Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
671
1,000
OFISA Mifugo Manispaa ya Shinyanga, Velan Mwalukwa, ametiwa mbaroni kwa kumtolea lugha chafu Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira.

Mwalukwa, ametiwa Mbaroni jana wakati wa mkutano wa Mbunge Katambi, Kata ya Ibinzamata alipoitwa kujibu tuhuma zinazo mkabili, za kudaiwa kuhozi ardhi ya Mwananchi Zacharia Tingwa mkazi wa kata hiyo, na kutoa lugha zisizo za staha kwa mbunge huyo.

Kabla ya kuanza kujibu tuhuma hizo, Mwalukwa alianza kumtolea lugha chafu na za kumkejeli mbunge huyo, hali ambayo ili mkasilisha Katambi na kuagiza awekwe chini ya ulinzi kwa utovu wa nidhamu, na kisha baadae akachukuliwa na Polisi.

Aidha Katambi akizungumzia tukio hilo, alisema amesikitishwa na mtumishi huyo wa umma, kumdharau Mbunge tena Naibu Waziri mbele ya wananchi, na hivyo kuamua kumchukulia hatua, ili liwe fundisho kwa wengine.

"Huyu mtu anaonekana ana dharau na jeuri, mimi ana nifanyia hivi je Mwananchi wa kawaida, na hasa huyu ambaye ana mgogoro naye, si ndiyo balaa kabisa, hebu ngoja tumtia adabu ili tuone jeuri yake ipo wapi," alisema Katambi.

"Suala hili la Mgogoro baina yake na huyu Mwananchi, nitalivalia njuga Tena bahati nzuri na Mimi ni Mwanasheria, na sita pendelea upande wowote ule, mwenye haki na hilo eneo atapata haki yake," aliongeza.

Katika hatua nyingine Katambi, aliwahidi wananchi wa Ibinzamata kuwa ataendelea kutatua changamoto ambazo zinawakabili, ikiwamo Sekta ya Afya, Elimu, ujenzi wa Barabara, pamoja na kushughulia malipo ya Wastaafu kutoka chama cha ushirika mkoani Shinyanga SHIRECU.

Awali Mwanchi huyo Zacharia Tingwa, akitoa malalamiko yake ya kudhurumiwa ardhi, alidai kuwa eneo hilo ni lake, lakini Ofisa huyo Mifugo amekuwa akitumia Pesa ili amnyang'anye na kufikia hatua ya kuweka familia yake yote rumande na kumtolea vitisho.
 
Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,111
2,000
OFISA Mifugo Manispaa ya Shinyanga, Dk. Velan Mwalukwa, ametiwa mbaroni kwa kumtolea lugha chafu Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira.Cha kujiuliza ni Bwana Katambi kamuita huyu Mzee mbele ya kadamnasi kumuhoji kama Nani na kwa mamlaka gani?,
Mkutano ulikuwa ni wa wa Serikali au Mkutano wa Kisiasa wa mbunge?
Kama wa kiserikali Je Naibu waziri (Tena asiye na dhamana na mada husika) akihisi kutoheshimiwa anaweza kuagiza Askari kumkamata raia?
Kama wa Mbunge, je mbunge anaweza kumuita na kumuhoji Mtumishi kwa tuhuma tu, na wasipoelewana kuagiza askari wamkamate?
Kwa nini asipeleke malalamiko kwa Mamlaka ya kinidhamu ya Daktari huyo?

E6pXyHHWUAEJsBT.jpg
MWALUKWA.JPG

Bwana Mwalukwa ni huyu hapa pia:
Namtazama CV yake huyu Daktari nabaki kujiuliza huyu Mzee kwa taaluma yake na uzoefu wake miaka kadhaa serikalini ndo ambaye hajui heshima kwa viongozi au amekuwa provoked. Kwa tabia za Katambi za kupenda kuminyana nina mashaka na hii ishu.

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,928

View attachment 1859868 View attachment 1859876

Bwana Mwalukwa ni huyu hapa pia:
Namtazama CV yake huyu Daktari nabaki kujiuliza huyu Mzee kwa taaluma yake na uzoefu wake miaka kadhaa serikalini ndo ambaye hajui heshima kwa viongozi au amekuwa provoked. Kwa tabia za Katambi za kupenda kuminyana nina mashaka na hii ishu.

Maofisa wengine mikoani wanakua miungu kwa kujiwezesha kimapato hadi wanadharau utawala. Naibu waziri ni kiongozi inabidi kumtii sio kupimana nae nguvu.
 
Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,111
2,000
Maofisa wengine mikoani wanakua miungu kwa kujiwezesha kimapato hadi wanadharau utawala. Naibu waziri ni kiongozi inabidi kumtii sio kupimana nae nguvu.

Naibu waziri mwenye Dhamana ya ....... ...

Kuna mgawanyo wa Madaraka mkuu, tatizo lililokuwapo hapo ni la jinai. Na si Mbunge amuite mtumishi na kuanza kumuhojihoji. Kumbuka huo ulikuwa mkutano wa Mbunge jimboni.
 
Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,111
2,000
Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira naye anaagiza mtu awekwe ndani kwenye Mkutano wa kisiasa kama Mbunge.

Kwa nini alimuita Mtumishi kumuhoji mbele ya wananchi?

Sasa Waziri wa vijana na ajira anapotaka kutatua Mgogoro wa Ardhi si VITUKO hivi
 
Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,715
2,000
Ndugu zangu sikilizeni video,
Huyo bwana mifugo anadharau za wazi sana halafu nijeuri.
Nendeni YouTube mtaelewa
 
Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,404
2,000
Huyo bwana mifugo hana dharau yeyote na wala hajamkashifu huyo mbunge, isipokuwa huyo mbunge ndie alimtukana huyo mwananchi, mbunge hana mamlaka ya kushughulikia kesi za ardhi zipo mamlaka zenye uwezo huo.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
8,943
2,000
Huyo ofisa hajafundishwa ADABU kwa wakubwa zake?!!!

Naunga mkono hoja ya kuwekwa chini ya ulinzi!!!

#KaziIendelee
OFISA Mifugo Manispaa ya Shinyanga, Velan Mwalukwa, ametiwa mbaroni kwa kumtolea lugha chafu Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira.

Mwalukwa, ametiwa Mbaroni jana wakati wa mkutano wa Mbunge Katambi, Kata ya Ibinzamata alipoitwa kujibu tuhuma zinazo mkabili, za kudaiwa kuhozi ardhi ya Mwananchi Zacharia Tingwa mkazi wa kata hiyo, na kutoa lugha zisizo za staha kwa mbunge huyo.

Kabla ya kuanza kujibu tuhuma hizo, Mwalukwa alianza kumtolea lugha chafu na za kumkejeli mbunge huyo, hali ambayo ili mkasilisha Katambi na kuagiza awekwe chini ya ulinzi kwa utovu wa nidhamu, na kisha baadae akachukuliwa na Polisi.

Aidha Katambi akizungumzia tukio hilo, alisema amesikitishwa na mtumishi huyo wa umma, kumdharau Mbunge tena Naibu Waziri mbele ya wananchi, na hivyo kuamua kumchukulia hatua, ili liwe fundisho kwa wengine.

"Huyu mtu anaonekana ana dharau na jeuri, mimi ana nifanyia hivi je Mwananchi wa kawaida, na hasa huyu ambaye ana mgogoro naye, si ndiyo balaa kabisa, hebu ngoja tumtia adabu ili tuone jeuri yake ipo wapi," alisema Katambi.

"Suala hili la Mgogoro baina yake na huyu Mwananchi, nitalivalia njuga Tena bahati nzuri na Mimi ni Mwanasheria, na sita pendelea upande wowote ule, mwenye haki na hilo eneo atapata haki yake," aliongeza.

Katika hatua nyingine Katambi, aliwahidi wananchi wa Ibinzamata kuwa ataendelea kutatua changamoto ambazo zinawakabili, ikiwamo Sekta ya Afya, Elimu, ujenzi wa Barabara, pamoja na kushughulia malipo ya Wastaafu kutoka chama cha ushirika mkoani Shinyanga SHIRECU.

Awali Mwanchi huyo Zacharia Tingwa, akitoa malalamiko yake ya kudhurumiwa ardhi, alidai kuwa eneo hilo ni lake, lakini Ofisa huyo Mifugo amekuwa akitumia Pesa ili amnyang'anye na kufikia hatua ya kuweka familia yake yote rumande na kumtolea vitisho.
Aa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom