Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

hii serikali ya ajabu sana yaani inataka iungwe mkono na wananchi huku haitaki wakisikie inachopanga kukitekeleza pamoja nao.
sijajua ni GENIUS GANI kaishauri kufanya huu uvunjifu wa haki ya kupata habari mchana kweupe.
washauri wa CCM ni wa kiwango cha chini mno.
 
Naona hapa hata huelewi wananchi tunataka nini. Sisi hatujali wabunge wanajengaje hoja, tunachotaka ni kuona kinachojadiliwa bila kufanyiwa uhariri. Suala la kujenga hoja ama la sio lengo letu wananchi. Hivyo viwanda navyo mtavijenga kwenye kificho? Tunataka tuone kwa macho yetu na sio kusubiri eti mbunge bunge litakapokwisha aje atulishe matango pori. Wabunge wenyewe wa kuwasubiri waje watueleze kilichojifiri huko bunge ni hawa wala rushwa?

ni vema mwananchi mwenyewe akachuja mbivu na mbichi
 
hawa jamaa wakae wakijua kuwa ule ukumbi ni wetu tuna haki ya kusikia na kuona wanachokifanya mle ndani, kama hawataki kuonyesha bunge haina maana ya wao kuendelea kukaa mle heri tukaufunge ukumbi wetu. watafute vichaka vya kufanyia kazi zao ni vichakani pekee ambapo watu hufanya kazi mafichoni.
 
ni vema mwananchi mwenyewe akachuja mbivu na mbichi

Halafu hawa wanaoendesha bunge kijima ndio wanawaongopea wananchi eti Tanzania itakuwa nchi ya viwanda. Ni kipi kinachowafanya wajadili hayo mambo mazuri kwa kificho?
 
hakuna kazi halali inayoweza kufanywa kwa kificho wao wanafanya kazi gani humo ndani? yaani kujadili masuala ya wananchi tuyafanye behind closed doors?
 
Fanyezi kazi kusikiliza Bonge hakutasaidia chochote kwa maisha ya wanamchi wa kawaida
 
hii serikali ya ajabu sana yaani inataka iungwe mkono na wananchi huku haitaki wakisikie inachopanga kukitekeleza pamoja nao.
sijajua ni GENIUS GANI kaishauri kufanya huu uvunjifu wa haki ya kupata habari mchana kweupe.

tatizo mwenezi wa chama kawa waziri wa habari,bado anaendeleza mbinu za fitna alizokuwa anafanya akiwa katibu mwenezi.Kajisahau na Magufuli anamwangalia tu
 
Halafu hawa wanaoendesha bunge kijima ndio wanawaongopea wananchi eti Tanzania itakuwa nchi ya viwanda. Ni kipi kinachowafanya wajadili hayo mambo mazuri kwa kificho?

wanachojaribu kufanya ndio kinawashushia heshima tofauti na wanavyofanya.
 
Mara nyingi watu ambao wao kwanza ni chama
na taifa baadae ndo huwa na matatizo ya kiufahamu. Mfano bunge lililopita baadhi ya wabunge walipaza sauti wakisema mikataba ya
gase ni mibovu hivyo isisainiwe; kwa ushabiki wa kichama watu fulani aidha kwa kujua au kufuata mkumbo wa chama, wakasema wapinzani ni waongo na wachochezi.

Haya wakaambiwa tena escrow ni hela za umma chama chetu kikasema hamna siyo za umma na watu washangilia eti wapinzani ni waongo!!

wakaambiwa tena elimu yetu imeharibiwa na big result now! tena wakasema hayo ni mambo ya upinzani tu; waakambiwa tena serikalini kunaufisadi mkubwa unafanyika; wakasema wapinzani ni wakupuuzwa!!

katika yote hayo wabunge wa chama chetu walikuwa "ndiyoooooooooooooo"

Sasa majipu yanatumbuliwa eti nao tena wamegeuka "heeee raisi anafanya kazi nzuri" wakati majipu hayo yamekuwepo mda wote wa miaka tangu uhuru hadi leo lakini mda wote chama chetu na wabunge wake "ndiyoooooooooooo"

Leo wanachama wetu nao eti wanashangilia utumbuaji majipu!! ama kweli ni wafuata upepo misili ya nyumbu,

Ikitokea raisi akasema wote waliotumbuliwa warudi kazini hawana makosa, utawasikia wanachama wetu "ndiyooooooooooooooo"

sasa hapo ndo ujue watanzania hawana ufahamu bali chama chetu kidumu hata kama kitaamua kutuuza ni sawa tu si ndiyo chama chetu jamani utaifa baadaye.
Ni hivii wanajua itakuwa ni aibu kwa serikali kwa kuwa wabunge wa chama chetu hawajazoea kuikosoa serikali. Leo wabunge watawala wanaweza pinga hoja fulani kesho Mkulu anatangaza kumtumbua muhusika ambaye wabunge wa CHAMA walimtetea kwa nguvu zote. Nadhani Hapa mkulu anataka kurekebisha kitu....labda akiona wabunge wake wameshajielewa anaweza akaondoa marufuku hiyo...
 
Ndiyo maana enzi za mzee wa chama kimoja mpaka chakula tulikaa foleni.

naona unataka kupoza machungu kwa kuhamishia mada kwa Nyerere,haya daraja la kigamboni lilishapewa jina nyerere.Najua uliumia sana,asante kwa kutambua mchango wa upinzani.
 
Fanyezi kazi kusikiliza Bonge hakutasaidia chochote kwa maisha ya wanamchi wa kawaida

Kwa nini tusizime kabisa vituo vya television mpaka jioni wakati tunapokuwa tumerudi makazini? Huoni hata hao wanaoonyesha vipindi wakati wakazi ni kama wanapoteza muda?
 
Fanyezi kazi kusikiliza Bonge hakutasaidia chochote kwa maisha ya wanamchi wa kawaida

Hizi akili nyingine huwa nashindwa kuzielewa,kusikiliza bunge maana yake hufanyi kazi?Sitashangaa siku ya uchaguzi ukija kusema,kafanyeni kazi kwani kupiga kura hakutawasaidia chochote.
 
ni jambo la ajabu sana watu wazima tena kuna wanaume kabisa wanalilia kuangalia tv. kuna watu humu itakua wananyanganyana remote na wake zao na watoto.
 
ni zamu ya wabunge wa chama chetu kudai posho na kupiga usingizi. masikini watanzania...
 
Back
Top Bottom