Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

...kwa hiyo tangu Nyerere aondoke watanzania tunachagua mafundi paa wakato hata msingi wa nyumba hakuna? mnaanza kuropoka taratibu mtajikuta mnajitukana wenyewe.

Hakuna siku nchi inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itapata Rais mwingine wa KWANZA.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Ustadhat!mimi naona tuwalaumu walee wanaojitapa kudai uhuru wa nchi hii !nikisema walee najua unanielewa tu!Ni walee wanaolalamika kutengwa!yaani wale jamaa zako wanaosema Nyerere aliwakandamiza!
Iweje waweze kudai uhuru halafu washindwe kuweka misingi?au walimsusia nyerere?au ni porojo zao tu za vijiweni?

Basi kama msingi ni mbovu yatupasa kubomoa jengo...!
Kumbe ndio kazi inayofanyika sasa...yaani tunabomoa jengo na kuanza upya!Hapa tupo pamoja lakini this time hatuwezi kumtumia mkandarasi yule yule wa chanikiwiti!
 
ZeMarcopolo
Kupendwa na watu maana yake ni kufanya mambo yote kwa kuzingatia misingi ya haki, utu bila ubaguzi wala dhulma na kutoa huduma zote za msingi kwa raia unaowaongoza dhidi ya maadui ujinga, umasikini na malazi

This is nothing but naivety. Nadiriki kusema hujawahi kushiriki kwenye siasa, ungeshiriki hata katika level ya kijiji usingesema hivi.
 
Mshikamano wa kitaifa alioujenga Nyerere je, unathaminiwa na jamii? Je, Nyerere alisema nini kuhusu serikalki tatu? Je, wanasiasa na jamii ya leo inasema nini kuhusu serikali tatu? Je, alichofundisha Nyerere
kinafanana na kinachosemwa na jamii?

nyerere alkuwa copy and paste nia yake ya dhati ilikuwa serikali moja ila hakujua jinsi ya kuifikia ni rahisi kufika kwenye serikali moja kupitia serikali tatu kuliko kupitia serikali mbili. nyerere hakuona hilo. alipiga mahesabu vibaya hakujua kuwa kuna paradox. kwamba kwenda moja sio mpaka upitie mbili unaweza pitia tatu.
 
kuna kitu nimejifunza hivi karibuni harafu nimekikubali sana kwamba raia wa kawaida hajali nani anatawawala ikulu anachojali ni mkate uwpo mezani. je nyerere alihakikisha kwamba hata yeye akiondoka madarakani watanzania wanapata mkate kama kawaida?. hapana aliweka maZingira kwamba mwinyi akija nae atumie utashi wake. hakuweka misingi imara na thabiti ambayo kama nchi tulitakiwa kufuata kama waLIvyfofanya china. ni kana kwamba alijua atatawala milele hivyo hakuandaa watu wa kuendeleza mawazo yake ambayo from my heart nakubali yalikuwa mazuri kwa nchi maskini kama yetu (nchi maskini zinafaa ujamaa lakini tajiri inafaa ubepari
). halarafu mkuu usifurahie elimu ya bure maana mara nyingi inakuwa sio bora vyuo vyote ambavyo viko kwenye ivy league ni binafsi, ni nyerere aliekuwa na mawazo mgando kwamba tutapata elimu bora bure!, hayo sio maono.


e


Kwanza; unapojadili tuende kipengele kwa kipengele naomba upitie upya maelezo yangu kisha kwa kila kipengele jadili

ukilinganisha na hawa wasasa na pia kosowa udhaifu wa JK nyerere usitowe majibu ya jumla ambayo hayaleti maana halisi

Pili unataka kuniambia elimu ya sasa ni bora kwasababu ni ya malipo kwa failure ya 90%?


quote_icon.png
By adolay

Hebu fafanua tuijadili vizuri hapo kwenye red, mimi naanza halafu wewe pinga hoja zangu......tujadiliane.

-Madini
Alikuachieni tena kwa ahadi kwamba mtavuna mkiwa teyari

-Elimu
wakati wake JK Nyerere, japo walifaidika wachache lakini wote masikini kwa matajiri walisoma shule za aina moja na waliofaulu waliendelezwa mpaka mwisho, leo hii watu binadamu fedha, walalahoi shule za kata hakuna chochote....

-Dawa za kulevya,
Wakati wa nyerere mlipata kusikia ujinga wa madawa haya kama ilivyo sasa na jinsi watanzania wanavyoteketea?

-Afya,
Pamoja na uchache wa dhahati na vituo vya afya, ukienda kutibiwa unapata dawa za uhakika, bure wahudumu na madakitari walifundwa na walikuwa wazalendo wa kweli.

-Polisi, jeshi na usalama wa raia,
Wakati wa Nyerere vikosi hivi vilitawaliwa na nidhamu ya hali ya juu, uzalendo na ushilikiano kwa raia, walihifadhi siri za serikali kwa umakini mkubwa leo hii kila kitu ni upuuzi tu

-Mbuga za wanyama na maliasili

Mliwahi kusikia meli kusafilisha meno ya tembo?, Ndege kubebe twiga, Loliondo kupigwa mnada na akina Katabalo kuuwawa?

-Udini na mshikamano miongoni mwa raia wa tanzania
Mliwahikusikia watu kugawanyika kama ilivyo sasa kwa mitazamo ya udini, ukabila na ukanda? (Tulisifika duniani kote kwa jina moja - tuliitana Ndugu FaizaFoxy, Ndugu Red Giant nk)

Mnataka misingigani nyinyi??? unaweza kumpeleka punda hadi mtoni lakini jukum la kunywa au asinywe maji linabaki kuwa hiari yake sio mchungaji.
 
Hilo ni kosa kubwa sana kati ya makosa yaliyowahi kufanywa na kiongozi wa nchi. Usilitaje wala usilikumbushe.

Ni maoni yako sikatai lakini; nakuhakikishia wewe huijui nchi hii vizuri wala historia yake pengine hata somo hilo hukusoma kabisa, mwalimu hakukufundisha au hukulipenda ukawa unashinda shule au kulala darasani ukaishia kusikia habari za wadanganyika mtaani ukaziamini na ndo umezitumia kujibu hili swali kirahisi na kijuujuu! Kama wewe msomi huwezi sema AZIMIO LA ARUSHA HALINA FAIDA KABISA na unajigamba; Eti, hutaki kulisikia kabisa! Embu rudi darasani uanze kusoma upya elimu yako ya siasa na Historia ndo uje uchangie humu usije ukakera watu bure!
 
Unapotaka kufananisha mtu aliyekaa madarakani miaka 23 na aliyekaa miaka 8 unaonyesha ukosefu wa upeo, lakini hata utakapoamua kufanya hivyo kwa kutumia vitu vinavyopimika utaona aibu mwenyewe.

Mwalimu hayupo, lakini maadui zake bado wameendelea kumshambulia. Sasa hivi maadui wa Mwalimu wanataka kuleta serikali tatu ili kuangusha nguzo ya mwisho ya legacy yake. Sijui watu hawa wananufaika vipi na chuki waliyo nayo kwa Mwalimu!

Kwa hiyo muda wa miaka 8 hautoshi kufanya maana? Jaribu kufikiri hali ilivyokuwa enzi za ukombozi pindi mwalimu anachukua nchi,fananisha na mwaka 2005 wakati Chekibobu anachukua nchi. Tafiti na ulinganishe mambo haya,
1) Hali ya uchumi
2) Elimu kwa watu wetu,madaktari,wanasheria,walimu na wataalamu wa fani nyingine.
3) Teknolojia.
Anza na hayo kwanza, usimtetee tu huyu kichwa nazi.
 
b) kwahiyo mwalimu hakuwa na malafiki, hebu tuthibitishie kwa mifano kisha utuambie akina, kaunda, samola, oliverthambo nk walikuwa akina nani kwake...

Mpaka hapo umeshathibitisha kuwa hakuwa na marafiki. Mimi nilifikiri utatataja wazee wa Musoma, Dar es Salaam, Iringa, Dodoma na kwingineko nchini!

Ukitaka kujua kuwa Mwalimu hakuna na marafiki angalia jinsi familia yake ilivyoachwa na mfumo hivi sasa. Hivi unadhani Nyerere angekuwa na marafiki mtu kama mama Maria Nyerere angeweza kudhurumiwa kiwanja?

Madingi wengi walioiga mfano wa Mwalimu wamestaafu hawana marafiki na wanaishi maisha magumu baada ya kutoka kwenye nafasi zao. Huo ndio ukweli wenyewe. Siku hizi mtu anayeishi kama Nyerere anaonekana mshamba!

Je, ni legacy gani ya Mwalimu tunayoithamini?
 
Ndio maana nimekuwa nikiwaambia washabiki wa serikali tatu kuwa likipitishwa hilo tu inabidi tujiulize Nyerere tunamuenzi kwa kipi maana Ujamaa na Kujitegemea tulishaupungia mkono siku hizi tunajivunia misaada na ubepari. Ndio maana tunaona vyama vinavyoahidi mabadiliko vikipokea rundo la pesa toka Ujerumani za kuendesha shughuli zake. Nyerere alihamasisha vyama viendeshwe na michango ya wanachama.

Umoja wa kitaifa ndio kilichobaki ambacho kwa kuleta serikali tatu tunakuwa tumeshauvunja rasmi umoja huo.

Uongozi kwa maslahi ya Umma siku hizi unaonekana ni ushamba na ujinga, uongozi siku hizi ni kwa maslahi binafsi hata wagombea Urais wanaweka vigezo kuwa wahakikishiwe pesa iwapo watashindwa uchaguzi la sivyo hawashiriki!

Je, legacy gani ya Nyerere itabaki?

kwani taifa la Tanganyika litakuwa halina umoja wa kitaifa?Zenj sijui km watawapia chini pemba, au pemba wataungana na mombasa na Lamu au kila kitu kitakuwa km Iraq?

Nyerere kuna mengi ya kumuenzi hata yaliyoshindwa, muungano ukivunjika utakuwa umevunja mpango mmoja kukamilisha mwingine..yaani fate ya wazenj...tayari tuu wameshaanza kuuza haki ya kusajili meli..tayari ni maliberali.....na mengine mengi kufuatia ...wa unguja wanawaita wapemba wa kijijini...
 
Mkuu, unaelewa maana ya MSINGI lakini?

Fundi paa anaweza kuweka msingi?
Sasa tuungane kwa pamoja tusichague tena mafundi paa. Tuchague watu wataotujengea misingi imara itakayoweza kushughulikia ufisadi kikamilifu, wauza unga kikamilifu majangili kikamilifu. TUNAWAJUA VIZURI SANA nani wanaujasiri wa kutuwekea misingi bora na imara tusijitie upofu.
 
Hilo ni kosa kubwa sana kati ya makosa yaliyowahi kufanywa na kiongozi wa nchi. Usilitaje wala usilikumbushe.

Sina hakika kama katika wachangiaji wa THREAD hii ni wasomi wa Siasa au ni waumini wa Hadithi zinazotolewa mabarazani na wanazuoni wasio na uelewa wa siasa zaidi ya tunzi za hadithi km hizi.

Sijui km kwa uchangiajibwa kiwango cha chini hivo ipo haja hata ya kuweka mambo sahihi hapa..... siamini km wapo wanaohitaji maoni yenye utashi .... kusema "AZIMIO LA ARUSHA" ni kosa kubwa kwanza ni kubwa ukilinganisha na lipi? la pili ... Azimio lina makosa yapi yalioainishwa? namwisho huo mbadala wa Azimio umetufikisha wapi kama taifa ambapo Taifa halikufika wakati wa Azimio?
 
Unapotaka kufananisha mtu aliyekaa madarakani miaka 23 na aliyekaa miaka 8 unaonyesha ukosefu wa upeo, lakini hata utakapoamua kufanya hivyo kwa kutumia vitu vinavyopimika utaona aibu mwenyewe.

Mwalimu hayupo, lakini maadui zake bado wameendelea kumshambulia. Sasa hivi maadui wa Mwalimu wanataka kuleta serikali tatu ili kuangusha nguzo ya mwisho ya legacy yake. Sijui watu hawa wananufaika vipi na chuki waliyo nayo kwa Mwalimu!
sio kwamba watu ni maadui wa mwalimu, ila ni kwamba serikali mbili ni impractical. mkuu hivi we huoni hilo.

.
 
akili ndogo ni tatizo sana.
Namnukuu
"tatizo lenu mnachukua mambo yasiyo ya msingi na kuacha mambo ya msingi"
WAPI AZIMIO LA ARUSHA?-mwinyi aliliu
WAPI MASHIRIKA YA UMA?- mkapa aliuza kila kitu.
WAPI HIFADHI YA MALIASRI?-kikwete anauza kila kitu kwa fujo.
 
3. Je hudhani kwamba kambi ni matokeo ya hila na ulafi wa madaraka kwa maana ya kwamba hakuna haki ila lazima mimi nishinde? fafanua tafadhali...

Hili swali ungemuuliza Dr. Slaa, wakati anawafukuza uanachama wale wa kambi ya Zitto na kuwapa jina la masalia huku akimpa msamaa kijana wake Ben Saanane ilikuwa ni matokeo ya hila na ulafi ?
 
Maajabu makubwa sana!!! Makosa ya Nyerere unayaona kirahisi sana, lakini cha kushangaza makosa ya Kikwete huyaoni!!!! Nyerere alifanya makosa hata mwenyewe alikubali alipokuwa hai lakini bado alikuwa ni kiongozi bora kwa kiwango cha juu kabisa aliipenda Tanzania na Watanzania kwa moyo wake wote. Hakuwa fisadi mwenye uroho wa utajiri wa haraka haraka kama Mwinyi, Mkapa na Kikwete na pia alifanya maamuzi mengi mazuri kwa Tanzania na Watanzania ambayo hadi hii leo miaka 28 tangu ang'atuke madarakani bado tunajivunia nje na ndani ya Tanzania. RIP Mwalimu.

Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
 
kwani taifa la Tanganyika litakuwa halina umoja wa kitaifa?Zenj sijui km watawapia chini pemba, au pemba wataungana na mombasa na Lamu au kila kitu kitakuwa km Iraq?

Nyerere kuna mengi ya kumuenzi hata yaliyoshindwa, muungano ukivunjika utakuwa umevunja mpango mmoja kukamilisha mwingine..yaani fate ya wazenj...tayari tuu wameshaanza kuuza haki ya kusajili meli..tayari ni maliberali.....na mengine mengi kufuatia ...wa unguja wanawaita wapemba wa kijijini...

Taja angalau jambo moja la kumuenzi Mwalimu kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom