Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

Hili swala mbona linapasua vichwa watu sana na kwanini kila kukicha watu wanalirudia kama si kutafuta kick? sijaona mahali popote duniani ambapo wabunge wa upinzani wanapigania agenda moja tu ya kurusha matangazo ya bunge live kama Tanzania. Maana hivi sasa hapa UK bunge lipo linaendelea na majadiliano na zaidi hayo sioni station yoyote inayoonyesha live hicho kikao chao cha budget zaidi ya siku moja katika wiki wakati kuna kipindi cha maswali na amjibu ya waziri Mkuu na hiyo ilikua jana baada ya kumalizika kila station iliurudi katika matangazo yao ya kawaida. lakini kina Msigwa wanataka kutuaminisha kuwa watatutalia matatizo yetu kwa kuonekana live wakitukanana kama tulivyoshuhudia katika vikao vilivyopita.angalieni

Ni vema kama ungeweka pia mijadala mizito yenye maslahi kwa Umma ambapo ilisababisha serikali ichukue hatua madhubuti.Kuleta hizo video peke yake zinazoonyesha mtafaruku ni kujaribu kutuaminisha kuwa bunge halina maana na kazi yake ni vurugu.Kwenye mawazo kinzani lazima msuguano utatokea,hilo likitokea basi ni bahati mbaya lakini cha msingi suluhu ipatikane.Huko uingereza unakosema,kuna chanel maalum ya bunge ambapo yeyote anayetaka kurusha bunge basi anachukua kutoka kwenye feeder.Uhuru upo wa chombo chochote kuonesha au kutoonesha,uko huko hujui chochote mpaka sisi tukuhabarishe mambo ya huko?shame
Unazidi kupotosha kuwa wapinzani wanapigania agenda moja,hujui hata yanayoendelea bungeni sasa wewe umejuaje kuwa wanapigania agenda moja?Au unachanganya wapinzani na sisi wananchi ambao ndio tunalalamikia bunge kupewa uhuru wa kuoneshwa na chombo chochote kinachojisikia kufanya hivyo.
Hilo la msigwa umemnukuu wapi na lini akisema bunge kurushwa ndio litamaliza matatizo?Hapa tunazungumzia uhuru wa kupata habari bila kuhaririwa.
Ona mabunge haya ulimwenguni,sio tanzania tu migongano inatokea
 
NDIYO tunataka hivyo kwa kuwa wanatuwakilisha sisi na tuliwachagua sisi...tunataka tuone ni mbunge gani anayetukana badala ya kuchangia hoja ili bunge lijalo tumpige chini. sasa kama unamficha tusimuone huyo mtukanaji si tutakuwa tunamrejesha bungeni kila mara? na je, wale wanaolala bungeni badala ya kutuwakilisha vema tutawajuaje ili tuwapige chini uchaguzi ujao? huu ndio umuhimu hasa wa kuonyesha bunge laivi ili kuwawezesha wananchi kuwajua vizuri wawakilishi wao na kisha kuwachukulia hatua wakati wa uchaguzi. umeona eeh?
Mbunge gani aliyepigwa chini kutokana na huo uoneshaji bunge live?
Bunge lililopita tumeona wabunge waliyofanya mambo ya hovyo huko bungeni na bado wamerudi tena bungeni safari hii.
 
Mbunge gani aliyepigwa chini kutokana na huo uoneshaji bunge live?
Bunge lililopita tumeona wabunge waliyofanya mambo ya hovyo huko bungeni na bado wamerudi tena bungeni safari hii.
Mawaziri wa4 wamepigwa chini,mfano wassira.Kule kulala bungeni ndio kumemshusha.Lete pia mfano wa waliofanya mambo ya hovyo na matukio tuweke kumbukumbu sawa
 
Mbunge gani aliyepigwa chini kutokana na huo uoneshaji bunge live?
Bunge lililopita tumeona wabunge waliyofanya mambo ya hovyo huko bungeni na bado wamerudi tena bungeni safari hii.
wananchi ndio waamuzi, kama ukiona hivyo basi ujuwe wananchi wanaowakilishwa na hao wabunge hawajaona kama 'HAYO MAMBO YA OVYO' unayosema WEWE yanamzuia mbunge wao kuwatumikia. hivyo basi, nakubaliana nawe bunge lionyeshwe laivu....tuachane na wale wapuuzi wanaodai kwamba wananchi wasiowaone wawakilishi wao wanavyowawakilisha.
 
Ina maana usipoonesha live ndio matusi yataisha?Bunge ina kamati ya maadili,huko ndiko wabunge wanapochukuliwa hatua.Eti kisa mbunge fulani katukana ndio uwanyime wananchi haki ya kuangalia bunge!pathetic
Wabunge wanatafuta umaarufu pale bungeni na ndiyo maana vinatokea vituko,na kibaya ongezeko kubwa la watizamaji bunge ni kutaka kuona hivyo vituko.
 
SIFIKIRI KAMA HILI LA KIZUIA BUNGE NI AJENDA YA RAIS WETU MPENDWA NAKATAA KWA 100%,KWA VYOVYOTE HILI NI AGIZO LA CHAMA KIPENDACHO USIRI NA FARAGHA
*wizi huitaji faragha ili ukamilike
*faragha ndizo zilizotufikisha hapa tulipo.
*faragha na mwizi hawa ni ndugu moja.
NINGEFURAHI SIKU MOJA ENDAPO RAIS ANGETAMKA MIKATABA YOTE YA SEREKALI KUANZIA SASA ITAKUWA INAPITIA KWANZA BUNGENI.
 
Huu upuuzi waliofanya ccm utakuja kuliingiza taifa kwenye mtikisiko mkubwa au mgogoro mkubwa wa kiuchumi
Yani nchi iingie kwenye mtikisiko kisa bunge kutooneshwa live?ama kweli waafrika tuna matatizo.
 
Wabunge wanatafuta umaarufu pale bungeni na ndiyo maana vinatokea vituko,na kibaya ongezeko kubwa la watizamaji bunge ni kutaka kuona hivyo vituko.

so what?Cha msingi ni haki yetu ya kujua kodi yetu inapangiwaje matumizi na kwa vigezo vipi,hayo ya vituko wabanane wao wenyewe namna ya kurekebishana.
 
Back
Top Bottom