Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

tatizo mwenezi wa chama kawa waziri wa habari,bado anaendeleza mbinu za fitna alizokuwa anafanya akiwa katibu mwenezi.Kajisahau na Magufuli anamwangalia tu
sasa wananchi watazijuaje sera na malengo ya serikali wanayolilia tuiunge mkono? duh
 
Mhimili wa bunge ni shida; hautaki wananchi wajue kinachoendelea bungeni. Mhimili wa serikali unajitahidi kuwapa wananchi habari hata jana tulishuhudia uzinduzi wa daraja la kigamboni live.
 
Ni hivii wanajua itakuwa ni aibu kwa serikali kwa kuwa wabunge wa chama chetu hawajazoea kuikosoa serikali. Leo wabunge watawala wanaweza pinga hoja fulani kesho Mkulu anatangaza kumtumbua muhusika ambaye wabunge wa CHAMA walimtetea kwa nguvu zote. Nadhani Hapa mkulu anataka kurekebisha kitu....labda akiona wabunge wake wameshajielewa anaweza akaondoa marufuku hiyo...

unajua wabunge wa CCM mpaka sasa HAWAJUI kama business as usual kwa maana ya "ndiyoooo" au utaratibu mpya wa kuchambua hoja.
 
ni jambo la ajabu sana watu wazima tena kuna wanaume kabisa wanalilia kuangalia tv. kuna watu humu itakua wananyanganyana remote na wake zao na watoto.

Hizi ndizo akili za madc watarajiwa,kweli Tz ina hazina si ya rasilimali pekee bali pia wajinga wajinga.
 
ni jambo la ajabu sana watu wazima tena kuna wanaume kabisa wanalilia kuangalia tv. kuna watu humu itakua wananyanganyana remote na wake zao na watoto.

Ningeshangaa sana kama usingeongea pumba ya kiwango hiki.
 
Wanataka wahariri then waje na habari nzuri tulizozoea kusikia,michakato na upembuzi yakinifu.
hii ni sawa na upuuzi haina logic kabisa kuwanyima wananchi haki yao ya msingi. halafu unakuja kuwahadithia kama watoto wadogo.
 
ni kweli kabisa mkuu. CCM hayataki madudu yao yaonekana na yanafahamu fika kwamba wapinzani wanapata sifa sana bungeni kwa kuwatetea wananchi wakati CCM wanatetea matumbo yao.
 
ni kweli kabisa mkuu. mafisiemu hayataki madudu yao yaonekana na yanafahamu fika kwamba wapinzani wanapata sifa sana bungeni kwa kuwatetea wananchi wakati ccm wanatetea matumbo yao.

wapinzani ndio wanaonekana watetezi wa wananchi
 
Awamu ya watafuta sifa kwenye vyombo vya habari.Hapa giza tu.
 
Nat
Wanabodi,

Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.

Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani. Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza, Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu. Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi. Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja Kigamboni kwa kuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwa sababu walikuwa makazini.

Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:

1.Wabunge wengi wa CCM kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni, hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania, hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo. Hii imepelekea kuishushia serikali na CCM heshima kwa wananchi.

2.Wabunge wengi wa CCM kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali, hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa. Hapa tunaona hata Dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili (rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi), hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.

3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja, kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.

4.Wabunge na mawaziri wa CCM kulala bungeni hovyo, hili huwashushia heshima sana.

5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.

Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama. Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni, ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo. Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu, kwani zote zimeprove failure. Mwenye kuelewa ataelewa, wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.
Tutafute namna ya kuilazimisha serekali ili ifuate matakwa ya wananchi, nafikiri wabunge wa upinzani wamefanya upande wao,Swali ni wananchi wanachukua uamuzi gani ili serekali iwasikilize?
 
Serikali yetu ipo juu ya sheria, mahakama zetu ni za walalahoi, serikali inaingilia mahakama na kuvuruga kila kitu, mahakama ikigoma, hapo kuna kung'olewa meno
 
Bunge kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live, kunawapunguzia nini Wabunge jukumu lao la kuishauri na kuisimamia Serikali?

Wakae ndani humo humo waisimamie Serikali kwa hoja zenye mashiko sio fitina fitina na uchochezi tu, baadhi Wabunge wanataka kugeuza Bunge kama ukumbi wa kufanya siasa ili kujipatia umaarufu mwepesi mwepesi huku wakionekana live.

Sasa tuone kama Bunge lisiporushwa live watatueleza walikwenda Bungeni kuonekana live, au walikwenda kuwasilisha hoja za msingi juu ya matatizo ya wananchi na kuisimamia Serikali kuhakikisha inawajibika?
wewe JUHA kweli. sasa wewe mwananchi utapata wapi mrejesho juu ya uwajibikaji wa mbunge uliyemtuma kukuwakilisha bungeni kama unashabikia kufichwa kwa taarifa za bunge? majitu kama wewe ndio mnapelekea nchi hii isipige hatua za maendeleo. waachieni akina lugumi waendelee kukuibia kimyakimya.
 
Back
Top Bottom