Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Kiswahili sio kimoja kaka, Ni kama kiingereza tu, Uk wana Chao, USA wana chao, Jamaica wana Chao, Nigeria wana Chao,

Shelisheli wana Kiswahili chao, kuna sehemu ya Madagascar pia wana chao, Kenya Nairobi na Mombasa kuna tofauti, DRC wana chao, tembea uone kaka, acha kubisha uko nyuma ya QWERTY
kiswahili ni kimoja tu ila kinatofautiana matamshi kulingana na eneo husika....hakuna viswahili vingi wala vingereza vingi big NO!!!
 
Ndio sawahili ni neno LA kiarabu ndio maana lugha hii imejaa maneno ya kiarabu mengi hicho cha ki Congo sidhani kama ni kiswahili nimetolea mfano wagiriyama coz ni indigenous tribe ya coast ya Kenya na ukiwasikia utaona kama kuna kiswahili kidogo ambao si kiswahili Bali ni kibantu kwa kuwa kiswahili kiliborrow maneno ya kibantus including from giriyama so hatuwezi sema giriyama ni kiswahili.

Kwa nini unasema Kiswahili kimeborrow maneno ya Kibantu na sio Kiswahili Kimeborrow Maneno ya Kiarabu?, Dada Kibantu kilikuwepo kabla ya Kiarabu, hivyo Kiarabu ndio kimeingia ndani ya Kiswahili, So waarabu waliita Lugha waliyoikuta Sawael, yaani Ya watu wa Pwani

Mfano ni huu, Wabantu waliokuwa Pwani walikuwa wanajua kuhesabu vizuri tu, so katika namba kumi (Moja, mbili, tatu, nne, Tano, Sita, saba, nane Tisa Na kumi) walizozikuta Waarabu wao wakaingiza namba tatu tu, Sita, Saba na Tisa, sasa utasemaje Kiswahili Kimetohoa Kibantu wakati ukweli unaonekana kuwa Kiarabu ndio kimeingia ndani ya Kiswahili?
 
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili
Oman ina mchanganyiko wa Arabs wazawa na waarabu wenye asili ya afrika mashariki tena wengi kutokea Tz ,na wengi hao wazungumzao kiswahili baba zao waliloea afrika kabla oman haijagundua petrol wakafanya biashara huku..lkn nchi ilipokuja kupata mwamko kiuchumi sultan quaboos akawaomba wote waliouhamishoni warudi nyumbani kuijenga nchi!wengi wakarudi oman wakabeba watoto na wake zao ambao ni waafrika sasa waliondoka wanakijua kiswahili hadi leo ukienda muscst usimtete mtu kwa lugha ya kiswahili!hata Baba wa taifa hayati Julius alishangaa hilo pale alipofanya ziara oman
 
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili

Oman ilingiliana na Zanzibar baada ya Mwinyimkuu wa unguja kuomba msaada wa watu wa oman kuja kuwatoa wareno ambalo walingia ukanda wa mashari ya bahari ya pwani ikiwamo zanzibar, mombasa ,tanga, kilwa,pemba, mozamnique.
Wa Oman waliitikia wito wa ndugu zao wa Zanzibar na kuleta wana jeshi karibu elfu 10,000 kuoambana na wareno...
Waliwatoa Mombasa na wareno wameacha alama ile fort jesus, wakawatoa kilwa Unguja na baadae pemba ambayo ilikua ngome yao.
Zainzibar waliacha old fort pale forodhani.
Baada ya kufurushwa katika pwani hii wareno waka kimbilia msumbiji ambako walibaki mpaka walipo tolewa na Samora na Frelimo.

Wa Oman walibaki zanzibar na waliomba kurudi nyumbani ndugu zao wakawambia wabaki tu kwani wareno watarudi tena... hivyo wakabaki kama kikosi cha jeshi na baadae waoman wakiafanya Zanziabr na pwani hii kuwa second home, wakahamia kwa wingi na baadae wakapewa wao dhima ya kuendesha nchi.
Hatimae Zanzibay na Oman ikawa nchi moja , Ufalme mmoja ambaye alikuwapo Zanzibar na Mjii mkuu ukiwa Zanzibar.

Hivyo Oman na Zanzibar zilikua nchi moja ya Muungano kama huu wa sasa na Tanganyika.
Oman wanaongea kiswahili karibu 70% ...sababu ni hii historia ya kuwa ikikua ni nchi moja.

Na wale mawaziri 3 waliokuja wote wamezaliwa Zanzibar lakini Oman imewaamini na kuwapa madaraka makubwa mmoja akiwa waziri wa mafuta na gas.....
 
Asiyetaka Muungano atoke yeye atuachie Zanzibar (kwa maana ya ardhi)
Na wakileta mchezo hata hiyo Omani tutaifanya kuwa sehemu ya Jamuhuri ya Muungano

Hii ni mbinu ya watawala wa kitanganyika kuuficha udini walio nao dhidi wa watu wa zanzibar kusingizia muungano na warabu....ila wao wazungu walowatawala hawana neno wanawasaidia na kujenda makanisa na mashule...
Zanzibar aitaka kushirikiana na ndugu zao utasikia muungano , uwarabu ...ujinga mtu ambao watu wengi wa znz wameanza kungamua ...
Hata hii ziara ya kirafiki kuna mijitu imechukia na kununa kweli kweli wakati kuna meli ilikua ikja ya kikristo kuleta vitabu vya kikristo...
 
Kwa nini unasema Kiswahili kimeborrow maneno ya Kibantu na sio Kiswahili Kimeborrow Maneno ya Kiarabu?, Dada Kibantu kilikuwepo kabla ya Kiarabu, hivyo Kiarabu ndio kimeingia ndani ya Kiswahili, So waarabu waliita Lugha waliyoikuta Sawael, yaani Ya watu wa Pwani

Mfano ni huu, Wabantu waliokuwa Pwani walikuwa wanajua kuhesabu vizuri tu, so katika namba kumi (Moja, mbili, tatu, nne, Tano, Sita, saba, nane Tisa Na kumi) walizozikuta Waarabu wao wakaingiza namba tatu tu, Sita, Saba na Tisa, sasa utasemaje Kiswahili Kimetohoa Kibantu wakati ukweli unaonekana kuwa Kiarabu ndio kimeingia ndani ya Kiswahili?

Mimi sijakataa kiswahili kime borrow both kibantu na kiarabu
 
Mimi sijakataa kiswahili kime borrow both kibantu na kiarabu

Kiswahili hajikaborrow Kibantu, bali Kiswahili ni Kibantu, kilichochukua maneno ya Kiarabu, Kiingereza, Kireno, Ki Persia, Kijerumani kwa upande wa Pwani
Na kwa DRC ni Kibantu kilichokopa maneno ya Kifaransa
 
Nimeona baadhi ya watu waliokuja na Meli ya mfalme wa Oman wakizungumza Kiswahili vizuri. Nilitaka kujua kama kwenye taifa hilo uzungumza Kiswahili
Naam wapo waarabu wenye asili ya kitanzania na wengi wao wanatoka Zanzibar.
 
Wako wazanzibari wengi ndugu wa mfalme wa Oman ambao wakitaka kuhamia Oman huwa rahisi kwao na wakienda huwa na haki Sawa na raia wa Oman huwapa vyeo vya serikali au ajira, siasa nk hivyo ukiwaona usishangae Wengine ni wazaliwa wa darajani Zanzibar waliohamia Oman kwa ndugu zao tena wamehamia wakiwa na umri mkubwa
Achilia Zingbari kuna ndung hadi Tabora,Mwanza na hata Shy.Sehemu zote hizi kuna muingiliano mkubwa sana.
 
Kumbe kweli Watanzania ni wepesi sana kusahau, Miaka 52 iliyopita hawa jamaa walikuwepo hapa Tanganyika na wengine walikuwepo Zanzibar. Sanjar na hayo hawa Watu walikuwa wameishazaliana hivyo hawakuondoka!
 
Sio 98%, na ujue Kiswahili kinatofauti na eneo na eneo, ukikisikia kiswahili cha DRC hakina kabisa maneno ya Kiarabu na kama yapo ni kachachesana, kiswahili chao kimejaa Kibantu na maneno ya kifaransa
Hicho ni cha kuokoteza tu
 
Kwani wakituacha kiuchumi kuna tatizo gani?? Tumeachwa kiuchumi na nchi ngapi ???
Acha fikra za kimaskini nyie ndo wale mnaomsifia magu ' eti sasa hivi tunaheshimiana mtaani'
SO WHAT mkuu?
Watatuacha vipi tupe sababu. Maana oman pia ku watu wamechoka. . Tuanzie hapo

Jamaica na Nigeria hawaongei English...Jamaica wana PATOIS na Nigeria Pidgen....ni kiingereza kibovu kilichochanganywa na maneno yao lakini hakitambuliki mashuleni ila mtaani tu. Shuleni wanatumia kiingereza fasaha cha Uingereza.

Asante mkuu Nilikuwa sijui hili sababu niliwahi kaa Zanzibar miezi minne nilikutana na raia wa Oman mahotelni Wanaoongea kiswahili barabara nikajua ni wazanzibari tu Asante kwa clarification

Idadi kubwa ya wenye asili ya Oman,waliishi Tanganyika(Tanzania bara).Kuanzia Mtwara,Tanga,Tabora,Shinyanga,Mwanza,Sumbawanga,nk.Na mpaka leo vizazi vya hao watu wapo,japo wengi wemchanganyika na makabila ya asili kwa kuoana.
 
Jamaica na Nigeria hawaongei English...Jamaica wana PATOIS na Nigeria Pidgen....ni kiingereza kibovu kilichochanganywa na maneno yao lakini hakitambuliki mashuleni ila mtaani tu. Shuleni wanatumia kiingereza fasaha cha Uingereza.
Bora umeliambia hilo LIJINGA,halina hata fikra,Unaita "KIINGEREZA"ukimaanisha lugha ya waingereza halafu useme eti RWANDA wana "kiibgereza chao"kimetoka wapi?
Aibu kuwa na watu kama huyo"Kituko"wakajiita wameenda shule.
 
Neno Swahili,ni neno la kiarabu,linatamkwa Sahel(kwa maana ya Pwani.Kiswahili no cha pwani tu,kama jina la lugha hiyo ilivyoitwa na waarabu,kiswahili,yaani lugha ya Pwani,hivyo vingine vinavyoitwa kiswahili,ni kuongeza tu,kisichokuwamo,kikatiwa katika mahali sipo.
Liambie hilo LIJINGA
 
Back
Top Bottom