Mwe waangalifu member wezangu, mnawekwa kwenye mtego. Kuna watu wanatafutwa hapo. Kama mnavyokumbuka mwezi wa pili baadhi ya member wa JamboForum walikamatwa na Jeshi la polisi Dar es salaam.
Katika njia za kijasusi za kupata information hii ni mojawapo. Kuwa makini!!!!!! nina kaufahamu kadogo ka haya mambo narudia tena kuwa makini. Msijaribu kupiga simu, kureplay mail hata kwa mail address unayoifahamu, usiende katika hiyo hospital/kituo cha polisi kuulizia hiyo habali.
Siku nikipata wasaa nitawapa ni namna gani mtu anavyoweza tumia address yako, au password kwa wale wenye uwezo mkubwa katika mambo ya Mtandao(IT)
By profesional sio IT person lakini kuna kamchezo kadogo unaweza ukakafanya na ukapata infromation toka kwa mtu, na ukawasiliana kama vile mnafahamiana.
Ushauli wa bure, usipende kureplay mail, na hata kama ukireplay basi chukua mail address ya mtu huyo huyo toka katika address book yako.
Yameisha wahi nitokea ninayafahamu. Kuwa makini
Nimeichanganua hiyo habari kwa kina, kwa wale ambao mmesoma mambo ya utafiti(Research) mnaweza kubaliana nami. Check mtiririko mzima wa hiyo discussion toka kwa kwa huyo ndugu yake. Anatoa taarifa flani baada ya kuulizwa na kwa ufupi mno. Naweza sema kwa kutega, wee piga hiyo simu uone. Akiipata namba yako umekwisha lupango ni yako au kama sio risasi kwa sababu ya kumwumbua mweshimiwa flani katika JF