PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 454
- 631
Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema akiingia Ikulu atarejesha hadhi ya Bunge madhubuti lenye hoja, usimamizi na uwajibishaji wa serikali, badala ya kuwa la kusifia.
Amesema hataki kuona bunge la “machawa” wanaomsifia rais muda wote badala ya kuikosoa serikali inapokosea, akisisitiza kuwa serikali yake itahakikisha Bunge linakuwa huru na lenye nguvu ya kweli ya kuisimamia serikali.
Mwalimu amebainisha kuwa wabunge watawezeshwa kuwa na watafiti wa kuwasaidia kuandaa hoja zenye tija kwa taifa na wapiga kura wao, ili mjadala bungeni uwe wa hoja na si wa vioja.
“Tunahitaji Bunge makini, lenye hoja, si Bunge la kusifia tu. Sitaki wabunge wa kupiga makofi tu, nataka wabunge wa kusimamia masilahi ya wananchi,” amesema Mwalimu akiwa Urambo, mkoani Tabora, wakati akiendelea kuomba ridhaa ya kuingia Ikulu.