Mkuu FairPlayer,
Swala la vita vya Kagera limekuwa likipotoshwa na watu kwa muda mrefu. Nina hakika kwamba maamuzi ya Nyerere kumpiga Idd Amin, yangeweza kufanywa na Rais yeyote yule ambaye angekuwa madarakani wakati huo. Huwezi ukavamiwa halafu ukakaa kimya bila kujitetea au kulinda mipaka yako.
Ni ukweli ambao haupingiki kwamba mapinduzi ya Obote hayakumfurahisha Nyerere. Obote alikimbilia Tanzania na kuomba hifadhi lakini pia alikuwa bado anatamani kurudi madarakani. Kitendo cha Nyerere kukubali kumweka Obote Dar es Salaam kwa namna yoyote ilikuwa ni kujitakia matatizo kwa sababu Idd Amin lazima alijua kwamba Obote anaweza kuitumia Tanzania kuandaa mashambulizi ya kumrudisha madarakani, kwa hiyo kitendo cha Obote kukubaliwa kuishi Dar es Salaam kiliongeza kutoaminiana kati ya Uganda na Tanzania na given kwamba Nyerere hakuitambua serikali ya Idd Amin mara baada ya mapinduzi.
Hilo la Obote kutaka kurudi madarakani ni kweli lilifanyiwa majaribio mwaka 1972, lakini liliwahusisha akina Museven na wapinzani wengine ambao walikuwa ni vijana wa Obote. Obote alijua kwamba alikuwa na support kubwa within Uganda na kumbe he was wrong na ndio maana hawakufanikiwa. Kwa bahati mbaya kabisa zoezi hilo halikufanikiwa na matokeo yake ilikuwa ni kumfanya Amin arushe mabomu Mwanza na Bukoba. Kwa kuwa Nyerere alijua kosa lake, wala majeshi ya Tanzania na serikali yake hawakujibu kitu waliishia kimya kimya.
Tension iliendelea kwa muda mrefu, akina Museven walifungua kambi za mafunzo ya vijana wa kutoka Uganda ambao walikuwa wamekimbilia Tanzania. Lakini kwa kuwa kitengo cha usalama cha Amin kilikuwa makini sana, habari zilimfikia Amin kuwa Tabora (to be specific, Kigwa) kulikuwa na kambi za vijana wa Uganda chini ya Museveni. Kwenye makubaliano ya Mogadishu ya ku-difuse tension kati ya Tanzania na Uganda, Uganda ilitoa condition ya kufungwa hiyo kambi ya Kigwa na Nyerere alikubaliana nao na ilifungwa. Ndipo Museven alipohamia Nachingwea ambako ilikuwa ni ngumu sana kwa Amin kujua kinachoendelea kwani mikoa ya huko kusini ilikuwa na askari wengi sana na wengine walikuwa masalia ya askari wa marehemu Samora. Wakati haya yote yakitokea Nyerere alisha-give up plan yoyote ya kumsaidia Obote kurudi madarakani baada ya makubaliano ya Mogadishu.
Mimi nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiamini kwamba Tanzania ndio ilimchokoza Idd Amin mwaka 1978, lakini ukweli ni kwamba Amin ndiye aliichokoza Tanzania. Tanzania haikuwa imejiandaa kwa vita ya aina yoyote ile na Uganda na ndio maana ilichukua karibu mwezi mzima kwa Tanzania kuanza vita rasmi tangu siku askari wa Amin walipobomoa daraja la mto Kagera na kupandisha bendera ya Uganda ndani ya mpaka wa Tanzania.
Kuthibitisha hili, askari waliokwenda frontline mwanzoni kabisa mwa vita walitoka Songea, vikosi vya kusini ndio pekee ambavyo vilikuwa tayari na ninadhani ni kwa sababu Nyerere alikuwa anahofia zaidi nchi za kusini kuliko nchi za kaskazini na magharibi mwa Tanzania. By then Banda alikuwa haeleweki na pia hali ya Msumbiji ilikuwa bado iko tete na Angola pia moto ulikuwa unawaka na Zimbabwe walikuwa bado hawajapata uhuru. So, vikosi vya kusini vyote vilikuwa viko ready masaa 24 kwamba lolote likitokea ni swala la kusogeza zana na kazi inaanza.
Hii clip angalia/sikiliza kuanzia 05:22 na kuendelea mbele kidogo ili umsikilize Amin kwa kauli yake mwenyewe akiwa anatamba na bendera ya CCM.
Vita vya Kagera (Kagera War) - Part 1 of 4 - YouTube
Sasa swali linakuja, je, baada ya huo uhuni alioufanya, ni Rais gani wa nchi angekaa kimya bila kujibu? Ndugu zangu wachagga hata ukiingia hatua moja ndani ya mpaka wa kihamba yake atakutokea na panga. Ndio ije kuwa umevuka mpaka, umevunja daraja na kuua wananchi wake halafu akuache tu?
Kuna wengi ambao wanasema kwamba tulitakiwa ku-reclaim ardhi ambayo ilikuwa imechukuliwa na then tuishie hapo. Lakini kuishi ujirani na mtu kama Amin ni kujitakia matatizo, maana huwezi jua next atakuja na nini. Nyerere alishafanya assessment ya na kujiridhisha kwamba Amini alikuwa anapigika tu na kwa msaada wa akina Museveni ambao walikuwa na contacts within Uganda. Kama Tanzania ingefanya kosa la kumwacha Idd Amin madarakani basi tungeendelea kuwa kwenye tension siku zote na kusubiri mpaka Mungu amchukue Amin na huwezi jua ni nani angefuata baada ya Amin.
Ni kweli Tanzania tulikumbwa na hali ngumu ya uchumi mwanzoni mwa miaka ya 80 na kuendelea, lakini it