Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Wengi wanaongea mengi mabaya juu ya Nyerere, ila ninachofahamu tu ni kwamba Nyerere alikuwa na kichwa kizuri, na hata mataifa mbalimbali duniani yanajua juu ya ukweli huo. Akiongea kitu hata mataifa makubwa yalikuna vichwa.
Alikuwa mtetezi wa wanyonge na katu hakunyamazia dhuluma dhidi ya raia.
Aliweka ardhi kuwa mali ya wananchi na kuwa na kauli nayo tofauti na leo.
Alianzisha utaratibu wa malipo ya watumishi serikalini kupunguzwa kwa wale wenye vyeo zaidi ya moja ili kuwa na uwiano wa mapato.
Na yeye akiwa mfano si kwa kuonyesha utendaji kwa kuwanyooshea vidole wengine ila maisha yake ni kielelezo fika.