Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

Naona sasa watabeba hadi shuka
Hivi hii imani ya kuamini mbunge akiwa wa upinzani tu basi anafanya kazi na wa ccm hafanyi kazi imetoka wapi hii imani? Mara ngapi tunaona wabunge wabunge wa upinzani hawachangii chochote bungeni,tunamuona Lissu na Mnyika tu?
 
Wanabodi,

Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.

Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani. Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza, Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu. Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi. Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja Kigamboni kwa kuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwa sababu walikuwa makazini.

Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:

1.Wabunge wengi wa CCM kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni, hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania, hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo. Hii imepelekea kuishushia serikali na CCM heshima kwa wananchi.

2.Wabunge wengi wa CCM kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali, hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa. Hapa tunaona hata Dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili (rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi), hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.

3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja, kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.

4.Wabunge na mawaziri wa CCM kulala bungeni hovyo, hili huwashushia heshima sana.

5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.

Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama. Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni, ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo. Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu, kwani zote zimeprove failure. Mwenye kuelewa ataelewa, wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.
ahsante kaka kwa ukweli umeuweka bayana,CCM kwa sasa tumbo joto,so wana jaribu kurudisha nguvu kama zama za kale wakati walipo jua muda wao uko ukingoni.
 
Wawe wanatuonesha basi na waliyoyafanya katika majimbo yao,sio kutaka kuwaona wakiwa bungeni live.
 
Sasa kama nilikupiga na magongo halafu sijui kuongea kingereza kwa ufasaha na ukashabikia nikuchakachue unataka bunge live la nini kwani we UKAWA? msubiri taarifa za chama chetu cha kale miaka 50 ilyopita
 
Hamna kazi za kufanya?
je wale wanaoonyeshwa vipindi vingine vya TV wakati wa kazi asubuhi hawana kazi ya kufanya au vipindi hivyo ni kwa ajili ya misukule? unaonaje vituo vyote vya TV na redio vikifungwa muda wa kazi badala ya kuzuia mijadala ya bunge tu ndio isionekane? na je kipindi cha maswali na majibu kinachoonyeshwa saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana huu sio MUDA WA KAZI? naomba ufafanuzi juu ya hoja hizi mkuu FaizaFoxy.
 
kuna kipindi TBC walikuwa wanalipia na kurusha ligi ya uingereza live,sasa hivi bunge wanasema gharama,akitokea wakulipia wanageuza kibao.Ndio tatizo katibu uenezi kuwa waziri wa habari,bado anafanya kazi yake ya kueneza na kujenga chama.
ila kwa upuuzi huu anaoufanya sasa hajengi chama ila anabomoa.
 
Mada iko kwenye kuonekana live. Kwani hizo hoja haziwez kutoka had wawe live? Wapiganie haki zetu na wawe wanarudi kutupa mrejesho majimboni kwetu sio kila siku tuwe tunawaona kwenye tv. Tunataka maendeleo sio nani kasema nini bungeni.

oky,vizuri kama umekubaliana na mimi kuwa lazima wabunge watoe hoja.je,wasipokuja kukupa mrejesho?je,wakija wakakupa mrejesho wa uongo?Utapimaje kama wanasema ukweli?
 
Fanyezi kazi kusikiliza Bonge hakutasaidia chochote kwa maisha ya wanamchi wa kawaida
Kama wewe unaona iwe hivyo kwanini ushauri na wabunge wafutwe kabisa ili nchi hii iendeshwe na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa mikoa wa CCM?
 
Umenena vyema ila no.2 na 3 sioni utofauti uliopo kimantiki
 
kama ni hivyo,kwanini isiangaliwe namna ya kuwadhibiti wanaotukana?mkono ukichafuka unaukata?unauosha na maisha yanaendelea.Kuna mabunge mpaka wanapigana lakini bado wanarusha live.cheki hii,

Sioni watu humu kukelwa na mambo ya hovyo yanayofanywa na wabunge kule bungeni ila watu wao wanalilia kuona bunge live tu,kutokuonesha bunge live ndio itakuwa mkono umeoshwa baada ya mtoto kuuchafua. Hayo mabunge wanayopigana hayawezi kuwa ndio kiigezo chema hapa,maana isije siku tukawa tunalalamika aibu ya mbunge kuzungumzia shanga bungeni mkaja na mfano wa bunge lenye kufanya mapenzi bungeni.
 
Hujaomba kazi kwa Dangote?

Hujaomba kazi kwenye kampuni zaidi ya 20 za gas?

Wageni wamejazana Tanzania kwa fursa zilizokuwepo za kazi za kila aina lakini hamzioni.

Sishangai kwanini huzioni kwani time ya watu kufanya kazi wewe unataka kutazama bunge.

Kalagabaho.
halafu pia hajaomba kazi kwenye VIWANDA vya magufuli?
 
Ni haki yetu kama wananchi kuangalia Bunge live. Sasa nauliza wabunge wa upinzani mbona wapo kimya??
kwani wabunge wa CCM wao hili haliwahusu au wanaCCM wao hawana haja na taarifa kama hizi?
 
Sioni watu humu kukelwa na mambo ya hovyo yanayofanywa na wabunge kule bungeni ila watu wao wanalilia kuona bunge live tu,kutokuonesha bunge live ndio itakuwa mkono umeoshwa baada ya mtoto kuuchafua. Hayo mabunge wanayopigana hayawezi kuwa ndio kiigezo chema hapa,maana isije siku tukawa tunalalamika aibu ya mbunge kuzungumzia shanga bungeni mkaja na mfano wa bunge lenye kufanya mapenzi bungeni.

Ina maana usipoonesha live ndio matusi yataisha?Bunge ina kamati ya maadili,huko ndiko wabunge wanapochukuliwa hatua.Eti kisa mbunge fulani katukana ndio uwanyime wananchi haki ya kuangalia bunge!pathetic
 
Back
Top Bottom