Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

je wale wanaoonyeshwa vipindi vingine vya TV wakati wa kazi asubuhi hawana kazi ya kufanya au vipindi hivyo ni kwa ajili ya misukule? unaonaje vituo vyote vya TV na redio vikifungwa muda wa kazi badala ya kuzuia mijadala ya bunge tu ndio isionekane? na je kipindi cha maswali na majibu kinachoonyeshwa saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana huu sio MUDA WA KAZI? naomba ufafanuzi juu ya hoja hizi mkuu FaizaFoxy.

hawezi kukujibu,kwenye bold huo ndio ushahidi kuwa kigezo si kubana matumizi,wala muda wa kazi.Hapa ni kufukia makando kando ya serikali,hii inaruhusu serikali kutoa maelezo tu bila sisi kupata kusikia upande wa pili ambao ndio wawakilishi wetu wana maoni gani.Huu ni ujinga na ubwege wa hali ya juu
 
Well said,
Uhuru wa habari ni jambo jema. Hakuna binadamu mwenye akili timamu ataacha kujishugulisha na kipato chake akaangalia TV hata kama ni filamu. Nadhani Serikali iache bunge liwe live, Ukilinganisha na mfano wa uingereza kuwa kuna studio za bunge, Tanzania 'freedom of expression' and 'infstructure' hazijafika huko.
Bunge liwe live, ... by the way bunge halikutani siku 365 za mwaka
 
RAIS MAGUFULI RAIS WETU KWA MAMLAKA ULIYONAYO TENGUA SUALA HILI!
""TENGUA USINGIZI BUNGENI""
""TENGUA TUWAJUE VILAZA""
""TENGUA TUWAJUE MADOMO ZEGE""
""TENGUA TUWAONE TULIOWACHAGUA WANATUWAKILISHA VEMA AU LA""

cc:-
Rais
spika
katibu wa bunge
n.b:-
Tutawatambuaje wabunge wetu ambao hawatuwakilishi vyema.
 
Hivi wale wabunge ambao walikuwa wakiongea maneno ya hovyo na matusi kiasi cha kushindwa hata kuangalia bunge ukiwa na mtu unayemuheshimu,ndiyo michango ambayo watu mnataka kuiona kutoka kwa wabunge wenu kwa kuoneshwa bunge live? Huu uoneshaji bunge live una faida zake na hasara zake.
NDIYO tunataka hivyo kwa kuwa wanatuwakilisha sisi na tuliwachagua sisi...tunataka tuone ni mbunge gani anayetukana badala ya kuchangia hoja ili bunge lijalo tumpige chini. sasa kama unamficha tusimuone huyo mtukanaji si tutakuwa tunamrejesha bungeni kila mara? na je, wale wanaolala bungeni badala ya kutuwakilisha vema tutawajuaje ili tuwapige chini uchaguzi ujao? huu ndio umuhimu hasa wa kuonyesha bunge laivi ili kuwawezesha wananchi kuwajua vizuri wawakilishi wao na kisha kuwachukulia hatua wakati wa uchaguzi. umeona eeh?
 
Wanabodi,

Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.

Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani. Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza, Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu. Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi. Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja Kigamboni kwa kuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwa sababu walikuwa makazini.

Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:

1.Wabunge wengi wa CCM kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni, hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania, hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo. Hii imepelekea kuishushia serikali na CCM heshima kwa wananchi.

2.Wabunge wengi wa CCM kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali, hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa. Hapa tunaona hata Dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili (rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi), hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.

3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja, kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.

4.Wabunge na mawaziri wa CCM kulala bungeni hovyo, hili huwashushia heshima sana.

5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.

Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama. Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni, ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo. Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu, kwani zote zimeprove failure. Mwenye kuelewa ataelewa, wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.
ikumbukwe jk anaonekana dhaifu kwakuwa alitoa uhuru wa kukosolewa,sasa wengine wanataka kusifiwa muda wote which is wrong, no one is perfect...
 
Sasa kufungiwa kuona bunge time za kazi ndiyo umedhulumiwa?

Badala ya kushukuru umesaidiwa uende ukafanye kazi za kukuingizia kipato wewe unalialia.
mbona vipindi vingine havizuiwi muda wa kazi? kama suala ni kazi mbona vipindi vingine vya TV na redio havizuiliwi kuonyeshwa wakati wa kazi? kushikilia msimamo kwamba CCM mnazuia kuonyesha bunge laivi kwa sababu ya 'KAZI' inadhihirisha ni jinsi gani ulivyo JUHA!
 
Chukuweni TV channels majimboni kwenu mtuoneshe mnafanya nini wakati hamna vikao vya bunge.

Bungeni mkatunge sheria na tutawaona kupitia feeder na streaming za tovuti ya bunge, kwanza teknolojia itayotumika itatuwezesha kutazama tuyatakayo.

Kuna wabunge wamekaa miaka mitano hawajasimama kuongea au wamesimama mara chache sana lakini majimboni mwao wanapita bila kupingwa kwa kuwatumikia wananchi wao.

Mpaka sasa sijaona faida ya kuwa na bunge live. Saa nyingine wanakaa masaa kupiga na kuhesabu kura, inahusu nini kukaa muda wote unapoteza kutazama? Si ungoje matokeo tu?

Iwe live isiwe live walitakalo walio wengi ndiyo litapita.
IKIWA UNASHABIKIA WALIO WENGI WAPITISHE CHOCHOTE WATAKACHO, MWISHO WA SIKU NI NANI ANAYEUMIA KAMA SIO WEWE MWANANCHI WA KAWAIDA? HEBU ANZA KUJITAMBUA WEWE BIBI KIROBOTO!
 
Wananchi tunamwamini Magu kupita kiasi na hii ni kutokana na kuwa na ushirikiano nasi na anasema tumsaidie kupambana na ufisadi. Namshauri Magu awe wazi aache bunge lirushwe live asipotii wananchi watapoteza imani ambayo hakuna wa kuirudisha tena, hakuna atakayemsaidia au kumwombea tena. Achukue tahadhari mapema......!
 
Ndugu acha kulalama. Hizo sababu zote tunazijua. Lete solutiona kwamba tutumie pressure gani kurudisha matangazo live.
 
Hivi hii imani ya kuamini mbunge akiwa wa upinzani tu basi anafanya kazi na wa ccm hafanyi kazi imetoka wapi hii imani? Mara ngapi tunaona wabunge wabunge wa upinzani hawachangii chochote bungeni,tunamuona Lissu na Mnyika tu?
unajua utaratibu wa kuchangia bungeni unakuwaje? acha ujinga wewe!
 
Tutajuaje kuwa wabunge wetu wanawajibika?Yaani tuletewe story tu kama za vijiweni
Hili swala mbona linapasua vichwa watu sana na kwanini kila kukicha watu wanalirudia kama si kutafuta kick? sijaona mahali popote duniani ambapo wabunge wa upinzani wanapigania agenda moja tu ya kurusha matangazo ya bunge live kama Tanzania. Maana hivi sasa hapa UK bunge lipo linaendelea na majadiliano na zaidi hayo sioni station yoyote inayoonyesha live hicho kikao chao cha budget zaidi ya siku moja katika wiki wakati kuna kipindi cha maswali na amjibu ya waziri Mkuu na hiyo ilikua jana baada ya kumalizika kila station iliurudi katika matangazo yao ya kawaida. lakini kina Msigwa wanataka kutuaminisha kuwa watatutalia matatizo yetu kwa kuonekana live wakitukanana kama tulivyoshuhudia katika vikao vilivyopita.angalieni
 
Back
Top Bottom