NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

Hongereni sana nyote mlionaaccess ya nyaraka hizi maana sasa mmfenya macho yetu yaone.Muda wa ukombozi umefika.
 
Mkuu Mbona tumsikia hao kwenye wekundu ni NUSU ya bei ya hawa CCCC, hebu msihukumu kabla ya kujua mambo, iletwe proposal ya hao China Merchants nadhani ndio tutajua mbichi na mbivu, hivi hivi tutakuwa tunasema jambo tusilolijua.

Mkuu......Wizi ni Wizi tu........Uhuni ni Uhuni tu..........kuhujumu ni kuhujumu tu........HAKUNA kitu kinachoitwa kuhujumu/wizi/uhuni NUSU.............wananchi tumewapa dhamana ya uongozi hawa watu sio ili watuletee upuuzi/wizi/hujuma namna hii......halafu mijitu inayooneka imeenda shule na sifa kem kem........Waziri Nundu, Naibu wake, Katibu Mkuu wao......na maafisa wote (waliosaini barua) walioingia kwenye michongo hiyo ni wa kufukuzwa.....period.......
 
Ebanaee huyu Nundu asipojiuzuru watanzania tuandamane hadi magogoni. Hivi inakuwaje jamani? Mbona wenzetu walianzisha maandamano na wakafanikiwa kuziangusha serikali zao?
 

Ndugu yangu Mwita Maranya hiyo kitu ya eyes on hands off iko kwenye makaratasi tu; mawaziri wanaingilia hadi jikoni bila hivyo watakufa njaa.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Pasco jana nilikuona ulipokuwa unamshauri Mh. Nundu kabla hajaanza kuongea na waandishi wa habari.. Ungemsaidia kama ungemshauri atangaze kuachia ngazi kwanza.. Halafu baadae atoe dukuduku lake na kuweka kila kitu wazi.. Kwa kusema kile alichokisema jana watu wengi watakuwa na shaka na credibility yake.. Watakachoona ni yeye kujaribu kupambana kubaki na uwaziri..
 
kila siku wanasafiri nje kumbe nchi ishauzwa hii...nundu anamtupia mpira naibu wake
 

Kwani MoU iliyowekwa hapa JF ni ya CCCC au CMH?
 
ama kwa hakika watanganyika bado tunasafari ndefu sana, ikiwa viongozi wetu wanauza ardhi yetu na rasilimali zetu kwa vipande vya nguo na juice ya machungwa toka south afrika ilihali zinapatikana hata bahresa.
 
Kwa ushahidi wote huu, maamuzi ya msingi yasipochukuliwa basi nitaconfirm kuwa serikali hii inahitaji uongozi wa wananchi kwa sasa ili kurekebisha mfumo ulipo.
 

Mkuu kwanza tunasubiri doccuments na nondo za utetezi wa mambo anayoyafanya Nundu, ikiwa ni pamoja na kujiumbua kwa waandishi wa habari na kitendo cha yeye kushindwa kusema na kuwasilisha docs kwenye kamati. Lakini pili, hakuna kibaraka humu na pengine usiwe kama huyo waziri wewe ni mtu unayeheshimika sana katika jamii, usihukumu watu, humu watu wanataka data na doccuments ambazo tunasubiri za kujibu hizi zilizopo si maneno tu, ambayo yeyote anaweza kuyasema. Maneno kama "nani alimpa ruhusa kwenda kuhongwa" yanahitaji kubebwa na ushahidi wa kutosha maana ni tuhuma nzito kutolewa na Waziri dhidi ya Waziri mwenzake. Kama Mfutakamba amehongwa anastahili kushitakiwa na Nundu asaidie Takukuru (japo haina meno) kumshitaki Naibu wake na Naibu naye kama ana data (hajawahi kusema) naye asaidie dola kumshughulikia Nundu. Hapa hakuna anayebebwa katika mawaziri wala watendaji wako wa serikalini na mashirika yao yanayomeza fedha za umma kila kukicha.

Jambo linalonifurahisha ni kauli yako kwamba kuna mkono wa RA na kwamba Serukamba amewekwa madareakani na RA.... Ukweli ni kwamba kama ni mkono basi si wa RA bali ni EL ambaye ndiye mtu wa Serukamba na nimefurahi pia kusikia kutoka kwako kwamba hii kashfa ya bandari ni zaidi ya Richmond!! Kumbe Richmond ilikuwa kashfa? Kumbe EL na RA hawakuonewa kuwa ni magamba? Naona hapa tuko pamoja, na kwa kweli kama Mfutakamba na yeyote awe Nundu ama nani, wakihusika na ulaji, hakuna wa kubaki wote waondoke. Pia tusaidie kutuambia, taratibu zinasemaje Naibu Waziri ama Waziri akisafiri anamuaga nani? baada ya hapo ndio tuangalie kama kweli alikosea ama la?

Pia, nadhani Nundu asikwepe kama anataka atuambie pia na Dk. Kawambwa naye amekula fedha ili list iwe ndefu na Mkulo naye amekula kwenye hili la Bandari, hakuna kuuma maneno na wote kama wanahusika waache "wafu wazike wafu wenzao" tusimtetee mtu hapa, lakini pia tusifanye ukasuku, tumwage data na ushahidi, wa wazi. Nundu alete hapa hiyo LAPTOP yake aliyoingia nayo katika kamati akasema hana Doccuments. Tuache kushambuliana binafsi tujenge HOJA kwa HOJA, wezi wang'oke tu.
 
"KUJIHUDHURU" ndo nini? kingereza sawa sio lugha yetu, lakini jamani hata kiswahili kinatushinda?
 
Hivi wakuu kwani hata mipango ya serikali kwa ajili ya maendeleo ni SIRI? mbona naona barua zote zimegongwa mihuri "secret" au ndo michezo michafu imetawala hata kwenye miradi ya maendeleo?
 
Ni ajabu kwelikweli namna mambo yanavyokwenda kwenye wizara hizi, ukiziangalia kwa makini unagundua kuwa barua hizi zinatakiwa ziwe zimetoka kwenye taasisi mbili tofauti ambazo zinafanya kazi moja (moja, ya Nundu, inaonyesha kuegemea CMHI na nyingine ya "Futakamba?" inataka mradi huo utekelezwe na CCCC na pia serikali itoe dhamana na mradi huu).

Kwa haraka haraka utaona kuwa mradi wa Nundu una unafuu zaidi kwa serikali ingawaje hakuna taarifa zinazoenyesha gharama kuweza kuthibitisha maoni yangu. Wenye taarifa za gharama za miradi hii miwili (CMHI na CCCC) watusaidie ili tuweze kuchangia tukiwa na taarifa sahihi
 
Kumbeee....sasa nimejua ni kwanini staff wa TPA wanatanua sana hapa jijini: magari ya bei mbaya, wanaburudika na whisky za bei mbaya, wanachukua vimwana vya uhakika, kwao kwenda UK na Dubai ni kama kwenda Kariakoo, kwa ujumla wanatisha kwa pesa. Miaka 45 ni ili wanao na wajukuu waendeleze matanuzi. This is too much now, bora wavuliwe gamba!
 

Well said mkuu!
 
Nundu na wenzake wote wamenasa katika mtego mmoja,...waondoke,..hatutaki kusikia utetezi:doh:

Mwalimu alijenga berth zote 12 pesa alitoa wapi?, yaani leo nchi hii inashindwa hata kujenga hizo berth mbili tu?:A S shade:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…