Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Kaka mimi wala sipingi hilo, na hilo linajulikana na liko wazi na ndio maana chote kitaitwa kiswahili, tofauti ninayoisema mimi ni kuwa, Kiswahili chetu ndio kina Kiarabu, Kibantu, Kiingereza nk, lakini sehemu zingine Kiswahili hakina kabisa maneno ya Kiingereza unakuta Kifaransa, pia kina asilimia chache sana ya maneno ya Kiarabu na sehemu kubwa ni Kibantu
Rahisisha kwa kusema!
Rahaja ya kiunguja (ambacho ndo tunakitumia) kimekopa maneno mengi kutoka lugha za kiarabu, kireno, kiingereza, kihindi n.k
 
Rahisisha kwa kusema!
Rahaja ya kiunguja (ambacho ndo tunakitumia) kimekopa maneno mengi kutoka lugha za kiarabu, kireno, kiingereza, kihindi n.k

Na ndio nasimamia hapo, na swali kubwa la kujiuliza ni kuwa kabla ya Waarabu kuja, kulikuwa hakuna Lugha iliyokuwa inatumika?, kwa uhakika ilikuwepo na hatuwezi kusema Mimi nimesoma chuo na najua Kiswahili ni Kiarabu

Asante
 
Na ndio nasimamia hapo, na swali kubwa la kujiuliza ni kuwa kabla ya Waarabu kuja, kulikuwa hakuna Lugha iliyokuwa inatumika?, kwa uhakika ilikuwepo na hatuwezi kusema Mimi nimesoma chuo na najua Kiswahili ni Kiarabu

Asante
Hapo nakupinga!
Kiswahili sio Kiarabu, ni kibantu
 
We ushamba umeacha lini?, hivi hata hujui Kiswahili kilivyogawanyika?, Kiswahili kina matabaka kaka, ngoja basi nikufahamishe na uelewe tofauti ya kiswahili cha Tanzania na Kikongo
Cha Tanzania kina mchanganyiko wa Kiarabu, Kibantu, Kiingereza nk, Lakini kiuhalisia maneno Mengi ya Kiarabu yana Kibantu chake, kwa sisi huku Tanzania maneno ya kiarabu bado mengi yanasimama kwenye lugha yetu, lakini kwa Congo maneno almost yote ya Kiarabu hayatumiki na mbadala wake wanatumia maneno ya Kibantu na Kifaransa,
Sasa basi kwa Mkongo akiongea Kiswahili cha kwao kwa sisi Watanzania tunaelewa anachokiongea, lakini sisi tukiongea Kiswahili chetu chenye Kiarabu wanapata shida san kujua tunachoongea
Na hata Congo yenyewe Kiswahili pia kina tofauti, East Congo angalau tunaweza kuongea vizuri, lakini Katanga ni shida kabisa, na Kinshansa almost hakuna Kiswahili

Acha ushamba wewe
Hujui hata maana ya rahaja na utohozi..!
 
Ni kweli kwa Kiswahili kinachotumika Pwani ya East Africa (Tanganyika, Zanzibar, Mombasa nk) lakini si kweli kwa Kiswahili cha DRC, cha DRC labda kila only 10%ya Kiarabu, lakini Asilimia kubwa ni Kibantu kisha Kifaransa

Hicho cha Congo sijui ila maana ya sawahili ni pwani kwa kiarabu so hicho cha Congo sio kiswahili ni kama tuseme kigiriyama ni kiswahili wakati si kweli maana ukiwasikia wana ongea maneno mengi ni ya kiswahili
 
30% ya Raia wa Oman wametoka/wana asili ya Tanzania....

Acheni kukariri kuwa Kiswahili kina asili ya Kiarabu kwa asilimia kadhaa, basi Mwarabu atasikia Kiswahili na kuelewa, au Mswahili atasikia Kiarabu na kuelewa....

Mwarabu aongee Kiarabu hapa, wewe Mswahili hutaelewa hata robo....
Mswahili aongee Kiarabu Mswahili hataelewa hata robo.....

Ila ni rahisi kwa Mwislam anayeijua Quran kujifunza Kiarabu na kuongea kwa haraka, kuliko Mswahili ambaye haijui Quran.....

NB:
I have experience about Oman, coz nimeishi Muscat!
 
Kiswahili sio kimoja kaka, Ni kama kiingereza tu, Uk wana Chao, USA wana chao, Jamaica wana Chao, Nigeria wana Chao,

Shelisheli wana Kiswahili chao, kuna sehemu ya Madagascar pia wana chao, Kenya Nairobi na Mombasa kuna tofauti, DRC wana chao, tembea uone kaka, acha kubisha uko nyuma ya QWERTY
HATA CHA COMORO TOFAUTI
 
bila kusahau kuna wahenga wa oman pia hapa Tanzania kama

Abushiri Ibn Salim AL Harthi

Abushiri ibn Salim al-Harthi - Wikipedia

24225_abushiri_revolt.jpg
 
Hicho cha Congo sijui ila maana ya sawahili ni pwani kwa kiarabu so hicho cha Congo sio kiswahili ni kama tuseme kigiriyama ni kiswahili wakati si kweli maana ukiwasikia wana ongea maneno mengi ni ya kiswahili

Kumbuka hilo jina limeanzishwa na Waarabu Wakiwaita watu wa pwani na lugha yao waliyoikuta hapo pwani, so kabla ya kuja Waarabu hao watu wa Pwani alikuwa wanaongea lugha gani?
 
Kiingereza ni kimoja pia,hao wengine wameamua kuumiza matamshi ya baadhi ya maneno,ndiyo maana unaambiwa kuna FORMAL ambayo ni ya UINGEREZA hakuna kiingerza cha Naijeria wala kongo,isipokuea INTONATION tu na hiyo inatokana na lugha zao eanazotumia.
Usijifabganye kama kuna kiingereza cha KIHAYA wala KiSUKUMA,ni lafudhi na matamshi tu yaliyoathiriwa na lugha fulani ama za makabila au Mataifa,unawezaje kusema KIINGEREZA cha NAIJERIA wakati umeshasema"KIINGEREZA?"
HII MAANA YAKE NI LUGHA YA UK.
Usiwe mvivu wa kufikiri.
 
Kumbuka hilo jina limeanzishwa na Waarabu Wakiwaita watu wa pwani na lugha yao waliyoikuta hapo pwani, so kabla ya kuja Waarabu hao watu wa Pwani alikuwa wanaongea lugha gani?

Ndio sawahili ni neno LA kiarabu ndio maana lugha hii imejaa maneno ya kiarabu mengi hicho cha ki Congo sidhani kama ni kiswahili nimetolea mfano wagiriyama coz ni indigenous tribe ya coast ya Kenya na ukiwasikia utaona kama kuna kiswahili kidogo ambao si kiswahili Bali ni kibantu kwa kuwa kiswahili kiliborrow maneno ya kibantus including from giriyama so hatuwezi sema giriyama ni kiswahili.
 
Back
Top Bottom