Operation Sangara: Chadema yajipanga Upya

Selous

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
1,325
144
WanaJF;

Naomba tujadili hii kitu inayoitwa Operation Sangara. Hata kama imeanza but i think some of comments can be implemented.

Ijapokuwa sijui content ya hii operation but all in all ni kuamsha wananchi ili wadali mabadiliko yenye tija kwa kila raia. Kwa watakaopenda watajiunga na CHADEMA na wengine watadai mabadiliko either CHADEMA kwenye, JAMIIFORUMS, CCM, DP, CUF n.k. Yaani kuimarisha.

Kwa kuwa mimi ni mshabiki wa CHADEMA na pia mkazi wa kanda ya ziwa, napenda kuungana na CHADEMA kwenye hii operation kwa kuwa naamini ina maslahi kwa taifa langu.

Kwa kuwa hapa JF tupo watu tofauti na tunaamini kuwa vyama vyetu havijakuwa tokea kwenye shina na kwa kuwa sijui kwa undani wa hii project na kwa kuwa wananchi sasa wanataka mabadiliko yaani wamekata tamaa, na kwa kuwa kuna watu wanaipenda sana hii nchi hata kama wapo ccm kama FMES. Sasa naomba tutoe mapendekezo yetu jinsi ambavyo hii operation ingefanyika na ikaleta tija.

Nafikiri mikutano ya hadhara kwenye miji mikuu ya mikoa haifai. Ila ikiwezekana wanaCHADEMA nendeni kama mwenge yaani kijiji hata kijiji na ikiwezekana tembeeni na kapu kuomba muwezeshwe ili ujumbe ufike kwa kila mtu.

Chocheeni uhasama kwa watu against mabaya yote yafanywayo na CCM na govt yake. Tumieni mifano ya sehemu husika.

Mwiko: usizungumzie ufisad ya RA na timu yake kwa wananchi wa kawaida hasa kule alikopita na kumwaga pesa mana bado wengi hawajui impact yake.

Makongamano ya ndani na watu wa rika mbalimbali ni muhimu ili kujau shida na matamanio ya watu.

Nitafikiria tena, nikipata nitaweka hapa,

Asanteni
 
Sasa usipozungumzia ufisadi wa RA CCM wataendelea kupeta vijijini, au? Lazima wananchi waamshwe wajue jinsi nchi yao inavyofisadiwa na nani.
 
Sasa usipozungumzia ufisadi wa RA CCM wataendelea kupeta vijijini, au? Lazima wananchi waamshwe wajue jinsi nchi yao inavyofisadiwa na nani.

Kaka trust me;

Yani watu wamechoka kiasi kuwa ukimpatia tonge basi atakushukuru utafikiri Mungu mtu. Watu hawafikiri maisha ya kids zao hata kidogo. Ndo maana nasema kama watakuwa na muda wa kuhakikisha wanatoa somo mpaka yule mbumbu wa kanga na tshirt aelewe kuwa matatizo ya Busolwa yameshababishwa na RA basi waseme kwa ufasaha.

i used to do this na wanaelewa.
 
CHADEMA yahofia machafuko nchini


Sasa "helkopta' kutua kila kijiji mpaka kwa Nyerere,

Ushirikiano na vyama vya upinzani wazikwa rasmi

Na Said Mwishehe

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza kuanza kwa ziara ya nchi nzima ya uongozi wa juu wa chama hicho kwa ajili ya kukutana na Watanzania wote, kutekeleza mkakati wake maalumu unaoitwa Operesheni Sangara, ambao unalenga kulikomboa Taifa lisikumbwe na machafuko.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe, alisema lengo la operesheni hiyo ni kuwafahamisha wananchi kuhusu wajibu wao wa kulikomboa Taifa kwa kuwa kuna dalili mbaya kwa nchi zilizoanza kuonekana.

"CHADEMA imeamua kuanzia kesho (leo), tunazindua operesheni maalumu ambayo viongozi wa ngazi zote wa chama, watazunguka nchi nzima kuwaunganisha Watanzania wote katika harakati za kuikomboa nchi kwa mara ya pili, baada ya ile ya kwanza iliyofanywa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, alipukuwa na TANU," alisema Bw. Mbowe.

Kiongozi huyo aliyeanzisha kampeni za juu kwa juu kwa kutumia helkopta, alisema wataanza mkoani Mara ambapo watafanya kazi ya kuwaunganisha wananchi bila kujali itikadi zao za dini, kabila wala vyama vya siasa kwa wiki mbili na baada ya hapo, watakwenda Mwanza na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa.

"Viongozi wote wa chama, kesho (leo) tutakuwa Mara kwa ajili ya kuzindua rasmi operesheni yetu, tunaomba Watanzania watuunge mkono kwa kuwa nia yetu ni njema. Tuaamini tutafanikiwa ingawa tutaifanya kazi hiyo bila fedha," alisema Bw. Mbowe.

Alisema sababu za operesheni hiyo zimetokana na kuonekana kwa mambo mengi ambayo yalikuwa hayatokei kwa Taifa. Alitoa mfano wa tukio la wananchi kupiga mawe msafara wa Rais Jakaya Kikwete, kuwa linaonesha inchi inaendeshwa bila kufuata utawala wa sheria.

"CHADEMA sasa tumesimama imara kuhakikisha Taifa linakwenda mahali ambapo wananchi hawataishi maisha ya shida kama waliyonayo sasa, tutaungana na Watanzania wote na kutafakari kwa kina nini kifanyike ili kujikomboa katika wimbi la umasikini," alisema.

Aliongeza kuwa nchi imegawanyika katika makundi mawili ya matajiri na masikini. Wale matajiri wanaoishi maisha mazuri na kusomesha watoto nje, lakini kundi kubwa la watu masikini wanakosa pa kukimbilia na kuishia kusomesha watoto wao katika sekondari za kata ambazo hazina walimu wala vifa vya kufundishia.

Wakiwa mkoani Mara watakwenda kijiji cha Butiama kuona na Mama Maria Nyerere kumueleza nia yao ambayo inalenga kuunga mkono mapambano ambayo awali yalikuwa yakifanywa na Hayati Mwalimu Nyerere.

Aliaomba Watanzania wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli, kutoa misada ya aina yoyote ambayo wanahisi inaweza kuwasaidia katika operesheni yao, iwe unga au maji na kusisitiza kuwa katika operesheni hiyo, watalala kwa wananchi na hawatalipana posho kwa kuwa hawana kitu.
Pia watapanga chama upya katika mitaa na kuwa na mabalozi kila kijiji.

Akizungumzia ushirikiano uliokuwepo kati yao na vyama vingine vitatu ambao walikubaliana, Bw. Mbowe alisema kwa sasa wameamua kujitoa kutokana na kuona vyama wanavyoshirikiana navyo, baadhi havina nia njema dhidi yao.
 
safi , ni kweli ukienda igurubi wilayani igunga ukizungumza ufisadi wa rostam wananchi wale hawatakuelewa kwa jinsi walivyopigika, sasa ukifika pale anza na ufisadi wa mwenyekiti wa kijiji alikula pesa za kujenga kisima cha maji zilizotolewa na rostam aziz, ukienda kwenye kata unazungumzia jinsi katibu katibu kata alivyokula pesa za mgao wa kila kijiji zilizotolewa na rostam, unapofika wilayani unazungumzia jinsi rostam aziz alivyoiba mabilioni benki kuu akisaidiwa na ccm ili alete bilioni moja igunga lakini akaleta milioni kumi tu!

ukifika tabora mjini au makao makuu ya mkoa, unaeleza jinsi rostam alivyokomba mabilioni ya epa, badala ya kuleta tabora ijengwe barabara ya lami toka tabora kwenda nzega, akapeleka huko iran, na kununua ndege!
 
safi , ni kweli ukienda igurubi wilayani igunga ukizungumza ufisadi wa rostam wananchi wale hawatakuelewa kwa jinsi walivyopigika, sasa ukifika pale anza na ufisadi wa mwenyekiti wa kijiji alikula pesa za kujenga kisima cha maji zilizotolewa na rostam aziz, ukienda kwenye kata unazungumzia jinsi katibu katibu kata alivyokula pesa za mgao wa kila kijiji zilizotolewa na rostam, unapofika wilayani unazungumzia jinsi rostam aziz alivyoiba mabilioni benki kuu akisaidiwa na ccm ili alete bilioni moja igunga lakini akaleta milioni kumi tu!

ukifika tabora mjini au makao makuu ya mkoa, unaeleza jinsi rostam alivyokomba mabilioni ya epa, badala ya kuleta tabora ijengwe barabara ya lami toka tabora kwenda nzega, akapeleka huko iran, na kununua ndege!


tatizo la Tanzania ni watu wa mjini.
Vijijini tumeamka tupo gado, na m/kiti ama balozi wa kitongoji akitufisadi huwa tunamkamata na na sungusungu kumchapa viboko na tunamkataa ktk kijiji.
Ikija swala la diwani/mbunge sisi huwa tunachagua mtu anayetufaa bila kuangalia itikadi zao na ndio maana ukiangalia kwa makini wabunge kutoka vijijini huwa mara nyingi wana alternate mara cuf,mara ccm ,mara chadema,mara udp hapo huwa tunatafuta wakutufaa.

Tatizo la Tanzania ni ninyi watu wa mjini hasa ngazi ya wilaya hadi Taifa Chunguzeni jinsi mnavyochaguwa wa bunge wenu na madiwani wenu mkiona mnafanya vizuri ktk uteuzi wenu ndipo njooni mtuelimishe sisi wa vijijini

Angalieni watu wa mjini mmeshindwa kufanya lolote kwa MAFISADI wenu wa mjini eti nalo mje mtuelimishe!!!! Hivi ninyi watu wa mjini ni nani aliyewaloga?

Maana haya mafisadi yangekuwa level yetu tungeyakamata tukayachapa viboko harafu tukayaamulu yatoweke ktk vijiji vyetu mara moja ,Ninyi watu wa mjini mmeshindwa kufanya lolote.

Na kwa kiwango ambacho mlivyo ma kondoo mnataka mje mtuelimishe ili iwe je? mkituelimisha?
sisi huku vijijini hatuna Polisi polisi wako mjini kwenu,huku hatuna mahakama mahakam yako mjini ,huku hatuna magereza magereza yako mjini kwenu.Sasa mnakuja kutuelimisha ili iweje?? maana haya mafisadi mnaishi nayo huko mjini.

Na kama tatizo ni CCM basi ninyi watu wa mjini ndio mnapaswa mtuombe sisi watu wa vijijini tuje tuwaelimishe AMa kwa vile mna uwezo wa kufikia media ndio mnaamua kutufanyia UFISADI sisi watu wa vijijini??

Kama kuichagua CCM nyie wasomi na wa mjini ndio vinara kwa hilo Angalia kama kinondoni na ILALA walishawahi chagua upinzani??

Angalia morogoro mpinzania wamemchagua lini? nenda dodoma mpinzani kachaguliwa lini haya ingia mwanza niambie ninyi watu wa mjini mpinzani katokea?
Haya kule Arusha na mbeya pia Iringa jamani wapinzani mmewachagua?

Angalia vijijini Biharamulo sio mjini wala hakuna high school ,Tarime napo sio mjini japo kuna chuo cha ualimu,Bariadi napo si mjini na hakuna hata high school na kwingineko naamini ukimtuoa NDESAMBULO wengine wote wapinzani watoka vijijini.
Sasa mnataka kuja kutuelimisha kwa lipi??

sisi Watanzania wa vijijini tumesha declare TATIZO letu LIMESABABISHWA na wasomi wetu kutusaliti,Limesababishwa na watu wa mjini waliokaribu na media na huduma mhimu KUTUSALITI.
Wasomi wetu vijana wetu tumewatuma gulioni kuhemea chochote huko mjini ili watachopata huko watuletee sisi wa vijijini tusio na shule tumegeane LAKINI badala yake wametugeuka na kutuharamia ,wasomi wamekatalia mjini na huko wanatumia kalamu zao tulizowapa sisi kutumaliza harafu wakitia dhihaka eti waje watuelimishe sisi tuliona umuhimu wa elimu na kuamuwa kuwatuma huko.

Watu wa mjini MIMI nafikiri hakuna haja ya kuja kutuelimisha sisi watu wa vijijini ila mnachotakiwa kuanza nacho anzeni huko huko mjini kwenu na kwa wasomi wenu kuhubiri PATRIOTISM NA SOLIDARITY .HILO NDILO TATIZO KTK NCHI YETU na mizizi yake mibovu imeanzia mijini na kwa wasomi.
 
Tatizo jingine ninslolions ni kues kes dsbsbu move hii imeanzishwa na Chadema,kuna hatari ya kuonekan mopre of a political than a societal movement. Hali ilivyo nchini hivi sasa we need to go beyond politics kuikomboa nchi. Nilipoisona kijuujuu, naamini hii ni moja ya move ambazi n=zikitumiwa vizuri inaweza kuleta mapinduzi, lakini isifanywe kisiasa
 
Tatizo jingine ninslolions ni kues kes dsbsbu move hii imeanzishwa na Chadema,kuna hatari ya kuonekan mopre of a political than a societal movement. Hali ilivyo nchini hivi sasa we need to go beyond politics kuikomboa nchi. Nilipoisona kijuujuu, naamini hii ni moja ya move ambazi n=zikitumiwa vizuri inaweza kuleta mapinduzi, lakini isifanywe kisiasa

Ndio hapo mkuu tatizo ndilo hilo badala kuifanya move ya kujikomboa watu wanaiegemeza ktk chama fulani eti wakifikiri kuchagua chama cha upinzani ndio mwanzo mzuri na kuchagua upinzani ndio demokrasia.

Tunasahu kabisa hakuna wakati ambapo watanzania walichagua wapinzani wengi ktk ule uchaguzi wa 1995 ulikuwa na wabunge wengi wa upinzani.

Harafu tunajaribu kuzidanganya akili kuwa kila anayevumbua UFISADI ana nia njema ama ndio mwanzo na moto tumeuwasha wa ukombonzi Na tunasahu kabisa kuwa Mzee DEKAYA naye amevumbua ufisadi mwingi tu humo humo ccm lakini sijaona moto wowote .

Na wakati huo huo huyu jamaa kasababisha mawaziri kadhaa kujiuzulu mfano IDD SIMBA,nadhani MBILINYI waziri wa fedha n.k

Kuna chama kinatumia advantage hiyo kutaka manipulate HEWA na ukweli ni kuwa nchi ile IMEVAMIWA na chakufanya ni sisi wote haswa wa mjini wahubiri PATRIOTISM na SOLIDARITY.

Hivi vyama ni vya kifisadi tu.
 
Chadema wanapata wapi pesa za kukodisha Helicopter for the whole Sangara Project?

Why other Opposition Parties fail?
 
Tatizo ni utengano wa vyama vya siasa,Sidhani kama CHADEMA inaweza kushinda peke yao..Mbinuu ya kuwagawa hawa wapizania ndiyo njia ya CCM kushinda kwa kishindo.Mie naona ni vyema vyama hivi vikaungana na kuwa hama kimoja ii viwe na sera moja..CUf ina nafasi kubwa kama CHADEMA

Kwa mtazamo wnagu mapinduzi ya kweli yataanzia Zanzibar baada ya CUF kushinda tena na kushika hatamu
 
Mimi naona kama safari imeanza maana waswahili wanasema aanzaye na uluzi iishia na kuimba sasa Chadema imeanza na uluzi wataimba tu na kitaeleweka tuwaunge mkono kwa wingi wetu naamini kitaeleweka.
Tuombe Mungu.
 
Gembe....Mhh mapinduzi yataanzia Bara....na hayo ndio makosa ya CUF wanaona Zanzibar ni rahisi kuliko Mainland...(Kutokana na ukubwa wa mainland na elimu ya watu)...

Wahafidhina wa CCM znz hawapo tayari kuona wanashare hio "National Cake" na wenzao!!! Let see "Sangara project" inavyoweza kuwaamsha wananchi
 
CHADEMA wazidi kuitesa CCM




Mwenyekiti Mbowe akihutubia Musoma mjini




na Kulwa Karedia



MAMIA ya wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake jana walijitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ‘Operesheni Sangara’, ambapo wito ulitolewa kwa Rais Jakaya Kikwete kuwafikisha mahakamani mafisadi wote walioiba fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA).

Wito huo ulitolewa mjini hapa na Katibu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wakati akihutubia mamia ya wananchi kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Mkendo.

Alisema endapo Rais Kikwete atashindwa kuwashughulikia mafisadi hao, ni bora kuwaachia wafungwa wote waliomo katika magereza mbalimbali nchini.

Mkakati wa ‘Operesheni Sangara’ umelenga zaidi kupeleka madaraka kwa wananchi kuanzia ngazi za chini hadi taifa, ili kujenga uwezo wa chama.

“Napenda kumwambia Rais Kikwete kwamba sasa muda wa Rais Kikwete kuona kipimo cha uongozi wake ni Oktoba 31 pale atakapowafikisha mahakamani mafisadi wote… lakini kama hatafanya hivyo, tunasema wafungwa wote walioko gerezani waachiwe, ili haki itendeke kwa wote,” alisema Dk. Slaa.

Alisema iwapo Rais Kikwete atashindwa kufanya hivyo atasababisha wananchi kuendelea kupoteza imani kwake, kama sasa ambapo wamefikia hatua ya kupiga mawe msafara wake.

“Ni jambo la ajabu mkuu wa nchi kutupiwa mawe akiwa katika shughuli za serikali. Hii inaonyesha wazi jinsi wananchi walivyoanza kuchoshwa na serikali yake… tunasema kama ataendelea na mwenendo huu anastahili kuondolewa hata kesho,” alisema Dk. Slaaa.

Alisema kushindwa kwa serikali ya Kikwete kutoa maisha bora kwa kila Mtanzania kumetokana na wasaidizi wake wengi kujali masilahi binafsi, badala ya kutumikia umma.

Alisema tangu Rais Kikwete alipoingia madarakani wananchi walikuwa na matumaini makubwa, lakini hivi sasa wamekata tama, baada ya kunyanyaswa na watu waliopewa dhamana ya kuwasaidia.

Dk. Slaa alisema pamoja na hatua atakazochukua Rais Kikwete juu ya mafisadi, bado CHADEMA italipua bomu la ufisadi wa sh milioni 155 zilizoibiwa katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba kupitia Kampuni ya Meremeta inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Rais tulimwambia mambo mengi kuhusu wizi wa fedha za umma, lakini tunashangaa kuona ameamua kushughulikia EPA peke yake, nawaambia jamani tulimwambia atupatie maelezo, lakini amekuwa akitukwepa kila siku.

“Ufisadi mkubwa uliofanywa kwenye Kampuni ya Meremeta chini ya JWTZ sasa tunasema tutawasha moto hadi kuona waliochukua fedha hizi wanajulikana,” alisema Dk. Slaa.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, alisema serikali ya CCM imechoka na sasa umefika wakati wa kukaa kando na kuachia kizazi kipya ambacho anaamini kuwa kitaleta mageuzi ya kweli.

“Chama kimejaa mafisadi, wanalindana, wamechoka hata kwa mawazo, tunasema wakazi wa Musoma mna wakati wa kufanya maamuzi kama yaliyofanywa na ndugu zenu kule Tarime, ambako CCM tuliibwaga bila ubishi na leo hii tukifanya tathmini ya gharama za maisha, mtaona serikali ya Kikwete ilivyosababisha umaskini kuongezeka,” alisema Zitto.

Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi, Zitto alisema taifa limeuzwa, kwani rasilimali zote muhimu zikiwemo madini, samaki, mbuga zimeuzwa kwa wakezaji kutoka nje ya nchi.

“Tumekuwa na rasilimali nyingi ambazo zimeuzwa kwa wawekezaji wa nje… hata bajeti yetu ya serikali imeendelea kubaki tegemezi, kwani mpaka sasa wafadhili wanatoa asilimia 34. Hii ni aibu kubwa, tukatae fedheha hii,” alisema Zitto.

Aidha, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye alifungua rasmi operesheni hiyo, alisema huo ni mpango uliobuniwa na CHADEMA bila kujali jinsia, rangi wala itikadi, kwa lengo la kulikomboa taifa.

“Leo hii (jana) tumeanzisha vuguvugu la kweli lenye kuleta mapinduzi mapya na tumeamua kuzindulia hapa Musoma, kwa sababu ya kumuenzi hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye ni mzaliwa wa mkoa huu,” alisema Mbowe.

Katika mkutano huo, wanachama zaidi ya 400 wa CCM walirudisha kadi zao na kukabidhiwa za CHADEMA, wakiwamo mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Vijana (mkoa), Gewa Anthony, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Musoma (UVCCM), Hamis Tumbo.




juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 48 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
SAWA KABISA TUNATAKA WATU WENYE MAONO NA MIKAKATI YA KIMAENDELEO WAHAMASISHE TAIFA HILI, NA MIKAKATI HIYO IWE YA KUDUMU. TUMECHOKA NA WATU - MAFISADI WANAOTURUDISHA NYUMA KILA SIKU KWA KUTETEA MATUMBO YAO YASIYO NA SHUKRANI

na MMM, TZ, - 20.10.08 @ 08:18 | #48917

Mkakati huu ni mzuri na utaendeleza vuguvugu la mageuzi ya fikra nchini.

Ila nadhani uanzishwe mkakati mwingine wa kudai tume huru ya uchaguzi. Kwani kura zinaibiwa sana na sio kila wanaopenda mabadiliko wanao ujasiri kama wa Tarime. Pale Tarime tume iliiba kura lakini ikaingiwa na hofu.

Mimi, siamini kwamba kwa uchaguzi wa haki Kikwete aweza kumzidi Mbowe kwa wingi wa kura.Hali ya nchi sasa na tofauti kabisa. Baadhi ya mikoa ambayo tungesema watu wake wako nyuma kimtizamo, hivi sasa wanamwita rais "the comedy".
Hapo usitegemee kura kwenda kwa mtu wanaemwita msanii.

na Raphael Komto, Tz, - 20.10.08 @ 09:24 | #48929


CCM wajanja ndo maana hata wakawarubuni wale ze comedy wawe tbcii wasiendelee kuwaumbua.

Freeman unatisha songa mbele mwana tupo pamoja nawe

na Mukaru Ng'ang'a, china, - 20.10.08 @ 09:52 | #48936

Napenda kuwapongeza Viongozi wa CHADEMA na wanachama wao wote kwa juhudi na fikra mbadala juu ya ukombozi wa taifa hili. Hakika sasa Watanzania tunakila sababu ya jisifu kwamba tumepevuka kiakili na kisiasa kwajili ya Chama hiki kwa mikakati yote inayobuniwa hasa katika kipindi hiki cha ufisadi.

Wana CHADEMA na Wananchi wote wenye uchungu na taifa hili ebu tushikamane sote kwa pamoja tuwaunge mkono viongozi hawa Wazalendo waliotayari kwa gharama yoyote kuwapigania wanyonge pamoja na taifa lao.

Kwa mtazamo huu, napenda kuwafahamisha wana CCM wote kuwa mwisho wenu umekaribia. Kwa mtindo wa kulindana uliopo sasa unaenda kukisambaratisha Chama chenu; hadi sasa wananchi na wanachama wenu waliowengi wameishapoteza tumaini kuhusu CCM. Kwa udhibitisho zaidi ni kule Mbeya ambapo wananchi wameishajikatia tamaa na hawana imani na serikali yao tena. CCM someni alama za nyakati!!!

HONGERENI SANA WANACHADEMA WOTE!! Kwa mikakati hii mwaka 2010 Bunge la TZ likaliwa na Wabunge wengi toka CHADEMA. Viongozi na Wabunge wa CHADEMA tumewaona umoja na umahili wenu katika harakati zote za kumkomboa Mtanzania. Nawapongeza sana!!!

Ninachowaomba Viongozi wa CHADEMA ni kwamba jihadharini sana na chachu toka kwa vyama vingine. Ebu simameni kama mlivyo! Jifunzeni kwa yaliyotokea Tarime; Kuweni makini na vyama vingine. Wapinzani wa CHADEMA siyo CCM tu, bali ni vyama vyote vya upinzani.

na Elias Allen , Kilimanjaro, - 20.10.08 @ 09:57 | #48938

CCM MMEKWISHA. KIKWETE KAAMUA KUFARIKI NA KINA CHENGE NA LOWASSA WAKE. HAYA. CHADEMA MUENDE VIJIJINI NDANI ZAIDI. NA NYIE MCHUNGE UFISADI. TUTAWAPA UBUNGE. NENDENI KAJIIMARISHENI MBEYA KUNA DEAL.

na CCM, TANZANIA, - 20.10.08 @ 10:14 | #48946

Njooni na morogoro nina kadi ya CCM naona inanisumbua,naona sasa muda wa kufanya mapinduzi umefika na mniletee hizo kombati za kiwanamapinduzi!CHADEMA IDUMU NA CCM IENDELEE KUPIGA SOGA HIVYOHIVYO WAMUULIZE YALIYOMPATA KENEDDY KAUNDA WA ZAMBIA!

na Makotso, morogoro, - 20.10.08 @ 10:32 | #48955

Viongozi wa CHADEMa, na wanachadema na watanzania wote wenye mapenzi mema, hongereni kwa Mkakati huu wa kimapinduzi. Mimi nawapongezeni akina Mbowe, Dr. Slaaa, Zitto kabwe na wengineo. Mungu abariki jitihada zenu, kweli nyie ni chama makini. Ni kweli watu wamechoka na CCm na sera zake hazikidhi mahitaji ya Watz. hapa kenya mambo ni ya kimapinduzi pia. Watu wanataka maendeleo siyo domokrasia. leo huko Amerika Collnell Paul Powell aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ikulu ambaye ni Mwana Republican amesema hadharani kwamba anamuunga mkono Barak Obama na atampa kura yake, lakini hatujasikia uhasama kwake, na kutishiwa na rais wa Republican, hizi ndizo siasa zilizokomaa, lakini Tanzania mtu akijitoa chama tawala, basi maisha yake yapo hatarani. Tuache siasa za kulazimisha na vitisho. Tujernge demokrasia ya kweli ili watu wawe huru kumchagua wanayempenda, kulazimisha uongoz\i matokeo yake ndiyoo kama tunavyoshuhudia matukio mbali mbali. haya huko Afrika Kusini waziri wa zamani wa Ulinzi Lokera naye kajitoa chama tawala ANC, anasema anaanzisha chama kipya, lakini hatujasikia vitisho kwake, tujifunze, na sasa tunaishi katika dunia ya Utandawazi, mambo ni uwazi na uhuru wa mtu binafsi kuamua baadhi ya mambo kama hayo ya upigaji kura. Tanzania tunang'angania siasa za chama kimoja hadi lini waingereza wanasema" If you dont welcome change, change will change you" Maana yake kwa wenzangu wa Maguu na litembo ni kwamba " Usipoyakubali mabadiliko, mabadiliko yatakubadili wewe, tena kwa nguvu." Mkakati huu ni kiboko, ndeneni vijijini pia muwape wananchi mwanga na uelewa wapi nchi inakwenda. mambo mawili yanatakiwa nchini Tanzania (a) Kuandika katiba mpya ya vyama vingi na (b) Kuunda Tume mpya ya uchaguzi ya vyama vyote, huu ndiyo mkakati wa Wanakenya kwa sasa, Watanzania tunangoja nini hadi machafuko yatokee? Kumbuka wahenga husema " Usipoziba ufa, utajenga Ukuta." Serikali ya Awamu ya nne, tafadhali sana, someni alama za nyakati, fungueni masikio, akili, macho na mioyo yenu, andaeni mapinduzi ya kistaarabu. Mungu ibariki Tanzania na wanaharakati wote bila kujali itikadi, kwani Tanzania ni ya watanzania wote bila kujali chama, dini,kabila wala cheo. Unabii wa Mwalimu Nyerere unaendelea kutimia siku hadi siku, na asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Usidharau wosia wa wazee, Nyerere alitoa woasia mwingi sana, ambao naona unakejeliwa katika vyombo vya habari, kwa maana kwamba, tunawadanganya wananchi kwamba tunajali wosia wake kwa kuuweka katika Tv, lakini hatuufuati. Mtumishi wa Mungu JK Nyerere, utuombee. Amina.

Padre Mapunda Baptiste (M.afr)
Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki -CUEA,
Idara ya Mawasiliano ya jamii,
Tangaza College,
Nairobi/Kenya.

na Ffr. Baptiste Mapunda, Nairobi/Kenya, - 20.10.08 @ 10:45 | #48960

Viongozi wa CHADEMa, na wanachadema na watanzania wote wenye mapenzi mema, hongereni kwa Mkakati huu wa kimapinduzi. Mimi nawapongezeni akina Mbowe, Dr. Slaaa, Zitto kabwe na wengineo. Mungu abariki jitihada zenu, kweli nyie ni chama makini. Ni kweli watu wamechoka na CCm na sera zake hazikidhi mahitaji ya Watz. hapa kenya mambo ni ya kimapinduzi pia. Watu wanataka maendeleo siyo domokrasia. leo huko Amerika Collnell Paul Powell aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ikulu ambaye ni Mwana Republican amesema hadharani kwamba anamuunga mkono Barak Obama na atampa kura yake, lakini hatujasikia uhasama kwake, na kutishiwa na rais wa Republican, hizi ndizo siasa zilizokomaa, lakini Tanzania mtu akijitoa chama tawala, basi maisha yake yapo hatarani. Tuache siasa za kulazimisha na vitisho. Tujernge demokrasia ya kweli ili watu wawe huru kumchagua wanayempenda, kulazimisha uongoz\i matokeo yake ndiyoo kama tunavyoshuhudia matukio mbali mbali. haya huko Afrika Kusini waziri wa zamani wa Ulinzi Lokera naye kajitoa chama tawala ANC, anasema anaanzisha chama kipya, lakini hatujasikia vitisho kwake, tujifunze, na sasa tunaishi katika dunia ya Utandawazi, mambo ni uwazi na uhuru wa mtu binafsi kuamua baadhi ya mambo kama hayo ya upigaji kura. Tanzania tunang'angania siasa za chama kimoja hadi lini waingereza wanasema" If you dont welcome change, change will change you" Maana yake kwa wenzangu wa Maguu na litembo ni kwamba " Usipoyakubali mabadiliko, mabadiliko yatakubadili wewe, tena kwa nguvu." Mkakati huu ni kiboko, ndeneni vijijini pia muwape wananchi mwanga na uelewa wapi nchi inakwenda. mambo mawili yanatakiwa nchini Tanzania (a) Kuandika katiba mpya ya vyama vingi na (b) Kuunda Tume mpya ya uchaguzi ya vyama vyote, huu ndiyo mkakati wa Wanakenya kwa sasa, Watanzania tunangoja nini hadi machafuko yatokee? Kumbuka wahenga husema " Usipoziba ufa, utajenga Ukuta." Serikali ya Awamu ya nne, tafadhali sana, someni alama za nyakati, fungueni masikio, akili, macho na mioyo yenu, andaeni mapinduzi ya kistaarabu. Mungu ibariki Tanzania na wanaharakati wote bila kujali itikadi, kwani Tanzania ni ya watanzania wote bila kujali chama, dini,kabila wala cheo. Unabii wa Mwalimu Nyerere unaendelea kutimia siku hadi siku, na asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Usidharau wosia wa wazee, Nyerere alitoa woasia mwingi sana, ambao naona unakejeliwa katika vyombo vya habari, kwa maana kwamba, tunawadanganya wananchi kwamba tunajali wosia wake kwa kuuweka katika Tv, lakini hatuufuati. Mtumishi wa Mungu JK Nyerere, utuombee. Amina.

Padre Mapunda Baptiste (M.afr)
Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki -CUEA,
Idara ya Mawasiliano ya jamii,
Tangaza College,
Nairobi/Kenya.

na Ffr. Baptiste Mapunda, Nairobi/Kenya, - 20.10.08 @ 10:45 | #48961

Chadema lazima muwe na Strategic Plan ya kupata wanachama wengi zaidi hususan Vijana toka kona zote za nchi hii kwa kuanzai maeneo yote yenye machimbo ya madini ndiko vijana waliko athirika zaidi,katika miji yote mikuu nchini ambako wengi hawana ajira wala kipato cha uhakika na wengi wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku,katika wilaya zote zilizoko pembezoni mwa nchini hususan mipakani ambako wamesahauliwa kabisa na serikali ya CCM,wnafunzi wote wa vyuo vikuu ambao wana wakati mgumu sana katika ufadhili wao vyuoni,kwa walimu wote nchini ambao wamekabiliwa na migogoro mingi kuhusu hali duni ya maisha yao kazini,kwa wauguzi na madaktari,kwa waumini wa dini mbalimbali ambao wanapinga na kuchukizwa vikali na ufisadi,na kwa wapenda maendeleo wote nchini.Hakuna ubishi kwamba nchi yetu hivi sasa inakabiliwa na hali mbaya sana kiuchumi na kimwelekeo.That Hope for a Better Future is Gone with the Wind!Lazima Vijana wote kote nchini watambue kwamba ni kweli ni CCM ilyotufikisha hapa tulipo.Lakini ile iliyotufikisha hapa tulipo ni ile CCM iliyokuwa ya kwetu sote watanzania.Lakini kutokana na kiburi na dharau ya baadhi ya wazee ambao wao ndio wanaokiona chama cha CCM ni kampuni yao binafsi ndipo vijana wengi wakaamua kujiunga na vyama vingine vya siasa kwa nia njema kabisa ya kuliokoa Taifa letu.Uongozi wa sasa wa CCM umechoka ile mbaya.Bado umegubikwa na mawazo ya ndoto za Alinacha!Maneno mengi kuliko vitendo na kwa hakika maneno hayaendani na vitendo!Hakuna njia nyingine bora zaidi ya kuliokoa Taifa letu kwa manufaa ya vizazi vijavyo isipokuwa kwa kuwalazimisha CCM wapumzike kwanza japo kwa kipindi kimoja tu cha miaka mitano ijayo hapo itakapofika mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu!Vijana ndiyo wenye sauti na uwezo wa kuipumzisha CCM irudi darasani ikajipange upya na huku wakijifunza toka kwa wenzao wa upinzani jinsi nchi inavyopaswa kuongozwa kwa maslahi ya watanzania wote.Ni jukumu la vijana kuhamasishana baina yao tukielekea uchaguzi mkuu ujao 2010 kwamba CCM kwa sasa imechoka haina pumzi tena ya kukabiliana na Ufisadi unaoiangamiza nchi hivi sasa.Viongozi wanaogopana na kulindana kwasababu kila mmoja anatambua maovu ya mwenzake na kwa hiyo kila kiongozi anaogopa kumfunga mwenzie kengele mguuni!Hatuwezi kuendelea na Uongozi dhaifu kiasi hicho!We have to break away from the chains,we have nothing to loose!Kila kijana na kila mzalendo wa dhati atatakiwa kuipa CHADEMA kila aina ya ushirikiano katika kufanikisha malengo hayo.

na masharubu, Dodoma,Tanzania, - 20.10.08 @ 10:59 | #48966

nimekusoma padre!!!

na lukas - 20.10.08 @ 08:12 | #48970

Niungane na mwanamaoni mmoja hapo juu kuikumbusha CHADEMA kuwa wapinzani wa chadema si ccm tu, bali vyama vyote. Lakini nyongeza yangu ni ya kuwaomba wanaCHADEMA popote pale walipo kumwomba Mungu alete katika chama hiki hekima ya kuwa na siasa za kupingana bila kupigana. Hii busara itathibitisha umakini ambao kila mtanzania upo katika chama hiki.
Mbija Mbogolo, Dar es Salaam

na mbija mbogolo, Dar es salaam, - 20.10.08 @ 08:30 | #48976

ee bwana kweli mabadiliko tumekubali kilchobaki ni ku sisitiza vyuon hasa elim ya juu wabadilike na kua wanachadema wote ili mabadiliko ya kweli yafanyike bila kuchelewa mana wasomi ndio wenye zamana kubwa ya kushawish mabadiliko

na kabalaa tinto, tabora, - 20.10.08 @ 08:33 | #48980

Tuwaungeni mkono hawa majemedari.Ni kipindi kizuri sana tuwaunge mkono ili tupigwe sindano ya kuondoa ganzi kichwani kwani tumeteswa sana na hawa watu.Wametudhlilisha sana,bila hata haya.Tunawezaje kuwachangia japo vipesa ?

na kalimbo, dar, - 20.10.08 @ 08:37 | #48983

HIYO NI STRATEGIC NZURI YA KUJENGA MAZINGIRA MAZURI YA KUFANYA VIOZURI KATIKA CHAGUZI ZIJAZO NAPENDA KUWAPONGEZA KWA KUPONGEZA KWA HILO KWA SABABU ZIFUATAZO
1. WANANCHI WENGI WAMECHOKA NA WAMEKATA TAMAA SANA WANAHITAJI MABADILIKO YA KWELI, NA BAHATI MBAYA SANA TUPO KATIKA KIPINDI AMBACHO WATU WAMECHOKA SIASA ZA KISANII ZE COMEDY KWANI WAMEGUNDUA HAZINA MASLAHI KWAO ZAIDI YA KUWANEEMESHA WACHACHE YAANI MAFISADI

2.WATANZANIA WENGI SASA WAMEKUWA NA MUAMKO WA MAMBO YA KISIASA WANAHITAJI TU SUPPORT TOKA KWA WANASIASA WENYE NIA NA MABADILIKO YA KWELI.

3.NCHI IPO KATIKA CHANGAMOTO NYINGI ( UFISADI , MIGOMO YA WALIMU NA WANAFUNZI WAZEE WA E.A) NA IKIWA KAMA WAPINZANI WATATUMIA CHANGAMOTIO HIZO KAMA MTAJI NAFIKIRI KWENYE UCHAGUZI WA 2010 WATAKLUWA KATIKA POSITION NZURI SANA.

KAMA SENETA OBAMA TUNATAKA MABADIKO NA TUNA ANAAMINI TUNAWEZA....



na A G PAUL, DAR, - 20.10.08 @ 08:47 | #48987

OK!C JAWAHI KUPIGA KURA TOKEA NIMEZALIWA KATIKA HEKALI HIZI ZA TZ,LAKINI KWASASA NITARUDI HOME TZ KUWAPIGIKURA CHADEMA 2,ILA NAO HAPO BAADAYE WASIJE WAKATULETEA ZE COMEDY YAO 2TAWAVUA ZILE COMBAT ZAO MWI2 BILA KUJIJUA,.

na BRIGEDIA, CUBA, - 20.10.08 @ 08:50 | #48989

Kamandoo Mbowe,Dr.Slaa na Zitto,safi sana na mkakati huo,lakini kwanza nendeni vijijini mkafungue vichwa vya Watanzania waliokata tamaa na viongozi walioko madarakani na hawajui wafanye nini na hali ngumu ya kimaisha inayowakumba miaka kenda nenda rudi.

Dr.Slaa,Mbowe na kijana machachari,Zitto Kabwe,Mbeya tunawahitaji sana tena sana tuwape siri tulionayo mioyoni mwetu,tunawasubiri kwa hamu kubwa sana Wakombozi wetu,fanyeni ziara mikoa yote,wilaya zote,kata zote na viji vyote hapa Tanzania,lAKINI kwa hapa Mbeya fanyeni haraka kabla hatujapoa na maudhi yaliyofanywa na viongozi wa MAFISADI katika ziara yao.Njoni haraka ili tutoe picha halisi juu ya msimamo wetu juu ya Taifa letu linaloenda kufa badala ya kukua kutokana na Viongozi kuwa viongozi wa kundi la MAFISADI,Nchi ina nuka UFISADI na Mkuu wa nchi kuwalinda MAFISADI kwa nguvu zake zote badala ya kuchukua hatua za kisheria,sisi wananchi wa kwaida ambao hata mmoja wetu atakapoonekana labda ameiba kijiko cha jirani yake,kinachofuata kwa mtu huyo ni hatua za kisheria kuchukuliwa!lakini kwa mtu au watu waliochukua walio chota Mapesa EPA wanaambiwa warudishe pesa hizo na hatua za kisheria zitafuata!Watu wa Mbeya tuna KIULIZO hiki:kwanini mtu huyu wa kawaida aliyeiba kijiko cha jirani yake anafungwa badala ya sheria kuamuru arudishiwe kijiko chake aliyeibiwa?

Ndo maana tulimpokea hivyo mkuu wa nchi kwa sababu kawalinda MAFISADI!
NJOONI MBEYA, TUNAWASUBIRI KWA HAMU NA HISIA ZA HALI YA JUU SANA.

Tunaanda MAPOKEZI YENU(CHADEMA),kama MASHUJAA NA WAKOMBOZI WA TAIFA HILI.
MUNGU, BARIKI TANZANIA,BARIKI CHADEMA
Tumeanda kadi ili kuhamia CHADEMA
CCM watukome!


na Mpoki Mwakingwe, Mbeya, - 20.10.08 @ 09:35 | #49007

KIKWETE KATUHARIBIA NCHI.NYERERE ALISHAMWONA HAWEZI KUONGOZA.2005 RAIS ALIPASHWA KUWA SALIM KAMA CCM WANGEKUWA SERIOUS,WAKAMFANYIA MTIMA NYONGO MZEE WA WATU.HAYA SASA.

na ODILLO - 20.10.08 @ 09:37 | #49008


Kuna haja ya kuhakikisha moto huu hauzimiki hadi tuone mabadiliko ya kweli. Wana CCM pia wanatakiwa kuunga mkono juhudi hizi kwani CCM yao siyo ya Nyerere bali ya mafisadi.

Kulaghaiwa kwa kanga na mashati ya kijani sasa basi.

Tanzania mpya isonge mbele

na Deo Mutalemwa, Karagwe, - 20.10.08 @ 09:43 | #49014

ZITTO,MBOWE NA DR.SLAA fanyeni haraka kuja Mbeya!twawasubiri sana.

na Kalosi Mwandosya, Kyela,Tanzania, - 20.10.08 @ 09:44 | #49015

Bigup sana Wabongo,sasa mmeamka kaisi kwamba nashindwa kuamini machoni pangu
MUNGU BARIKI WATANZANIA WENYE UZALENDO NA NCHI YAO NA UWA NGUVU ZOTE ZA MAFISADI(CCM)

na Patric Kingunge, Dar, - 20.10.08 @ 09:52 | #49019

viongozi wachadema shoneni kombati nyingi tu mtupatie vijana, saa ya ukombozi wetu imewadia. tukomboeni na utumwa huu wa ccm, tumechoka kabisa kugeuzwa mbuzi wa kafara.
Tunawangoja kwa hamu kubwa ccm mwaka 2010, ili tuwagalagaze kabisa.

na yohanes paul, Daresalam, - 20.10.08 @ 09:57 | #49022

Katika maoni ya wengi naona wameshauri muende vijijini, ni kweli kabisa maana kuna mikijiji mingine mijitu ni *******,yamechoka na maisha lakini bado yana abudu ccm, kayazibueni mikichwa muwaambie ccm ndio kupe wao

na arnoldinho, arusha, - 20.10.08 @ 10:32 | #49030

ndg zangu wa chadema, hakuna la kuongeza tafadhali tuelezeni hizi kombati zinauzwa maduka gani,tunahitaji kuzivaa na kwenda mstari wa mbele, mimi sina chama na itikadi naweka pembeni nawaunga mkono mia kwa mia tunahitaji kulikomboa taifa, msiende vijijini tu fungueni matawi bora vyuo vikuu ndani na nje ya nchi, tunahitaji kuikomboa hii nchi, msannii anaiangamiza,,jemedadari mdobwedo aliyefyata mkia kwa mafisadi kwa nini asipigwe mawe kama mbwa koko???...nimewasoma nipo bega kwa bega nanyi...toeni tenda kwa wafanyabiashara tupate kombati hizo hatuhitaji za bure..sisi si mafisadi tutalala njaa tuikomboe nchi hii...wale wa CCM piganeni kwa taifa lenu msiangalie itkadi fateni dhana igeni mfano wa Gen. Collin Powell while endorsing Obama...Operation Sangara...Big UP Commando Mbowe, Zitto,John,Slaa

na hondohondo, same, - 20.10.08 @ 11:23 | #49058

Big up sana CHADEMA.
Huu moto mmeuwasha msiuzime, jitahidini muende kila pembe ya nchi ili kuwahabarisha wapiga kura. Saa yaukombozi ni sasa. No retreat No Surrender

na Josef, Vienna, - 20.10.08 @ 11:43 | #49068

mi nashukuru sana mfumo wa vyama vingi fikiria kingekuwa kimoja(ccm) halafu uozo huu.yaani we acha tu

na dzii, ire, - 20.10.08 @ 11:53 | #49072

Shukrani nyingi kwa CHADEMA kwa kutufumbua macho wananchi, asanteni sana sababu sasa nina matumaini ya kuiona Tnzania HURU na yenye kuongozwa na wenye akili sio wachawi.
MUNGU awabariki mpate nguvu zaidi.

kama nilivyosema narudi nyumbani kupigana sababu nimeona mwanga.

na kijijini kwetu sitimbi, Belgium, - 20.10.08 @ 11:58 | #49075

kwanza kabisa nawapongeza viongozi wa CHADEMA komandoo jemedari Mmbowe,dr slaa,zitto,lissu na mnyika kwa mioyo yenu thabiti mliyoionesha ktk kupambana na misukosuko iliyokuwa ikielekezwa kwenu na mafisadi walioamua kukidhoofisha chamachenu ktk mapambano dhidi ya ufisadi.pili tunawapongeza kwa ushindi wenu ktk jimbo la tarime.hii imeonyesha ni jinsi gani wananchi wa tarime walivyo na imani kubwa kwenu.ivyo bac tunawomba mmpite wilaya hadi wilaya ili kuwaelimisha watanzania kujua haki yao.tunawaomba mje kilimanjaro kuchukua hizi kadi za kijani zinatuboa sanaaaaaaaaaaaa.ALUTA CONTINUE

na benny kwayu, Tanzania, - 20.10.08 @ 12:03 | #49080

SALAAM KWA MBOWE/DK SLAA/ZITTO.

PANDENI KWANZA AMBAKO CCM HAIKUBALIKI. NENDENI MBEYA.

na Mkwetu, TZ, - 20.10.08 @ 12:11 | #49086

mosi nianze kwa kuwapongeza wananchi wa tarime na watu wote wa mkoa wa mara hakika mnasitaili kuwa watu wa mkoa alipozaliwa baba wa taifa letu la tanzania.ushindi wa chadema si wenu tu watu wa tarime bali ni wataifa zima la tanzania dhidi ya udhalimu,ukilitimba ubeberu na umafia wa chama tawala,kitendo cha kuihama ccm ni cha kupongezwa na kila mwananchi mwenye mapenzi mema na nchi hii, kwani uwezi kujidai kuwa wewe ni msafi wakati huo uko katikati ya uvundo,kama ningelikua rais kikwete, hakika ningesoma alama za nyakati kwani tulikotoka ni mbali lakini tuendako ni mbali zaidi mhe,chukua hatua nchi inaelekea kukushinda moja ya alama hizo za watu kukuchoka ni pamoja na yale yaliyotokea mbeya.tunza uliyokwisha yafanya uepuke fedhea mbeleni, kwani ushauri wangu kwako usigombee kipindi kingine pumzika uwe mshauri.

na innocent hezekiah, tanzania, - 20.10.08 @ 12:25 | #49090

Natangaza kujiuzulu kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete October 31 endapo hatawafikisha Mahakamani wafuasi wake wa CCM waliomaliza nchi kwa miaka 3 ya utawala wake.Hip hip Hureeeeeeeeee CHADEMA kaza Buti tuko nyuma yenu.Tunataka Kombati za chama jamani msivae wenywewe.Kama safari hawataji Mafisadi tunataka Mandamano ya nchi nzima November 01, 2008.

na OLE LETIPIPI, TANZANIA, - 20.10.08 @ 12:31 | #49093

HAKI HUINUA TAIFA. PASIPO HAKI NCHI HUANGAMIA. SONGENI MBELE HUKU MKIMTANGULIZA MUNGU MSIIGOPE HAO WATISHAO, TUKO PAMOJA.

na GODBETTER, UKONGA , - 20.10.08 @ 12:34 | #49095

Freeman,Zitto na mzee wangu DR. Slaa mwendo mdundo , tupo pamoja wazee kwa gharama yeyote ile mpaka kieleweke.

na kharimu, MTWARA, - 20.10.08 @ 12:35 | #49097

Safi kabisa watoa hoja! Mbeya bado moto haujapoa kwani si mnajua nini kimetokea kule? Mbeya ni eneo hatari na CCM inalitambua hilo, ni eneo ambalo wananchi wamefumbuka macho na masikio kwa kipindi kirefu sasa. Maeneo kama Kilimanjaro, Arusha, Tabora na Kigoma wananchi wake wanaweza kubadilika haraka. Maeneo kama Dododoma, Iringa, Singida na yanayofanana na hayo yataitaji nguvu za ziada hata hivyo ninaamini kwamba hakuna kisichowezekana! The wind of change is all over us and we can feel it, together we can wage a fight for a better life and win! Vamos Muchachos!

na Jojo, Dar, - 20.10.08 @ 12:39 | #49099

Chadema mnafanya kitu nilichokuwa nakifikiria muda mrefu.
Hongereni Sana.

OPERESHENI HII IANZIE VIJIJINI HALAFU IISHIE MIJINI. MAANA VIJIJINI BADO WAKO GIZANI, WANADHANI BADO CCM NI YA MWALIMU NYERERE, CCM YA SASA IMEINGILIWA HAIFAI. HATA BABA WA TAIFA ANGEKUWAPO HAI ASINGEVUMILIA KUWAPO KATIKA CHAMA HIKI, LAZIMA ANGERUDISHA KADI LICHA YA KUWA KADI YAKE NDIYO YA KWANZA KATIKA USAJIRI.

NINA IMANI KUBWA SANA KUWA CHADEMA KINAWEZA KIKATUPA MATUMAINI KATIKA HALI YETU HII YA KUKATA TAMAA.

MAANA MPAKA SASA NAJUA DAR ES SALAAM CHADEMA INA VITI KADHAA VYA UBUNGE, IRINGA.

HALAFU MSISAHAU KWENDA MBEYA KUPATA MIKAKATI MAANA WALE WATU WANAELEWA KUWA SISIEMU ILE YA MWALIMU ILIKUFA PAMOJA NAE, ILIOPO SASA NI MAJITU YASIYO NA SONI.

HATIMAE TUTASHINDA.
BRAVOO!!!



na Nabaki Tanzania, stock/swe, - 20.10.08 @ 12:41 | #49101

the great leader in this world is one who can change the situations that are complex to people as Tanzanians today.HONGERA Sana kamanda MBOWE,ZITO NA SILAA Kwa mkakati mliouanzisha tuko pamoja.we need change in tanzania.

na ngofi complex, tanzania, - 20.10.08 @ 13:01 | #49110

Ndugu zangu Watanzania,ukombozi upo mikononi mwetu CCM walidhani uongo,ukiritimba na ufisadi wao utakuwa siri siku zote!! na lazima tukumbuke " Those who made peaceful revolution impossible,are the one make violence revolution inervitable" Kwa miaka zaidi ya 30 uongozi wa CCM umeonyesha dhahiri bila kificho hautufai na let us send them home!!! Silaha yetu ni karatasi wao wana bunduki na mamluki, basi nasisi tuwambie yatosha, CCM sio chakula ukikosa utakufa na sio mama wala baba yangu hapa duniani.
Watanzania Tarime wameanza na wengine let us continue"" But let us remember we need to devote all enegry of brain,spirit and body kuwaondoa yaani kuwaphaseout CCM and its legacy Tanzania, Wakikupa fedha chukua kwani ni zile zile za EPA na RICHMOND wanazorudisha. Just Imagine Our Government,they need instructions from Capitol Hill to govern us??!! Shameful shameful.
Na dhambi hii itawatafuna tu,no way out.
Tanzania let us continue,let us continue!!! God is walking!!!

na fidelis, Shinyanga,Tanzania, - 20.10.08 @ 14:00 | #49172

Tangu mwanzo niliwaambia kuwa CCM Tarime ni marehemu na kinachobakia ni mazishi tu. Kumbe si Tarime tu, dalili za awali zimeanza kueleza na mkoa wa Mara kwa ujumla, na kwingineko. Wanaume msichoke tupo nyuma yenu. Mumeshudia jinsi wakazi wa Mji huu wa Musoma wana mapenzi makubwa na chama chenu. Mwaka jana aliyekuwa Waziri Mkuu( Lowasa) alipotembelea Musoma kikazi, si zaidi ya watu hamsini walihudhuria kwenye kikao chake kwenye uwanja Abeid Hapa Musoma. Vivas Mbowe.Mapambano yameanza. Nawaagiza,nendeni haraka mbeya baadada ya hapo muelekeo Kagera na Kigoma kwa ajilia ya Operation Sangara, kuna MAVUNO YA KUTOSHA. Kikwete Mjinga sana,anamponda Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa sera zake za ujamaa na kujitegemea, ili aendelea kuwakumbatia mafisadi wake. Tena ukome kuponda sera za mzee wetu, muache apumzike kwa amani. Kama hutaki kumuenzi funga hilo domo, lakini majibu utayapokea hapo 2010.KIDUMU FIKRA ZA MWALIMU NYERERE.

na Mwenyehaki Daima, Musoma., - 20.10.08 @ 14:04 | #49173

Mje Kilimanjaro,hasa Same,hatuoni Dr.Matayo anachofanya hapa,lazima angoke 2010,mama Malechela Kilango ok,lakini huyu mwingine huyu,tunamtafutia mbada wake.

Same iko wazi,CHADEMA.

na Keba, Kilimanjaro, - 20.10.08 @ 14:15 | #49181

Ndio tulipata taabu sana enzi za Mw. Nyerere lakini wote tulikuwa sawa, mafisadi hawakuwepo, wote tuliajiriwa, wote tulisoma bure kwanzia chekechea hadi chuo kikuu hata baadhi yetu hadi ulaya tulikwenda tena bure! tulitibiwa bure, watoto wa shule tulipanda mabasi bila bugdhi! Leo hii JK anasema ukiyafikiria haya utadhani ni wendawazimu!!! Hoja hapa ni haki sawa kwa wote na sio kwa tabaka la watawala tuu.

na Chaves, Dar, - 20.10.08 @ 14:22 | #49184

Komaa Dk.Slaa Zitto na Mbowe, kundi kubwa tuko pamoja na nyinyi.Hata wakati unatoa habari za ufisadi viongozi wengi wa serikalai walijifanya kukanusha na wengine wakajifanya wangekwend mahakamani, lkn hakuna aliyethubutu, maana aibu ilikuwa mbele yao. walingo'oka KANU sembuse ccm! Banda alishang'oka, kaunda alifatia, Mugabe mwenyewe kakalia kuti kavu. lazima ccm wajue ya kuwa "the time is no more on their side" kaza mmwendo kamanda Mbowe

na john, Dar, - 20.10.08 @ 14:50 | #49211

Naomba moto huu ambao chadema wameuwasha tusiruhusu mafisadi wauzime.Pia naomba kwa dhati ya mwenyezi Mungu Watanzania tuumke tuweke itikadi zetu pembeni tupambane kufa na kupona hadi tuwashinde mafisadi.ikibidi hata Rais wetu kwakuwa ameamua kuwalinda tusimuonee haya naye tumwadabishe,hatuhitaji urembo tena.Migomo
inayoendelea tusiache joto hili likapita hivi hivi walimu kazeni msimamo wekeni silha chini hadi kieleweke.Kama mafisadi wanaiba hela wanaachiwa serikali inashindwaje kuwalipa walimu wanaovuja jasho kila siku.Haiwezekani tukaze uzi Tanzania ni yetu sote wala si yao pekee yao.

na john jumanne, Arusha, - 20.10.08 @ 14:57 | #49215

Baada ya hapo rudini DAR haraka mkawaelimishe wazaramo ,wamatumbi na wandengereko kuhusu mabadiliko. Hawa watu ni rahisi sana kununuliwa kwa kanga ,kofia na fulana za CCM . Waige mfano wa tarime

na adili, uk, - 20.10.08 @ 15:23 | #49223

Wachangiaji tupo pamoja, ni muda wa ukombozi.
Ila na wewe muandishi kuwa makini siku nyingine, kama watu waliohudhuria na kuhutubiwa na dr Silaa ni mamia, hao maelfu waliomshangilia Zitto walitoka wapi? Can you be serious??

na mlugaluga, danganyika, - 20.10.08 @ 15:29 | #49225

Kwa hali ilivyo sasa uchaguzi ujao mwakani na ule wa 2010 CCM watakuwa na hali ngumu sana.Kitu cha msingi ni kuendelea kudai tume huru ya uchaguzi. Haiwezekani m/kiti wa tume ya uchaguzi ateuliwe na rais wakati wakati rais naye ni mihongoni mwa wagombea, kwa vyovyote vile lazima atamlinda boss wake.
CHAEMA VEMA.

na Kunenga, Dar tz, - 20.10.08 @ 15:47 | #49229

wazo zuri,chadema inapaswa kuungwa mkono na watanzania wote wapenda maendeleo kwani kampeni hii itawasidia wananchi kujua ufisadi unaofanywa na viongozi walio juu. keep it up mbowe, slaa zito.

na denis, dar, - 20.10.08 @ 15:48 | #49230

kufuata mkondo kama maji watz tunaweza kweli ila come 2010 wengine wetu wanaotoa maoni mazuri kuipinga ccm na raisi wao ndio watakua warahisi kuvaa kofia,tshirt hadi chu.pi za ccm.tusidanganyane kama nafsi inakataa usilazimishe leo kushabikia upinzani ili kesho udefect urudi ilikotoka.say No and mean it instaed of hanging on the fence!!!

na lukas - 20.10.08 @ 16:00 | #49234

KWA HALI HII, HII NCHI TUNAWEZA KUIKOMBOA KWENYE MAKUCHA YA MATHALIMU MAFISADI WALIOITEKA!!! UNAJUA HATA MIJINI WATU WANAHITAJI KUELIMISHWA KWANI LABDA NI UELEWA AU KUTOKUFUATILIA MAMBO!!!
NI RAHISI KUONA MAGAZETI YA MTANZANIA, RAI NA MENGINE YANAYOJIHUSISHA NA MAFISADI NA KUANDIKA HABARI ZA KUFIKIRIKA AMBAZO NI ZA UZUSHI BADO YANANUNULIWA NA WATANZANIA!!! JAMANI HAYO MAGAZETI MNAPOTEZA HELA ZENU KWANI SI YALE YALIYOZOELEKA KWANI KAMPUNI ILISHANUNULIWA NA MAFISADI!!! MSIPOTEZE HELA ZENU BURE WASOMAJI WA MAGAZETI!!!!

na TY, Tanzania, - 20.10.08 @ 16:11 | #49236

Nawapongeza wachangiaji wote kwa maoni yao mazuri. Pongezi kwa Viongozi wa CHADEMA, wantarime na nanyi wananchi wa maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Pamoja na maneno mengi mazuri ya watangulizi, nukuu hii izidi kukumbukwa "Natangaza kujiuzulu kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete October 31 endapo hatawafikisha Mahakamani wafuasi wake wa CCM waliomaliza nchi kwa miaka 3 ya utawala wake" Kombati za chama jamani twazihitaji.. "Kama safari hii hawatajwi Mafisadi, basi tunataka Mandamano ya nchi nzima November 01, 2008" Nina imani CHADEMA itakuwa imejipanga vizuri kufikisha Mpango huu 'Operesheni SANGARA'kwa wananchi wote TZ. Hakika tieni bidii operation hii ifike hadi vijijini.
Angalizo; Mafisadi wanaweza kuibuka na kutaka kutibua mpango huu, kamwe wasithubutu na endapo watafanya hivyo basi walipuliwe kwa kasi ya kutisha .....wakome!
Juhudi hizi ni chachu muhimu na zinahitaji watu tujitoe, tulipofika hivi sasa kila mwenye akili ya kugh'amua mambo anajua nani kapunguza upepo katika tairi. Wanachi wote nawaomba tuache mbali itikadi zetu za kichama, kulindana na kulinda chama, mbadala tuweke mbele utaifa wetu. Mapinduzi yoyote yale yanagharama yake. Mungu wang'amue macho raia wako watanzania. Amina.
 
Ama kweli sisiemu safari hii mna kazi kweli kweli.
Angalia mwisho wenu hauko mbali. Endeleeni kuota ndoto za mchana.
 
Siwezi kutegemea Makamba kubuni mkakati kama huu au hata kukopi na kupesti. He's too old and corrupt!!!!!!!!!Mimi nasifu ubunifu wa mikakati na mbinu za utekelezaji wa Operesheni Sangara
 
na Kulwa Karedia, Musoma



KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema anao ushahidi unaoonyesha kuwapo kwa makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanayojipanga kumzuia Rais Jakaya Kikwete kupitishwa tena na chama hicho kugombea urais kwa kipindi cha pili mwaka 2010.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo nzito inayoweza kuibua mjadala mzito wa hoja wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Kigera, Musoma mjini, ambako viongozi wakuu wa CHADEMA wako huko wakiendesha kile walichokipachika jina la ‘Operesheni Sangara.’

Bila ya kuyataja makundi hayo, Dk. Slaa, mmoja wa viongozi wa upinzani ambao wamekuwa mstari wa mbele kukabiliana na ufisadi ndani ya serikali, alisema mipango hiyo ya siri inatokana na kuwapo kwa mambo ambayo hayaridhishi serikalini.

“Nina ushahidi tosha wa kuwepo kwa njama hizo ndani ya CCM kwamba kuna makundi yaliyokusudia kutopitisha tena jina lake (Rais Kikwete) mwaka 2010 kuwania urais kwa kipindi cha pili,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kutokana na ukweli huo basi, serikali na hususan Waziri wa Habari, Utamaduni na Maendeleo ya Michezo, hakuwa na sababu za kulifungia gazeti la MwanaHALISI kwa miezi mitatu, kwa kuandika habari iliyoelezea kuhusu kuwapo kwa mpango huo dhidi ya Rais Kikwete.

Alisema hali hiyo ni sababu tosha inayomwezesha Rais Kikwete kuchukua hatua za kumfukuza kazi waziri huyo ambaye alichukua hatua kali dhidi ya gazeti ambalo liliandika habari aliyodai ni ya kweli.

Kauli hiyo ya Slaa imekuja siku chache tu baada ya serikali kupitia wasemaji mbalimbali, kulishutumu MwanaHALISI kwa kuandika habari ambayo ilidaiwa kutokuwa na ukweli.

Pamoja na serikali kutoa tamko la kuikanusha habari hiyo, taarifa kama hiyo ya MwanaHALISI iliyokuwa ikizungumzia kuwapo kwa mpango wa kumzuia Kikwete kugombea tena urais mwaka 2010 ilipata kuandikwa na gazeti la kila wiki la Rai, Aprili mwaka huu.

Katika gazeti hilo la Rai, iliandikwa kwamba, waziri mmoja katika serikali ya Kikwete ambaye alichukua fomu za kutaka kugombea urais ndani ya CCM mwaka 2005, alikuwa ameshajaribu kujenga kundi ambalo lina nia ya kumsimamisha yeye (waziri huyo) kugombea urais kupitia chama hicho tawala.

Katika hatua nyingine, akizungumza jana katika mkutano huo, Dk. Slaa alisema alikuwa amenasa taarifa zilizokuwa zikionyesha kuwapo kwa mpango wa CCM kujaribu kuwanunua viongozi kadhaa wa kambi ya upinzani wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani uliofanyika Tarime hivi karibuni.

“Nimefanikiwa kupata nyaraka zilizosainiwa na Makamba (Katibu Mkuu wa CCM) ambazo zililenga kuwanunua viongozi wa vyama vya siasa katika uchaguzi mdogo kule Tarime... hili tunalifanyia kazi haraka,” alisema Slaa.

Hata hivyo wakati Slaa akitoa madai hayo, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Makamba alikuwa ni kiongozi wa juu wa kwanza wa CCM kuipongeza CHADEMA kwa kushinda ubunge na udiwani Tarime.

Mbali ya hayo, Dk. Slaa alieleza masikitiko ya CHADEMA kutokana na kile alichokieleza kuwa kitendo cha serikali kusitisha misaada katika Kata ya Kigera, eneo hilo la Musoma, kwa sababu tu inaongozwa na diwani wa chama cha upinzani.

Alisema kwa mfano mwaka 2006 serikali ilitenga zaidi ya sh milioni 14 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kwangwa, lakini ujenzi wake ulisitishwa ukiwa katika hatua ya mwanzo na kusababisha usumbufu kwa watoto kukosa elimu.

Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA alisema ni ajabu kwamba baadhi ya viongozi ambao wanapaswa kuwajibika kwa wananchi wamegeuka miungu watu.

Akiwa katika kata hiyo, Dk. Slaa alizinduwa tawi jipya la Bondeni, ambalo lilikuwa chini ya himaya ya CCM, ambako viongozi wake wote wamejiunga na CHADEMA.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Wilaya (UVCCM), Charles Maera, alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona CCM imepoteza dira ya kuwaletea maendeleo.

Katika eneo hilo, zaidi ya wanachama 100 wa CCM walirudisha kadi za uanachama na bendera ya chama hicho tawala na wakajiunga na CHADEMA, ikiwa ni kuunga mkono kile walichokieleza kuwa ni vuguvugu la mageuzi ya kweli.

Mbali ya Dk. Slaa, viongozi wengine wa CHADEMA waliopo katika ‘Operesheni Sangara’ mkoani Mara ambao jana walikuwa wametawanyika katika kata 13 za Musoma na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, wabunge Said Arfi, Lucy Owenya na Mhonga Said.
 
Haya ni baadhi ya maoni ya watu walio changia hii habari.
Na bado! CHADEMA wamewashika sehemu mbaya sana CCM.

Sasa tunashuhudia CCM ikijimaliza yenyewe. Hongera JK kwa kuwa mzalendo wa kwanza kuiangamiza CCM.

Sura na tabasamu lako ndani ya ngozi ya kondoo linakimaliza chama.

na cosmas - 21.10.08 @ 09:01 | #49407

maoni yangu ni kumwomba rais kikwete achukue tahadhari juu ya tuhuma hizo za kuwepo kwa makundi ndani ya chama chake, akipuuza atakuja kuwapigia magoti kubenea na dr slaa.
ni kweli kundi hilo lipo.kwa kuwa rais anakuwa neutral, anauma huku kwa wananchi na kwa mafisadi ili asionekane mbaya kumbe ndo anaharibu mambo.tabia yake ya kusema hadharani nitashughulikia mafisadi huku akiwakumbatia ndo chanzo cha kuwaboa wenzake hao hadi kuamua kuanzisha mtandao wao ili kumtoa 2010

na janeth, mbeya, - 21.10.08 @ 09:12 | #49410

nasikitika sana waziri wa habari badala ya jushukuru kupewa taarifa tata za gazeti la mwanahalisi azifanyie kazi na kushukuru kwa onyo hilo yeye kakurupuka na kufungia gazeti sasa je, atapata wapi tena taarifa yeye ilikuwa kupokea kuchuja fanyia kazi.
Kwamtaji huu hatutafika nchi ya AHADI.
tupunguze pupakufanya kazi na kutumia madaraka kwa akili kuliko nguvu

na mtemi, tanzania, - 21.10.08 @ 09:42 | #49419

"ukiona chama kinakimbiwa na vijana basi ujue hiyo ni dalili tosha kuwa chama hicho kinakufa" Mwl. JULIAS KAMBARAGE NYERERE.

na mkongwe, tz, - 21.10.08 @ 09:47 | #49423

"Ukiingiia kwa mtandao utatoka kwa mtandao" hayo ndiyo yanamla kwikete Mwalimu alisema "Dhambi ya ubaguzi huwa haiishi kabisaaa" Na itakutafuna sana mkuu wangu kikwete.

na SPC Zoooo!, Tanzania, - 21.10.08 @ 09:53 | #49424

Hilo ndilo tatizo la kuwa na mtoto wa mgogongoni na mtoto wa tumboni.Ukishakuwa
na ubaguzi hata ndani kwako kama Baba wa familia umekwisha na heshima yako inashuka.Hayo ndiyo yanayompata ndugu JK sasa hivi.Ukifuatilia sana hata watupa Mawe Mbeya ni wana CCM.Hakuna mtu wa chama cha upinzani mwenye akili finyu kama hizo.CCM walizoezeshwa pesa kila mahali anapokuja kiongozi.Walitegemea JK amekuja na mshiko mbeya kumbe sera za mshiko zimefilisi nchi. JK hakuwa na mshiko wa kubeba ila kuja kutangaza vita dhidi ya mauaji ya Alibino.Mtanzania yeyote mwenye mapenzi mema na nchi hii anatakiwa akiogope chama cha CCM kama Ukoma.

na OLE LETIPIPI, TANZANIA, - 21.10.08 @ 10:06 | #49435

Cosmas nimmekusoma. Sasa nakubaliana na maaskofu waliosema Jk ni "CHAGUO LA MUNGU" Maana "anaiongoza" nchi kwenye mageuzi. Hongera JK.

na mlugaluga, danganyika, - 21.10.08 @ 10:12 | #49439

Mimi nataka kila nikisikia wapinzani wanaonge,ningependa waongee ni kwa jinsi gani wanajipanga,ni kwa jinsi gani wanawaeleza wananchi wa vijijini umuhimu wa kuchukua hatua,umuhimu wa kujiandaa na mapinduzi mapaya ndani ya boksi la kupigia kura,nataka nisikie wakienda vijijini,wakiwaeleza ni kwa jinsi gani chama tawala kimehalalisha maisha magumu wa watu wote,sitaki kusikia wakiwaeleza wananchi migogoro ndani ya CCM,so what?,nataka waende moja kwa moja kwenye hitimisho,wananchi wanataka wasikie nyinyi mtawafanyia nini zaidi ya unyanyasaji na wizi wa hazina yetu.

Nisingependa kabisa wapoteze mda kujadili migogoro ndani ya chama cha mafisadi,kwa mwananchi wa kawaida haoni connection zaidi ya kuona mchanganyiko wa ideas.Narudia CHADEMA chonde chonde inabidi mtafute political strategiest watakaowapa muongozo mfanye nini,muongee nini,kwa kiasi gani,na sio kujiongelea tuuu ili mradi ndio hoja iliyopo.be serious,be specific,be strategic,be proactive while CCM are still sleeping.wacha magazeti yaandike mgongano yanawasaidia,nyie gonga angle nyingine inayoyagusa maisha ya kawaida ya wanaowasikiliza.msirudierudie ya magazeti si wamekwishasema,semeni,zungumzeni ambayo magazeti hayajasema hasa yale mambo ya kawaida ya kimaisha.

na romwald, USA, - 21.10.08 @ 10:15 | #49440

Ingelikuwa mafisadi wameshughulikiwa kama gazeti la mwanahalisi nchi ingelikuwa mbali sana.Ndani ya wiki moja gazeti lishafungiwa lakini mafisadi miaka mingapi sasa hakuna moja lililofanywa isipokuwa kudanganywa tu

na kiroboto, kiwengwa, - 21.10.08 @ 10:18 | #49442
 
na Kulwa Karedia, Musoma

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema anao ushahidi unaoonyesha kuwapo kwa makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanayojipanga kumzuia Rais Jakaya Kikwete kupitishwa tena na chama hicho kugombea urais kwa kipindi cha pili mwaka 2010.

Dr. Slaa anaelekea kwenye siasa za Mtikila za kulipua mabomu hata pale pasipo na hayo mabomu.

Ushahidi alio nao ni wa aina gani, kideo, audio record, barua au ni wa aina gani? Natumaini hatasema kuwa mke wake ndiye aliyemtonya.
 
Hiyo ishu ipo wala sisiemu hawahitaji kutumia nguvu nyingi kuizima kama vile kufungia magazeti.

Kwa wasio amini wasubiri siku siyo nyingi wataona sisiemu itakavyoanza kugawanyika.Kilichitokea Mbeya na kwingineko ni dalili tosha za sisiemu kupoteza nguvu na mwelekeo.

Wengine tunajua kila kitu na kinavyopangwa na hao watakaomgeuka mzee hivi karibuni.

Hata hivyo ieleweke kuwa hao watakaompinga Kikwete watafanya hivyo kwa kuwa ni haki yao kikatiba ingawa sisiemu itawaona kama wasaliti.

Mkakati huu umeshaanza na fuatilia chaguzi za viongozi wa jumuiya za sisiemu (wazazi, vijan na wanawake) utagundua jambo.
 
Sisi kama Watanzania wenye 'muamko' tunafurahi kuona kwamba CHADEMA japo wanajitahidi 'kuwakosoa' CCM. Lakini je? Ingekuwa wao wangefanya nini juu ya matatizo yanayokabili nchi? na kwamba wakija kushika nchi hawatakuwa na 'njaa' kama viongozi wetu wa sasa? Ningependa viongozi wa CHADEMA wawe wanatupa analysis na solutions juu ya matatizo yanayotukabili Watanzania kwa ujumla na sio kukaa tu na kuikosoa CCM....mnaonekana kama vile ni 'washika mkia' wa CCM, acheni kushika mkia na pandeni farasi wenu ili mshindane nao....kwa njia ya kuwaeleza Watanzania juu ya mbinu zenu za kuendeleza nchi!
 
Back
Top Bottom