Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

Siasa ni biashara,na biashara ni matangazo,serikali kula muda ipo inajitangaza na kutangazwa kuwa inafanya kazi ilikujenga imani kwa wananchi,muda huo haitaki wananchi wajue madhaifu yake kupitia bunge..ngoja tujipe moyo tutayajua tu hata kwa njia zingine.
 
Shame on me? No, shame on u brother, kwani hakuna namna nyingine ya sisi kujulishwa kilichokuwa kikiendelea Bungeni iwe na Wabunge wetu au hizo Media, badala ya watu kukaa mwanzo mwisho wanaangalia live, nyinyi hamna kazi za kufanya?
mbona kipindi cha MASWALI & MAJIBU kinaonyeshwa laivu kati ya saa 3 asubuhi na saa 7 mchana. je, huu sio MUDA WA KAZI? na je, mbona vipindi vingine vya TV huwa vinarushwa muda wa kazi? je, ni nani anayetazama vipindi hivyo? na kama muda wa kazi ndio hoja, vipindi vinavyorushwa usiku wa manane (MUDA WA KULALA) vinatazamwa na nani? jibu hizi hoja kwa ufasaha ili malofa, wapumbavu na wanywa viroba tuelewe.

cc: FaizaFoxy
 
Bunge kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live, kunawapunguzia nini Wabunge jukumu lao la kuishauri na kuisimamia Serikali?

Wakae ndani humo humo waisimamie Serikali kwa hoja zenye mashiko sio fitina fitina na uchochezi tu, baadhi Wabunge wanataka kugeuza Bunge kama ukumbi wa kufanya siasa ili kujipatia umaarufu mwepesi mwepesi huku wakionekana live.

Sasa tuone kama Bunge lisiporushwa live watatueleza walikwenda Bungeni kuonekana live, au walikwenda kuwasilisha hoja za msingi juu ya matatizo ya wananchi na kuisimamia Serikali kuhakikisha inawajibika?
Bahati yako tcra wananiona lakini ulikuwa halali yangu kukushona matusi yote makubwa duniani.....yakiwemo na yanguoni lkn basi huu mfumo wa zuia matusi na bunge ofline umekupakichwa na sii bure wewe ni moja kati yawaliopitisha upuuzi huu wa kuweka vitu ofline maana uwezo wako wakujenga hoja ndo vile tena,lkn nadhani weweeeeee ni......😵!
 
Shame on me? No, shame on u brother, kwani hakuna namna nyingine ya sisi kujulishwa kilichokuwa kikiendelea Bungeni iwe na Wabunge wetu au hizo Media, badala ya watu kukaa mwanzo mwisho wanaangalia live, nyinyi hamna kazi za kufanya?
Yaani wewe kama ni shule basi unapaswa ukarudie tu,maana hoja zako uzitowake ni zero,sasa watakapo baliki madudu huko gizani mnataka mje msingizie eti na wapinzani walikubali? Au nini maana ya vyombo vya habari kwako? Nikuwaonesha mawaziri na wakuu wa mikoa wakiachishwa kazi ama nini??!!! Au kwako habari ni kuzuia UINGIZWAJI WA SUKARI NCHINI WAKATI SUKARI SASA TUNANUNUA 2800 HUKU KIJJNI KWETU? au wewe siyo mtanzania hivyo huna ukijuacho basi pole tuache sisi waTz marofa tuhoji vitu vya kutujenga.
 
mbona kipindi cha MASWALI & MAJIBU kinaonyeshwa laivu kati ya saa 3 asubuhi na saa 7 mchana. je, huu sio MUDA WA KAZI? na je, mbona vipindi vingine vya TV huwa vinarushwa muda wa kazi? je, ni nani anayetazama vipindi hivyo? na kama muda wa kazi ndio hoja, vipindi vinavyorushwa usiku wa manane (MUDA WA KULALA) vinatazamwa na nani? jibu hizi hoja kwa ufasaha ili malofa, wapumbavu na wanywa viroba tuelewe.
Ndg yangu wewe hakuna mwenye timamu atakujibu,hao wanaotetea ofline bunge ndo kwanza sukari wananunua 2400 na hawajui kuwa ni wapi wanaweza kujadili na kutatua mgogoro.
 
huwezi ukajua na kumpangia muda mtu aliejiajiri kufanya kazi hizo radio na tv zipo masaa 24 ni kwa ajili ya nani? waanze kutangaza saa mbili usiku tutimize hapa kazi tu.

Hiyo saa mbili usiku ni nani alikudanganya? Au unaota?

Bunge lenyewe limetangaza kuna feeder yao itarusha matangazo yote na channel yoyote ya tv wanaweza wakachukua hapo na kurusha wapendavyo, si kujazana kila channel na mitambo yao bungeni.

Mambo yanaendeshwa kisasa zaidi.
Tumieni vichwa vyenu japo kufikiri kiduchu siyo kuviwacha mizigo juu ya mabega.
 
Kuna umuhimu wa bunge kuonekana live kwa upande mwingine sioni umuhimu sababu kipimo cha mbunge sio kujenga hoja au kuonekana byngeni. Kipimo sahihi cha mbunge ji nini anafanya katika jimbo lake. Lowasa, mwandosya na wengine wengi wamefanya makubwa majimboni mwao na wakaonekana bora sio kisa et walikua wakichangia sana bungeni au kuonekana mara kwa Mara.mnyika alikua msemaji mzuri sana bungeni lkn jimboni kwake hamna kitu. Wananchi tunataka maendeleo majimboni kwetu sio porojo za kwenye tv.
Na hii itasaidia hii nchi kila mbunge kupiga kazi jimboni kwake coz ndo itakua sehem ya yeye pekee kuonekana tofauti na mwanzo mbunge akionekana bungeni tu kashamaliza kazi hata kurudi jimboni kujua nini kinaendelea hataki.anajua tu umaarufu wa bungeni utambeba.nadhani sasa tutawaona wabunge wetu majimboni maana bila hivo imekula kwake.
 
Yaani wewe kama ni shule basi unapaswa ukarudie tu,maana hoja zako uzitowake ni zero,sasa watakapo baliki madudu huko gizani mnataka mje msingizie eti na wapinzani walikubali? Au nini maana ya vyombo vya habari kwako? Nikuwaonesha mawaziri na wakuu wa mikoa wakiachishwa kazi ama nini??!!! Au kwako habari ni kuzuia UINGIZWAJI WA SUKARI NCHINI WAKATI SUKARI SASA TUNANUNUA 2800 HUKU KIJJNI KWETU? au wewe siyo mtanzania hivyo huna ukijuacho basi pole tuache sisi waTz marofa tuhoji vitu vya kutujenga.

=bariki
 
Chukuweni TV channels majimboni kwenu mtuoneshe mnafanya nini wakati hamna vikao vya bunge.

Bungeni mkatunge sheria na tutawaona kupitia feeder na streaming za tovuti ya bunge, kwanza teknolojia itayotumika itatuwezesha kutazama tuyatakayo.

Kuna wabunge wamekaa miaka mitano hawajasimama kuongea au wamesimama mara chache sana lakini majimboni mwao wanapita bila kupingwa kwa kuwatumikia wananchi wao.

Mpaka sasa sijaona faida ya kuwa na bunge live. Saa nyingine wanakaa masaa kupiga na kuhesabu kura, inahusu nini kukaa muda wote unapoteza kutazama? Si ungoje matokeo tu?

Iwe live isiwe live walitakalo walio wengi ndiyo litapita.
 
Naanza kumkumbuka kikwete, huyu jamaa anasema tumuombee mungu iliatuongoze vizuri wakati huo uo anaatumia nguvu nyingi ili kuzuia wanainchi wasijue kinachoendelea ndani ya bunge sasa mtu aliyehamua kufanya kazi kwa ajili yetu leo hataki tutumie vyombo vyetu wenyewe tunavyoviendesha kwa kodi zetu ili kutuletea habari, ina maana hataki tujue ukweli na anaturudisha kipindi kile cha giza na pia nina hisi ktk nchii hii hawapendi wanainchi wajue nini kinaendelea duniani na mambo yanayoendelea hapa tanzania, walikuwa wanasema wanapata kura nyingi kutoka vijijini ambako asilimia kubwa hawana umeme na hayo magazeti kwao ni hanasa na ndio mambo wanayopenda kuona yanabaki hivyo kwa baadhi ya wanasiasa,
Karne hii uwezi kuzuuia nguvu wa press maana mwisho wa siku aibu itakuwa yako, sasa najiuliza hivi kweli kwa mambo haya tutakuja kujua au kutangaziwa mikataba ambayo serikali imeingia kama madini na gesi
Tutamkumbuka kikwete kwa kuwa karibu na vyombo vya habari, na kuwa mvumilivu na ndio siasa au demokrasia hiyo, uko tuendako naona giza, tumetoka gizani miaka ya 80 na ndiko huko tunakorudi na sio muda mrefu ngoja tuone
 
Wanabodi,

Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.

Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani. Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza, Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu. Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi. Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja Kigamboni kwa kuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwa sababu walikuwa makazini.

Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:

1.Wabunge wengi wa CCM kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni, hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania, hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo. Hii imepelekea kuishushia serikali na CCM heshima kwa wananchi.

2.Wabunge wengi wa CCM kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali, hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa. Hapa tunaona hata Dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili (rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi), hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.

3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja, kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.

4.Wabunge na mawaziri wa CCM kulala bungeni hovyo, hili huwashushia heshima sana.

5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.

Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama. Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni, ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo. Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu, kwani zote zimeprove failure. Mwenye kuelewa ataelewa, wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.

Huo ni mtihani kwa Raids JPM kama ana nia njema hawezi kukubali Bunge liendeshwe 'gizani' kulinda mafisadi. Hawa watu wanajilipa mamilioni kwa kodi za wanyonge halafu wanataka wananchi haohao wasijue fedha yao inavyotumika? Kama ni hivyo Bunge la nini? Narudia: Hiki ni kipimo cha Utawala Bora wa JPM.
 
Hiyo saa mbili usiku ni nani alikudanganya? Au unaota?
.

Tumieni vichwa vyenu japo kufikiri kiduchu siyo kuviwacha mizigo juu ya mabega.

pumba zingine bwana unaweza ukafikiri aliendika anaakili kumbe takataka kabisa mala fanyeni kazi muingize kipato mala litarusha lenyewe mala tutarekodi tutarusha matukio muhimu jambo moja lina majibu mengi sana halafu yasiyotekelezeka!!!! cha kushangaza hayo yote majibu yanatoka serikalini wanazid kujikanyagakanyaga msimamo hamna ina maana ni waongo inatumika kila aina ya kauli na nyie makada mnayabeba bila hata kuyafikilia mnayabwaga tu mwisho wa siku ni aibu hakuna namna.

walikuwa wapi kuyafanya hayo mapema hadi bunge limeanza zimeanza ngonjera zao hizo na kujitapa tapa na hayo hapo chini uliyoyaandika?

Bunge lenyewe limetangaza kuna feeder yao itarusha matangazo yote na channel yoyote ya tv wanaweza wakachukua hapo na kurusha wapendavyo, si kujazana kila channel na mitambo yao bungeni.

Mambo yanaendeshwa kisasa zaidi

mi nshakwambia fuatilia lugha ya picha ya january makamba.
 
Chukuweni TV channels majimboni kwenu mtuoneshe mnafanya nini wakati hamna vikao vya bunge.

Bungeni mkatunge sheria na tutawaona kupitia feeder na streaming za tovuti ya bunge, kwanza teknolojia itayotumika itatuwezesha kutazama tuyatakayo.

Kuna wabunge wamekaa miaka mitano hawajasimama kuongea au wamesimama mara chache sana lakini majimboni mwao wanapita bila kupingwa kwa kuwatumikia wananchi wao.

Mpaka sasa sijaona faida ya kuwa na bunge live. Saa nyingine wanakaa masaa kupiga na kuhesabu kura, inahusu nini kukaa muda wote unapoteza kutazama? Si ungoje matokeo tu?

Iwe live isiwe live walitakalo walio wengi ndiyo litapita.
Akili ya kushikiwa!
 
maku ana ubavu wa kufanya kinyume na itakavyo ccm,isitoshe serikali ya Maku inataka iwe inasifiwa tu,kwa kila kitu haitaki kukosolewa hivyo suala la bunge kutoonyeshwa live Maku analifuraia sana
 
um
Tatizo hili jambo hujadiliwa kwa mitazamo ya kiccm na kiupinzani,tukubaliane tu kwamba kuna ubaya na uzuri wake wa kuonesha bunge live.

umefanya tathmini ukajua hasara ni zipi na faida ni zipi?
 
Back
Top Bottom