Operation Sangara: Chadema yajipanga Upya

Kuzuia mikutano ya Chadema ni njia moja wapo ya kukifanya chama hicho kipendwe zaidi na wananchi wa Mbeya vijijini kwasababu, kitendo cha kuwazuia kitawapa shauku ya kutaka kujua kitugani ambacho CCm na serikali yake vinaogopa wananchi wasiambiwe na Chadema; wanarudia makosa yale yale ya Makamba kutaka kutumia uCCM wake kuzima mjadala wa EPA!! Mbinu za kuzuia mikutano ya Chadema zilishindwa Tarime na Mbeya pia zitashindwa hasa ukijua kuwa wanaMbeya wanausongo na serikali hii; sasa karibu mwezi mzima hawana umeme!!
 
Mbona walizimdua acheni uzushi mbona walizindua mpwa wangu amehudhuria na kanieleza in detail yaliyohutubiwa
 
Mbona walizimdua acheni uzushi mbona walizindua mpwa wangu amehudhuria na kanieleza in detail yaliyohutubiwa

Unabishana na gazeti ? Unapinga barua ya polisi ? Unawa tuhumu waandishi kwamba wana wasingizia polisi ama una maana gani .Wewe ndiye uache zako maama wenzako tuko Tanzania wewe unangoja hadi mpwa wako akueleze wakati hana hata habari ya kinacho endelea anakufukuza shilingi saa ngapi atajua ya mkutano huu ?
 
Date::12/13/2008

Tayari operesheni hiyo imeshafanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa baada ya kupata kibali cha Jeshi la Polisi, lakini chombo hicho cha dola wilayani Mbeya kimedai badi hakijaelewa dhana hiyo ya Operesheni Sangara, ikiwa ni siku chache baada ya katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kukiri kuwa mkakati huo wa Chadema ni sumu.

Barua iliyoandikwa na Jeshi la Polisi wilayani Mbeya yenye kumbukumbu namba MB/A.24/30.B/232 na iliyosainiwa na mkuu wa polisi wa wilaya, SP Msuya, inamuelekeza katibu wa chama hicho cha upinzani wilayani hapa asifanye mkutano huo kutokana na kutoelewa maana ya neno la "Oparasheni Sangara".

Tuna jeshi moja tu la Polisi, IGP mmoja. Inakuwaje jeshi hilo chini ya IGP mmoja kutoa kibali cha Operesheni Sangara kwa mikoa ya kanda ya ziwa halafu jeshi hilo hilo liseme halijui maana ya Operesheni hiyo kwa mikoa mingine particularly Mbeya. Huu nao ni ufisadi mtupu, wanafanya hivyo baada ya Makamba kushtuka huku wakikabiliwa na Uchaguzi mdogo wa bunge.
Chadema wakiona wanazidi kuwekewa ngumu na huyo Kamanda wa Polisi basi nawashauri Chadema wabadilishe jina la Operesheni hiyo kwa Mkoa huo lakini lengo likiwa ni lile lile (Operesheni Sangara)
 
Lakini hilo Jina OPeresheni Sangara lina maana nzuri sana ukililiangalia kwa jicho la tofauti, Sangara aweza kuwa 'CCM' ambaye ni samaki mkubwa (chama kikubwa) ambacho kama sangara wafanyavyo kazi yake imekuwa ni kumeza samaki wengine ( kutufisadi na kuua vyama pinzani) kwahiyo huyu sangara akiondolewa katika ziwa letu Tanzania, samaki wengine wadogo wataweza kukua vyema just thinking...

CHADEMA SONGENI MBELE HUYU SANGARA AONDOLEWE ILI NASI VISAMAKI VIDOGO VIDOGO TUWEZE OGELEA KWA AMANI NA KUFAIDI VIRUTUBISHO VYETU ALIVYO TUJALIA MAULANA!
 
KIKAO cha Baraza la Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza (UVCCM) kimeilaani mikutano ya hadhara ya Chadema iliyopewa jina la Operesheni Sangara na kudai kuwa ilikuwa ikiwadhalilisha wananchi.


Akizungumza jana mbele ya kamanda wao wa vijana mkoa wa Mwanza Balozi Gertrude Mongella, mwenyekiti wa UVCCM mkoa Cornel Magembe alisema Chadema inapaswa kuwaomba radhi wananchi kwa kuwafananisha na samaki aina ya sangara ambao wamekuwa wakivuliwa katika mikutano yao hiyo walioamua kuipa jina la operesheni sangara.


Magembe alisema jina operesheni sangara limetumika kwa lengo na nia ya kuwadhalilisha wananchi kwa vile lengo lao operesheni hiyo ilikuwa ni kuvuna wanachama wengi basi wananchi wamegeuzwa samaki ambao wamekuwa wakitupiwa chambo na ndoano na kisha kuvuliwa jambo ambalo alidai kuwa ni udhalilishaji.


"Sisi kama vijana wa CCM tunalani wananchi kuitwa Sangara, wamefananishwa na samaki ambaye hunaswa kwa ndoano baada ya kulishwa chambo, huwezi kuwadharau wapiga kura wako na kuwaita sangara jambo hili tunalilaani," alieleza mwenyekiti huyo wa vijana.


Alisema kwa kutumia neno hilo Chadema inamaanisha kuwa wanachama wote wapya waliojiunga na chama hicho katika harakati hizo za operesheni sangara wao ni sawa na samaki kwa vile wamevuliwa kwa kupewa chambo na kisha kunaswa na ndoano.


"Tunaamini kuwa chadema wangeweza kutumia majina mengine yenye busara zaidi lakini walilitumia neon hilo kwa makusudi zaidi wakiwa na maana thabiti ambapo ukitafakari zaidi utabaini kuwa maana yao kubwa katika kuimarisha chama ilikuwa ni kuvuna wananchama jambo ambalo tunalitafsiri kama ililenga kuwadhalilisha wananchi," alieleza.


Akizungumza na viongozi wapya wa UVCCM walioteuliwa katika uchaguzi mpya wa chama mwaka huu, kamanda wa vijana ambaye pia ni rais wa bunge la Afirika Balozi Gerturde Mongella aliwapongeza vijana kwa kutoa tamkio hilo la kulaani wananchi kudharirishwa na kuitwa sangara.


Mongella alisema kuwa wao kama wanasiasa wanakubaliana na siasa za hoja na wala siyo siasa za kudhalilisha wananchi na kuwaita sangara.


"Nawaunga mkono vijana kwa kulaani wananchi kuitwa sangara, wamedhalilishwa, kusema hivyo hatumaanishi kupinga vyama vingi laa tunamaanisha tunapingana na majina ya kudhalilishana, CCM haikatai kukosolewa na vyama vya upinzani lakini upinzani pia uanapaswa kukubali pale unapokosea na kuokiri hadharani,"alieleza Mongella na kusisitiza operesheni sangara imekosea njia katika siasa kutokana na kuwa na tafsiri ya kudhalilisha.


Hata hivyo mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mwanza Boniface Lyimo ilisema Operesheni Sangara haina maana ya kuvua wananchi bali vita dhidi ya mafisadi na ilikuwa na lengo la kupita kuwahamasisha wananchi kupambana na mafisadi wakubwa ambao walifananishwa na sangara.


"Oparesheni sangara ni mkakati ambao chama chetu kimeubuni kwa lengo la kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa mafisadi wakubwa tuliowafananisha na sangara, ilizinduliwa katika siku ya kuadhimisha tarehe ya kutangazwa kwa orodha ya mafisadi wanaoitafuna nchi na ambao baadhi yao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi wa fedha za umma. Haina maana ya kuwadharilisha wananchi," alieleza na kufafanua kuwa tayari operesheni hiyo imeshafanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuhamia mkoani Mbeya katika kampeni za uchaguzi mdogo wa huko.


Alisema kuwa kwa ufafanuzi Operesheni Sangara ni ziara maalum za kujenga Chadema, kuhamasisha uwajibikaji wa viongozi na kutetea rasilimali za taifa na kwamba neno Sangara ni jina la samaki ambalo linawasilisha azma ya chama kuweka mkazo wa kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania.


"Opareshen Sangara inakwenda sambamba na kuhamasisha wananchi kujiunga na Chadema na inasimamiwa na uongozi wa taifa na ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Chadema wa mwaka 2006 mpaka 2010 wa kueneza chama na sera zake kwa umma na kuhamsisha mabadiliko kwa lengo kuweka tumaini jipya la demokrasia ya maendeleo, kufanya hivi siyo kudhalilisha wananchi nadhani wanapungukiwa uelewa," alieleza.

Source:Mwananchi
 
Kawaida ya CCM kuspin maneno kwa lengo la kufanikisha azma zao kisiasa. Kwa hiyo sio jambo la ajabu kwa viongozi wa ccm kutoa kauli kama hizi.
 
Hi Mongella kesha maliza lile soo la wizi na matumizi mabaya ya ofisi ya Bunge kule mahali kabla hajawa kamanda ? Huko CCM kuna vituko .Yule mama ndiye Kamanda wa vijana ? Ina vijana huko hakuna ?Spin si lolote wao wajenge hoja na si kujifanya kuwatetea wananchi kwa maneno yale huku wanawatesa na kuwaibia kia kukicha .
 
Siajelewa kwa nini kichwa cha thread na habari yenyewe kama vimeoana vizuri.
 
Makame: Operesheni Sangara 'ruksa'
Jackson Odoyo
MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame amekiruhusu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuendelea na mikutano yake ya kampeni zake za Operesheni Sangara mkoani Mbeya ili zisiathiri harakati za uchaguzi wa ubunge unaoendelea katika mkoa huo.

Chadema haishiriki kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge cha Mbeya Vijijini baada ya mgombea wake, Sambwee Shitambala kuenguliwa na tume ya uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyogundulika kwenye kiapo chake.

Hata hivyo, chama hicho kilisema kuwa kitaendelea na mikutano ya Operesheni Sangara, ambayo lengo lake limekuwa likielezewa na chama hicho kuwa ni kufagia ufisadi na kurejesha maadili ya taifa ambayo yamepotezwa na baadhi ya watu wenye ubinafsi.

Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame alisema operesheni Sangara haihusiani kabisa na uchaguzi kwa sababu chama hicho hakina mgombea katika uchaguzi huo.

“Mikutano ya Chadema haiwezi kuathiri hali ya kampeni za uchaguzi kwa sababu Chadema haina mgombea na sheria za uchaguzi hazizungumzii chama ambacho hakihusiki katika uchaguzi, hivyo wao wako huru kuendelea na ratiba yao kama walivyoipanga,” alisema Jaji Makame.

“Moja ya kanuni za tume ya uchaguzi ni kusimamia vyama vinavyoshiriki katika kampeni hadi siku ya uchaguzi na moja ya mambo tunayoyatazama wakati huo, ni mahusiano baina ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi. Endapo msuguano kati ya vyama hivyo utajitokeza, tume ya uchaguzi inaweza kuviita kwa ajili ya usuluhishi.”

Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo siku moja baada ya katibu mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa kusema kuwa wataendelea na ratiba yao ya Operesheni Sangara kwa sababu walishaanza harakati hizo mapema hata kabla ya uchaguzi huo kuwepo.

Hata hivyo, kauli ya Dk Slaa ilionekana kuongeza wasiwasi kwa baadhi ya wanachama kwamba, mikutano yao ya kampeni ingekosa baraka za tume wakati huu ambao vyama vinavyoshiriki vinaendelea na kampeni za kunadi wagombea wao.

Kuhusu suala la vurugu kutokea wakati wa kampeni hizo ama kuwepo kwa malalamiko kuhusu kampeni za Operesheni Sangara, Jaji Makame alisema sheria na kanuni za tume yake haziwezi kutumika katika vurugu baina ya vyama visivyo shiriki katika uchaguzi na vile vinavyoshiriki bali watakaohusika katika vurugu hizo hushughulikiwa na Jeshi la Polisi.

“Sisi tunasimamia kampeni za uchaguzi, hatusimamii vurugu wala kampeni za Operesheni Sangara. Hiyo ni kazi ya polisi; ndio wenye jukumu la kuhakikisha kwamba, vurugu hizo hazitokei na endapo zitatokea wataamua sheria ichukue mkondo wake au la,” aliongeza mwenyekiti huyo.

Alifafanua kuwa kutokana na maandalizi mazuri waliyofanya katika uchaguzi huo wa Mbeya Vijijini, ana hakika shughuli za kampeni zitafanyika vizuri na hatimaye uchaguzi utafanyika katika tarehe iliyopangwa.

Hata hivyo, Jaji Makame alipoulizwa kwamba maamuzi ya tume yake kuiondoa Chadema katika uchaguzi huo yanafanana na maamuzi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya, Samuel Kivuitu aling’aka na kusema:

“Sitaki uniulize maswali ya kipuuzi na wala sitaki unifananishe na Kivuitu kwa sababu Kivuitu ni wa Kenya na mimi ni Jaji Makame wa Tanzania na Tanzania si Kenya, hivyo naomba usitishe maswali ya aina hiyo.

“Nina kuomba uniulize maswali yanayohusiana na uchaguzi wa Mbeya na si vinginevyo ama ulitaka tuipendelee Chadema ndipo ujue tumetenda haki."

Source: Mwananchi Read News
 
yawezakana KANDA YA ZIWA ni NCHI NYINGINE na MBEYA ni NCHI NYINGINE ndio maana Jeshi la POLICE MBEYA waka kataa huwezi jua wanatumia ramani ya wapi labda ZAMBIA au MALAWI na Kanda ya Ziwa wana tumia ya Tanzania? Hatuwzi jua SP Msuya anatoka pande ipi asie soma magazeti wala kuangalia Televishni za Tanzania, au ndugu zangu wa Mbya tuambieni wnzetu huko huwa mnapata chanel zipi za TV yawzkana za Tanzania hazifiki ndio maana SP Msuya ame wakatalia Chadma wasifanye mkutano.

2. Yawezekana hiyo ikawa janja ya CCM kukwepa waziwazi ushindani wa demokrasia maana hakuna asiyejua kuwa CHADEMA inaogopeka katika nyanja za za siasa kweny vyama vyote vya siasa, CHADEMA inaupinzani wa hali ya juu. Mtajasikia baada ya uchaguzi kufanyika wakaruhusia kufanya mkutano wao.
 
Waislam nchini wapinga oparesheni Sangara
Geofrey Nyang'oro na Zaina Malongo

WAUMINI wa dini ya kiislam wamepinga oparesheni sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuws chama hicho na operesheni hiyo, haina manufaa kwa uisalam kwa kuwa imejaa ukabila, ubinafisi na udini


Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kongamano la kiisilamu, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam, walisema oparasheni Sangara imekuwa ikimchafua rais Jakaya Kikwete bila sababu licha ya mambo mengi mazuri, aliyoyafanya kwa taifa.


Shekhe Saidi Mwaipopo aliwataka waisalamu kutambua kuwa chama hicho, hakina msaada wowote wa maendeleo ya uislamu kutokana na chama hicho kujaa ukabila udini na ubinafisi.


"Napenda waislamu muelewe kuwa chama cha Chadema hakina msaada wowote juu ya uislamu na kimekumbatia udini, ukabila na ubinafisi kutokana na sababu hiyo, tutatembea nchi nzima kuwaeleza wanachi ukweli wa jambo hili na kuwataka wasikiunge mkono chama hicho,"alisema Mwaipopo.


Akizungumzia Oparasheni Sangara, alifafanua imekuwa ikichafua rais Kikwete bila ya sababu za msingi kwa kuwa rais huyo tangu ameingia madarakani amesababisha mafisadi kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.


Pia alisema kipindi hiki cha Rais Kikwete kumekuwa na uhuru mkubwa wa kuabudu kutokana na serikali yake kuruhusu mihadhara ya kidini ambayo, ilikuwa ikizuiliwa na serikali ya awamu ya tatu.


Mwaipopo alisema kama oparesheni Sangara ingekuwa ni ya kweli basi ingekuwa tayari kutaja baadhi ya sifa ambazo Rais Kikwete amekuwa akizifanya badala ya kumchafulia jina lake kila inaopoendesha mikutano yake.


Alisema kutokana na ubinafisi wa chama hicho, kimeshindwa kuviunga mkono vyama vya upinzania vya Chama cha Wananchi (CUF) na Sauti ya Umma (SAU) vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya vijijini ambao unaotarajia kufanyika mwezi huu.


Katika hatua nyingine, Mwaipopo aliwataka viongozi wa dini za kiislamu Mashekhe na Maimamu kuingia kwenye siasa kuanzia nafasi za serikali za mitaa hadi ubunge ili kwenda kuwatetea wananchi.


Alisema kama viongozi hao wa dini hawatajitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi mambo yao, mengi yataendelea kukwama kutokana na kukosekana kwa watetezi kwenye vyombo vya maamuzi kama ilivyokuwa kwenye mahakama ya kadhi.


Akisoma tamko la waislamu hao, kuhusu OIC na Mahakama ya Kadhi katibu wa Baraza la habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita) Shekhe, Sadick Godigodi alisema wamekubaliana kwa kauli moja kusubiri kauli itakayopotolewa na serikali.


Kutokana na hatua hiyo, waislamu hao wamesimamisha maandamano waliyokuwa wamepanga kufanyika mapema mwezi huu kwa lengo la kuishinikiza serikali kutoa tamko lake kuhusiana na Mahakama ya Kadhi na OIC na walisema kuwa watatoa kauli yao baada ya serikali kutoa tamko.


Mwananchi Read News
 
Last edited by a moderator:
He! Yameshakuwa haya. Yaani kuikosoa serikali kwa uzembeaji wake na ufisadi kumeshageuzwa kuwa mashambulizi dhidi ya rais ambaye ni Muislamu?
 
Why CHADEMA only?Waislamu hao wametumwa? na nani? or say is like this
Waislam+Chadema+JK+OIC+Mahakama ya Kadhi=???? au ndio wale walioonyeshwa na ITV wakigawana pesa?
 
Kama kuna roho mbaya inayotaka kuichafua na kuigawa TANZANIA ni siasa za udini. Na kwa hali niionavyo mimi naona siasa zetu zimeanza kuluekezwa sana kwenye mitazamo ya kidini badala ya kuziacha zenyewe zijiendeshe. Hii ni sumu kali na mbaya sana kwa jamii yetu. Leo viongozi wa dini kubwa kama Uislamu kuanza kuisema CHADEMA si dalili njema!

Ila kitu kimoja naamini hawa wametumwa na nia yao si nzuri kwa TAIFA letu. Na huu mkakati wao kwamba viongozi wa dini wagombee nyadhifa mbalimbali za kisiasa sidhani kama kuna mtu aliwakataza/alikatazwa/amekatazwa. Kama misikiti imewachosha na wanaona kuingia kwenye siasa ndo njia ya kupitisha agenda zao za siri, basi nia yao si njema kwa Taifa letu na ni watu wa kutopewa hata ujumbe wa nyumba kumi!!.

Ndugu zangu waislamu tuwe makini na sumu hii tunayotaka kunyweshwa na hawa viongozi uchwara wanaojiita wa kiislamu, wababaishaji na haiyumkini wana harufu ya ufisadi ndani yao!
 
Hongereni sana waislamu kwa mambo mawili. Kwanza kwa kuonyesha kuwa operesheni sangara imeshaanza kuzaa malengo yaliyotarajiwa-imewagusa watu na wamenaza kutoa mwitikio hata kama mwitikio wenyewe ni wa aina hii.
Pili kwa kuipandisha chati Chadema kwa sababu pamoja na kuwa critic zenu hazina miguu ya kusimamia, lakini inaonyesha kuwa mmeshajua Chadema ni nini.
 
Hongereni sana waislamu kwa mambo mawili. Kwanza kwa kuonyesha kuwa operesheni sangara imeshaanza kuzaa malengo yaliyotarajiwa-imewagusa watu na wamenaza kutoa mwitikio hata kama mwitikio wenyewe ni wa aina hii.
Pili kwa kuipandisha chati Chadema kwa sababu pamoja na kuwa critic zenu hazina miguu ya kusimamia, lakini inaonyesha kuwa mmeshajua Chadema ni nini.

CUF at work , baada ya yale ya Mbeya sasa wamehamia kwenye makongamano.Hapa tuna amini kwamba Chadema ni wapinzani wa kweli na CUF wamekuwa wakitumika .Ushahidi tosha kabisa .Watanzania si wajinga na wataendelea na kuunga mkono Chadema.Hivi hili Mzee Jasusi Kongamano lilikuwa kwa ajili ya Chadema pekee ama maendeleo ya Waislam na maslahi katika vyama vya siasa ? Nimeshindwa kuelewa ama kwa vile sijasoma habari nzima maana nimepata kicgefu chefu kabla sijaenda mbali ?
 
Hii ipo sana TZ, na tutaendelea kuyaona. Kuna viongozi wa Dini waliowahi kusema kuwa JK ni chaguo la Mungu, na hio ilikuwa inamaanisha walikuwa wanaiunga mkono CCM na walio CCM.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom