Nyuma ya pazia Bunge live

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
17,142
26,132
Wanabodi,

Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.

Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani. Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza, Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu. Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi. Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja Kigamboni kwa kuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwa sababu walikuwa makazini.

Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:

1.Wabunge wengi wa CCM kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni, hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania, hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo. Hii imepelekea kuishushia serikali na CCM heshima kwa wananchi.

2.Wabunge wengi wa CCM kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali, hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa. Hapa tunaona hata Dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili (rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi), hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.

3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja, kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.

4.Wabunge na mawaziri wa CCM kulala bungeni hovyo, hili huwashushia heshima sana.

5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.

Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama. Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni, ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo.

Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu, kwani zote zimeprove failure. Mwenye kuelewa ataelewa, wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.
11141222_234341680264366_1467486594332651248_n.jpg

 
Wanabodi,
Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.
Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani.Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza,Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu.Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi.Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja kigamboni kwakuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwasababu walikuwa makazini.

Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:

1.Wabunge wengi wa ccm kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni,hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania,hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo.Hii imepelekea kuishushia serikali na ccm heshima kwa wananchi.

2.Wabunge wengi wa ccm kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali,hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa.Hapa tunaona hata dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili(rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi),hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.

3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja,kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.

4.Wabunge na mawaziri wa ccm kulala bungeni hovyo,hili huwashushia heshima sana.

5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.

Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama.Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni,ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo.Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu,kwani zote zimeprove failure.Mwenye kuelewa ataelewa,wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.
Mwisho wa siku watasema bunge limekubaliana hata kama wengine wanapinga na hawataki tusikie hoja zinzotolewa kupinga jambo lolote
 
Mwisho wa siku watasema bunge limekubaliana hata kama wengine wanapinga na hawataki tusikie hoja zinzotolewa kupinga jambo lolote

tunaelekea kubaya,hawa wanaoshangilia wanaona wanawakomoa upinzani bila kujua mwananchi ndiye anayepiganiwa haki zake
 
Mimi namshangaa Magu anachoogopa ni nii? Kama anasema tumuombee sisi watanzania huku anatuwekea ukungu kwenye mambo yanayotuhusu si muelewi vile!

wananchi wamemkubali Magufuli na utendaji wake,akilazimisha kukibeba chama anaweza jikuta kinakuwa mzigo kwake na chenyewe ndio kinamvuta chini.
 
Nasikia hata waandishi wanaoruhusiwa kuingia bunge ni hawaruhusiwi kuwa na kamera wa tape recorder jambo la ajamu sana kuzuia vitendea kazi

Tutajuaje kuwa wabunge wetu wanawajibika?Yaani tuletewe story tu kama za vijiweni
 
Back
Top Bottom