Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Mi nashauri mkubaliane kutokukubaliana. Mwandishi ameelezea utofauti kati ya Baba na Rais bora wa Taifa,kila mtu ameelewa,labda kama mtu hakubali. Halafu ameonyesha kuwa asili ya ubaba wa taifa ama jina hilo haikutokea kanisa katoliki wala si Roma wanaotoa jina hilo kwa viongozi wa nchi hapa duniani,iwe za kiislamu au kikristo. Hata hatukuwahi kusikia aliyetoa jina hilo alikuwa kardinali Rugambwa au Pengo! Mi nadhani imechukuliwa kifamilia zaidi kwamba...kiongozi wa familia huwa ni mwanamume. Na kwa bahati ni kwamba wanaharakati wengi katika ukombozi na mapinduzi ya nchi zao,walikuwa wanaume... Kifamilia kuna mambo ambayo hayakamiliki hadi baba aje.. Heshima ya ubaba,ni kuonesha uongozi,msimamo,ujasiri,vision,na maamuzi ambayo hata kama yatapingwa na watoto au wake zake,ya baba yanakuwa ya mwisho.. Someone can correct me ila huo ndiyo ufahamu wangu.

no replies regarding this?!
 
Aliokuwa mdogo 1967 basi mpaka leo ni mdogo, amma kweli wewe una matatizo ya ufaham si makosa yako. Kiislaam mtu akisha balekh (balehe) ni mtu mzima na kiserikali baada ya miaka 18 kwa kwetu hapa si mdogo tena hata mahakamani anahuikumiwa kama mtu mzima. Nyie ndio katika wale msiothamani mchango wa mtu eti ni mdogo. Tatizo ni ufaham wako finyu. Tena nnakuhisi u mdogo sana kama si ki umri basi ki ufaham.

Na hizo unazoziita pumba zimekuingia a hauna majibu. Bora unyamaze tu.
Weye dada mdogo mbona mkorofi namna hiyo? Yaani hata kaka zako hutuheshimu siyo? Nimekufatilia fika na ninajua niongealo. Ni haki yako kujiridhisha kwamba nisemalo sio kweli lakini hilo halibadilishi ukweli kwamba kiumri nimekuzidi sana. Wadanganye vijana humu jamvini lakini sio mimi. Samahani, ukweli ndio huo. Kalagabaho!
 
Hayo yote unaotetea yanakwenda kinyume na mafundisho ya Uislaam. Hakuna baba zaidi ya baba yako aliyekuzaa. Huo mwingine wote ni Ukatoliki.

hakuna baba zaidi ya aliye kuzaa 'Kwenye Uislam hili ni neno zito sana na lina maana kubwa sana,sababu ni agizo la mbora wa mitume Marehemu muhamad. Alipolaumiwa na uma baada ya kulala na kwewe mke wa mtoto wake wa kupanga akapewa aya na Allah wake na kutoa strict order kwa waumini wake 'Waislam' kwa kupiga marufuku kuita baba mtu ambaye sio biological baba wako,hivyo akajipa uhalali wa kuishi na mkwewe,HAIWEZEKANI kwa Muislam wa Ukweli kukubali kutumia neno baba wa taifa au baba kwa mtu asiye wa kumzaa.
 
Mkandara, mstari ambapo Nabii Ilyas anawaambia Waisraeli kuhusu "baba" zao wa zamani; unafikiri inamaanisha wale waliowazaa au wazee waliowatangulia?
Mkuu wangu hata kwa kusoma tu ukiambiwa baba zao wa zamani haiwezi kuleta maana kabisa. baba zao wa zamani ndio watu gani kwa nini isiwe babu zenu maana ujumbe huu unawalenga Umma wa Ilyas na wazazi wao. Halafu kiarabu ni lugha ngumu sana kuitafsiri hivi hivi tu kwa kutumia ufahamu wa watu wako. Na mara nyingi wala sio swala la dhehebu, Fiqhi au Itikadi bali mtafsiri ndiye hutegemea yupo wapi na atatumia maneno gani kwa lugha yake yeye..

Kwa mfano Mkenya ukimpa kuandika Biblia anaweza kabisa kuita andika Bibi yako akiwa na maana mkeo halafu ni msomi walobobea kiswahili chuo kikuu cha Nairobi..Sasa mkianza kubishana hapo wakati hakuwa na maana hiyo itakuwa kazi mpya..Kwa hiyo ni vizuri zaidi kujua chimbuko la lugha yenyewe maana hata ktk kiarabu wanatofautiana sana ktk matumizi ya maneno kama unavyoona sisi na Warundi, Wakenya na kadhalika..

Alivyokwambia Topical ndivyo na muhimu uffahamu tu ya kwamba ktk Uislaam huwezi kumwita mtu baba kama sii mzazi wako. Ila kitamaduni mimi namwita Nyerere, nafanya kitchen party, send off na kadhalika tofauti na Faizafoxy ambaye yeye hatambui vitu hivi.. Nyerere namwita baba wa taifa kwa maana ya Utanganyika.
 
Mi nashauri mkubaliane kutokukubaliana. Mwandishi ameelezea utofauti kati ya Baba na Rais bora wa Taifa,kila mtu ameelewa,labda kama mtu hakubali. Halafu ameonyesha kuwa asili ya ubaba wa taifa ama jina hilo haikutokea kanisa katoliki wala si Roma wanaotoa jina hilo kwa viongozi wa nchi hapa duniani,iwe za kiislamu au kikristo. Hata hatukuwahi kusikia aliyetoa jina hilo alikuwa kardinali Rugambwa au Pengo! Mi nadhani imechukuliwa kifamilia zaidi kwamba...kiongozi wa familia huwa ni mwanamume. Na kwa bahati ni kwamba wanaharakati wengi katika ukombozi na mapinduzi ya nchi zao,walikuwa wanaume... Kifamilia kuna mambo ambayo hayakamiliki hadi baba aje.. Heshima ya ubaba,ni kuonesha uongozi,msimamo,ujasiri,vision,na maamuzi ambayo hata kama yatapingwa na watoto au wake zake,ya baba yanakuwa ya mwisho.. Someone can correct me ila huo ndiyo ufahamu wangu.

Kama tupo kwenye surat hii kweli si hoja sasa!
 
hakuna baba zaidi ya aliye kuzaa 'Kwenye Uislam hili ni neno zito sana na lina maana kubwa sana,sababu ni agizo la mbora wa mitume Marehemu muhamad. Alipolaumiwa na uma baada ya kulala na kwewe mke wa mtoto wake wa kupanga akapewa aya na Allah wake na kutoa strict order kwa waumini wake 'Waislam' kwa kupiga marufuku kuita baba mtu ambaye sio biological baba wako,hivyo akajipa uhalali wa kuishi na mkwewe,HAIWEZEKANI kwa Muislam wa Ukweli kukubali kutumia neno baba wa taifa au baba kwa mtu asiye wa kumzaa.

Disco limeshavamiwa na mmasai kaingia na Sime pamoja Rungu..
 
topical nakuomba radhi kwanza... Hoja hii haina nguvu,ama inakosa majibu kwa nini? Ilikuwepo tangu saa 9! Hata FF hakuwahi kuchangia,ingawa naamini kaisoma!
 
Mkuu wangu hata kwa kusoma tu ukiambiwa baba zao wa zamani haiwezi kuleta maana kabisa. baba zao wa zamani ndio watu gani kwa nini isiwe babu zenu maana ujumbe huu unawalenga Umma wa Ilyas na wazazi wao. Halafu kiarabu ni lugha ngumu sana kuitafsiri hivi hivi tu kwa kutumia ufahamu wa watu wako. Na mara nyingi wala sio swala la dhehebu, Fiqhi au Itikadi bali mtafsiri ndiye hutegemea yupo wapi na atatumia maneno gani kwa lugha yake yeye..

Kwa mfano Mkenya ukimpa kuandika Biblia anaweza kabisa kuita andika Bibi yako akiwa na maana mkeo halafu ni msomi walobobea kiswahili chuo kikuu cha Nairobi..Sasa mkianza kubishana hapo wakati hakuwa na maana hiyo itakuwa kazi mpya..Kwa hiyo ni vizuri zaidi kujua chimbuko la lugha yenyewe maana hata ktk kiarabu wanatofautiana sana ktk matumizi ya maneno kama unavyoona sisi na Warundi, Wakenya na kadhalika..

Alivyokwambia Topical ndivyo na muhimu uffahamu tu ya kwamba ktk Uislaam huwezi kumwita mtu baba kama sii mzazi wako. Ila kitamaduni mimi namwita Nyerere, nafanya kitchen party, send off na kadhalika tofauti na Faizafoxy ambaye yeye hatambui vitu hivi.. Nyerere namwita baba wa taifa kwa maana ya Utanganyika.

Tuko sawa mkuu; thanks.
 
Well, tafrisi ya Sheikh Al-Farsy ilitangulia tafsiri ya Barwani. Yeye Barwani anasema hivi kuhusu tafsiri yake: "Kwa hivyo kama ilivyo mkinika Tafsiri hii ya AL-MUNTAKHAB imejaribu kuepuka khitilafu za kimadhehebu katika mambo ya Fiqhi na Itikadi. Kwa sababu hii na kwa kuwa imejaribu kueleza mambo ambayo yamekwisha hakikishwa na ilimu za sayansi, ndio nikavutika nayo mimi na nikataka kuiandika kwa lugha ya Kiswahili, ili Waswahili wenzangu wasio jua Kiarabu wapate nao kuifahamu na iwaongoze kama ilivyo niongoza mimi. Kwa kuwa urefu wake ni wa wasitani, wa kutosha kufahamisha, na si wa kuchosha, basi nimeona ni mnasaba sana kwa wasomaji wa Kiswahili ambao wamekwisha onjeshwa utamu wa Qur'ani kwa tafsiri za Sheikh Al-amin bin Aly Mazrui na Sheikh Abdulla Saleh Al-Farsy au walio isikia ikisomwa tafsiri ya Jalaleini misikitini."

Tafsiri ya Barwani iko karibu sana na maana ya Kiarabu.

weka mstari mzima wa 37:126
Qur 37:125: "Mnamuomba (na kumuabudu) Ba'l na mnamuacha aliye M-bora wa waumbaji (na ndiye Muumbaji peke yake)"

Qur 37: 126: "Mwenyezi Mungu -Mola wenu na Mola wa wazee wenu wa mwanzo!
 
topical nakuomba radhi kwanza... Hoja hii haina nguvu,ama inakosa majibu kwa nini? Ilikuwepo tangu saa 9! Hata FF hakuwahi kuchangia,ingawa naamini kaisoma!

Mkuu samahani sana,

Nakubaliana na wewe kabisa katika kutokubaliana..

Tuko pamoja mkuu.
 
Qur 37:125: "Mnamuomba (na kumuabudu) Ba'l na mnamuacha aliye M-bora wa waumbaji (na ndiye Muumbaji peke yake)"

Qur 37: 126: "Mwenyezi Mungu -Mola wenu na Mola wa wazee wenu wa mwanzo!

Tafsiri ya "wazee wenu" wa mwanzo haiko katika Kiarabu. Angalia tafsiri nyingine za mstari huo wa 37:126 zinasema (msisitizo wa mstari wa kwangu)

"God, your Lord and Cherisher and the Lord and Cherisher of your fathers of old? (Yusuf Ali)

"Allah, your Lord and Lord of your forefathers" (Pickthall)

"Allah, your Lord and the Lord of your fathers of yore?" (Shakir)

"Allah - Who is your Rabb and the Rabb of your forefathers?" (Malik)

Sasa wote utaona wanatafsiri neno Ābā'ikumu (baba zenu). Haizungumzii "wazee wenu" japo kimsingi ndio maana yake lakini literally ni 'baba' siyo 'wazee' vinginevyo hata kwenye Kiingereza wangetumia neno kama "elders" au kitu kama hicho. So, nakushauri uombe radhi kwa kusema kitu ambacho Qurani haisemi. Mtu yeyote anayefahamu kiarabu japo kidogo au hata Kiebrania anatambua neno "ab" linahusiana na "baba" na neno "aba" hata kwenye Biblia linasema ni "baba". Siyo "mzee".
 
Kwanza kabisa huielewi Qur'an, na pili unaongelea Ismail kama vile hafai kumuita Ibrahim "baba" wakati yeye ndio baba yake. hapo sasa? sijui kusudio lako ni nini? Ulitaka Ismail asimuite baba yake baba? maana hapo sijakuelewa kabisaaaa!

Halafu ukija kwenye 37: 125-126, Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?

Hivi ukiambiwa mnamwacha Mbora wa waumbaji Mwenyeezi Mungu, Mola mlezi wenu na Mola Mlezi wa Baba zenu wa zamani.

Huoni hapo kuwa msisitizo upo kwenye "Mlezi" (Rab)? na hii ndio ukirudi kwenye post zangu za nyuma nikaisema kuwa sisi hatuna sifa ya Ubaba kwa mola wetu tuna sifa ya Mlezi, kwa kuwa baba lina mapungufu.

Isitoshe, hapo wanaambiwa wao na baba zao wa zamani, Mlezi wao ni Mola wasimuwache. Sasa wewe na baba yako ni nani wa zamani? na mlezi wenu ni nani?

Usiijaribu Qur'an, hiyo haina makosa. Unapoambiwa soma, ina maana uisome. Haichakachuliki, nilikuambia siku nyingi.

Hapo hatukuzwi baba wa yoyote hapo anatukuzwa "Rab" Mola Mlezi.

Kwa hiyo unakubaliana kuwa mtoto anaweza kumuita baba yake "Baba" na Qurani haikatazi hilo? Na kuwa inaruhusiwa kuwaita watu waliotuzaa kuwa ni baba na haina makosa katika Uislamu?
 
Niliwahi kuambiwa na kufundishwa umuhimu wa kuandika kwa kifupi bila kupoteza maana au kupoteza ujumbe. Nahisi nahitaji kukuambia nilichoambiwa.
 
Hayo wala sina tatizo nayo, hayo ni "by the way" mimi nipo kwenye u "baba" tu.
Baba Mtakatifu, Baba Askofu, Baba Mchungaji wakondoo, na sasa mnataka kutubambikia "baba" wa Taifa. Kama si udini ni nini? Pelekeni u baba wenu kanisani huku mitaani Muacheni nyerere abaki kuwa Rais wa Kwanza wa JMT.

FaizaFoxy, wakati mwingine uwe unapata hata kaujasiri kidogo wa kuukiri ukweli pale unapokosea. Kama kuna nchi ambayo imetoa mchango mkubwa lakini bila mafanikio katika kuleta kile ninachokiita "chokochoko za kidini" hapa nchini kwetu ni Pakistan. Udini ulisababisha nchi ya India iigawanyike vipandevipande na kuzaa nchi za Pakistan na baadaye Bangladesh. Mwanzilishi na aliyeongoza hizo harakati na ambaye hadi leo anatambulika kama Baba wa Taifa la Kiislamu la Pakistan aliitwa Muhammad Ali Jinnah (1876-1948);
Baba-e-Qaum (بابائے قوم) - Father of the Nation - Islamic State of Pakistan.

Muhammad Ali Jinnah, a 20th century politician and statesman, is regarded as the founder of Pakistan. He served as leader of The Muslim League and Pakistan's first Governor-General. He is officially known in Pakistan as Quaid-i-Azam قائد اعظم "Great Leader" and Baba-e-Qaum بابائے قوم "Father of the Nation".
Hapo sasa FaizaFoxy, mwongo mkubwa, mzandiki na mchochezi - unasaliti imani yako.
His birthday is a national holiday in Pakistan. Jinnah rose to prominence in the Indian National Congress initially expounding ideas of Hindu-Muslim unity and helping shape the 1916 Lucknow Pact between the Muslim League and the Indian National Congress. He proposed a fourteen-point constitutional reform plan to safeguard the political rights of Muslims in a self-governing India.
Haya tayari tunayashuhudia hapa kwetu Tanzania, kila siku malalamishi ya kubaguliwa shauri ya mfumo Kristo.
Jinnah, advocating the Two-Nation Theory, embraced the goal of creating a separate state for Muslims as per the Lahore Resolution.
Kuna mchochezi anaitwa Mohamed Said, mfuasi mzuri sana wa siasa za Pakistani - eti anaandika historia mpya ya Tanganyika ! Lengo ?
The League won most reserved Muslim seats in the elections of 1946. After the British and Congress backed out of the Cabinet Mission Plan Jinnah called for a Direct Action Day to achieve the formation of Pakistan.
Muhammad Ali Jinnah alikufa mwaka moja baada ya kuanzishwa kwa taifa la Kiislamu la Pakistani.

FaizaFoxy, yawezekana wewe ni Muislaam safi na unaujua Uislaam kuliko hawa Wapakistani lakini ukweli ni kuwa Pakistan, nchi iliyoanzishwa kwa misingi ya Kiislaamu inaye Baba wa Taifa. Nakuapia kuwa hutaweza kuubadilisha huo ukweli huko Pakistan hata ukifunga mwaka mzima na kulia hadi utoe damu, na hapa Tanzania hata ukitambika huwezi kuufuta ukweli kuwa Baba wa Taifa letu ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
Wewe unayajuwa mafundisho ya dini yangu? ngoja nikupe darsa kidogo; hakuna mahali nnafundishwa kuwa na baba zaidi ya baba yangu mzazi, katika mafundisho ya dini yangu, hata ndugu ya baba yangu sipaswi kumuita baba ni "Ami" yangu, hata Mtume Muhammad siwezi kumuita baba, kwenye Qur'an nafundishwa hivi:

Qur'an 33:40
Muhammad si baba wa yeyote...

Ikiwa hata mtume wa Mungu na kipenzi cha Waislaam, Muhammad (SAW) siruhusiwi kumuita baba, leo nikamuite Nyerere "baba", kwa kisa gani?

Nnaweza kuwa na wazee na nnatakiwa niwaheshimu lakini siwezi kuwa na baba asiyenizaa. Hata mume mwingine wa mama yako huruhusiwi kumuita "baba" Kiislaam.

Usiongelee dini za watu kama huzijui, uliza.

Kwanza, umenukuu vibaya aya ya Qurani Tukufu na utuombe radhi kwanza. Umenukuu nusu na kuacha taswira kwamba Qurani inasema Mohammed hakuwa na mtoto yeyote (kwamba hakuwa baba wa yeyote). Aya nzima inasema

Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Sasa sijui kwanini umenukuu aya ya Qurani vibaya hivyo tena kwa kuipotosha. Sasa TUOMBE RADHI KWANZA kwa kuinukuu vibaya tena na kupotosha maana yake.
 
Nna uhakika unaelewa maana ya nukta tatu baada ya sentensi na nimeweka namba ya aya na hayo maneno yapo na ni kama ulivyoyanukuu wewe, Jee kuna tofauti ya nukuu yangu na yako? nukta tatu humaanisha nini?

Naona bado una usongo wa kukutaka uombe msamaha kule kwenye jukwaa la Mohamed Said kwa kunukuu kwako aya za Qur'an visivyo. Hapo mimi bado hujanipata, hakuna kosa hapo, utachekwa ukiniambia hujui maana ya hizo nukta tatu na reference juu.

Yaani, unahalalisha kunukuu nusu na kupotosha maana kuwa ni kitu sahihi? Hivi mtu akitumia ulichosema wewe (na hana hiyo aya) si anaweza kuamini umemaanisha kuwa Mtume hakuwa baba wa "yeyote" wakati si kweli? Omba radhi kwa sababu japo yawezekana ulifanya kwa nia njema maana yake imepotoshwa na you know better.
 
Baba yako ni baba yako, hakuna mahali niliposema huwezi kumuita baba yako baba, lakini huwezi kumuita baba ya mwenzako baba unamuita kwa heshima "Ami" hata kama ni mume wa mama yako ambae si baba yako mzazi Kiislaam huwezi kumuita baba. Na hatuna vyeo vya u Baba katika Uislaam kama vile Baba Mtakatifu, Baba Askofu, Baba Mchungaji, Baba wa Taifa. Hakuna hizo katika Uislaam kuna baba yako tu mzazi basi.

Hakuna mahali nilisema huwezi kumuita baba yako baba. Naona unaongea kama vile kuna mahali nilisema siwezi kumuita baba yangu baba au niliwahi kumuambia mtu asimwite baba yake baba. Unanshangaza.

Ni wapi nilisema Qur'an inakataza usimuite baba yako baba?

Sasa na hii ya kusema "baba zenu wa zamani" yaani wazee waliotutangulia nayo ina makosa? Maana sijaona mahali popote ambapo Qurani inakataza kuwaita wazee waliotutangulia kama ni "baba zetu".
 
Back
Top Bottom