NSSF ipo taabani kifedha

Katika hii mada ya NSSF,jamani mtu akitaka kujitoa ambaye alikuwa voluntary inakuwaje na malipo huchukua muda gani? Tafadhalini wakuu

nenda ukiwa na barua ya kuacha kazi, kitambulisho chako cha nssf na picha mbili. ukikamilisha zoezi pale ofisini utaambiwa uende kuchukua hundi yako baada ya siku 14 kama sikosei tangu ukamilishe ujazaji fomu. siku 14 za kazi hivyo ondoa jumamosi, jumapili na sikukuuu
 
Ni vizuri tuwe na uhakika wa Jambo Kama hili Kabla hata halijaletwa hadharani, kwani habari zisizo na uhakika zinaweza kuleta madhara Mengi kwa wananchi.

Huu mfuko unawahusu wananchi wengi sana, na kuwatajirisha mshituko bila na kuwa full details na information kunaweza kuwapa heart attack watu.

Mods this has to be investigated and removed immediately Kama hakuna ukweli, it's very dangerous, at this time leading to election tutaona tetesi nyingi sana.
Kuthibitisha nenda ukawaulize contractors wote wanaojenga miradi mikubwa ya nssf watakueleza yaliyowakuta.
 
Gulwa

Ramadhani Dau kila siku ,anajenga Ghorofa Jipya huyu mzee bwana ,wee mwache tu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hawa watu wanawekeza kisiasa na sio kwa faida, hakuna udhibiti wa matumizi ya fedha za uwekezaji na thamani ya pesa kwenye miradi. Wizi wizi wizi na serikali inahusika kwani ndio uchochoro wa kuchukua pesa. Bora mjitoe mapema kwa wale waliopo huko NSSF. Mtalia muda si mrefu
 
Mbona mi ninavyojua kujiunga ni hiari ndugu yangu au kuna mashirika ambayo wanalazimisha kujiunga na mfuko flani?
Maana mimi nilichagua mwenyewe mfuko wa kujiunga
kuna kwingine kabla ya kusaini mkataba unaletewa fomu ya hii mifuko,hasa NSSF!
 
Mbona mi ninavyojua kujiunga ni hiari ndugu yangu au kuna mashirika ambayo wanalazimisha kujiunga na mfuko flani?
Maana mimi nilichagua mwenyewe mfuko wa kujiunga

Mkuu hata wewe kufungua akaunti kwenye benki yoyote ni hiari yako

Lakini kama benki hiyo unasikia kwamba funds zako haziko salama lazima kuhoji.

By the way.,...Kama mfuko mmoja ukifilisika manake sekta ya Hifadhi ya jamii itayumba.....Hakuna atakayekuwa na imani nayo.

Na ujue kuweka hifadhi kwenye mifuko ya jamii ni lazima kisheria........Kwa hio hata anayeweka fedha zake PPF akisikia NSSF inayumba...he/she must be concerned

Hope utakuwa umenielewa
 
Kwa sasa hivi wameanzisha utaratibu wa kinyonyaji ambao bila kufanyiwa kazi utawaumiza sana wachangiaji kwani unapokuwa umestaafu au kuacha au kuachishwa kazi utalazimika kwenda kwenye tawi la NSSF ambapo ndipo michango yako inapelekwa na si ulikofungulia a/c.

Mfano unafanya kazi na mkazi wa Mwanza ila makao makuu ya kampuni yako Iringa hivyo ulifungua a/c Mwanza ila michango yalikua yakifanyika Iringa basi utalazimika kuyafuatia madai yako Iringa tofauti na hapo mwanzo.

Kama madai yako yatahitajika kufanyika pale yalipokua yakifanyika malipo ya michango iweje basi tawi la NSSF wapokee michango ya mwanachama ambae yuko ktk eneo lingine?

Walipaswa pia kuwaambia wachangiaji hao wayapeleke kwenye tawi la NSSF ombapo mwanachama atapaswa kufuatilia madai yake. Mtu amestaafu kazi Mwanza na madai yake ni sh laki tatu tu atakapokwenda Iringa kufuatia mafao yake kwa gharama zake mwenyewe atapata nn hapo? Au ndio wanawakatisha tamaa wastaafu ili waachane na madai yao ambayo ni jasho lao?
 
Kama magorofa yanayoweza kughrimubilioni 35 wanainflate hadi billion 70 wataachaje kufilisika ..Mfano Mzizima towers na Moshi complex
 
Gulwa

Ina ukweli fulani kwani juzi naona sita kaanza ki aina kumchomoa kijana wake na kumpeleka kwenye bodi ya wakurugenzi ya tpa,
 
Last edited by a moderator:
Gulwa

JF siyo sehemu ya porojo usipende kuokota maneno kwenye vijiwe vya mapuya na kuleta JF.

Hao makadandarasi wa wapi ambao hawajalipwa kwa akili yako nyepesi unadhani NSSF wanafanya kazi na wamwaga zege wa mtaani ikifika jioni wanapanga mstari na kuwalipa, huyo mtu wako kakuingiza chaka.

Ahasante.
 
Last edited by a moderator:
NSSF ni wapuuzi kweli yani mimi niliacha kazi mahali wananisumbua mwezi wa tatu sasa itakuwa kweli hawana hela mara oooh kampuni yenu ilikuwa hailipiii hapa mpaka tuombe ruhusa toka makao makuu tukulipe kwa hapa yani mradi tuu wanakusumbua hapa niko kampuni nyingine imebidi niwahame.

yani wenzao wanalegeza mashariti wao wanakaza sasa hivi ni kuwaacha solemba tu watapata akili na hao wafanyakazi wanaotubenyulia mdomo na hela zetu soon wanapata redandance sasa hivi hakuna kubembelezana
 
Mkuu nimepata kutoka reliable source ila siwezi kutaja hapa kwa sababu zinazoleweka

Haipo sababu yoyote na kwa yeyote awaye asiamini taarifa zako. Tumeona mara nyingi mambo yote ya ufisadi nchini hapa na mabaya yote yanayofanywa na viongozi na watendaji waliopo serikali kuu na hata kwenye halimashauri zetu yanaibuliwa kama sio na mitandao ya kijamii basi ni vyombo vya habari yakiwemo magazeti au wabunge bungeni tena waliopo upinzani. Ni mara chache sana ripoti hizi kuonekana za uongo sana sana zitabezwa na watawala na vibaraka wao na ukweli unapodhihirika taifa limeshapata hasara kubwa.

Mifano ni mingi iliyobezwa mwanzoni lakini ukweli ulipodhihirika taifa limefilisika. Meremeta na nduguze,majengo pacha b.o.t,richmond,escrow n.k. kutaja michache na mikubwa. Hapo hujataja mikataba ya kifisadi. Sasa kama hili la nssf limepigiwa kelele muda mrefu. Serikali na chama chake kinashinikiza uongozi wa shirika kuikopesha fedha kuendesha miradi mikubwa kama madaraja ya kigamboni ambayo haiwezi kurudisha gharama.

Bado ulikuwepo mpango wa kujenga daraja kuunganisha bara na visiwani kwa kuchota hela huko huko kwenye shirika huku wakielewa fedha hizo ni za kuwalipa wafanyakazi wanaostaafu kila wakati. Bora hata serikali ingekuwa inarejesha hiyo mikopo.Hayo hayo yapo m.s.d. na kwenye mabenki yetu makubwa. Sasa serikali nayo haina fedha hivyo madeni yatarithishwa serikali itakayoingia madarakani.

Deni la taifa nalo lipo juu na linaongezeka. Viongozi waliotufikisha hapo wanatujia kwa mlango wa uani kutuomba uongozi na kutupa matumaini. Hiyo nafuu kwa mwananchi wa kawaida itapatikanaje kwa viongozi wale wale walioshindwa kwa miaka zaidi ya hamsini? Mimi sijui ila tufikiri kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom