Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Oman wanazungumza Kiswahili pia?

Kaka ELI-91 , unajua ni ngumu sana kuelewa ninachokiandika na ninachojaribu kukieleza
Mfano, kwa sisi East Africa tunasema MIMI ambayo ina accent ya Kiarabu lakini Kiswahili cha Congo wanasema MIYE ikiwa ni accent ya Kifaransa
Pesa tunasema Fedha-kiarabu wao Congo wanasema Faranga

Ukiongea siku za juma kama tunavyoongea sisi huku hakuna Mkongo atakayekuelewa, utawachanganya kabisa wao wanatumia namba au maneno ya kifaransa
Jumatatu-Siku ya Kwanza (Lundi)
Jumanne-Siku ya Pili (Mardi)
Jumatano- Siku ya Tatu (Mercredi)
Alhamis-siku ya nne (Jeudi)
ijumaa-siku ya Tano (Verdred)
Jumamosi- siku ya Posho (Samedi)
Jumapili-Siku ya Mungu (Demanche)
We mpuuzi neno "faranga"siyo neno la kibantu ni matamshi mabovu ya neno"FRANC" ambayo ni fedha ya UFARANSA!shwain.
 
Kama unajua kuanzia advance hukusoma,HGL,HGk napia chuo hukusoma masuala ya lugha basi usitoe maelezo ambayo siyakwe,tuliosoma lugha as professional tunaona unapotosha
Toa tofauti siyo katazo bila hoja,wanaume tumejikita kwenye hoja siyo mipasho na matamko.
 
Umeni-quote mimi ilhali ujumbe umemkusudia ELI-91 sio?

Ni hivi nyie mliojifunza kiswahili mkiwa Sekondari endeleeni kuamini kiswahili ni KIBANTU ila sisi tuliozaliwa ndani ya kiswahili na kupitia madrasa, tunajua athari ya lugha ya kiarabu ndani ya kiswahili. Hicho cha Congo ndugu sio kiswahili, ni lugha tu nyingine yenye maneno mengi au kadhaa ya kiswahili.
Exactly,LUGHA NASIBU YA PWANI YA AFRIKA MASHARIKI.
Huyo lofa analeta bara huko DRC,tumejifunza kutaaji(blending)ili tutamke fasaha.
 
Kiswahili sio kimoja kaka, Ni kama kiingereza tu, Uk wana Chao, USA wana chao, Jamaica wana Chao, Nigeria wana Chao,

Shelisheli wana Kiswahili chao, kuna sehemu ya Madagascar pia wana chao, Kenya Nairobi na Mombasa kuna tofauti, DRC wana chao, tembea uone kaka, acha kubisha uko nyuma ya QWERTY
ni kama kilivyo kiingereza cha kule Ireland ni tofauti na cha england.Kumbuka tofauti iliyopo kati ya americani English na British English
 
Utofauti wa kiingereza cha Marekani na uingereza.

waingereza- maize.
wamarekani- corn.

Waingereza - dustbin
Wamarekani-gabage can.

Waingereza-biscuit
Wamarekani-cookies.

Waingereza- mobile/cell phone
Wamarekani-payphone.

Waingereza-Father
Wamarekani-Daddy

Waingereza-you and me
Wamarekani-you and I

Waingereza- colour
Wamarekani-color

Mifano mingi sana
Marekani ni koloni la Uingereza na lugha yao ni kiingereza,hayo maneno wanayapindisha tu kuongeza msamiati wa maneno yao maarufu ya mtaani,kama hapa kwetu "TAPELI",KULA BATA"
 
Kiingereza ni kimoja pia,hao wengine wameamua kuumiza matamshi ya baadhi ya maneno,ndiyo maana unaambiwa kuna FORMAL ambayo ni ya UINGEREZA hakuna kiingerza cha Naijeria wala kongo,isipokuea INTONATION tu na hiyo inatokana na lugha zao wanazotumia.
Usijidanganye kama kuna kiingereza cha KIHAYA wala KiSUKUMA,ni lafudhi na matamshi tu yaliyoathiriwa na lugha fulani ama za makabila au Mataifa,unawezaje kusema KIINGEREZA cha NAIJERIA wakati umeshasema"KIINGEREZA?"
HII MAANA YAKE NI LUGHA YA UK.
Usiwe mvivu wa kufikiri.
kuna kiswahili cha kimvita na kimakunduchi
 
wazanzibar ni wale wale wa Oman kwani jeuri ya kuvunja MUUNGANO unadhani wanaitoa wapi.. na wakijitoa leo kwenye Muungano wanatuacha kiuchumi haki ya Mungu
Na hiyo ndio sababu moja wapo kwa CCM kung'ang'ani huu mungano,CCM wanajua fika kuwa kama mungano utavunjika CCM itaumbuka,kwa maendeleo yatakayo patikana Zanzibar utakuwa ndio mwisho wa CCM Tanganyika kwani wananchi watajua kuwa CCM ni wababaishaji tu...,

Moja katika propaganda zao Kubwa ambayo CCM imefanikiwa kuwasambaratisha wazanzibari ni msemo wa "Warabu watarudi Zanzibar",Moja kati ya ujinga mkubwa wa CCM Zanzibar kuikubali propaganda hii na kuzidi kuwaminya wazanzibari wenzao,wanachosahau kuwa kama maendeleo yatakuja Zanzibar yatawanufaisha wazanzibari wote wakiwemo CCM na wasio wanachama wa CCM...

Waswahili wanasema "Mgaa gaa na ubo hali wali makavu",hawa wazanzibari badala ya kukaa na kula meza moja na wenzano wa Oman wao wanaikubali hii propaganda ya kubaguawana....

Kule Oman waziri wa Elimu ni mzanzibari wazairi wa Mafuta ni mzanzbari,wazairi wa Utalii ni mzanzibari wenye vyeo vikubwa jeshini ni wazanzibari,waprofesa na watu wenye elimu kubwa katika nyanja tafauti ni wazanzibari waliko karibu na Mfalme watoa ushauri ni wazanzibari..

Nchi ya Oman iko tafauti na nchi nyengine za Kiarabu imendelea sana,watu wake wanaishi maisha mazuri,kwa wle wanaoishi ulaya huwezi kumuona Muomani anaishi kwa kutafuta maisha ulaya,utawaona warabu wengini tu .....
 
We ushamba umeacha lini?, hivi hata hujui Kiswahili kilivyogawanyika?, Kiswahili kina matabaka kaka, ngoja basi nikufahamishe na uelewe tofauti ya kiswahili cha Tanzania na Kikongo
Cha Tanzania kina mchanganyiko wa Kiarabu, Kibantu, Kiingereza nk, Lakini kiuhalisia maneno Mengi ya Kiarabu yana Kibantu chake, kwa sisi huku Tanzania maneno ya kiarabu bado mengi yanasimama kwenye lugha yetu, lakini kwa Congo maneno almost yote ya Kiarabu hayatumiki na mbadala wake wanatumia maneno ya Kibantu na Kifaransa,
Sasa basi kwa Mkongo akiongea Kiswahili cha kwao kwa sisi Watanzania tunaelewa anachokiongea, lakini sisi tukiongea Kiswahili chetu chenye Kiarabu wanapata shida san kujua tunachoongea
Na hata Congo yenyewe Kiswahili pia kina tofauti, East Congo angalau tunaweza kuongea vizuri, lakini Katanga ni shida kabisa, na Kinshansa almost hakuna Kiswahili

Acha ushamba wewe
Hakuna kiswahili cha Kongo ....hzo zote ni pijini tu!! Kiswahili n kimoja tu chenye mpangilio/muundo wa sentensi zake katka mfumo wa lugha zote za kibantu na kikiwa kimekopa maneno mengi mno kutoka katka lugha ya kiarabu!! Wanachoongea wakongo wawe wa mashariki au wasukuma wa kanda ya ziwa inakuwa ni pijini tu yenye kutokezwa na taathira ya lugha za makabila yao haipo hata katka lahaja mahsus...hivyo huwez ukakipa tawi ya kuwa n kiswahili cha sehem fulan. Kinaachongelewa bungeni(Kiswahili+kiingereza=KISWANGLISH) Huwez ukakiita kiingereza cha tanzania....imetokea tu kwa sabab ya wahuska kukosa (kuwa na na uhaba vichwan mwao) misamiat ya kutosha ya lugha zote mbili!!. KISWAHILI NI KIMOJA TU KILE CHA SHAABAN ROBERT NA SAADAN KANDORO ....Tunachoongea sie leo hii!!
 
Asiyetaka Muungano atoke yeye atuachie Zanzibar (kwa maana ya ardhi)
Na wakileta mchezo hata hiyo Omani tutaifanya kuwa sehemu ya Jamuhuri ya Muungano
Usultani wa Zanzibar ulitoka Oman.Rejea Sultani Seyyid mpaka Sultan Jamshid
 
Shinyanga nilikaa ni kweli kuna waarabu wasukuma wenye asili ya Oman. Wanaongea kisukuma na kiswahiili hacha tu wako kibao shinyanga wengi wako maganzo nk
Kwa hiyo hawa waarabu tunaowaona mikoani kumbe ni waomani ? Mbona pia kuna wayemeni?
 
Hili la kutanuwa muungano wetu hadi Oman lipo vizuri sana, yaani mtu unatinga Muscat na kitambulisho cha kupigia kura tu. Tumuuzie mfalme wa Oman hili wazo.
Ukitamani Omani mbona hutaiacha Shelisheli?
 
Tatizo watanganyika ustaarabu zero, Zanzibar washakuchokeni mtaweza Oman?
Ni wale wenye asili ya uarabuni ndiyo wamechoka na ndiyo walikuwa wanatawala enzi za usultani.Hawa wengine wenye asili ya bara hawajachoka wako poa tu hawana makeke na Muungano
 
Ili kumaliza utata kwetu tunaofuatilia uzi huu, hebu tuwekee paragraph moja ya kiingereza cha UK na nyingine ya kinaijeria na zote zikiwa na ujumbe mmoja.
Tofauti itatokea kiisimu na kiistilahi
 
Back
Top Bottom