Nmb yapata ceo mpya

PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
58
BANK YA NMB inatarajia kuwa chini ya CEO mpya ambaye anaitwa Mark Wiessing
, ambaye kabla ya kuja NMB alikuwa managing director wa ZANACO BANK, Bank ya biashara huko zambia, Mark wiessing anarajiwa kuanza kazi tarehe 15/11/2010.
CEO aliyemaliza mkataba wake bwana BEN CHRISTEEANE, anatarajiwa kurudi kwao UHOLANZI, baada ya kumkabizi kazi bwana Mark Wiessing.
 
Huyo bw ben aliibadilisha sana nmb ikawa na faida kubwa kuliko bank zote,ingawa mkapa aliwahi kusema nmb ni hasara tupu lazima iuzwe ilikua mei mosi uwanja wa taifa!
 
wadau wa NMB wanasema hata huyo CEO mpya naye ni MZURI ameibadilisha sana ZANACO BANK, profit yao imekuwa kwa zaid ya 15%,
 
sio hao ma-ceo wanaozibadilisha hizo benki, bali ni serikali na wadaou wengine kwa ujumla........... fikiria kwa mfano benki ambayo mishahara yote ya wafanyakazi wa serikali inapitia humo kwa nini isipate faida?......... total wage bill kila mwezi ni sh. hapi? na kwa mwaka kuna miezi mingapi?.............. na proportion ani ya mishahara huwa saved na ngapi uwa immadietely withdrawn........... hiyo inayokuwa saved inaihakikishia benki liquidity ya kiasi gani?............. so sera yenyewe ya serikali ni catalyst tosha ya steady growth kwa NMB............. but hongera ma-ceo ............. at least mmeonyesha kitu amabacho wansiasa wetu hawakuamini kuwa kipo................
 
Mkuu NMB ina wanahisa wa nje wanaoshikilia hisa nyingi. Hivyo sio ajabu kwa CEO kuletwa na wao kulinda masilahi yao.

Hakika nakubalia na wewe.....mtizamo wangu...ni kwamba ni hivi unajua kuwa CEO need some qualification na proved achivement ambazo zinatambulika..ili kupewa dhamana ya kuongoza bank kama hiyo....sitakatai...wao kuleta mtu wao wanaye mwamini....je watanzania hawapo wanao wenza kuwa na uwezo kama huo...?
 
BANK YA NMB inatarajia kuwa chini ya CEO mpya ambaye anaitwa Mark Wiessing
, ambaye kabla ya kuja NMB alikuwa managing director wa ZANACO BANK, Bank ya biashara huko zambia, Mark wiessing anarajiwa kuanza kazi tarehe 15/11/2010.
CEO aliyemaliza mkataba wake bwana BEN CHRISTEEANE, anatarajiwa kurudi kwao UHOLANZI, baada ya kumkabizi kazi bwana Mark Wiessing.

Huyo anayekuja kuchukua nafasi ya Ceo anachangamoto ya kuboresha huduma kwani benki ya NMB inawateja wengi sana kiasi kwamba mpaka wanashindwa kutoa huduma nzuri kwa wateja, ingawaje wanapata faida kubwa sana
 
Wabongo hatuwezi kuongoza katika hizi nafasi si unajua udhaifu wetu kwenye kuchakachua tu
angalia taasisi ndogo za serikali tu zinatushinda
 
Wabongo hatuwezi kuongoza katika hizi nafasi si unajua udhaifu wetu kwenye kuchakachua tu
angalia taasisi ndogo za serikali tu zinatushinda

yaani hapo akiwekwa mmbongo utasikia makeke yake ..yaani atakuwa anaajiri ving'asti mwanzo mwisho hata kama hawajui kushika kalkuleta watakamata u bank teller
 
sio hao ma-ceo wanaozibadilisha hizo benki, bali ni serikali na wadaou wengine kwa ujumla........... fikiria kwa mfano benki ambayo mishahara yote ya wafanyakazi wa serikali inapitia humo kwa nini isipate faida?......... total wage bill kila mwezi ni sh. hapi? na kwa mwaka kuna miezi mingapi?.............. na proportion ani ya mishahara huwa saved na ngapi uwa immadietely withdrawn........... hiyo inayokuwa saved inaihakikishia benki liquidity ya kiasi gani?............. so sera yenyewe ya serikali ni catalyst tosha ya steady growth kwa NMB............. but hongera ma-ceo ............. at least mmeonyesha kitu amabacho wansiasa wetu hawakuamini kuwa kipo................

Mbona walipokuwa wamatumbi wanaomgoza hiyo Benki ilikuwa dhoofu hali, na conditions za kupitishia mishahara huko zilikuwako?
 
Mbona CRDB inaongozwa na mbongo na inasonga mbele? watanzania tuache kudharau uwezo tonao ila tunanyimwa tu!!
 
Uyo CEO mpya aanze na izi foleni wasidhani ni SIFA kuwaweka foleni walimu for 6 hours kwa ATM.
Am sure they are paid mishahara mikubwa to think and come up with altenatives ka kila tatizo
 
Hivi wabongo hakuna wanao weza nafasi hizi?
wapo wabongo wenye uwezo lakini ni wachache sana tena sana, unajua wabongo wengi tunafanya kazi bila ya kuweka malengo na mipango ya kushika nafasi kubwa kama hizo, nafasi kama CEO wa benki ya NMB ni position kubwa sana na mtu kupata nafasi kama hiyo unatakiwa uwe una historia nzuri ya utendaji kazi wenye mafanikio ya kuridhisha kwenye taasisi zinazofanana na NMB. Sio kama hawapo wabongo wenye uwezo wapo watu kama kina Kimei, wakurugenzi mbalimbali wa BOT, na baadhi ya watu walioshika nafasi kama hizo ktk mabenki binafsi nchini.

Kikubwa nachokiona ni kujipanga sisi kama watanzania kujiendeleza na kufanya kazi kwa ufanisi ili tuweze kupata uzoefu mkubwa na mafanikio ya kutuwezesha kushika nafasi kama hizo. Otherwise tutaona majina yaleyale kwenye uongozi na kuletewa watu kutoka nje kama tusipojitahidi kuongeza ufanisi, elimu na tija katika kazi
 
KUMBUKA CRDB ni PRIVATE NI YA WATU WENGI, HIYO NMB UKIWEKA WABONGO KWANZA ATAANZA KUWEKA MJOMBA SHANGAZI MTOTO WA BIBI MARA WIZI MARA DEMU WANGU. HIYO CRDB UKIFANYA UPUUZI UNAFUKUZWA BOARD NI KALI KAMA NYUKI WANATAKA FAIDA WEWE KAMA CEO.

LEO HII OFISI NGAPI ZA SERIKALI WABONGO WAMEZIGEUZA MZAHA, OFISI INAYOFANYA VIZURI SASA NI TAMISEMI NAWAPA BIG UP SANA.
 
huyu CEO anayeondoka hajafanya vizuri kabisa. NMB inajulikana kama "the sleeping giant". Ni aibu hii benki. Ina bahati sana kwa kuwa ni kubwa by default. Mishahara ya wafanyakazi wa serikali inapitia pale. kama ingekuwa wafanyakazi wa serikali wanauhuru wa kuchagua benki wanaoitaka basi ingekuwa shughuli.

hii benki inamiliki sehemu nyingi tokea zamani lakini bado inashindwa na crdb bank ambayo inapanga sehemu kibao. wao town centre dsm wana branch 2, wakati wenzao wana 5

halafu uongozi wao wote umejaa wageni kasoro CFo waziri
 
huyu CEO anayeondoka hajafanya vizuri kabisa. NMB inajulikana kama "the sleeping giant".

Si kweli Ndugu yangu kwani mengi yamefanyika na kama ungejua kuwa MKAPA alitaka hii benki ife usingesema hayo leo, Mfano kilichofanyika ni kuwepo kwa ATM nyingi kupita benki yeyote kwa sasa zipo 300+ na mwaka ujao wanaongeza zingine 100. Matawi sasa 138.Ni aibu hii benki. Ina bahati sana kwa kuwa ni kubwa by default. Mishahara ya wafanyakazi wa serikali inapitia pale. kama ingekuwa wafanyakazi wa serikali wanauhuru wa kuchagua benki wanaoitaka basi ingekuwa shughuli.

Sio defaulty ndugu yangu watu wamefanya kazi, ndio maana leo unaona ipo hivyo. Kuhusu kulipwa walimu ni TENDA ndugu yangu ambayo NMB huwa wanashinda kwa ajili ya kupila hiyo mishahara ya hao wafanyakazi.

hii benki inamiliki sehemu nyingi tokea zamani lakini bado inashindwa na crdb bank ambayo inapanga sehemu kibao. wao town centre dsm wana branch 2, wakati wenzao wana 5

Nadhani utakuwa umesahau MOROGORO ROAD NA KKO BRANCH, by the way kwa sasa BANK HOUSE inafanyiwa ukarabati na itakuwa na uwezo mkubwa zaidi.

halafu uongozi wao wote umejaa wageni kasoro CFo waziri[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom