Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi asema serikali itaendelea kuitunza demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa 2024/25

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
1692785148007.jpeg

Rais Hussein Mwinyi amekuwa ni mgeni rasmi katika Mkutano wa Kitaifa wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji 2024 na uchaguzi mkuu 2025

Katika ushiriki wake, Rais mwinyi amezindua mpango wa kukuza mjadala ya vyama vingi na kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika siasa na uchaguzi.

Akizungumza kuhusu hali ya demokrsia, Rais amezungumza yafuatayo kuhusu hali ya demokrasia nchini. Ametaja mchakato wa mabadiliko ya sheria yaliyofanyika pia ameongelea suala la vyama vingi na namna ambayo demokrasia ya vyama vingi ilivyolindwa nchini.

Amesema kwa pamoja mambo mengi yamefanikiwa. Aidha amewapongeza TCD kwa kuandaa mkutano huu kwa kujadili hali ya demokrasia. Na amewapongeza viongozi wa siasa na wa serikali waliohudhuria katika mkutano. Ametoa wito wa TCD kuendeleza kuandaa mikutano hii ili kuendeleza demokrasia kwa kuwa inaonesha ukomavu wa kisiasa katika nchi yetu. Rais Mwinyi pia amepongeza CSO's na viongozi wa dini waliohuduhuria.

Rais Mwinyi amesema mapendekezo ya wadau yaliyotolewa katika mkutano huu yatafanyiwa kazi. Mapendekezo yaliyotolewa na wadau ni mengi ikiwa ni pamoja na kurejea mchakato wa katiba mpya, kubadili sheria za uchaguzi na kuwa na usimamizi mmoja kwa chaguzi zote.

Aidha Mwinyi amesema serikali itaendelea kuitunza demokrasia nchini.
1692785222460.jpeg
 
Back
Top Bottom