Binafsi nakubaliana sana hoja kwamba though Nyerere was intelligent but was very poor in Economic philosophies, alijali sana siasa bila kuangalia Watanzania tutapata nini kiuchumi, mbaya zaidi kujihusisha na vita visivyo na msingi kama vya Mozambique, SA, Angola na nchi zote za SADC, Nampa 40% success na 60% failure, so totally he failed!
Inategemea na wewe unautazama vipi Uchumi. Kama wewe unachukulia kipimo cha uchumi ni mafanikio yake basi kweli Nyerere hakuwa mzuri ktk uchumi, lakini sidhani kama watu woote waloanzisha biashara na zika fail are poor in economics philosophies bila kutazama factors zilizosababisha biashara hiyo kushindwa na sii mtu mwenyewe kuwa sababu.
Ebu tuangalie na tumpime ktk aloyafanya na tuweke ni wapi alikosea ktk uwekezaji maana ni Nyerere aliyetujengea Reli ya Tazara, viwanda vyote hadi tulikuwa tukitengeneza wenyewe zana za kilimo, baiskeli, nguo, viatu, kusafisha na kukata almasi, viwanda vya Korosho, Pamba na Kahawa to finished product, shirika la Ndege, TRA, UDA, vyama vya Ushirika na kadhalika..Mikopo yote alochukua nje haikuwa kuiendesha serikali bali kujenga miundombinu ya uzalishaji.. ni makosa yapi ya kiuchumi ambayo aliyafanya wakati leo hii ndani ya Ubepari na ubinafsishaji hakuna hata kitu kimoja tunachoweza kuivunia as made in Tanzania! tena vichache tunashindwa hata kuviendeleza tumefikia kuuza hadi ARDHI ambayo ndio tafsiri ya Uhuru wetu..
Wachina ambao walikuwa wakitengeneza vitu feki kama sisi, wakiwa na shida kama sisi wameweza vipi wao kujiendeleza na miundombinu ile ile alowaachia MaoTse Tung kufikia leo kuwa Taifa linalokuza uchumi wake kwa haraka kuliko mataifa yote duniani! India acha kote huko Indonesia na Singapore hawa wote walikuwa maskini kama sisi kuishia mwkaa 1985 wala usichukulie toka Uhuru.. Wako wapi leo? mbona wao wameweza kuiendeleza, kuiboresha hadi wakafanikiwa na sii kuibomoa kama sisi kisha bado tunatazama makosa ya nyuma na sii tunayoyafanya sasa hivi..
Nitakwambia sababu haswa ya manung'uniko yetu, tumeshindwa kujitazama sisi wenyewe kwanza kwa sababu hatutaki kuujua ukweli wa nafsi zetu sisi wenyewe. Sisi ni Wachawi wakubwa, wanafiki na kubwa kuliko yote maaskini wa roho na mali. Nitarudia kusema tena na tena kwamba - we are ignorant, greed and selfish kwa sababu ya umaskini wa roho. Ni bora mwenyezi Mungu akupe Utajiri wa roho akunyime mali, kuliko Utajiri wa mali na akakunyima utajiri wa roho..
Ogopa sana mtu maskini wa roho mwenye ambition kwani mafanikio yake yatagharimu kuliko uloyaona kwa mwalimu.. Na mifano mnaiona leo kwani Ufisadi, Udini, Ukabila, U mimi na kadhalika ni matumda ya Umaskini wa roho..MONEY, POWER and FAME will be their set goals!.
Sii makosa ya Nyerere, sisi wenyeweKweli tumeshindwa kuona makosa yetu, tumekula au tumeuza hadi mbegu...now this U may call lack of BASIC economic philosophies..Utakulaje mbegu yako! hii akli kweli kama sii Ulimbukeni, Ulafi na Ubinafsi...Tumesha kula mtaji na kuharibu vyanzo vyote kiasi kwamba hatuwezi hata kulipia matumizi ya ndani, tumemaliza vyote sasa tunauza hadi ardhi kwa sababu tumemaliza kote lakini bado wa kumlalamikia ni Nyerere..
Je, ni kipimo gani mnachotumia kupima mafanikio ya kiongozi....Hivyo vita vya kusini mbona nchi zote hizo zilifanikiwa kupata Uhuru wake? au haya sio mafanikio isipokuwa mnatazama ilitugharimu kiasi gani?..Hivi kweli tunaijua gharama ya Mozambique ambayo sii huru leo!..Jamani acheni kufanya mzaha na maswala haya, ni vizuri sana tukitazama sisi wenyewe tunashindwa kipi badala ya kuendelea kutafuta mchawi..Hii roho ya kimaskini na inatuponza kila siku.