Zakaria Maseke
Member
- Apr 26, 2022
- 64
- 98
NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD (NMB) VS (DHIDI YA) NEEMA AKEYO, CIVIL APPEAL NO. 511 OF 2020, CAT.
Mwandishi: Zakaria Maseke
Advocate Candidate
Hii kesi inahusu mfanyakazi (Neema Akeyo) ambaye alifutwa kazi isivyo halali kwa sababu za ubaguzi wa kidini ambapo alikuwa anaenda kufanya ibada siku za jumamosi kama haki yake Kikatiba ya uhuru wa kuabudu.
Lakini pia, sheria haikufatwa ipasavyo wakati wa kumfuta kazi Neema Akeyo, mfano hakupewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuamua kumuachisha kazi.
Watu wengi wameshaiongelea sana. Lakini kutokana na umuhimu wake nimeamua kuitafsiri tena na kuipost ili iwafikie watu wengi hasa waajiri. Kumekuwa na hulka ya kuwanyima wafanyakazi uhuru wa kuabudu, kwa kuwapangia kazi siku za Ibada.
Tuanze na FACTS (STORI YA KESI):
-Neema Akeyo aliajiriwa na Bank ya NMB kama Bank teller, Wilaya ya Karatu.
-Ajira hiyo ilianza tarehe 27/10/2010 mpaka tarehe 5/6/2015 alipofutwa kazi na NMB kwa sababu ya kutoenda kazini (utoro) siku za jumamosi na kutotii mwajiri.
-Neema akaenda kushtaki au kulalamika kwenye Commission for Mediation and Arbitration (CMA) yaani Tume ya Usuluhishi na Uamuzi/Upatanishi, akidai kwamba alifutwa kazi kimakosa na kwamba alipwe fidia kwa kitendo hicho cha NMB kuvunja mkataba wa ajira.
MBELE YA TUME:
-NMB ikakana kuvunja mkataba, ikasema mlalamikaji (Neema) alifutwa kazi kwa sababu halali na kwamba taratibu zote zilifuatwa.
-NMB ikasema kwamba, mlalamikaji alifutwa kazi KWA SABABU YA KUSHINDWA KWENDA KAZINI SIKU ZA JUMAMOSI (UTORO) ambapo ilikuwa ni kinyume na makubaliano ya kazi na kinyume cha sera na kanuni za NMB.
-Baada ya kusikiliza kesi mpaka mwisho, mwamuzi wa Tume aliridhika kwamba, mlalamikaji (Neema) hakufutwa kazi kihalali (was unfairly terminated), na kwamba utaratibu haukufatwa.
-Tume ikasema kwamba, hakuna ushahidi kutoka NMB unaothibitisha kwamba Neema hakuwa anaenda kazini siku za Jumamosi.
-Pia, hata baada ya mlalamikaji kukutwa na makosa, hakupewa nafasi ya kujitetea.
-Hivyo Tume ikasema Neema hakufutwa kazi kihalali.
-Tume ikaamuru, Neema alipwe mshahara wa miezi 36 kama fidia.
NB: (Usiporidhika na maamuzi ya Tume (CMA) unaomba revision (mapitio) kwenye Mahakama ya kazi (Labour Court) - ambayo ni Mahakama Kuu divisheni au kitengo cha Kazi. Zingatia sijasema unakata rufaa (appeal), kuna tofauti kati ya Appeal na Revision.)
-NMB hawakuridhika na maamuzi ya Tume, wakafungua maombi Mahakama kuu, wakiomba maamuzi ya Tume yapitiwe upya.
MAHAKAMA KUU:
-Neema akashinda kesi tena dhidi ya NMB.
- Mahakama Kuu ikatupilia mbali maombi ya NMB, na kupigilia msumari maamuzi ya Tume yaliyompa Neema tuzo ya kulipwa mshahara wa miezi 36.
-Mahakama Kuu nayo ikasema Neema hakufutwa kazi kihalali, na kwamba utaratibu haukufatwa.
-Mahakama Kuu pia ikasema, NMB wameshindwa kuthibitisha kwamba mlalamikaji alikuwa haendi kazini siku za jumamosi.
-Zaidi sana, Mahakama Kuu ikaongezea kwamba, kwanza KITENDO CHA NMB KUTAKA MFANYAKAZI WAO AENDE KAZINI SIKU ZA JUMAMOSI (wakati yeye jumamosi ni siku yake ya Ibada) ILIKUWA NI UBAGUZI AU UNYANYASAJI WA KIDINI (DISCRIMINATION) ambapo ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, na sheria za kazi. (Emphasis added).
-Nanukuu kwa kiingereza, “High Court found the appellant's (NMB) conduct to have amounted to discrimination against the respondent on religious basis which was contrary to the Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 and the Labour Laws.”
-Mahakama ikasema kila mtu ana haki ya uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 19, ibara ndogo ya kwanza na kifungu cha 7(a) cha sheria ya Ajira na Mahusiano kazini. [Article 19(1) of the Constitution and section 7(4) (a) of ERLA].
-Hivyo basi, Mahakama ikasema kwamba sera na Kanuni za kazi za NMB zinakiuka Katiba pamoja na Sheria ya Ajira, kifungu cha 7(4).
-NMB haikuridhika na maamuzi ya Mahakama Kuu.
NB: (Usiporidhika na maamuzi ya Mahakama Kuu, unakata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa ambayo ni Mahakama ya juu na yenye Mamlaka ya mwisho nchini Tanzania.)
-NMB ikakata rufaa Mahakama ya Rufaa.
MAHAKAMA YA RUFAA
-Kesi ilisikilizwa na Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa.
-Mawakili wa pande zote mbili wakawasilisha hoja zao (ambazo sitaziandika hapa ili hii makala isiwe ndefu sana ikakushinda kusoma).
-Baada ya kuwasikiliza Mawakili wa pande zote, Mahakama ya Rufaa ikakaa sasa kuamua, ‘Je, Mlalamikaji alifutwa kazi kihalali na kwamba sheria ilifatwa au la!’
-Mahakama ikakuta Neema, akiwa katika eneo la kazi, alikuwa anatendewa tofauti na wafanyakazi wengine kuhusu haki ya Ibada.
-NMB waliruhusu baadhi ya wafanyakazi akiwemo Branch Manager kwenda kusali wanavyotaka lakini wakati huo huo wakamzuia Neema asiende kusali.
-Mfano Waislam waliruhusiwa kwenda kusali Ijumaa, lakini Neema alikataliwa siku ya Jumamosi.
-Mahakama ya Rufaa ikakubaliana na Mahakama Kuu na kusema kwamba, hicho kitendo cha mwajiri (kumzuia mfanyakazi kusali siku ya Jumamosi), ni kinyume na ni ukiukwaji wa sheria ya kazi kifungu cha 7(4)(g).
-Hicho kifungu kinakataza ubaguzi dhidi ya mfanyakazi kwa sababu mbali mbali ikiwemo dini au Imani.
-Nanukuu kwa kiingereza “as correctly found by the learned Judge of the High Court, the act of the appellant (NMB) as an employer contravened the provisions of section 7(4) of the ELRA which abhors discrimination at place of work”
-Mwisho Neema Akeyo akashinda kesi tena.
-Mahakama ya Rufaa ikasema imejiridhisha kwamba mlalamikaji hakufutwa kazi kihalali (the termination of Neema Akeyo was substantively unfair).
-Mahakama ya Rufaa ikasema, Tume ya usuluhishi (CMA) na Mahakama Kuu walikuwa halali kuamuru alipwe mshahara wa miezi 36 kama fidia.
-Rufaa ya NMB ikatupiliwa mbali, hivyo NMB wakawa wameshindwa kesi. (The appeal was dismissed)
-Na kwa kuwa Mahakama ya Rufaa ndiyo Mahakama ya juu na yenye Mamlaka ya mwisho nchini Tanzania, ukishindwa hapo basi hamna pa kwenda labda uombe review (marejeo) ambapo Mahakama ya Rufaa itakaa tena kupitia (ku review) uamuzi wake upya.
Wito wangu kwa waajiri, heshimuni uhuru wa kuabudu kwa watu wote. Yeyote ambaye Mungu amekupa dhamana ya kuongoza watu wake, usitumie nafasi yako kukandamiza uhuru wa dini. Watu wakiomba ruhusa kwenda kuabudu, wape ruhusa.
Tunapoomba tunaombea taifa, shule, chuo, ofisi, kampuni n.k.
Kesi hii ipo mtandaoni kwa lugha ya kiingereza. Ukitaka kujisomea kwa undani zaidi. Ingia Google (Tanzlii website) andika National Microfinance Bank Ltd (NMB) Vs Neema Akeyo, 2020.
IMETAFSIRIWA na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke (0754575246 - WhatsApp).