NSSF ipo taabani kifedha

NSSF ipo taabani kifedha

NSSF walinunua nyumba za kota Magomeni kwa ujenzi wa nyumba, huu mradi nao umekwama?

Afadhali nilihamia LAPF

Mifuko yote imekopwa na serikali. Kila mfuko unaidai kiasi kikubwa cha fedha na ukiunganisha deni la mifuko yote ni karibia bajeti ya nchi kwa mwaka. Kwahiyo kuna kila dalili serikali ikashindwa kulipa haya madeni. Kwasababu serikali haipunguzi deni na muda unavyopita deni linaongezeka.
 
Nimepata taarifa kutoka kwa mtu wa ndani ya nssf kuwa hali ya mfuko huo kifedha ni mbaya sana kiasi cha kushindwa kulipa makandarasi wengi, na baadhi ya miradi hasa ya ujenzi kukwama.

Sababu kubwa inayotajwa kusababisha hali hiyo ni:

1.Serikali kukopa hela nyingi kutoka kwenye mfuko bila kurudisha.

2.Ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi waandamizi wa mfuko ambao wengi wamejilibikizia mali nyingi sana zilizopatikana kwa njia haramu.

Sisi wachangiaji tunazidi kuwa maskini, watu walipewa dhamana ya kutunza michango yetu wanakosa uaminifu.

Hii namba 2 sio kweli. NSSF inaongozwa kwa weledi wa hali ya juu chini ya Aldaktuur Aulamaa Ramadhani Dau. Alhaj huyu haibi, na hana tamaa. Usituchafue Waislam. Ritz
 
Last edited by a moderator:

PSPF ndio hakuna hata 100
 
Taarifa inaweza kuwa sahihi au la! Ila ngoja mi nitafute mahesabu yao yaliyokaguliwa nijiongezee taarifa zaidi.
Ndg zangu tujiongezee utamaduni wa kwenda mbali zaidi ya kusikia. Hii inanikumbusha JK alivyowahi kueajibu jirani zetu. Hivi mtu akapita na kukwambia eeh bwana eeh yule bwana unayemuona anapita ndo mume wa mama yako utaamini.
 
pia na udini unaletwa na dau,ukiwa muislam kuajiriwa ni kama kumsukuma mlevi vile.
 
Mwambieni Mbowe arudishe mkopo wa NSSF ambao amepanga kuwatapeli. Watu aina ya Mbowe ndio hao hao wanaoshiriki kuikwamisha mifuko yetu ya kijamii.

Mm nacho fahamu ni kwamba tukichagua Rais toka ufisadini hata watoto wetu watakuwa mafisadi!

Kumtuma tu ni hela, "bila Tshs 50 au 100/= " haendi dukani!!
 
Hii namba 2 sio kweli. NSSF inaongozwa kwa weledi wa hali ya juu chini ya Aldaktuur Aulamaa Ramadhani Dau. Alhaj huyu haibi, na hana tamaa. Usituchafue Waislam. Ritz

Juzijuzi kanunua mjengo upanga 3b.katoa wapi hizo hela?
 
Last edited by a moderator:
Zito hakukopa alipewa bure nae arudishe?tena alipewa wakati huo akiwa mwenyekiti wa PAC.this is rubbish.angekuwa emmanuel angepewa?wasubirie october
 
Lazima wafilisike tu. Huo wanaoita uwekezaji ni ufisadi tu. nyumba ambayo wangenunua kwa sh. milioni 60 Temeke wanainunua milioni 300. Unategemea nini?

Hiyo cha mtoto mkuu. Manji waliwahi kumkopesha bilioni 11 akajenga jengo kisha wao (NSSF) wakalinunua kwa bilioni 25 kama siyo 35.
 
Hii namba 2 sio kweli. NSSF inaongozwa kwa weledi wa hali ya juu chini ya Aldaktuur Aulamaa Ramadhani Dau. Alhaj huyu haibi, na hana tamaa. Usituchafue Waislam. Ritz

Nenda magerezani kama hutakuta waislam waliofungwa kwa wizi, huyu bwana ni fisadi anayetumia dini kuficha maovu yake
 
Iwekwe sheria kujiunga na hii mifuko iwe ni hiyari ya mtu.

Mkuu hauna taarifa? Sasa hivi ni hiari ya mtu kujiunga na mfuko apendao mara anapoajiriwa, ila walio kwenye ajira tayari hawaruhusiwi kuhama mfuko alionao. Wajulishe na ndugu zako na rafiki zako. The best mfuko kwa sasa ni LAPF ukifuatiwa na PSPF. Achana na NSSF, PPF na GEPF lao moja. Mfano mtu mwenye mshahara wa 2.5 million akistaafu baada ya kuchangia miaka 20 (240 months) kwa PPF, GEPF na NSSF anapata lumpsum ya Tshs. 38,793,103.45 wakati wa LAPF anaondoka na Tshs. 103,333,333.33. Na pensheni ya kila mwezi haitofautiani sana japo hao PPF, GEPF na NSSF wanalipa kubwa kidogo.
 
Fanya utafiti zaidi Mkuu... NSSF iko imara kuliko mifuko mingine ya hifadhi za Jamii... Ni kweli kuwa Serikali imekopa sana LAKINI kutokana na uongozi Imara wa Dr DAU ... NSSF inavitega uchumi vingi vya maana vyenye uhakika wa kuwalipa wadau wake wakati wowote ... Unafiq na Uzandiki wa kushambulia Taasisi zenye kuongozwa na watu wa imani tofauti na Vatican unajulikana ... Acheni Upuuzi ... mnatakiwa kutambua juhudi zao na kuwaenzi ....

Nimepata taarifa kutoka kwa mtu wa ndani ya nssf kuwa hali ya mfuko huo kifedha ni mbaya sana kiasi cha kushindwa kulipa makandarasi wengi, na baadhi ya miradi hasa ya ujenzi kukwama.

Sababu kubwa inayotajwa kusababisha hali hiyo ni:

1.Serikali kukopa hela nyingi kutoka kwenye mfuko bila kurudisha.

2.Ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi waandamizi wa mfuko ambao wengi wamejilibikizia mali nyingi sana zilizopatikana kwa njia haramu.

Sisi wachangiaji tunazidi kuwa maskini, watu walipewa dhamana ya kutunza michango yetu wanakosa uaminifu.

Hivi hao SSRA wanafanya nini ? ... hawaoni hii tofauti?
Mkuu hauna taarifa? Sasa hivi ni hiari ya mtu kujiunga na mfuko apendao mara anapoajiriwa, ila walio kwenye ajira tayari hawaruhusiwi kuhama mfuko alionao. Wajulishe na ndugu zako na rafiki zako. The best mfuko kwa sasa ni LAPF ukifuatiwa na PSPF. Achana na NSSF, PPF na GEPF lao moja. Mfano mtu mwenye mshahara wa 2.5 million akistaafu baada ya kuchangia miaka 20 (240 months) kwa PPF, GEPF na NSSF anapata lumpsum ya Tshs. 38,793,103.45 wakati wa LAPF anaondoka na Tshs. 103,333,333.33. Na pensheni ya kila mwezi haitofautiani sana japo hao PPF, GEPF na NSSF wanalipa kubwa kidogo.
 
Fanya utafiti zaidi Mkuu... NSSF iko imara kuliko mifuko mingine ya hifadhi za Jamii... Ni kweli kuwa Serikali imekopa sana LAKINI kutokana na uongozi Imara wa Dr DAU ... NSSF inavitega uchumi vingi vya maana vyenye uhakika wa kuwalipa wadau wake wakati wowote ... Unafiq na Uzandiki wa kushambulia Taasisi zenye kuongozwa na watu wa imani tofauti na Vatican unajulikana ... Acheni Upuuzi ... mnatakiwa kutambua juhudi zao na kuwaenzi ....

Kwa hiyo uongozi na dini ya mtu vina uhusiano? Hivi ninyi kwanini mnapenda kukimbilia dini wakati kinachoongelewa hapa ni facts na hoja. Sisi tunaweza kuweka picha na majengo makubwa ya kifahari yanayomilikiwa na viongozi wa nssf kwa kificho ambayo hayalingani na kipato chao. fisadi ni fisadi awe mkristu, mwisilam au pagani!
 
weka watu wajadili... wenzenu hawana bajeti ya Bar ...

Back
Top Bottom