Operation Sangara: Chadema yajipanga Upya

Hii ya Helikopta nadhani CHADEMA walishaelezea fedha za matumizi yake.
Mimi nilikuwa nazungumzia Operesheni Sangara. Unakumbuka hata enzi za Mwalimu Nyerere alipokuwa anapigania uhuru alitegemea michango na misaada ya raia. Hakulala hotelini alipokuwa anatembelea Watanganyika. Viongozi wa CHADEMA naona wameamua kuiga ukurasa huo.

Mkuu Jasusi,
Kumbuka kuwa Mwalimu Nyerere hadi Mungu alipomuita mbele ya haki alikuwa mwana CCM. Hivyo kumwiga Nyerere ni sawa na kuiiga CCM.
Ila karibuni mjifunze.
 
Mkuu Jasusi,
Kumbuka kuwa Mwalimu Nyerere hadi Mungu alipomuita mbele ya haki alikuwa mwana CCM. Hivyo kumwiga Nyerere ni sawa na kuiiga CCM.
Ila karibuni mjifunze.
LM,'
Ni Mwalimu huyo huyo aliyesema kuwa CCM si mama yake. Laiti viongozi wenu wa sasa wangejitahidi kumwiga Mwalimu angalau katika maadili, CCM kisingekuwa chama kichafu kama kilivyo hivi sasa. Lakini wamemtupa na zimebaki ngonjera tu za kumuwezi ( kwa maneno)
 
Jasusi,
Mie sikumbuki kama Mwalimu aliwahi kusema hili neno; Bali aliyewahi kulisema ni Mrema (Augustino Lyatonga).
 
Oparesheni CHENGU na VIMOLO itakuwa lini? mimi naona waiite oparesheni GOGOGO.
 
Dr. Slaa anaelekea kwenye siasa za Mtikila za kulipua mabomu hata pale pasipo na hayo mabomu.

Ushahidi alio nao ni wa aina gani, kideo, audio record, barua au ni wa aina gani? Natumaini hatasema kuwa mke wake ndiye aliyemtonya.

hata mimi ninao inaonekana wazi kabisa mbonaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
naamini kabisa humo humo CCM kunawanaoiungamkono chadema wanawape ufadhili wa pesa na habari vile vile... ukiachia wananchiwengine wa kawaida na hela zao wenye kiutakia mema tz

Hilo ni kweli, ni juzi tu mweyewe baada ya kutangazwa mpango huo nilikuwa kijiwe fulani cha wauza magazeti, bongo dar, vijana wengi wakijiweni wakawa wanashangilia na kuuliza hivi wapi hiyo michango inapelekwa wakazidi tania kwamba japo alfu wangetoa!.
Kwa hali hiyo ni wazi kwamba watu wamechoka na ufisadi na wako tayari kujitolea kwa mbadala hata kwa hali na mali!

swali je, ni wapi michango hiyo inapelekwa?
 
Hilo ni kweli, ni juzi tu mweyewe baada ya kutangazwa mpango huo nilikuwa kijiwe fulani cha wauza magazeti, bongo dar, vijana wengi wakijiweni wakawa wanashangilia na kuuliza hivi wapi hiyo michango inapelekwa wakazidi tania kwamba japo alfu wangetoa!.
Kwa hali hiyo ni wazi kwamba watu wamechoka na ufisadi na wako tayari kujitolea kwa mbadala hata kwa hali na mali!

swali je, ni wapi michano hiyo inapelekwa?

Na CAHDEMA wakamtie hapa hapa, kama wakiwa na plan, strategy na wapresent vizuri.. watafika mabli sana... imebakia hatua kidogo tuu wawavune watz wote... TUSIKATE TAMAA....
 
Mtumishi wa Mungu. Mwisho wa sisiemu upo hapa na Mungu yuko kazini. Siku si nyingi utajua kwa nini!

Mpendwa Unayechukia Mafisadi.
Unamaanisha mwisho wa CCM kuwa ndio 'mwisho wa Dunia' au?
Ninachojua ni kuwa siku moja chama kingine cha siasa kitatawala Tanzania, lakini hautakuwa mwisho wa CCM.
Hata NARK iliposhinda Kenya haikuwa mwisho wa KANU, maana bado ipo na siku moja itaibuka na kutawala tena nchi.
Hata Zambia aliposhindwa Mzee Kaunda haukuwa mwisho wa chama alichokuwa anakiongoza, lakini ukiangalia kwa sasa Bw. Rupia Banda ambaye ni Rais wa muda pia Rais mtarajiwa wa Zambia yeye ni 'kijana' wa mzee Kaunda.

Ninachoamini ni kuwa CCM bado ni chama kilicho na sera thabiti za kuiongoza nchi na chenye mvuto kuliko vyote hapa Tanzania, yanahitajika marekebisho madogo tu kukifanya kiendelee kuwa nambari wani.

Asante kwa changamoto.
 
Mtumishi wa Mungu ni kweli inawezekana kabisa ulikuwa bado mdogo wakati anayasema maneno haya. Usingeweza kuelewa mambo ya mwalimu:(

Mpendwa Mchukia Mafisadi,
Ninavyojua ni kuwa hotuba zote za Mwalimu Nyerere (RIP) zimerekodiwa.
Ningefurahi kama ungeniambia nitapata hii hotuba wapi katika mfumo wa video au audio.
Asante.
 
safi , ni kweli ukienda igurubi wilayani igunga ukizungumza ufisadi wa rostam wananchi wale hawatakuelewa kwa jinsi walivyopigika, sasa ukifika pale anza na ufisadi wa mwenyekiti wa kijiji alikula pesa za kujenga kisima cha maji zilizotolewa na rostam aziz, ukienda kwenye kata unazungumzia jinsi katibu katibu kata alivyokula pesa za mgao wa kila kijiji zilizotolewa na rostam, unapofika wilayani unazungumzia jinsi rostam aziz alivyoiba mabilioni benki kuu akisaidiwa na ccm ili alete bilioni moja igunga lakini akaleta milioni kumi tu!

ukifika tabora mjini au makao makuu ya mkoa, unaeleza jinsi rostam alivyokomba mabilioni ya epa, badala ya kuleta tabora ijengwe barabara ya lami toka tabora kwenda nzega, akapeleka huko iran, na kununua ndege!

Kwa taarifa yenu, Rostam alishaaga kwa wananchi wa jimbo lake la Igunga mara tu baada ya sakata la Richmond kumwangukia. Kwa mujibu wa mama yangu mdogo ambaye anaishi huko Igunga, Roastam alifanya mikutano ya hadhara na wananchi karibu wa vijiji vyote vilivyopo ndani ya jimbo lake. Akawaambia kwamba hategemei kugombea tena kwa kuwa ametajwa kwenye sakata la Richmond.

Wananchi walipoanza kumweleza matatizo yao, akawaambia kwamba wasubiri zile pesa alizokuja nazo Rais Bush wa Marekani alipotembelea Tanzania. Yeye hahusiki tena na kutatua matatizo yao. Kwa kifupi ni kama vile ameshajiuzulu isivyo rasmi huko Igunga! Hafanyi chochote kwa ajili yao, au kwa lugha rahisi ni kwamba, AMELITELEKEZA jimbo lake kwa kuwa hana mpango wa kugombea tena ubunge!!!!!!!

Sasa kwanini asijiuzulu tu, ili achaguliwe mbunge mwingine ? CHADEMA waanzie Igunga, waongee na wananchi, kisha hayo yakithibitika, basi washinikize Rostam kujiuzulu Ubunge ili awapishe watu ambao wako tayari kuwafanyia kazi watu wa Igunga!

Nchi hii inasikitisha sana!!!!
 
Saba mbaroni kwa kutaka kuivuruga CHADEMA

[Source Tanzania Daima]

na Kulwa Karedia, Serengeti

VIJANA saba wanaodaiwa kuandaliwa kufanya fujo katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamekamatwa na polisi.

Vijana hao walikamatwa jana jioni wilayani hapa mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na timu ya viongozi wengine wa chama hicho kuanza mikutano ya kunadi chama hicho kuanzia ngazi vijiji, kata, tarafa, wilaya hadi mkoa.

Vijana hao walikuwa na mabango yaliyosomeka kuwa ‘Hapa sio Tarime' walikuwa wamevalia fulana za CCM.

Habari zaidi zinasema kuwa vijana hao waliandaliwa kuvuruga mkutano huo ambao ulitarajiwa kuhutubiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe jana.

Hata hivyo kabla ya kuanza kufanya fujo, CHADEMA ilitoa taarifa polisi na hatimaye kukamatwa.

Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa alisema chama chake hakiwezi kutishika na hali hiyo inayotokana na kutumiwa na baadhi ya makada wa CCM.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, aliwataka wakazi wa Serengeti kuwa na msimamo wa kuunga mkono kambi ya upinzani kwa vile CCM imeshindwa kuwapatia maendeleo kwa zaidi ya miaka 48 tangu kupatikana kwa uhuru.

Katika hatua nyingine, Mbowe alishindwa kuhutubia mkutano wa hadhara kweye uwanja wa Mbuzi mjini hapa baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha uwanja kujaa maji.

"Nawaomba radhi sana wananchi wa Serengeti kwa kushindwa kuhutubia leo (jana) kutokana na mvua kubwa kunyesha hapa… nawahakikishia kwamba tunatafuta siku nyingine ya kuja kuwaeleza kile tulikikusudia katika mfululizo wa mikutano yetu," alisema Mbowe.
 
mh mie yangu macho, ila kwa mtindo huu wa povu la soda ni kuchoka si mda mrefu hizi ni mbio za marathon sasa uwe makini

ss tunajipanga na kuweka nguvu zetu huko mbeleni

nguvu mtego kwa hio chadema malizeni mambo yenu na ss tunakusomeni tukianza hamtonyanyuka
 
Ninyi kina nani?
 
Hii Topic nimeipenda.

Ni kama vile Mnaongea mawazo yangu wala sina cha kuongezea.
Mnanikumbusha ule msemo wa marehemu Mobitel wa

"MOBITELNOWYOUARETALKING"
 
Mpendwa Unayechukia Mafisadi.
Unamaanisha mwisho wa CCM kuwa ndio 'mwisho wa Dunia' au?
Ninachojua ni kuwa siku moja chama kingine cha siasa kitatawala Tanzania, lakini hautakuwa mwisho wa CCM.
Hata NARK iliposhinda Kenya haikuwa mwisho wa KANU, maana bado ipo na siku moja itaibuka na kutawala tena nchi.
Hata Zambia aliposhindwa Mzee Kaunda haukuwa mwisho wa chama alichokuwa anakiongoza, lakini ukiangalia kwa sasa Bw. Rupia Banda ambaye ni Rais wa muda pia Rais mtarajiwa wa Zambia yeye ni 'kijana' wa mzee Kaunda.

Ninachoamini ni kuwa CCM bado ni chama kilicho na sera thabiti za kuiongoza nchi na chenye mvuto kuliko vyote hapa Tanzania, yanahitajika marekebisho madogo tu kukifanya kiendelee kuwa nambari wani.

Asante kwa changamoto.

Marekebisho madogo?
Kuweka viraka juu ya kiraka ni marekebisho madogo.

Mtu mwongo siku zote huanza kujidanganya mwenyewe kwanza.

CCM inahitaji ile kitu inaitwa Overhauling.
Unafungua nuts na bolts zote kila kitu kinakuwa nje nje.
Sasa usidhani kwamba ni suala la kuosha na kufunga tena uchafu uleule.
Ni Frame/Block au skeleton tu inayo bakia sehemu zilizo bakia zote jalalani au kwenye tanuru la 1500C vikasafike kwa ndimi za mioto, patamu hapo.

Acha kujidanganya, zaidi acha kudanganya watu wengine.
 
Back
Top Bottom