Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,130
8,330
Nakumbuka mwanzoni kwa mwaka huu nilikua kituo Cha mafuta fulani nikijaza mafuta...wakati natoka akatokea kijana mtanashati akanisimamisha akanambia.

'Bro samahani kwa kukusumbua mmepata breakdown kidogo gari yangu imeisha mafuta na Sina Ela maana nilikua nmepaki Kariakoo wezi wamevunja gari kioo, wameiba kila kitu. Sina ata simu. Naomba unipe elfu tano ili ninunue petrol

Kwakuwa na mm nilikua na haraka sikuwa na elfu tano nilikua na teni..nikampa Hilo ten nikasepa.

Sasa Leo nipo hapo hapo sheli aka petrol station, huyo jamaa akanifuata, kwakuwa alikua amesahau akaleta stori hizo hizo..mm nikamwambia mbona kama nakujua.

Kuna siku ulinipigia stori hizo hizo hapa hapa nikakupa 10, vip na Leo unaleta the same story.

Jamaa akanishituki akapanda mkweche wake akasepa na sikuona kioo kilichovunjika maana alifunga vipo vyote. So it means kuna ombaomba siku hzi wanaomba wakiwa mwenye magari yao.
 
Ungempigia makelele ya mwizi apewe adabu mpuzi sana huyo....maana bila hivyo ataendelea kutapeli, ila pia kama vipi isimulie kwa vituo vya habari kama vile Wasafi ili tahadhari itolewe kwa umma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom