NSSF ipo taabani kifedha

NSSF ipo taabani kifedha

Nimepata taarifa kutoka kwa mtu wa ndani ya nssf kuwa hali ya mfuko huo kifedha ni mbaya sana kiasi cha kushindwa kulipa makandarasi wengi, na baadhi ya miradi hasa ya ujenzi kukwama.

Sababu kubwa inayotajwa kusababisha hali hiyo ni:

1.Serikali kukopa hela nyingi kutoka kwenye mfuko bila kurudisha.

2.Ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi waandamizi wa mfuko ambao wengi wamejilibikizia mali nyingi sana zilizopatikana kwa njia haramu.

Sisi wachangiaji tunazidi kuwa maskini, watu walipewa dhamana ya kutunza michango yetu wanakosa uaminifu.

Huwa nashangaa sana, yaani wamachama tunaokatwa mishaara yetu kila siku tuna hali ngumu ya maisha na wanaotutunzia wanaaisha mazuri sana. Hapo ndo utangundua aliyeturoga waafrika kashakufa.
 
Mwambieni Mbowe arudishe mkopo wa NSSF ambao amepanga kuwatapeli. Watu aina ya Mbowe ndio hao hao wanaoshiriki kuikwamisha mifuko yetu ya kijamii.
Mwambie Magufuli amtumbue jipu kama ni kweli la sivyo tutajua anatumbua dagaa tu na kuacha mapapa?
 
Mwambie Magufuli amtumbue jipu kama ni kweli la sivyo tutajua anatumbua dagaa tu na kuacha mapapa?
Wa kutumbua ni vigogo wa Nssf wanaotumia michango yetu kujinufaisha kwa kujiwekea mijengo ya kufa mtu na kununua magari ya kifahari .tunakuonea magufuli chukua hatua kwa hawa watu
 
Back
Top Bottom