Namna ya kufanikiwa katika biashara zenye mitaji midogo. Kufikia hadi 66% profit per day

africatuni

Member
Nov 13, 2023
52
104
Habarini wana jamii forums, Hope everyone is excited as I am! ni matumaini yangu wote tu buheri wa afya ya mwili na akili. Kwanza kabisa Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aliyetukutanisha siku ya leo, Kujumuika pamoja katika jukwaa hili kwa lengo la kupanua fikra na maono tuliyo nayo juu ya uchumi wetu..

Nianze kwa kunukuu "The best way in achieving anything is through taking it a day at a time" kwamba Jifunze kunyanyua hatua moja kila wakati ili kufikia malengo yako.

Kama kichwa kinavyojieleza vyema, Napenda leo tupeane dondoo chache na uzoefu kuhusu namna bora ya kuendesha biashara hususani zenye mitaji midogo.

Wafanyabiashara wengi tumeegemea zaidi katika kuboresha bidhaa zetu, kuzipa muonekano wa kishujaa, huku tukisahau ubora wa muundo wa biashara utakao tuwezesha kuuza bidhaa hizi.

Hivyo basi, uzi huu utajikita zaidi katika kupeana mbinu za kufanya bishara kwa mafanikio lakini pia mwisho nitatoa mfano halisi wa namna ambavyo binafsi nimetumia kanuni hizi na kufanikiwa kufikia 66% profit kwa siku moja tu!.
Turuke moja kwa moja kwenye mada,

ili kua na biashara imara inabidi uzingatie haya mambo nitakayo ainisha hapa chini..

1.Uongozi bora.
Ili ufanikiwe katika biashara ndogo lazima utambue kua wewe ni kiongozi, you are the CEO of your business na kiongozi bora wa biashara ni yule ambaye kila siku anatafuta mbinu za kuboresha huduma yake ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko, kujifunza kwa waliofanikiwa, ku update mawazo na mbinu anazotumia kulingana na utandawazi, kupunguza gharama za uzalishaji ili kuongeza faida.
Umechagua kua mjasiriamali basi tambua kua its a lonely journey, usiishi kama wengine jiwekee malengo anza kuyatimiza pole pole, huna muda wa kupoteza..every minute counts!

2. Fikia watu wengi.
Biashara ndogo zina faida kubwa sana, hufikia hadi 70-80% (percentage profit). Changamoto huwa pesa iliyopo katika mzunguko (cashflow) ni ndogo sana hivyo ata mafanikio yake ni kiduchu mno.

Suluhisho pekee, fanya kwa ukubwa.. zalisha bidhaa za kutosha wacha uoga! kama ni maandazi zalisha ata 500 kwa siku, tafuta machalii wazungushe mitaani nyumba kwa nyumba, kwenye mikusanyiko ..hakuna asiye taka vitafunwa asubuhi mlangoni kwake, chukua ata 70 waachie 30 wasambazaji..amka mapema pambania ndoto zako. Unavyo fikia watu wengi zaidi ndivyo unavyoongeza uwezekano wa kukutana na wahitaji. Bila shaka ukipita kwa watu 100, hukosi 40 wakukuungisha. Wanaokataa haina maana wamekukataa wewe labda yawezekana hawana uhitaji na bidhaa yako kwa wakati huo pengine kesho watakua wateja. Remember rejection is not personal!

3.Tumia watu.
Kaimisha watu majukumu (deligate power) ili uweze kuhudumia watu wengi kwa wakati.
Wengi tumekua tukifanya kila kitu peke yetu, matokeo yake tunahudumia watu wachache, faida kiduchu na zaidi udumavu wa biashara. Vijana ni wengi wapo mitaani tu hawana mbele wala nyuma..tafuta vijana wafundishe namna unavyofanya, wabebeshe maono ya biashara..muoneshe atapata nini kupitia wewe..usitamani maendeleo yako tu binafsi, beba pia na mzigo wakutamani vijana wako wafanikiwe kimaisha, wafundishe mbinu za biashara, wanoe wawe na fikra kama zako.. ikiwezekana walipe kwa asilimia za mauzo ili kuwapa hamasa ya kuongeza mapato.

4. Weka akiba. (Savings)
George clason mwandishi wa richest man in babylon anasema "I found the road to wealth when I decided that a part of all I earned was mine to keep. And so will you." kwamba yeye binafsi aliifikia njia ya mafanikio yake baada ya kutambua kua sehemu ya kila anachoingiza anapaswa kuhifadhi. Na wewe ufanye vivyo hivyo.

Nakusihi sana na Mungu akupe hekima katika hili ni lazima uweke akiba kama unahitaji kufikia malengo yako, na hii ndio siri namba moja yakufanikiwa katika bishara ndogo.
Tengeneza kibubu chako leo.. kila unapofunga hesabu zako tu! Mapato yako yote ya siku; toa sehemu isiyopungua asilimia 10 weka kwenye kibubu kabla ya kufanya chochote!.namaanisha chochote!, wala usijiulize mara mbili..isiwe chini ya asilimia 10.
Ukiweza kuhifadhi zaidi basi mafanikio yako yatakua kama ua kando ya chemi chemi.

Akiba yako hii ni kwaajili ya kukuzalia watoto na hawa watoto wakupatie wajukuu na wajukuu wakupatie vilembwe n.k..namaanisha kua, kazi pekee! pekeee! ya hii akiba ni kukuzalishia! Usitumie akiba yako kwa matumizi binafsi ya aina yoyote. Fedha hii utaitumia kuwekeza katika vitu vitakavyo kuingizia pesa.. Fedha inatulia kwa bwana mwenye nidhamu.

5. Usimamizi wa mtiririko wa pesa ( cashflow management)
Huu ndio msingi wa biashara yoyote ile, ukifeli hapa basi hakuna uwezekano wakunusa mafanikio. Jifunze kutambua kua biashara ni mtu (its a legal body) wafanyabiashara wakubwa wanatambua hili vyema; hivyo basi tofautisha mapato yake na yako, ikiwa na maana hela ya bishara haina undugu na wewe..
Jilipe mshahara ili uwe na nidhamu, epuka kuchukua pesa ya biashara kiholela holela ukijipa matumaini kua ni yako.

Nunua asset punguza liabilities. Asset ni chochote kinachokuingizia pesa mfukoni mwako, liability ni chochote kinachotoa pesa mfukoni mwako. Epuka kufanya matumizi yasiyo ya lazima. Fanya matumizi ya muhimu tu!.
Soko lina ongea linauwezo binafsi wa kushawishi, hivyo hakikisha unapoenda kufanya manunuzi unaandaa budget kabla, itakusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na milele daima, nunua vilivyopo kwenye budget yako pekee.
Faida yako unaipata unaponunua (profit is made when you buy) hivyo nunua bei ya chini kadri inavyowezekana, punguza matumizi ongeza mapato. Ainisha wazi matumizi, mapato, manunuzi katika vitabu kwa ajili ya kumbukumbu, itakujengea nidhamu ya fedha. Jua kuweka ela yako kwenye vitu vya msingi, mfano: iyo ela unayonunulia lunch kila siku ukiwa ofisini, weka kwenye matangazo, watu wakujue. Beba chakula chako kutoka nyumbani.

6.Jitangaze.
Zig zigler mwandishi wa Secrets of closing the sale anasema "The man who builds a better mousetrap—or a better anything—would starve to death if he waited for people to beat a pathway to his door. Regardless of how good or how needed the product or service might be, it has to be sold"
Kwa ufupi ni kwamba, chochote kile unachotaka kuuza unapaswa ukitangaze hakuna atakae ota kua unabidhaa bora ndani kwako.
Tafuta njia bora ya kutangaza bidhaa zako, tumia posters, social medias post kote, yani kasirika, taka kila mtu akujue funga speaker au vipaza sauti..

usikubali dhambi ya watu kutojua kua kuna saloon mpya imefunguliwa manzese. Usikubali watu kutojua maandazi yako yana nazi.. hichi unachojitofautisha na wengine kipe hype ya kutosha, watu wafahamu, wakupe nafasi ndani ya mioyo yao, Toa zawadi kwa mtu atakayeleta mteja mfano: Ukituletea mteja wa maandazi 10 unapata andazi 1 bure..au ukinunua maandazi 20 unapata 2 bure!! ...Kisha print aya maelezo ( ukitoa copy 100 total cost inakuja 5000/= @50) weka namba za simu alafu bandika mtaa mzima, kila kona ya mji yatapakae matangazo yako..fanya iv tuone kama hutakimbia wateja.
Be creative.. usikubali kulala kila siku bila wazo jipya la kuongeza watu. Coca-cola ijapokua na umaarufu wake hadi leo hukosi matangazo yake kila kona ya mji na Medias.

7.customer care.
Mteja ni mfalme. Mpe thamani kila mteja, muoneshe yeye ni wa muhimu sana kwako. Muulize maswali yatakayopelekea kutambua uhitaji wake kisha msikilize kwa makini ili uweze kuyatatua. Mtambue mteja kwa jina lake la kwanza kama unalifahamu. "Jim Farley discovered early in life that the average person is more interested in his or her own name than in all the other names on earth put together" ni ukweli usiopingika kua tunavutiwa zaidi na majina yetu kuliko majina mengine yote yaliyowahi kuwepo duniani.

Naendelea kunukuu "Remember, you do not sell a product or a service. You sell a solution to a problem or the satisfaction of a genuine need".
Siku zote kumbuka ya kua hauuzi bidhaa au kutoa huduma bali unauza suluhisho la tatizo fulani au unakidhi haja ya hitaji la muhimu. Kwa focus hii huwezi kumpatia mteja bidhaa isiyofaa, lakini zaidi itakutengenezea brand na jina kubwa.

Case study: Jikwamue kiuchumi kwa biashara ya barafu!.
Napenda kukupongeza wewe ambae tupo pamoja hadi sasa, hakika wewe ni mmoja kati ya wachache waliofanikisha au watakaofanikisha njia yao ya uhuru wa kifedha lakini pia ni muumini wa kweli wa kujifunza na hii ndiyo dhana inayotutofautisha na watu wengine.

Waswahili husema mkono mtupu, haulambwi. Wala koti la babu, haliwezi kukosa chawa.
Hivyo basi, Tazama biashara ya barafu ambayo ni moja kati ya biashara ndogo ila ikifanywa kwa ubora inaweza leta mafanikio makubwa na kukufungulia njia katika kuyafanikisha malengo yako. Tutaichakata mwanzo hadi mwisho, nimeifanya kwa muda mfupi tu! Lakini kwa mafanikio makubwa kwa kuzingatia kanuni zilizoainishwa hapo juu!
Woooow! Am really excited, hope you are eager to see how i can ellaborate this.

Baada ya kumaliza chuo, pale Muhimbili (MUHAS) nikarudi zangu kwetu kilimanjaro, sanya juu! Nikaweka mambo ya udaktari pembeni nikavaa sare za kitaa ..nikasema liwalo na liwe, sijali watu watanionaje after all mimi ndo director, CEO wa maisha yangu, so nitafanya chochote nipate pesa. Nilikua very focused na determination was indeed high enough.

Home kuna fridge kubwa tu la hisense nilimchukulia maza kipindi nipo chuo, baada ya kuomba sana kazi bila mafanikio nikaona mtaji ndani ya jokofu..what a day!! Na hapa ndipo safari yangu ya mafanikio ilianza.

• Nilianza kwa mtaji mdogo sana wa Tsh 4,800 tu.
Na nilianza kwa barafu za ubuyu, ujuzi wote nilitoa youtube ila kadri muda ulivyokwenda nilipata formula yangu makini sana! Nitashea apo chini remember: your profit is made when you buy, Kwahivyo kila siku nilikua nawaza namna ya kuzalisha bidhaa yangu kwa bei ndogo to maximize my profit.
Nilianza na lita 10 za maji ambazo ingridients na bei za kipindi icho ni kama ifuatavyo:-
1.unga wa ubuyu 1/2kg = 1,500
2.Kk sugar 2tbs = 500
3.sukari 1/2 kg = 1,300
4.vifungashio = 1,000
5. Vanilla 1tbsp = 200
6.Rangi = 300
4,800
Nachemsha kwenye kuni uo mchanganyo apo ad utokote kisha napack na kufreeze.

Katika kiwango hichi nilkua nazalisha pcs 110-120 za barafu kwenye 10l za maji.
next day ni mparangano nguo kuchanika ad ziishe. Narudi jion na sarafu za kutosha kama 10,000/= na kidogo.
So ukikokotoa apo,
10,000 - 4800 = 5200.
Net profit = 5,200.

Tafuta % profit
Faida /mapato × 100= % profit
5,200/10,000 × 100= 52%

Tupate wapi biashara kama hii,, where on earth?? 52 % asilimia ya faida.

Ukiweka fixed account au ukinunua hati fungani katika Bank wanakupa 9.5 -10% percentage interest kwa mwaka.
Ila ukiuza barafu unapata 52% kwa siku. Tell me where on earth to find this numbers?!

• Kila baada ya kumaliza kuuza nilikua natoa 5000/= cash naweka kwenye kibubu kabla ya chochote (always pay yourself first- robert kiyosaki rich dad poor dad). Sikutaka mambo ya 10% kwasababu nilikua nina hasira na mafanikio na zaidi sana nimeshaiona njia kwanini nizubae!
Roughly apo kwa mwezi inakuja 150,000/= lakini guess what baada ya mwezi na siku kadhaa ilikua double ya hiyo. 300k what a move!! Endelea chini ufahamu ilivyopatikana..

Ni dhahiri faida ni kubwa ila cashflow ni ndogo sana.
Kila wakati mimi kama kiongozi bora, sikuchoka kujifunza na kuendelea kutafuta namna ya kupunguza matumizi to maximize my % profit lakini pia namna ya kufikia watu wengi zaidi kuongeza cashflow.. waswahili husema mgaa gaa na upwa, hali wali mkavu... haikuchukua muda sana kabla ya kuja na recipe nyingine.

Tazama recipe mpya baada ya kua mbobevu:-
Kwasasa soko lilikua kubwa sana likaanza hadi kunizidi, nikaanza kufunga ndoo kubwa 20l kila siku, kazi ilikua sio ya kitoto vidole vinawaka moto lakini utamu wa mafanikio uliyazidi maumivu..hapa pia ilibidi ni watrain wadogo zangu kupunguza makali ya uchovu.

1.Ukwaju 2,000/=
2.Juice cola 20@ 80 (nunua jag) 1,600/=
3.Rangi 300/=
4.Flavour( vanilla, orange) 2tbsp 400/=
5.Unga wa ngano/ muhogo 1/4kg 500/=
6.vifungashio 2,000/=
Total cost 6,800/=
Chemsha mchanganyo wako! ..

Mabadiliko haya yalitokana na kujua kua wateja wangu walihitaji tu, utamu wakutosha! Ningetumia sukari na kk sugar kama mwanzo ningeendelea kunyonya faida yangu.
Hapa tunapata barafu 200-210 @ 100/=. Kokotoa apo!
200× 100 = 20,000/=
toa matumizi
20,000 - 6,800 = 13,200
Net profit = 13,200.

% profit= 13,200/20,000 × 100
=66%
Wooow!! Bila shaka unaweza kuchakata mwenyewe. Kutoka 52% hadi 66%, hii ndio maana halisi ya kiongozi bora. Asilimia 14 (66-52) zilikua zinapotelea kwa suppliers wangu. Usiridhike na hatua moja piga nyingine na nyingine.. "The moment you see one opportunity, you will see them forever"

Kama ilivyo ada, 12,000/= cash ilikua inaiingia kwenye kibubu kila siku, na kibubu changu kiliendelea kunona siku baada ya siku.

• Tazama mbinu nilizotumia kupata soko kubwa la barafu.
Barafu zangu nilikua nasambaza kwa baiskeli ndogo tu! Inayotumika zaidi na watu wa pwani (Mama twende sokoni)..nazipack kwenye ndoo kubwa chini na pembeni naweka box (nilikua sina dery).
nilianza na shule zangu 4, mbili za sekondari, mbili za msingi..navizia muda wa break ya saa 4 napeleka shule 1 kwasababu muda ni mchache, Na ile ya saa 7 namalizia izo tatu sirudi mara mbili shule moja ukikosa leo tukutane kesho..

Kuna baadhi ya shule wanapiga marufuku vitu kama iv, kwaiyo nilikua mjanja natafuta kachobingo cha kujibanza nje ya eneo la shule..wateja wangu walikua wakiniona natokea tu iv!, inakua vurugu..shule yote inanikimbilia, wanakuja kwa fujo sana ..hili jambo linaleta attention kwa walimu wanaanza kukuwinda...hii nayo ni moja ya changamoto niliyoipata.

Kipindi naanza nilikua nawaambia, ukiniletea wateja wa tano unapata yako moja..kwahiyo walikua wananifanyia kazi kwa bidii sana kunitafutia wateja..
Joe Girard mwandishi wa How to sell anything to anybody, anasema "Recruit your bird dogs and make sure you pay them well"
Hawa "bird dogs" ni wanajeshi wako, watakao kufanyia kazi kwa bidii kutimiza ndoto zako.

Kwahivyo wakati naandaa barafu nafunga izi za kunitafutia wateja..zenyewe naweka kidogo.

• Kadri siku zilivyosonga ndivyo mafanikio yalizidi kuongezeka na milango ya mafanikio kufunguka.. baadae kuna baadhi ya shule nikapata kibali cha kudumu, nikaongeza wasambazaji nakufikia watu wengi zaidi, hivi leo kupitia barafu nimekuza mtaji wa kufanya biashara kubwa zaidi.

Mwisho kabisa, Visualize this thing that you want. See it, feel it, believe in it. Make your mental blueprint, and begin to build.
—ROBERT COLLIER


Imeandikwa nami,
africatuni.
Dondosha uzoefu wako chini apa tuendelee kujifunza.!!
 
Inspired sana.

Kama vijana tungekuwa na uthubutu kama wako tusingelia njaa kimsingi pesa zipo mitaani na zinapatikana ukiweka mbinu ambazo ni sahihi kikubwa ni uthubutu, ubunifu, nidhamu na kuweka aibu pembeni.

Naomba nishare Uzoefu wangu kwenye biashara ya Music na movie library licha ya kuwepo kwa Smartphones hii biashara bado haijashake kiihivyo ukipata sehemu sahihi hususani vicenter vya wilaya au miji inayochipukia still utapata pesa.

Binafsi nimefanya kwa miezi miwili kutokana na ishu za kifamilia sikuweza kuendelea katika kipindi chote nilikuwa naona ukuaji kuanzia siku za mwanzo ambazo nilikosa mteja hata mmoja mpaka kupata loyal customers.

Mtaji ulikuwa ni Computer, Zabufa na meza mipango ilikuwa ni mingi na nilikuwa nikiona nikiyafikia malengo japo ilikuwa mwanzo mgumu ila nilikuwa nafurahia ukuaji wangu.
 
Habarini wana jamii forums, Hope everyone is excited as I am! ni matumaini yangu wote tu buheri wa afya ya mwili na akili. Kwanza kabisa Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aliyetukutanisha siku ya leo, Kujumuika pamoja katika jukwaa hili kwa lengo la kupanua fikra na maono tuliyo nayo juu ya uchumi wetu..

Unafanya biashara gani?
 
Inspired sana.

Kama vijana tungekuwa na uthubutu kama wako tusingelia njaa kimsingi pesa zipo mitaani na zinapatikana ukiweka mbinu ambazo ni sahihi kikubwa ni uthubutu, ubunifu, nidhamu na kuweka aibu pembeni.
Safi sana, asante kwa kutupa uzoefu wako! Na pole sana kwa matatizo yaliyokukumba.. "The moment you see one opportunity you will see them forever". Get your mind better and regain in position, you can make it to greater heights.
 
Habarini wana jamii forums, Hope everyone is excited as I am! ni matumaini yangu wote tu buheri wa afya ya mwili na akili. Kwanza kabisa Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aliyetukutanisha siku ya leo, Kujumuika pamoja katika jukwaa hili kwa lengo la kupanua fikra na maono tuliyo nayo juu ya uchumi wetu..
upewe maua yako mkuu
 
Back
Top Bottom