Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,772
- 730,048
Kuna maswali mengi muhimu ya kujiuliza kwenye hii biashara ya vituo vya nafuta mpaka inakimbiliwa na karibia kila mfanyabiashara?
Je magari yameongezeka sana nchini?
Je kumekuwa na urahisi wa upatikanaji wa bidhaa husika?
Je ni njia ya utakatishaji pesa na biashara haramu
Je kuna 'syndicate' ya mafuta ya mchongo?
Je kwanini vituo vingi vinavyoibuka ni kampuni mpyampya ngeni na sio zile kampuni kongwe kwenye tasnia nzima ya mafuta ?
Je taratibu zimerahisishwa kwenye kupata vibali vya ujenzi na uendeshaji wa vituo vya mafuta?
Hii ni mada ndefu itakayoangazia mambo mengi hivyo nitaomba uvumilivu wa wasomaji
1. Aina ya mafuta tuliyonayo Tanzania kama nishati ya kuendeshea vyombo vya moto vya usafiri wa barabarani, majini na angani pamoja na mitambo mbalimbali
Tunazo aina kuu mbili
Diesel na petrol na sasa tuna nyongeza ya gas ambayo bado haijawa maarufu sana..
Lakini vilevile kuna mafuta mengine yanayotokana na vyanzo vingine vya malighafi kama I.D.O. (Industrial Diesel Oil)
Sisi kama Taifa bado hatuna mafuta yetu pamoja na kusemekana kwamba tuna hifadhi ya kutosha sana ambayo inahitajika kuchimbwa. Hivyo kwa asilimia 100 mafuta yetu ni ya kuagizwa toka nje ya nchi
Kuna utaratibu wa kuagizwa kwa pamoja na kuna utaratibu wa makampuni makubwa ya mafuta kuagiza yenyewe.. Sina hakika kwasasa ni mfumo upi unatumika..
Kutokana na ukubwa na unyeti wa hii bidhaa serikali imeunda chombo maalum cha kushughulika nayo kuanzia
Kuagiza
Kuhifadhi
Kusambaza
Sera na mikakati yake
Sekta ya ujenzi wa miundombinu inakuwa kwa kasi hivyo kuvutia uwekezaji mpana wa sekta ya mafuta kutokana na mahitaji kuongezeka sana
Labda niseme ni hapa kwenye kuagiza/kusambaza, taasisi inayohusika na mahitaji kuongezeka ndio kumechangia ongezeko kubwa la ujenzi wa vituo hivi
2. Uzoefu kwenye biashara
Kutokana na mahitaji kuongezeka tungetegemea makampuni, taasisi na wadau wenye uzoefu na biashara hii wewe wa kwanza na wa mbele kwenye kupanua Soko
Kinachotatiza hapa ni sura ngeni kwenye sekta ndio zinahusika na mfumuko wa vituo hivi.. Kwanini wakongwe na wazoefu wana vituo vichache sana kulingana na wageni?
Ukweli ni kwamba wazoefu wa hii bidhaa na hii biashara wanajua kwa hakika gharama ya kujenga kituo kimoja chenye viwango stahiki vya kimataifa.. Kujenga kituo kimoja inahitajika ujipange hasa
Mtaji
Eneo la ujenzi kijiografia
Aina ya matank ya kuhifadhia mafuta
Upatikanaji wa mafuta safi, bora na salama..
Mtaji mkubwa huingia kwenye matank yanayozikwa ardhini, ujenzi wake mifumo na miundombinu mpaka mafuta kufika kwenye pump
Licha la kuchagua eneo zuri kibiashara lakini suala la kijiografia kwa maana ya udongo ni muhimu sana..
Hapafai mahali penye chemchem kwa chini ya ardhi
Hapafai mahali penye kiwango kikubwa cha chumvi na tindikali.. Hivi ni adui mkubwa kwenye chuma cha tank linalozikwa ardhini
Ripoti ya mjiolojia aliyethibitishwa na mamlaka huwa ni muhimu sana..
Nitaendelea sehemu ya pili
Naendelea
Je kuna mafuta ya mchongo?
Hili ni hakika kwakuwa walishakamatwa watu wametoboa bomba la mafuta na kujiunganishia mpaka kwenye makazi yao.
Wengine ni wezi wa mafuta ya yanayoenda nje ya nchi (transit) lakini vilevile ni dili za hayo hayo mafuta ya transit kuishia hapa hapa nchini wakati inaonesha yanasafirishwa nje ya nchi.. Hii inafanyikaje?
Gari ikishapakia mzigo depo na kupata nyaraka kuna mtu huondoka na nyaraka kwa bus mpaka mpakani (mpaka husika) na kugongewa mihuri kwamba mafuta yameshatoka nchini.. Baada ya hapo gari husika ya mafuta huishia yard zilizoko nyuma ya vituo vya mafuta na kuuzwa taratibu kupitia mobile tanks.. Hii ni biashara kubwa sana
Mobile tanks hizo maranyingi hubeba mafuta chini ya lita 5000 na kuzisambaza kwenye vituo vyenye uhitaji kwa mali kauli ama mkopo
Je kuna uchakachuaji kwenye mafuta?
Uchakachuaji upo tena sana.. Siku hizi si kupitia mafutataa tena bali ni kupitia I.D.O na condenset( mabaki toka kwenye gesi asilia.. Usipokuwa mjuzi unaweza kudhani condensate ni diesel
Kuhusu I.D.O mwaka juzi kule Kisarawe Mvuti nadhani kuna mchina alikamatwa akichakachua I.D.O na diesel
Naemdelea