Nzega: Rais Magufuli asema Demokrasia imeimarika sana nchini ndio maana wengine walijitoa kwenye uchaguzi, wengine wakashinda na kushindwa

Binafsi naamini vikwazo ni njia bora ya kuirudisha serikali ya nchi yoyoye kwenye mstari pale inapokengeuka.

Ila Tanzania tayari ni maskini sana, hivyo haihitaji vikwazo zaidi kuirudisha kwenye mstari. Hata kususwa tu inatosha.

Tatizo ni ufinyu wa uelewa wa watanzania. Tatizo letu ni kukosa uelewa kuwa viongozi wa CCM wamesababisha kwa kudhamiria kabisa kuizuia nchi kupata maendeleo yoyote.

CCM na viongozi wake wa awamu hii wanaua demokrasia ili wasihojiwe na yoyote wanapotekeleza mikakati yao kutokea kuzimu.

Hivyo nashauri vikwazo wawekewe viongozi wa CCM na mali zao na familia zao tu. Sisi raia wa kawaida tuachwe tuendelee na maisha ya kuikabili CCM mpaka tutakapoweza kuiondoa.

Mpaka sasa wapo viongozi wanaopaswa kunyimwa VISA za kwenda huko kwa "mabeberu". Mfano Bashite, Kabudi, Spika, Rais na baadhi ya mawaziri na wabunge.
 
Back
Top Bottom