Mimi nikiwa mfanyakazi wa Taasisi hii tangu kipindi ikiwa NBC Bank nasikitishwa sana na yanayoendelea humu ndani, Kwa kuwa haya mambo tumekuwa tukishauri kwa nyakati tofauti na kupuuzwa nimeona ni vyema niyalete humu ili wadau wote wajue yanayoendelea na Uongozi wa Benki Uweze kutupatia majibu na utatuzi kwani nimefurahishwa sana kuona NMB Bank Plc, wapo hapa Jamii forum na pia wameomba kupatiwa maoni, ushauri na pia malalamiko.
Hii Benki imekuwa ikifanya vizuri katika Nyanja za Kibiashara na kuweza kupata faida kubwa kila kukicha kwa kuboresha huduma mbalimbali kwa wateja wake kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayoendana na wakati huu.
Ila pamoja na hayo yote ya mafanikio kuna mambo mengi makubwa yamejificha kutokana na Uongozi wa Benki hii kutokuwa wakweli na kuendelea kuficha mambo ya hovyo yanayofanywa na Viongozi wenzao kwa kukumbatiana pasipo kuwajibishana kila mambo yanapoenda ndivyo sivyo.
Yafuatayo ni baadhi tuu ya matukio ya kutisha yaliyoikuta Benki hii na kupata hasara kubwa:
Hii Benki imekuwa ikifanya vizuri katika Nyanja za Kibiashara na kuweza kupata faida kubwa kila kukicha kwa kuboresha huduma mbalimbali kwa wateja wake kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayoendana na wakati huu.
Ila pamoja na hayo yote ya mafanikio kuna mambo mengi makubwa yamejificha kutokana na Uongozi wa Benki hii kutokuwa wakweli na kuendelea kuficha mambo ya hovyo yanayofanywa na Viongozi wenzao kwa kukumbatiana pasipo kuwajibishana kila mambo yanapoenda ndivyo sivyo.
Yafuatayo ni baadhi tuu ya matukio ya kutisha yaliyoikuta Benki hii na kupata hasara kubwa:
- Mwaka jana 2022 katika tawi moja la Kahama Benki hii ilipata hasara ya Tsh. 24 Bilioni kutokana na taratibu mbovu zilizowekwa na Uongozi wa Makao Makuu ila kitu cha kushangaza na kusikitisha wafanyakazi wadogo kutoka ofisi za Kanda ya Magharibi Tabora na wengine wa kutoka tawi la Kahama waliachishwa kazi kinyama huku wale wa Makao Makuu wakibadilishiwa nafasi zao na kuendelea kuiingiza taasisi hii katika hasara zaidi mfano halisi ni Bwana Isaac Masusu.
- Kumekuwa na tabia mbovu na ya kushangaza kutoka Idara ya Rasilimali Watu, Ikishirikiana na Idara ya Uchunguzi kufumbia mambo mengi ya msingi kwa Viongozi wa Makao Makuu wakiboronga huku wakawakandamiza wafanyakazi wa hali ya chini.
- Vitendo hivi vimekuwa vikifanya na Ndugu Emmanuel Akoonay na Onesmo Kabeho wote kutoka Idara ya Rasilimali watu wakishirikiana na Ndugu Faraja Ngawala na Prudence Mgalula wote Kutoka Idara ya Uchunguzi Makao Makuu.
- Pia kumekuwa na vitendo ya kudhalilisha wafanyakazi wengine kwa kuwaita kwenye usaili huku wakijua wazi nafasi Fulani inatanganzwa kwa ajili ya Fulani na baada ya usaili Yule Yule aliyedhaniwa inaipata japo hakuwa na vigezo kulinganishwa na wasailiwa wengine.
- Nafasi za Makao Makuu zile kubwa huwa zinajazwa na watu wa hapa hapa Makao makuu na mara nyingine toka nje ya Benki tena kwa upendeleo wa wazi wazi huku wakiachwa wale wa matawini wenye ujuzi na uzoefu maradufu.
- Nafasi ya Katibu wa Benki na Mkuu wa Idara ya Sheria hadi sasa haijajazwa yapata mwaka mmoja huku wakiendelea kukaimu watu wawili wasio na uwezo wa kutosha kwa nafasi nyeti kama hii ambayo ni kiungo kati ya Uongozi wa benki na Bodi ya Wakurugenzi.
- Nafasi nyingine zimekuwa wakipewa watu kwa upendeleo tena wale walioshindwa kufanya vizuri katika nafasi zao za awali, hapa naweka mfano Halisi ya nafasi ya Head of Reteil Banking baada ya nafasi ya awali kugawanywa mara mbili.
- Pia Nafasi ya Manager wa Kanda ya Magharibi na Kanda ya Dar es Salaam, pamoja na watahiniwa kufanyishwa interview muda mrefu tuu ila hadi sasa majibu bado hawajapata na kuna fununu nafasi hizo kupatiwa watu wenye Mazoea ya Kujipendekeza na kuwa wapambe na viherehere wa viongozi.
- Taarifa iliyopo ni kuwa Nafasi ya Zonal Manager Dar es Salaam Zone atapatiwa Isaac David Mgwasa na ya kanda ya Tabora wanatafuta Zonal Manager wa Kike.