Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,103
- 43,356
Nyerere ataendelea kuenziwa na hakuna mtu anayweza kufuta historia yake na mchango wake wa kipekee katika historia yetu kama taifa. Iwe ni katika Tanganyika au katika Tanzania. Nyerere ni baba wa Taifa la Tanzania kama alivyokuwa baba wa taifa la Tanganyika. Wazee wetu walitambua hivyo na walimheshimu hivyo. Sasa ni wazi watu ambao wana religious objection bila ya shaka inaruhusiwa kukataa na kama wanatoa pingamizi kwa misingi ya kidini inakublalika. Lakini, kupinga kwao kwa misingi ya imani hakuwezi kuwafanya watu wengine ambao hawana objection hiyo kukataa kufanya hivyo.
Upande mwingine nao ni kweli; kwamba wale ambao kutokana imani zao binafsi hawaoni tatizo kumuita Nyerere Baba wa Taifa au dhamira zao hazioni ubaya wa kufanya hivyo wanayo haki yakufanya hivyo pasipo kuonekana wanavunja jambo fulani. Sisi wengine kwa imani zetu ziwe za jadi au kidini hatuoni tatizo hilo na tunaona fahari kumtambua Nyerere kama Baba wa Taifa kwani tunajua siyo jamii ya kwanza kumtambua mtu aliyetoa mchango wa pekee katika uanzishwaji wa taifa kama baba wa Taifa.
Ndio hoja ya Mchambuzi na hata Mag3 kuwa mataifa yametambua waasisi wake kama Baba wa Taifa au Mababa wa Taifa. Kwa mfano, Palestina ikija kuwa nchi, taifa lile sitashangaa kama watamtambua Yassir Arafat kama Baba wa Taifa na siyo Abu Mazen.