Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Oman wanazungumza Kiswahili pia?

CCM Zanzibar wanafiki sana- Balozi mkaazi amesifia uhusiano mzuri kati ya Zanzibar na Oman. Fast forward election time, lugha inabadilika- CUF inataka kurudisha usultani Zanzibar, oh makombo ya sultan hameni nchi!
 
Muungano ukivunjika Zenji itakuwa kama Dubai, tumeishikilia Zenji kuiendeleza hatutaki nin sasa hiki

Wakipewa nchi yao huku bara mtaenda kuomba msaada huko Zanzibar
Tuwaoneshe mlango wa kutokea
 
Ni kweli kwa Kiswahili kinachotumika Pwani ya East Africa (Tanganyika, Zanzibar, Mombasa nk) lakini si kweli kwa Kiswahili cha DRC, cha DRC labda kila only 10%ya Kiarabu, lakini Asilimia kubwa ni Kibantu kisha Kifaransa
asali inaitwa uki kule congo. wanahesabu makumi kenda ni tisini.Masasi ni risasi
 
Oman na Zanzibar kama Israel ndani ya USA
We haushangia kila siku wanadai uhuru wao
 
Hicho cha Congo sijui ila maana ya sawahili ni pwani kwa kiarabu so hicho cha Congo sio kiswahili ni kama tuseme kigiriyama ni kiswahili wakati si kweli maana ukiwasikia wana ongea maneno mengi ni ya kiswahili
kuna lugha moja ipo Kenya wanachanganya maneno ya kiswahili na kiingereza.Iko redio moja inasikikia sana mkoani Kilimanjaro inarusha matangazo yao toka Kenya.Lugha haieleweki ni kiswahili au kiingereza.Kuna maneno pia ya lugha za katikati ya Tanzania.
 
Nimekuquote kwa sababu uliniquote sehemu ulitaka kuona tofauti ya lugha hizo

Siku zote mi huwa najua vizuri sana, mtoto wa Kiislam hawezi kukubali kuwa Kiswahili sio Kiarabu, ndugu yangu kujua kiswahili sio kupitia Chuo, kwa taarifa yako wako wengi waliozaliwa sehemu ya Waswahili na wala sio Waislam na wanakijua Kiswahili vizuri tu

Ngoja nikufahamishe kitu
Lugha hii inayoitwa Kiswahili ilikuwepo kwa Karne na Karne ikiitwa KINGOZI , na Wafanyabiashara wa zamani waliokuwa wakitoka Congo kuleta mizigo Pwani walikuwa wakiongea hiyo lugha, na Mizigo iliyokuwa ikifika pwani ilisafirishwa kwenda Uarabuni na hao Wabantu,

Waarabu walipofika hapa Tanganyika waliwakuta watu wa eneo lote la Pwani ya Tanganyika, Kenya wakiongea hiyo lugha na ndio wakaiita lugha ya watu wa Pwani,
Na Waarabu walioanza kufuata njia ya Wafanya biashara ya kwenda Congo, waliwakuta watu njiani wakiongea hiyo Lugha Hiyohiyo (maeneo kama Bagamoyo, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Kahama, Kigoma mpaka DRC) Usifikiri Waarabu ndio waliovumbua hiyo njia, hiyo njia ilikiwepo miaka na miaka na Waarabu waliifata tu wakiongozwa na Wafanya biashara wa Kibantu

Baada ya Wafanyabiashara wa Kiarabu kudominate hiyo njia taratibu wakaanza kuingiza maneno yao ya kiarabu na yakawa comon kwenye hicho KINGOZI, na kwa sababu walikaa muda mrefu athari yao kwenye hiyo lugha ni kubwa zaidi, mfano waarabu waliwakuta WANGOZI wanajua kuhesabu vizuri tu na wao Waarabu wakaongeza au kubadirisha matamshi ya namba tatu katika mtiririko wa kuhesabu mfano moja, mbili, tatu, nne, tano, "nane na kumi vyote ni Kibantu lakini Sita, Saba na Tisa ni Kiarabu, so sio kama hiyo Lugha walioikuta haina hizo namba, bali wao waarabu walizitumia sana hizo namba tatu kwa lugha yao na ndio zikatoholewa kuwa lugha rasmi, lakini mpaka leo ukisema Kenda watu wanajua ni Tisa

Pia kuna Maneno ya kutoka Persia yaliyoletwa na wachuhuzi wa kutoka huko, maneno kama chai, achari=pickle, Serikali, Diwani, Sheha nk,
kuna maneno pia ya KiPortuguese pia yapo ndani ya Kiswahili mfano leso" (handkerchief), "meza" (table), "gereza" (prison), "pesa" ('peso', money), nk.
Pia yapo maneno mengi tu ya Kiingereza, Kijerumani nk, japokuwa maneno hayo yameingizwa kwenye Kiswahili lakini sio kweli kwamba tulikuwa hatuna maneno ya Kiswahili yenye maana hizo, maneno machache sana ya Kisayansi na kitechnolojia ndio huwezi kuyakuta kwenye KINGOZI
Hapa umefanya nijiridhishe kwann kiswahi "halisi" cha kina oni sigala ni kigumu vile....

Naendelea kukufatilia.
 
kuna lugha moja ipo Kenya wanachanganya maneno ya kiswahili na kiingereza.Iko redio moja inasikikia sana mkoani Kilimanjaro inarusha matangazo yao toka Kenya.Lugha haieleweki ni kiswahili au kiingereza.Kuna maneno pia ya lugha za katikati ya Tanzania.

Hiyo sijui ni lugha gani au ni sheng? Maana wakenya kwa kuchanganya lugha kiswahili, kiingereza Mara Kikuyu, Mara kiluo.
 
Asiyetaka Muungano atoke yeye atuachie Zanzibar (kwa maana ya ardhi)
Na wakileta mchezo hata hiyo Omani tutaifanya kuwa sehemu ya Jamuhuri ya Muungano
Iwe sehemu ya jamhuri wakati kila uchao unawaomba?
 
asali inaitwa uki kule congo. wanahesabu makumi kenda ni tisini.Masasi ni risasi

Kweli kabisa kaka, na ndio maana nasema ukiwa Congo na ukaongea Kiswahili cha huku Kwetu wanapata shida sana kukuelewa, lakini wao wakiongea utawaelewa tu, japo pia unaweza pata shida kwenye maneno yenye asili ya Kifaransa
 
Hi
Kiswahini ni kiarabu
Hiyo ni nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni Kiarabu kama zilivyo nadharia nyingine NNE zilizobaki.

Ukweli ni kwamba utawala wa Oman tangu sultani wa kwanza hadi wa mwisho ulijikita katika matumizi ya lugha ya wenyeji ambayo ni Kiswahili. Kumbuka wakati Waarabu walipokuja Zanzibar walikuta wenyeji wa huko wakizungumza Kiswahili na sio kwamba wao(Waarabu) ndio walikuja na Kiswahili.

Kutokana na muingiliano wa muda mrefu baina ya wageni na wenyeji hasa wakati wa biashara ya utumwa ambapo watumwa wengi walipelekwa huko Oman na baada ya biashara hiyo kupigwa marufuku watumwa wengi ambao ni Waswahili walibaki huko huko.

Pia lazima ijulikane kwamba Oman ni taifa ambalo Watanzania wengi hususan kutoka Zanzibar pengine kutokana na suala la dini wanaishi
 
show them the way to quit if they do not to stick at united

Hakuna muungano unaolindwa Kwa nguvu zote .Huo unaolindwa Kwa maguvu ni Uvamizi.Na huu ndio tulionao.Ukweli hakuna Mzanzibari anayeutaka uvamizi huu
 
Hi

Hiyo ni nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni Kiarabu kama zilivyo nadharia nyingine NNE zilizobaki.

Ukweli ni kwamba utawala wa Oman tangu sultani wa kwanza hadi wa mwisho ulijikita katika matumizi ya lugha ya wenyeji ambayo ni Kiswahili. Kumbuka wakati Waarabu walipokuja Zanzibar walikuta wenyeji wa huko wakizungumza Kiswahili na sio kwamba wao(Waarabu) ndio walikuja na Kiswahili.

Kutokana na muingiliano wa muda mrefu baina ya wageni na wenyeji hasa wakati wa biashara ya utumwa ambapo watumwa wengi walipelekwa huko Oman na baada ya biashara hiyo kupigwa marufuku watumwa wengi ambao ni Waswahili walibaki huko huko.

Pia lazima ijulikane kwamba Oman ni taifa ambalo Watanzania wengi hususan kutoka Zanzibar pengine kutokana na suala la dini wanaishi

Oman hakuna binadamu hata mmoja aliyepelekwa huko Kwa sababu ya Utumwa. Wanunuzi wa watumwa walikuwa ni makanisa ya wazungu.Na katika kuziba historia Kwa kujifanya kujenga makanisa zile sehemu zilizokuwa na masoko. Amka kijana
 
Back
Top Bottom