Martin Maranja Masese: Fedheha Makubaliano Barrick na Serikali

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,402
74,004
Na Martin Maranja Masese

“FEDHEHA MAKUBALIANO BARRICK NA SERIKALI”

Julai 2019 Barrick Gold corporation ilinunua kampuni ya ACACIA Mining Plc kwa $428M. Hii ni baada ya mjadala wa muda mrefu kati ya BARRICK na ACACIA takribani miezi 5 ya mazungumzo BARRICK na ACACIA wakakubaliana thamani ya kampuni ya ACACIA ni $951M.

Awali majadiliano kati ya serikali na BARRICK yaliyofanyika Tanzania yaligomewa na ACACIA na wanahisa wengine wa ACACIA ambao wanamiliki karibu 36% ya hisa zote za ACACIA. Serikali iligoma kwenda mezani na ACACIA, wakaamua kukaa na BARRICK Gold Corporation.

Utaratibu wa wanahisa ndani ya ACACIA ni tofauti na kampuni nyingi, BARRICK ambaye ana hisa nyingi (74%) haingii kwenye mjadala kujadili makubaliano yake na serikali dhidi ya ACACIA. Wanahisa wengine wanayo nguvu ya kuweza kukataa mapendekezo ya BARRICK.

Mgogoro ulikuwa katika Mgodi wa Bulyanhulu na Buzwagi (ambao uzalishaji upo mwisho), CHINA walikuwa tayari kulipa gharama na fidia zote kwa BARRICK kununua mkataba wa uchimbaji (assessments tayari). BARRICK hawakuwa tayari kupoteza mgodi wa Bulyanhulu

Barrick Gold corporation wakaingia makubaliano na serikali ya Tanzania siku ya tarehe 19 Mei 2019 ingawa yaliwekwa wazi na kampuni ya BARRICK GOLD CORPORATION siku ya tarehe 19 Julai 2019 mara baada ya kufanikiwa kuinunua kampuni ya ACACIA Mining plc.

Kanuni za masoko ya mitaji zimewalazimisha BARRICK kuweka hadharani makubaliano yao na serikali ya Tanzania. Ingawa kanuni hizo haziibani serikali katika hilo (ukizingatia, TZ sio sehemu ya OGP hivyo haikulazimika kuweka wazi Bungeni makubaliano hayo na Barrick Gold corporation)

Serikali ilikubaliana na BARRICK italipwa $300M kama sehemu ya kumaliza mgogoro wote na sio tena ile fedha ya kununua NOAH (kishika uchumba/Good faith), lakini BARRICK watalipa kwa miaka 7 ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo ACACIA inaidai Tanzania.ACACIA GROUP ina madai ya marejesho ya VAT karibu $240M. Hivyo katika malipo ya $300M, fedha zitakazobaki baada ya kutoa madai ya VAT REFUNDS ni $60M. Hivyo serikali ya Tanzania inatoa ‘bakshishi’ ya $25M (wastani wa TZS 59bn) kwa Barrick Gold Corporation.

300M italipwa kwa miaka 7 lakini BARRICK wanapewa VAT REFUNDS ya $240M na wanapewa msamaha wa capital gains $85.6M (TZS 200bn). 25 Mei 2020 serikali lipokea TZS 250 bilioni kutoka katika ile TZS 695.6 bilioni kama nia njema (goodwill gesture). Malipo ya awali yangefuatiwa na malipo matano ya kila mwaka ya US$40 milioni kila moja.

Serikali imetoa msamaha wa VAT kwa BARRICK zaidi ya $85M (TZS 200bn) sehemu ya ‘faida ya mtaji - capital gains’ inayotokana na mauzo ya hisa za ACACIA kwa Barrick. Mapato hayo serikali iliyopoteza ni mapato halali. Barrick inainunua ACACIA kwa hisa ambazo Barrick hakuwa mmiliki, hisa zenye thamani ya $428M zenye capital gains Tax ya 20% ambayo ilipaswa kulipwa bila kutoa msamaha wa kodi (waiver).

“The government of TZ will receive its economic benefits shares through withholding tax, royalties, clearing fee, fuel and petrol levies, road tolls, local government levies, import duties, skills development levy and other similar fiscal levies, if any,” Muhimu hapa ni “if any”.

Serikali ya Tanzania itapata hisa za bure 16% Kutoka ACACIA lakini ni hisa dhaifu kutoka daraja B, haziruhusiwi kuuzwa, hutumii kama dhamana ya mkopo, hazina ‘voting point’ kwenye masuala mengine ya kampuni, gawio litaifikia seriali ya Tanzania baada ya kutoka daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Pia, Mwenyekiti wa bodi - ‘board of directors’ kwenye kampuni ambayo itaundwa baada ya mgawanyo wa hisa hizo 16% kwa serikali ya Tanzania, atachaguliwa kutoka kwenye wanahisa wa ‘daraja A’ na taarifa inaeleza “… a holder of Class B shares has no such right,”

Lakini pia, kinyume na matakwa ya sera zenye kuendesha masoko ya mitaji ba hata sheria ya madini (2010) iliyotungwa na bunge, serikali imekubali BARRICK kutoorodhesha hisa zake kwenye soko lolote la hisa Tanzania. Hivyo hawatauza 30% ya hisa kwenye soko la hisa la Tanzania.

Barrick Gold Corporation wamekubaliana na GoT baada ya mkataba wao kukamilika Bunge haliwezi kutunga sheria ambayo itabadili makubaliano na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa wakati wote ambao BARRICK watakuwa wanawekeza

Maana, Bunge la Tanzania limezuiwa kwa namna yoyote kutunga kanuni au sheria nyingine yoyote hata kama itachukua miaka 100 ambayo BARRICK watakuwa wanaendesha shughuli zao (fiscal stabilisation) Tanzania. Hivyo Barrick watafanya ambayo yanawafurahisha bila bunge kuingilia.

Mapendekezo ya Kamati zile mbili alizounda Rais Magufuli, kamati za makinikia zilipendekeza kuhusu mashauri yote yafanyike nchini, BARRICK wamegoma, hivyo kwenye makubaliano hayo wameruhusiwa kufungua kesi zao kwenye mahakama za usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ughaibuni.

Kampuni za uwekezaji kwenye madini zimezuiliwa kisheria-sheria mpya za madini) kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Sheria inazitaka kampuni kushughulikia migogoro yote ya kibiashara na uendeshaji katika mahakama za ndani ya nchi. BARRICK walitoa pendekezo lao na likakubaliwa.

BARRICK Gold Corporation wametaka migogoro yao ifanyikae kwa mujibu wa kanuni za The United Nations Commission on International Trade Law (UNCITRAL) Arbitration Rules na Rais wa kituo cha usuluhishi wa migogoro ya kibiashara cha Singapore ndio ambaye atateua wasuluhishi.

“the president of the Singapore International Arbitration Centre has been given the mandate to determine the arbitral seat upon failure by both sides to agree.” hivyo anaweza kuamua kuteua wajumbe kutoka pahali anapoona panafaa, habanwi kuteua wajumbe kutoka Tanzania.

BARRICK Gold corporation wataendelea kusafirisha makinikia nje ya nchi katika makubaliano hayo hakuna sehemu wamekubali kujenga ‘smelters’ nchini kama ambavyo kamati zile mbili zilivyopendekeza. Na wamekubaliana kuendelea kutumia benki za nje kutunza fedha zao za mapato ya ndani.

Tanzania Mining Companies (TMCs) shall not at any time have any obligation to establish beneficiation-including gold refining and concentrate smelting facilities - in the country. Kwa wakati wowote TMC hawatakuwa na mamlaka ya kupunguza au kuongeza vituo vya uchenjuaji makinikia

Tangu Barrick Gold Corporation wachukue umiliki wa North Mara na Bulyanhulu September 2019, uwekezaji wao umefika $1.995 billion. Hadi kufikia Julai 2022 katika ile $300M walifanikiwa kulipa $140M (kama sehemu ya kumaliza mgogoro). Hiyo ni kwa mujibu wa CEO Mark Bristow.

Taarifa ya BARRICK GOLD CORPORATION ina makubaliano mengi iliyoingia na serikali ya Tanzania, lakini kwa kiasi kikubwa BARRICK wameondoka kwenye meza za MAZUNGUMZO wakiwa washindi, mapendekezo yote ya Kamati zile za Rais Barrick haikuyapokea, na kama yalipokekewa, yalifinyangwa. Hayo ndiyo mambo, Profesa Palamagamba Kabudi aliyotuingiza. Rais Magufuli alifahamu, alifikishiwa haya makubaliano akiwepo ofisini. BARRICK ni washindi ndiyo maana hadithi ya NOAH kwa kila mtanzania imeyeyuka kama theluji wakati wa kiangazi.
#MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila

Taarifa ya BARRICK GOLD CORPORATION ina makubaliano mengi iliyoingia na serikali ya Tanzania, lakini kwa kiasi kikubwa BARRICK wameondoka kwenye meza za MAZUNGUMZO wakiwa washindi, mapendekezo yote ya Kamati zile za Rais Barrick haikuyapokea, na kama yalipokekewa, yalifinyangwa.

Hayo ndiyo mambo, Profesa Palamagamba Kabudi aliyotuingiza. Rais Magufuli alifahamu, alifikishiwa haya makubaliano akiwepo ofisini. BARRICK ni washindi ndiyo maana hadithi ya NOAH kwa kila mtanzania imeyeyuka kama theluji wakati wa kiangazi

#MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila
 
Huko chadema ana cheo gani?
Kwahiyo zile NOAH kwa kila Mtanzania zilipeperuka?😂
FB_IMG_1575390792397.jpg
 
Capital gain Tax na VAT ni kodi mbili tofauti ata aeleweki anaongea kitu.

Capital gain ailipwi na mnunuaji, bali muuzaji, kwa ACCACIA ndio alitakiwa alipe kama hakufanya hivyo.

Moreover capital gain tax rate in Tanzania ni 30% not 20% kama anavyodai. Halafu sio hela yote ya mauzo unalipa capital gain.

Muuzaji anaruhusiwa kutoa initial capital investment costs (with adjusted inflation to reflect current currency value). Anatoa gharama za wanasheria na tozo alizotumia kwenye kununua na kuuza assets/shares kwa hivyo $428m yote aiwezi kuwa subjected to capital gain.

Why not bother to educate oneself on issue of interest in a world which knowledge is somewhat free, rather than kuandika mashudu kama haya.

I don’t even understand why serikali huwa inapoteza muda na wanaharakati wa twitter (X) for the most huwa wanajazana hoja za ujinga mtupu.
 
Kwa taarifa yako huyo unayesema ni mpotoshaji, ameeleweka vizuri kwenye huo upotoshaji, kuliko ww ambaye unajioma mwerevu. Nyie ndio wale watu wa serekali ambao huwa mnaenda mahali kutoa elimu lakini mnaishia kuwachanya watu. Na hii ndio sababu sehemu kubwa shughuli za serekali zinafanyika kwa ufanisi duni, kwa ajili ya kuwa na wataalamu wenye viburi vya elimu, lakini wenye tija ndogo kwenye jamii.

Inaonekana ww ni mshamba fulani uliyekuja mjini ukubwani kwa ajili ya masomo, ndio maana una ulimbukeni wa elimu. Kiufupi ww ni mshamba wa nguvu na elimu yako isiyo na tija.
 
Ushamba ni kupotoshana na kuanza kupiga makelele ya kulaumu vitu ambavyo watu wanatoa vichwani kwao tu.

Business ni ‘going concern’ VAT returns unakata juu kwa juu on VAT payments unazotakiwa kulipa na wewe; it has nothing to do na malipo mengine. Na mtu pekee unawaeza mdai ni TRA not the other government bodies.

Mnawapa wananchi false premises ya mambo mengi sana which leads to false conclusions ya mambo mengi sana. Heck sometimes even the government is pressurised na kuishia ku-react kujibu mambo ya ujinga na mwishowe kutandikwa kweli na makampuni ya kigeni kwa hoja za upuuzi kama hizo.

Ushamba wangu ni wangu ahukuhusu.

The whole article is pathetic ni maneno yake tu, nothing to do with accounting mechanics.
 
Nasema hivi, nyie washamba mliokuja mjini ukubwani ndio mko maofisini kutunga Sheria na miongozo isiyotekelezeka, kisha wananchi wanapohitaji ufafanuzi mnaishia kutoa ufafanuzi usioleweka, huku mkichanganya vijimaneno vya kiingereza visivyo na kichwa Wala miguu kujifanya wasomi. Ndio maana mifumo mingi ya serekali ina ufanisi duni kutokana na washamba wa aina yako. Unakuta mtu Yuko hapa mjini Hana elimu yoyote ya maana, lakini anaendesha shughuli yake kwa ufanisi, huku taasisi ya serekali inayoendeshwa na wataalamu wa aina yako ikiendeshwa kwa hasara!

Nina uhakika Mimi hapa nilipo na elimu yangu ya kawaida ukinipa 200m na ww ukapewa 1b, baada ya miaka mitatu, Mimi nitakuwa na matokea ya maana kuliko ww uliyepata 1b. Sana sana utaishia kujaza makaratasi kabatini, na kuongea kiingereza chenye lafudhi ya kilugha na kuchanganya na kiswahili, lakini hutokuwa na lolote la maana.
 
Back
Top Bottom