Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Oman wanazungumza Kiswahili pia?

wazanzibar ni wale wale wa Oman kwani jeuri ya kuvunja MUUNGANO unadhani wanaitoa wapi.. na wakijitoa leo kwenye Muungano wanatuacha kiuchumi haki ya Mungu
Watatuacha vipi tupe sababu. Maana oman pia ku watu wamechoka. . Tuanzie hapo
 
Kiswahili sio kimoja kaka, Ni kama kiingereza tu, Uk wana Chao, USA wana chao, Jamaica wana Chao, Nigeria wana Chao,

Shelisheli wana Kiswahili chao, kuna sehemu ya Madagascar pia wana chao, Kenya Nairobi na Mombasa kuna tofauti, DRC wana chao, tembea uone kaka, acha kubisha uko nyuma ya QWERTY

Jamaica na Nigeria hawaongei English...Jamaica wana PATOIS na Nigeria Pidgen....ni kiingereza kibovu kilichochanganywa na maneno yao lakini hakitambuliki mashuleni ila mtaani tu. Shuleni wanatumia kiingereza fasaha cha Uingereza.
 
Wapo wengi Sana wazanzibari wenye uraia wa Oman. Wana wajomba kaka Dada nk jeshi la Oman wako hadi maafisa wakubwa wa jeshi wanaoongea kiswahili fasaha kabisa. Mfalme wa Oman Ana nduguze kibao Zanzibar pia hivyo kuna mwingiliano mkubwa wa Oman na Zanzibar
Zaidi ni Tanzania bara,ndio ina idadi kubwa sana ya watu wenye asili ya Oman.Kuanzia Bagamoyo,Tanga,Dar,Mtwara,Tabora,Shinyanga,Mwanza,Sumbawanga nk.
 
Sio 98%, na ujue Kiswahili kinatofauti na eneo na eneo, ukikisikia kiswahili cha DRC hakina kabisa maneno ya Kiarabu na kama yapo ni kachachesana, kiswahili chao kimejaa Kibantu na maneno ya kifaransa
Neno Swahili,ni neno la kiarabu,linatamkwa Sahel(kwa maana ya Pwani.Kiswahili no cha pwani tu,kama jina la lugha hiyo ilivyoitwa na waarabu,kiswahili,yaani lugha ya Pwani,hivyo vingine vinavyoitwa kiswahili,ni kuongeza tu,kisichokuwamo,kikatiwa katika mahali sipo.
 
Zaidi ni Tanzania bara,ndio ina idadi kubwa sana ya watu wenye asili ya Oman.Kuanzia Bagamoyo,Tanga,Dar,Mtwara,Tabora,Shinyanga,Mwanza,Sumbawanga nk.
Asante mkuu Nilikuwa sijui hili sababu niliwahi kaa Zanzibar miezi minne nilikutana na raia wa Oman mahotelni Wanaoongea kiswahili barabara nikajua ni wazanzibari tu Asante kwa clarification
 
Kama umesoma historia ya uhusiano wa Oman na Zanzibar hilo la kawaida sana. Wazanzibar wana nasaba kubwa sana na Waoman.
Idadi kubwa ya wenye asili ya Oman,waliishi Tanganyika(Tanzania bara).Kuanzia Mtwara,Tanga,Tabora,Shinyanga,Mwanza,Sumbawanga,nk.Na mpaka leo vizazi vya hao watu wapo,japo wengi wemchanganyika na makabila ya asili kwa kuoana.
 
Zaidi ni Tanzania bara,ndio ina idadi kubwa sana ya watu wenye asili ya Oman.Kuanzia Bagamoyo,Tanga,Dar,Mtwara,Tabora,Shinyanga,Mwanza,Sumbawanga nk.
Shinyanga nilikaa ni kweli kuna waarabu wasukuma wenye asili ya Oman. Wanaongea kisukuma na kiswahiili hacha tu wako kibao shinyanga wengi wako maganzo nk
 
Asiyetaka Muungano atoke yeye atuachie Zanzibar (kwa maana ya ardhi)
Na wakileta mchezo hata hiyo Omani tutaifanya kuwa sehemu ya Jamuhuri ya Muungano
Hili la kutanuwa muungano wetu hadi Oman lipo vizuri sana, yaani mtu unatinga Muscat na kitambulisho cha kupigia kura tu. Tumuuzie mfalme wa Oman hili wazo.
 
Ndio hivyo wanazungumza..kiswahili kina uwanda mpana sana wa uzungumzaji
 
Hili la kutanuwa muungano wetu hadi Oman lipo vizuri sana, yaani mtu unatinga Muscat na kitambulisho cha kupigia kura tu. Tumuuzie mfalme wa Oman hili wazo.
Tatizo watanganyika ustaarabu zero, Zanzibar washakuchokeni mtaweza Oman?
 
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili
Zanzibar koloni lao. Ukitaka kwenda oman kwa wepesi waambie ww ni mzinzabar. Ni Kama Mayotte kwa ufaransa
 
We ushamba umeacha lini?, hivi hata hujui Kiswahili kilivyogawanyika?, Kiswahili kina matabaka kaka, ngoja basi nikufahamishe na uelewe tofauti ya kiswahili cha Tanzania na Kikongo
Cha Tanzania kina mchanganyiko wa Kiarabu, Kibantu, Kiingereza nk, Lakini kiuhalisia maneno Mengi ya Kiarabu yana Kibantu chake, kwa sisi huku Tanzania maneno ya kiarabu bado mengi yanasimama kwenye lugha yetu, lakini kwa Congo maneno almost yote ya Kiarabu hayatumiki na mbadala wake wanatumia maneno ya Kibantu na Kifaransa,
Sasa basi kwa Mkongo akiongea Kiswahili cha kwao kwa sisi Watanzania tunaelewa anachokiongea, lakini sisi tukiongea Kiswahili chetu chenye Kiarabu wanapata shida san kujua tunachoongea
Na hata Congo yenyewe Kiswahili pia kina tofauti, East Congo angalau tunaweza kuongea vizuri, lakini Katanga ni shida kabisa, na Kinshansa almost hakuna Kiswahili

Acha ushamba wewe
Ili kumaliza utata kwetu tunaofuatilia uzi huu, hebu tuwekee paragraph moja ya kiingereza cha UK na nyingine ya kinaijeria na zote zikiwa na ujumbe mmoja.
 
wazanzibar ni wale wale wa Oman kwani jeuri ya kuvunja MUUNGANO unadhani wanaitoa wapi.. na wakijitoa leo kwenye Muungano wanatuacha kiuchumi haki ya Mungu
Kwani wakituacha kiuchumi kuna tatizo gani?? Tumeachwa kiuchumi na nchi ngapi ???
Acha fikra za kimaskini nyie ndo wale mnaomsifia magu ' eti sasa hivi tunaheshimiana mtaani'
 
Jamaica na Nigeria hawaongei English...Jamaica wana PATOIS na Nigeria Pidgen....ni kiingereza kibovu kilichochanganywa na maneno yao lakini hakitambuliki mashuleni ila mtaani tu. Shuleni wanatumia kiingereza fasaha cha Uingereza.

We huoni kuwa unajichanganya?, mara hawaongei Kiingereza, mara wanaongea Kiingereza Kibovu
 
Back
Top Bottom