ya Operesheni Sangara ilizunduliwa katika Mji wa Musoma mjini imesitishwa kwa wiki moja, ili viongozi wa CHADEMA kumsindikiza Mbunge mteule wa Jimbo la Tarime, Charles Mwera, kwenda bungeni kuapishwa.

Mpaka sasa operesheni hiyo imeshazunguka katika Wilaya ya Tarime, Rorya, Serengeti na Bunda; huku Wilaya ya Musoma Vijijini ikibaki kutokana shughuli ya kuapishwa kwa Mwera.

Operesheni Sangara itaendelea tena wiki ijayo ambapo itaihusisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Shinyanga, Tabora na Kigoma.
 
Marekebisho madogo?
Kuweka viraka juu ya kiraka ni marekebisho madogo.

Mtu mwongo siku zote huanza kujidanganya mwenyewe kwanza.

CCM inahitaji ile kitu inaitwa Overhauling.
Unafungua nuts na bolts zote kila kitu kinakuwa nje nje.
Sasa usidhani kwamba ni suala la kuosha na kufunga tena uchafu uleule.
Ni Frame/Block au skeleton tu inayo bakia sehemu zilizo bakia zote jalalani au kwenye tanuru la 1500C vikasafike kwa ndimi za mioto, patamu hapo.

Acha kujidanganya, zaidi acha kudanganya watu wengine.

Kama nimedanganya, shuhudia kudanganya kwangu; lakini kama nimesema kweli wanikejeli ya nini?

Bado CCM ni nambari wani.
 
Kama nimedanganya, shuhudia kudanganya kwangu; lakini kama nimesema kweli wanikejeli ya nini?

Bado CCM ni nambari wani.

Hivi wewe ni mchungaji wa mbuzi ama binadamu?
Maana unaanza kutuchanganya hapa...Jadili hoja na kuhusu ccm kuwa namba wani kwani ni nani ambaye hajawahi kuitumikia ccm maishani mwake?
ccm belongs to wananchi na wananchi hawaitaki tena na hivyo wataimalizia mbali...Chama mbadala na mawazo mbadala ndivyo tunahitaji.
 
Hivi wewe ni mchungaji wa mbuzi ama binadamu?
Maana unaanza kutuchanganya hapa...Jadili hoja na kuhusu ccm kuwa namba wani kwani ni nani ambaye hajawahi kuitumikia ccm maishani mwake?
ccm belongs to wananchi na wananchi hawaitaki tena na hivyo wataimalizia mbali...Chama mbadala na mawazo mbadala ndivyo tunahitaji.

Ni wewe umesema.
 
Sijasema kama wewe ni mchungaji wa mbuzi...Niliuliza kama ni wa binadamu.
 
Sijasema kama wewe ni mchungaji wa mbuzi...Niliuliza kama ni wa binadamu.

Ni hawa hawa wachungaji wa binadamu waliotuingiza mkenge kwamba JK ni chaguo la Mungu. Ona sasa wanaumbuka na wengine wanataka hata kuandamana maana waligundua alikuwa mhuni tu kwa kutowambia baadhi ya sera zake ambazo wamekuja zijua baadaye! ole wenu sisiemu!
 
Tatizo la ndugu zangu wa CHADEMA ni kushindwa kuwa na mipango endelevu. Watafanya recruitment ya nguvu halafu wakimaliza hakuna ufuatiliaji ama uhusishaji wa wanachama hao kuweza kutumia hiyo rasilimali watu. Hivi mmeshafanya zoezi la kutambua wanachama hai, wafu na wale wachukua kadi halafu wanapamba kabatini...

Tanzanianjema
 
Ni hawa hawa wachungaji wa binadamu waliotuingiza mkenge kwamba JK ni chaguo la Mungu. Ona sasa wanaumbuka na wengine wanataka hata kuandamana maana waligundua alikuwa mhuni tu kwa kutowambia baadhi ya sera zake ambazo wamekuja zijua baadaye! ole wenu sisiemu!

Mpendwa,
Mh. J.M. Kikwete bado ni chaguo la Mungu (Warumi 12:1-3)
 
Back
Top Bottom