Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Mchambuzi naomba Utusaidie Kidogo: Mwalimu Nyerere alipewa ubaba wa Taifa kwa sheria ipi ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania?.

Heshima ya Baba wa Taifa ni kwa mujibu wa sheria ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ilipitishwa na Bunge miaka ya nyuma. Ngoja nifanye utafiti ili kubaini undani wake;
 
Kwa hiyo una maana kwamba sababu za Kihistoria zinazoelezea kwa nini Mataifa yenye asilimia 90 hadi 99 ambayo raia wake wana imani tofauti kabisa na Ukristo kutumia msemo "Baba wa Taifa" unatokana na historia ya mataifa hayo "kutawaliwa na Wazungu (Wakristo)", si ndiyo?

Basi ni vyema (au kwa lugha nyingine, isingekuwa vibaya) kama ungewataja hao "Mababa wa Kanisa" kwenye nchi husika ambao, kwa tafsiri yako, ndiyo vyanzo vya jadi ya msemo wa "Baba wa Taifa" kwenye nchi husika.

Tukianza mlolongo huo itachukua muda mrefu sana. Point niliyokuwa naweka kwa huyu mwandishi wa article hii ambaye kashindwa kusahihisha makosa yake.

Amaeandika kwamba Marekani kuna "Baba wa Taifa" as singular, wakati anajua kabisa ni kuwadanganya WTZ. Marekani kuna "Founding Fathers" na siyo vile anavyosema yeye. Huu ni upotoshaji.
 
a
........Inachochea haja ya kujisomea ili tuapte kujenga hoja za kisomi, hoja tafiti na hoja chokonozi kama hii ya kwako. Wito wangu usiachie hapo maana watakija watu wenye mawazo mgando na matusi na kejeli kumbe wao hata mistari miwili kama yako hawawezi kuandika.

...... nitoe ushauri kuwa vyama vyetu usivichananye kama ulivyoonyesha kuwa kama ilivyokuwa kwa CCM na CDM hivyohivyo. Watanzania tuliokuwa wengi unatujua maana hatufanyi tafiti na hatujisomei kiasi kwamba mataifa jirani yanatudharau. ......

.........Hivyo basi nikuombe CCM-CDM au chama chochote iwe ni topic independent. Ila nikumbe uwatie moyo wananchama wa vyama hivi wenye uzalendo wa kweli wasife moyo. Sina shaka n uzalendo wa viongozi wa CDM hasa wa ngazi za juu ukiacha waliotumwa kama Shibuda. Hawa wanajitolea sana kwa manufaa ya taifa.Kwanza kwa taifa lenye hujuma kusimama hadharani ukawataja mafisadi wakiwemo viongozi wa juu sio mchezo.Halafu majimbo yalioongozwa na CDM ni mfano wa kuigwa kwa maendeleo ya watu kama shule, maji na afya.

....... Mwisho nami kama wewe Mwalimu ni Baba wa Taifa na bado ni Rais bora kwa vigezo vyako na vyangu

Nashukuru sana kwa maoni na ushauri wako. Ni sahihi kwamba suala la CCM/CHADEMA/VYAMA VYA UPINZANI halijengi sana katika mjadala huu ambao focus yake ni BABA WA TAIFA, bila ya kujali tofauti za itikadi za vyama; Lakini kusudio langu kutaja vyama vya siasa ni kwamba hata hizo itikadi zina mapungufu, na hakuna chama cha siasa hadi sasa ambacho kinaonyesha a different and home grown vision ya maendeleo ya nchi ambayo inawachukulia WorldBank/IMF/WTO na wadhamini wao OECD, kwamba hawa wote are supposed to complement our policies za kumtoa mkulima from poverty, hawa wakubwa kazi yao sio kutuamulia jinsi gani tufanye hivyo;

Nitalirekebisha hilo mkuu. Asante sana.
 
Mchambuzi - nimejaribu kusoma makala yako hapo juu. Kusemakweli umechambua mpaka mwisho. Mimi sina la kupunguza wa la kuongeza maana yamekalika. Yaani kama bado kuna mtu anayepinga Nyerere kuitwa BABA WA TAIFA basi huyo hana akili timamu. Ni wakumwacha jinsi alivyo maana pesa za mafisadi zinamlevya. Kwa niaba ya Watanganyika wote nakutumia shukrani nyingi sana kwa kazi nzuri uliyoifanya ya kuichambua mada hii kwa utaalam na ustadi uliotukuka! Mungu akubariki sana mchambuzi wetu!!!

Losomich,
Nashukuru sana; pamoja tutafanikiwa kulinda heshima ya baba wa taifa alietujengea jamii isiyo na malumbano na ubaguzi wa kidini au kikabila. Huwa nafarijika sana napofikiria baadae kwamba Jamii aliyotuachia baba wa taifa ni ile ya kutokuwa na any conscious kwamba yule unaemuona barabarani, au yule uliesalimiana nae, au yule unaemuonaga mara kwa mara mtaani kwako na kumsalimia na, kichwani kwako wala haiji akili ya kujiuliza ni mtu wa dini au kabila gani; unamtambua kwamba ni mtanzania tu kama wewe, sana sana labda ni aidha mwanamke au mwanaume, mzee au kijana, au mtu mwenye hali duni, au mwenye uwezo; consciousness juu ya dini ya mtu fulani hutokea iwapo tu labda raia huyo atakuwa na rozari yake visible, au kanzu/kibaraka shee etc.

Mungu amrehemu Baba wa Taifa; Because of him, We are United in Great Diversity;
 
Tukianza mlolongo huo itachukua muda mrefu sana. Point niliyokuwa naweka kwa huyu mwandishi wa article hii ambaye kashindwa kusahihisha makosa yake.

Amaeandika kwamba Marekani kuna "Baba wa Taifa" as singular, wakati anajua kabisa ni kuwadanganya WTZ. Marekani kuna "Founding Fathers" na siyo vile anavyosema yeye. Huu ni upotoshaji.



George Washington, the Father of Our Country



[TD="width: 10"]
trans.gif

[/TD]
[TD="width: 230"] Born: February 22, 1732
Died: December 14, 1799 The first president of the United States, George Washington, is often referred to as the Father of Our Country. He was known for his love of the land and farming, and his dislike of war. He was a distinguished general and commander in chief of the colonial armies in the American Revolution. He married a widow, Martha Dandridge Custis, and they lived at Mount Vernon, Washington's plantation in Virginia on the Potomac River.




[/TD]
Acha ubishi wa kijnga..... endeleeni na mjadala, nimeamua kuwa mtazamaji. Ila nimepata furaha sana kuona jinsi watanzania wengi wanavyomtetea Nyerere, no wonder we had Unity back then.
 
FAIZA FOXY,
Cc: TOPICAL

Mjadala wako juu ya neno baba unapotosha sana, tena kwa makusudi. Nadhani lengo lake ni kuharibu tu heshima ya BABA WA TAIFA letu kutokana na agenda binafsi, na inawezekana kabisa kuna juhudi mahsusi linalotoa somo na maelekezo hayo, wewe ukiwa mmoja wa wanafunzi au wafuasi wake. Hii ni hatari kubwa sana kwa umoja wetu Tanzania usiojali dini, ukabila wala jinsia, among other things.

Utafiti wangu mdogo tu kwenye Internet unaelezea ifuatavyo juu ya neno BABA - origin pamoja na matumizi yake:

SOURCE: Wikipedia.

As one of the first utterances many babies are able to say, baba (like mama, papa, and dada) has come to be used in many languages as a term for various family members:
  • father: Arabic, Chinese, Greek, Hindi, Bengali, Persian, Swahili, Turkish, Yoruba
  • grandmother: many Slavic language (such as Bulgarian, Russian and Polish), Yiddish, Japanese
  • baby: Afrikaans
These terms often continue to be used by English speakers whose families came from one of these cultures. In some cases, they may become more widely used in localities that have been heavily influenced by an immigrant community. Some senses were extensions of one of these family terms in the original languages ("old woman" from "grandmother", "holy man" from "father"). The "cake" sense comes through French from Polish baba ("old woman"). The Middle Eastern word baba (as in Ali Baba) is rather a term of endearment, and is ultimately derived from Persian بابا (bābā, "father")(from Old Persian pāpa; as opposed to the Arabic words ابو ('ábu) and أب ('ab), as well as the Turkish word ata; see also Papak) , and is linguistically related to the common European word papa and the word pope, having the same Indo-European origin.
Noun
Baba (plural babas)
1. A kind of sponge cake soaked in rum-flavoured syrup.
2. (esp. among people of East European ancestry) A grandmother.  
3. An old woman, especially a traditional old woman from an eastern European culture.  
4. (esp. among people of Indian ancestry) A father.  
5. (Hinduism, Islam, Sikhism) A holy man, a spiritual leader.  
6. A baby, child.  [
7. In baby talk, often used for a variety of words beginning with b, such as bottle or blanket.  
 
@mchambuzi

Kwanza, hoja yako ni dhaifu na ndefu bila sababu najisikia vibaya kupoteza muda kusoma habari ndefu yenye mantiki ndogo sana, kubembeleza watu kumkubali nyerere ha!

Pili, Mimi baba yangu ni mume wa mama yangu period..nyerere ni rais wa kwanza wa Tanzania siyo baba yangu na wala hawezi kuwa baba wa mtoto wangu NEVER ukimpenda sana jazeni vitabu lakini mimi na ukoo wangu hiyo sifa hatutampa hadi kifo...

Tatu, Unajua kabisa hana sifa hizo ndio maana mnalazimisha watu na kutafuta popularity..kibaya mnajitmebeza sana poleni

Kwangu mimi ni Baba wqa kanisa kwa mujibu ya mafundisho yao ya dini na faida walizopata kanisa chini ya utawala wake.

Mtu yeyote ambae amesoma shule anaelewa kwamba maana ya hoja sio "kubembeleza".
 
heshima ya baba wa taifa ni kwa mujibu wa sheria ya bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania ambayo ilipitishwa na bunge miaka ya nyuma. Ngoja nifanye utafiti ili kubaini undani wake;

bwana mchambuzi, nasubiri kwa hamu kubwa sana nione hiyo heshima ya ubaba wa taifa kutungiwa sheria bungeni, na kama hiyo sheria haipo msingi mzima wa hoja yako unayeyuka.

Nakukumbusha tu, if you have no concrete evidence of what you are talking about, you better not reach the conclusion!.
 

Binafsi suala la Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere sio suala la kujadili na mtu.Wala siwezi kuhoji ubaba wake kwa kadiri ninavyoelewa yeye alishakuwa na yake ya kutenda, katika usimamizi wa jamii kwa nyakati zile na mazingira inalazimu kuhalalisha aina zote za mapungufu aliyopitia......

Tupo katikati ya nyakati hizi mgogoro wa kisiasa katika kujenga mustakabali wa Taifa letu, 2015 ni kipenga..!
Ni lazima turejeshe tafakari hapa juu ya aina za siasa katika vyama vinavyoamua muelekeo wetu, hasa katika kudaka pale alipoishia Baba wa Taifa.
Ni wazi kuwa CCM imeshashindwa!!
Vipi kuhusu CDM??
Ni vipi kinabeba ndoto ile ya Baba wa Taifa??
Uchumi wa mchanganyiko ni siasa za kimalaya/ siasa koko zisizo na sura ya kueleweka katika kusimamia maslahi ya masikini wa vijijini.
Ifike sehemu tuchore mstari uliowazi kwa chama chenye uelekeo wa kushika dora (CDM) juu ya tathmini mpya juu ya Itikadi na Mlengo wa kati haufai katika kulivusha taifa hili na kurudisha uchumi kwa UMMA.
Na hiyo ndio ilikuwa ndoto ya Baba wa Taifa.

JouneGwalu,
Asante sana kwa mchango wako. Hakika suala la baba wa taifa halina mjadala kama lengo ni kuhoji uhalali wake. Lakini kama nilivyokwisha sema, wenye hoja hii inaonekana kama vile nia yao (pengine sipo sahihi) wanataka kulivunja taifa ili kwa kutafuta visingizio kwamba kuna sehemu fulani ya jamii haikuwa sehemu ya ukombozi wa awali uliozaa baba wa taifa aliyepo, na kwamba matunda ya harakati zile yanaliwa na wachache, na walio wengi wanaonewa n..k; hoja hii inawezekana (pengine sipo sahihi) ili kuhamasisha walio wengi, na hivyo kuhalalisha mapinduzi ya umwagaji damu, na hatimaye wao kujitengenezea historia mpya, taifa jipya, na hatimaye baba mpya wa taifa lao. Ningependa kusahihishwa kama mtazamo wangu haupo sahihi juu ya hisia zangu juu ya nini haswa watu wa namna hii wanataka kuleta au wapi wanataka tupeleka.

Nakubaliana na wewe kwamba siasa za 2015 zina determine mengi sana, na inaonekana ndizo zina shape kwende huko; Mimi kama Mtanzania sijali nani atakuwa rais wa tano wa Tanzania, atokee dini ile au ile, atokeee mashariki, kusini, kaskazini, magharibi, unguja, pemba, kwangu mimi hilo sio suala la msingi, muhimu kwangu ni rais ambae atatuongoza bila ya kujali tofauti zetu, ataongoza kwa mujibu wa sheria na katiba, atatoa fursa na haki sawa kwa wananchi wite bila ya kujali dini, makabila, au jinsia zao;

Kuhusu CCM kushindwa kazi, ni sahihi kwani hakina dira - kwenye vitabu kinasema kina itikadi ya ujamaa na kujitegemea, kwenye vitendo, soko huria kiholela; Kuwa na mwongozo wa Chama ambao kushoto una azimio la arusha, na kulia azimio la zanzibar, ni kujichanganya; huku ndiko kukosa dira kama alivyotamka Marehemu Kolimba karibia miaka 20 iliyopita, na kuonekana mwehu; CCM haina dira wala mwelekeo kwa miaka 20 (tangia azimio la arusha), chama kinaongozwa kwa Ilani za chaguzi, pamoja na kanuni ambazo kwa kiasi kikubwa hazifuatwi, na pia taarifa za hali ya siasa nchini zinazozaa mikakati mizuri sana lakini hazifanyiwi kazi ipasavyo;

Chadema kina watu makini sana, hilo halina ubishi; kwa mtazamo wangu, hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kujenga hoja katika CCM (wazee na vijana) kama Mnyika, Zitto, Lissu; nipo wazi kupingwa juu ya hilo;

Tatizo la CDM kwa mtazamo wangu ni kwamba, wakifanikiwa kupata uongozi wa nchi, wasipokuwa makini, watapoteza legitimacy yao haraka sana in the eyes of watanzania waliowachagua kwenda ikulu kutokana na mambo niliyoyaelezea hapo awali;
 
bwana mchambuzi, nasubiri kwa hamu kubwa sana nione hiyo heshima ya ubaba wa taifa kutungiwa sheria bungeni, na kama hiyo sheria haipo msingi mzima wa hoja yako unayeyuka.

Nakukumbusha tu, if you have no concrete evidence of what you are talking about, you better not reach the conclusion!.

Wakati naendelea na zoezi la kuleta taarifa rasmi juu ya uhusiano wa bunge na sheria juu ya baba wa taifa, ingekuwa vyema na wewe uendelee na zoezi to disprove uhalali huo ambao unahoji uwepo wake kwa mujibu wa sheria; na hoja yako kwamba kama haitambuliki kwa mujibu wa sheria inaangusha hoja yangu nzima, bila ya kutoa ufafanuzi wako wa kina in the context of mantiki nzima ya heshima hiyo kwa kiongozi aliyeongoza harakati za uhuru, haina mashiko; lakini una nafasi ya kufafanua hilo;
 
Huo utamaduni unasema mtu anaweza kuwa baba (apart from baba mzazi) anatakiwa awe na sifa zipi?

Hopefull atakuwa mtu ambaye ameifanyia familia, anafahamika katika familia kama somebody with usefull contribution (thinking aloud), au jirani mwema, ndugu mwema, huwezi kumuita dhulmaji baba ...BIG NO..

Sasa nyerere ana contribution gani kwetu, (sitaki kusoma ujinga wenu mlioujaza kanisani) kwa familia yangu kwa jamii yangu; ..NONE

NEVER hawezi kuwa baba..lakini nyie mkitaka mpeni na muiteni chochote..not me, US..etc..kuna ubaya mkuu wewe si umefaidi sana na nyerere muite baba yako who cares, don't tell me or teach me who deserve to be called father etc..
Mwalimu anaitwa Baba wa Taifa sio baba wa Topical, FaizaFoxy au WildCard! Hao wana baba zao. Upofu na ulevi wa UDINI unasumbua kwelikweli hasa unapokolezwa na chuki, wivu, fitna na mapungufu mengine ya kibinadamu. Tuacheni tunaomtambua kwa sifa hiyo tuendelee. Ninyi wengine muiteni kwa majina mengine mazuri aloopewa na wazazi wake, kanisa lake na taaluma yake.
Mchambuzi ametoa ufafanuzi ambao haujapata kutolewa kungine kokote kule na yeyote yule. Tunamshukuru sana.
 
Hivi nyerere ni baba wa taifa wa zanzibar?

Kama ndiyo, then how?
Kama siyo, then atakuwaje baba wa taifa la tanzania, wakati hakualify kuwa baba wa taifa wa zanzibar ambayo ni nchi, na pia ni sehemu ya tanzania?

Kama Uasisi wa Taifa la Tanzania ndiyo kigezo cha kuwa baba wa Taifa, Je mzee Karume?, naye si ni muasisi wa Tanzania?, kwa nini yeye siyo baba wa Taifa wa Tanzania. Zanzibar na Tanganyika si ziliungana kama equal partners au?, sasa vipi muasisi mmoja ndo aonekane kuwa baba wa Taifa na si mwingine?.

Mahatma Gandhi hakuwa raisi wala Wazirimkuu wa India, lakini mmemuita baba wa Taifa la India, kumbe basi UNAWEZA KUPEWA HESHIMA YA BABA WA TAIFA PASIPO KUWA RAISI WA KWANZA WA TAIFA HILO.

TANZANIA TUNA FATHERS OF THE NATION, SIYO FATHER OF THE NATION(MMOJA), MIONGONI MWAO NI WALE 17 WALIOTAJWA NA JK, NA WENGINE AKINA KARUME, ABDULRAHMAN BABU, NASSORO MOYO, KAWAWA , KAMBONA ETC.

NI VIZURI HAWA WOTE TUKAWAPA HESHIMA YA UBABA WA TAIFA NA SI NYERERE PEKE YAKE.
 
Naona umetubandikia m page wa Wikipedia ambao hauna maana zaidi ya kutujulisha neno baba ni nini.

Mimi muislaam na nimekupa hoja yangu kwa ufasaha kabisa na kuna mtu akajidai ooh hiyo sio hoja ya dini nikampa na aya ya Qur'an kuwa hata mtume wangu Muhammad (SAW) sipaswi kumuita "baba", baba ni aliyekuzaa tu. Na kwa kukuongezea tu, hata Mwenyeezi Mungu katika majina ya sifa zake 99 hakuna la "baba".

Naona kanisani ndio linatumika kuwaita "father" ambalo ni "baba" Kiingereza. Ma baba ambao hawaruhusiwi hata kuzaa.

Kwanini tutumie "terminology" ya kikatoliki kumuita Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika? kuna hata Mungu "Baba", kuna "baba" mtakatifu, kuna Baba mapadri, sasa mnatuletea "baba" wa Taifa, huu ni Ukatoliki na hakuna zaidi na hata uandike makala (zisizokuwa na mpango kama hii hapo juu, ambayo ndefu na haina maana hata kidogo) kwangu ni NO na nnauhakika kwa Waislaam wengi pia ni NO.

Kwanza uelewe kila "baba" si mwema, kuna mababa wanaowatia watoto zao matatizoni, wanaowakimbia watoto zao, kuna mababa hawatazami watoto zao, kuna mababa hawawapi elimu ya kutosha watoto zao, kuna mababa hawawapi chakula cha kutosha watoto zao, kuna mababa wanawawacha kwenye umasikini mkubwa watoto zao, kuna mababa wanawafanya watoto zao wanakuwa ombaomba.

Sijaelewa maana ya wewe kuweka li page la wikipedia, ulikusudia nini?

Mwalimu katuachia jamii ambayo hata watu wa dini nyingine wanaitana Sheikh, kuonyeshana tu heshima. Mungu amlaze mahali pema peponi baba wetu wa taifa, Mwalimu Nyerere.
 
Asante sana KEIL, WILDCARD, Mchambuzi na wengineo kwa mjadala mzuri.

Ngoja nibakie mtazamaji maana mie mtu akianza Uislamu au Ukristo huwa natamani nimpige BAN ya mwaka!!
 
Aliyakuta zaidi ya hayo, usitujaze ujinga kuwa kayaleta yeye, neno "Sheikh" kiarabu ni kama Kiswahili "Mzee" kwa hiyo ukisikia mtu anaitwa Sheikh Nyerere wala usishangae. Ni simply imemaanishwa Mzee Nyerere, lakini si "baba". NO.
Faiza,
Na "Maalim" inamstahili yule jamaa? Mbona mshari sana!
 
Aliyakuta zaidi ya hayo, usitujaze ujinga kuwa kayaleta yeye, neno "Sheikh" kiarabu ni kama Kiswahili "Mzee" kwa hiyo ukisikia mtu anaitwa Sheikh Nyerere wala usishangae. Ni simply imemaanishwa Mzee Nyerere, lakini si "baba". NO.

FaizaFoxy,

Assalaam aleykum na baraka na rehema za mwenyeji Mungu ziwe nawe.

Unaweza kushiriki kwenye mada mbali mbali bila kugusia DINI?. Nimeona una points sana tu ila inamweka mtu OFF ukishaweka UDINI ndani ya posts zako.

Ni ombi tu, maana kwa ukongwe wako humu sikumbuki kuona udini zamani humu, unless umebadili jina au ulikuwa mtazamaji tu.

Please
 
Asante sana KEIL, WILDCARD, Mchambuzi na wengineo kwa mjadala mzuri.

Ngoja nibakie mtazamaji maana mie mtu akianza Uislamu au Ukristo huwa natamani nimpige BAN ya mwaka!!
Na hasa pale Uislamu au Ukristo wako unapoonekana ni tatizo kwa watu wengine. Au pale nafasi, madaraka au wadhifa wako katika jamii unapohusishwa na DINI au KABILA yako bila sababu. Jamani, DINI hizi tumezirithi kwa wazazi au jamii tulimokulia. Sio zetu na hata kuzibadili tukitaka tunaweza. MUNGU hana DINI.
 
U "baba" unatumika kanisani kuanzia "Mungu baba", "Baba Mtakatifu", "Baba Padri", na sasa tunalazimishwa "Baba wa Taifa". Utamlazimishaje Muislaam atumie vyeo vya kanisani wakati dini yake hamruhusu? kama si udini ni nini?

Huko juu nimetowa mpaka aya ya Qur'an inayokataza hata Mtume Muhammad kuitwa "baba" nimeonesha pia kuwa hata katika sifa za Mwenyeezi Mungu Kiislaam, hakuna sifa ya ubaba. Na pia kiislaam "baba" ni yule aliyekuzaa tu, hata mume mwingine wa baba yako hupaswi kumuita "baba" labda kwa wasiyoyaelewa mafundisho ya Kiislaam.

Nakushangaa unapoona mimi nnaelipinga hili la udini wa kulazimishana kumuita mtu baba kama wafanyavyo wakatoliki lakini wanaolazimisha hili huwaoni kuwa wadini. Unanshangaza sana.
Mimi sipati shida kumuita Mzee "Ruksa" Alhaji Ali Hassan Mwinyi tangu akiwa madarakani ingawa neno "Alhaji" limekaa kidini zaidi kuliko "Baba wa Taifa"
 
Na hasa pale Uislamu au Ukristo wako unapoonekana ni tatizo kwa watu wengine. Au pale nafasi, madaraka au wadhifa wako katika jamii unapohusishwa na DINI au KABILA yako bila sababu. Jamani, DINI hizi tumezirithi kwa wazazi au jamii tulimokulia. Sio zetu na hata kuzibadili tukitaka tunaweza. MUNGU hana DINI.

umeandika mambo mazito sana,

thanks great thinker!
 
Uislaam haumlazimishi mtu kwenye dini na kwa mantiki hiyohiyo hatulazimishwi na mtu kwa dini yake. Kutulazimisha kumuita mtu mwingine "Baba" zaidi ya baba aliyetuzaa ni kutulazimisha mafundisho ya dini ya kikatoliki na hilo hatulikubali. Kumbuka hili ni Taifa la wenye dini na wasio na dini, vipi dini moja itulazimishe wengine kwa "title" zao?

Hilo la Mungu hana dini ni fundisho lako lakini sisi tunaamini Mungu ndiyo aliyotuletea mafundisho ya dini na dini aliyoileta ni Uislaam. Labda kwako wewe dini ina maanisha vingine na inavyomaanisha kwangu mimi, kwa kukujuza tu, Dini kwangu mimi "ni mfumo wa maisha" na mfumo wangu wa Maisha yangu ni Uislaam, wako sijui.
Faiza,
Hata URAIS ulianzia hukohuko kwenye DINI na hasa UKATOLIKI. Fanya utafiti utagundua michango ya DINI zetu kwenye mifumo hii ya utawala duniani kote. Wewe una jingine zaidi ya hili la kuisingizia DINI yako!
 
Back
Top Bottom