Umeni-quote mimi ilhali ujumbe umemkusudia
ELI-91 sio?
Ni hivi nyie mliojifunza kiswahili mkiwa Sekondari endeleeni kuamini kiswahili ni KIBANTU ila sisi tuliozaliwa ndani ya kiswahili na kupitia madrasa, tunajua athari ya lugha ya kiarabu ndani ya kiswahili. Hicho cha Congo ndugu sio kiswahili, ni lugha tu nyingine yenye maneno mengi au kadhaa ya kiswahili.
Nimekuquote kwa sababu uliniquote sehemu ulitaka kuona tofauti ya lugha hizo
Siku zote mi huwa najua vizuri sana, mtoto wa Kiislam hawezi kukubali kuwa Kiswahili sio Kiarabu, ndugu yangu kujua kiswahili sio kupitia Chuo, kwa taarifa yako wako wengi waliozaliwa sehemu ya Waswahili na wala sio Waislam na wanakijua Kiswahili vizuri tu
Ngoja nikufahamishe kitu
Lugha hii inayoitwa Kiswahili ilikuwepo kwa Karne na Karne ikiitwa KINGOZI , na Wafanyabiashara wa zamani waliokuwa wakitoka Congo kuleta mizigo Pwani walikuwa wakiongea hiyo lugha, na Mizigo iliyokuwa ikifika pwani ilisafirishwa kwenda Uarabuni na hao Wabantu,
Waarabu walipofika hapa Tanganyika waliwakuta watu wa eneo lote la Pwani ya Tanganyika, Kenya wakiongea hiyo lugha na ndio wakaiita lugha ya watu wa Pwani,
Na Waarabu walioanza kufuata njia ya Wafanya biashara ya kwenda Congo, waliwakuta watu njiani wakiongea hiyo Lugha Hiyohiyo (maeneo kama Bagamoyo, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Kahama, Kigoma mpaka DRC) Usifikiri Waarabu ndio waliovumbua hiyo njia, hiyo njia ilikiwepo miaka na miaka na Waarabu waliifata tu wakiongozwa na Wafanya biashara wa Kibantu
Baada ya Wafanyabiashara wa Kiarabu kudominate hiyo njia taratibu wakaanza kuingiza maneno yao ya kiarabu na yakawa comon kwenye hicho KINGOZI, na kwa sababu walikaa muda mrefu athari yao kwenye hiyo lugha ni kubwa zaidi, mfano waarabu waliwakuta WANGOZI wanajua kuhesabu vizuri tu na wao Waarabu wakaongeza au kubadirisha matamshi ya namba tatu katika mtiririko wa kuhesabu mfano moja, mbili, tatu, nne, tano, "nane na kumi vyote ni Kibantu lakini Sita, Saba na Tisa ni Kiarabu, so sio kama hiyo Lugha walioikuta haina hizo namba, bali wao waarabu walizitumia sana hizo namba tatu kwa lugha yao na ndio zikatoholewa kuwa lugha rasmi, lakini mpaka leo ukisema Kenda watu wanajua ni Tisa
Pia kuna Maneno ya kutoka Persia yaliyoletwa na wachuhuzi wa kutoka huko, maneno kama chai, achari=pickle, Serikali, Diwani, Sheha nk,
kuna maneno pia ya KiPortuguese pia yapo ndani ya Kiswahili mfano leso" (handkerchief), "meza" (table), "gereza" (prison), "pesa" ('peso', money), nk.
Pia yapo maneno mengi tu ya Kiingereza, Kijerumani nk, japokuwa maneno hayo yameingizwa kwenye Kiswahili lakini sio kweli kwamba tulikuwa hatuna maneno ya Kiswahili yenye maana hizo, maneno machache sana ya Kisayansi na kitechnolojia ndio huwezi kuyakuta kwenye KINGOZI