Nzega: Rais Magufuli asema Demokrasia imeimarika sana nchini ndio maana wengine walijitoa kwenye uchaguzi, wengine wakashinda na kushindwa

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,954
2,000
Aman iwe juu yenu wakuu,

Rais Magufuli akiwa njiani Wilaya ya Nzega kuelekea Shinyanga amewahutubia wananchi wa Wilaya ya Nzega na kuwapongeza viongozi wote walioshinda katika Uchaguzi wa Serikari za Mitaa.

Aidha, katika hotuba hiyo Raisi Magufuli akigusia kuhusu Uchaguzi wa Serikali za mitaa amesema kuwa "Demokrasia sio kushindwa tu, ni pamoja na kushinda lakini demokrasia ni pamoja na kujitoa.

Akifafanua kuhusu suala baadhi ya viongozi kujitoa katika uchaguzi huo, Rais Magufuli amehoji kuwa "Ukishajiona hauna nguvu, utashindana na wenye nguvu?"

Mwisho, Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote walioshinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwasisitiza viongozi hao kufanya kazi na kulinda amani na utulivu wa nchi yetu.

======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kitendo cha kususia uchaguzi na kujitoa katika uchaguzi pia ni demokrasia huku akikisitiza kuwa maendeleo hayana chama na kwamba Watanzania wanatakiwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Novemba 27,2019 wakati akizungumza na wananchi wa Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kukipongeza Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24,2019 ambapo baadhi ya Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vilisusia uchaguzi huo

“Ninapenda kuwashukuru sana ndugu zangu wa Isaka mmemaliza chaguzi, Nimeambiwa Chama Cha Mapinduzi kimepasua vizuri. Hongereni sana,maendeleo ndugu zangu hayana chama na demokrasia hata kujitoa nayo ni demokrasia,kususia uchaguzi nayo ni demokrasia”,amesema Rais Magufuli.

“Kwa hiyo nawapongeza kwa ushindi mkubwa mlioupata chama cha mapinduzi lakini maendeleo hayana chama ni lazima tushikamane wote kujenga taifa letu,tunachohitaji ni maendeleo,ukileta maji,wote watakunywa,uwe CCM, uwe CHADEMA,ukileta bandari hapa kila mmoja atafanya biashara”,ameongeza Rais Magufuli.

“Naomba Watanzania tutangulize mbele maslahi ya taifa letu,tuwe wamoja,tujenge Tanzania yetu”,amesema Rais Magufuli.

 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,319
2,000
Sasa wameshinda kwa asilimia 99.7, nafikiri na maendeleo kwa kipindi hiki yafikie asilimia hizo hizo kwa kipimo cha World Bank au UN au OECD.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
80,415
2,000
2221522_1574681195213.png
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,454
2,000
Halafu hawa jamaa wasitu potezee bundle zetu wengine hela yenyewe ngumu mtaani. Kama hotuba ni 40% plus ni kwa kisukuma waseme mapema sie wamakabila tusioongea hiyo lugha tuokoe muda na hela.
 

sawima

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
4,155
2,000
Halafu utakuta nyumbu wanampigia makofi paa paa paa! Basi kichwa kinavimba kinakuwa kikubwa hadi kg 200.
 

comrade wetu

JF-Expert Member
Nov 5, 2018
964
1,000
"Maisha ni magumu fedha hakuna watu wana hali mbaya wakina mama wananyang’anywa televisheni, friji kwa ajili ya mikopo. Tunaomba mheshimiwa tuachie fedha mengine yote hatuna tatizo na wewe,” amesema Abel Mpinga, mkazi wa Wilaya ya Igunga mbele ya Rais John Magufuli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom